Abduel Elinaza
MAANA YA NENO KUBATIZWA AU UBATIZO
Lugha za asili za biblia kabla ya tafsiri mbalambali ni kiebrania na kiyunani. Agano la kala
iliandikwa kwa lugha ya kiebrania na again jipya iliandikwa kwa kiyunani. Katika kuifasiri biblia kwa lugha zetu kuna baadhi ya maneno machache ambayo misamiati yake ilipoteza maana halisi iliyopo katika biblia. Kwasababu lugha zingine zunakuwa na mapungufu.
Katika biblia ya lugha ya kiebrania kuna neno “BAPTIZO” lenye maana ya UBATIZO kwa Kiswahili na kwa kiingereza BAPTIZM,
Katika biblia ya lugha ya kiyunani kuna neneo “BAPTO” lenye maana ‘kuzamisha au kuchovya”.
Mifano katika biblia kuhusiana na neno” BAPTO’ kuzamisha au kuchovya.
( 1 ). Tonge la ugali linavyotowelewa katika ugali kasha linazamishwa lote. Tendo hilo la kuziswa ni kubapto “bapto” katika kiyunani (YOHANA 13:26).
( 2 ). Kuchovya ncha ya kidole. Neno kuchovya hapo (LUKA 16:24) lina katika lugha ya kiyunani ni ‘BAPTO” bapto likiwa na maana kuchovya au kuzamisha.
( 3 ) Tendo la kuchovya vazi katika damu lina maana ya kubapto “ BAPTO” katika biblia ya ya lugha ya asili kwa kiyunani.
Kwahiyo biblia inapozungumzia juu ya ubatizo inazungumzia ubatizo wa maji tele.Yohana aliwabatiza watu wa Ainoni kwasababu huko nako kulikuwa na maji tele (YOHANA 3:23). Pia tunamuona mtumishi wa Mungu Filipo na owashi wakitelemka majini ili abatizwe katika maji tele (MATENDO 8:34-39). Walitelemka majini akambatiza kasha wakapanda kutoka majini (MATENDO 8:36-39).
WATU WANAOFUNDISHA JUU YA UBATIZO WA KUNYUNYIZIA MAJI KICHWANI AU USONI NAO PIA WANA MAANDIKO.
EZEKIELI 36:25 “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafuwenu wote, na vinyago vyenu vyote”. HESABU 8:5-7 “Kisha Bwana akanena na Musa. Na kumwambia, watwae walawi na kuwaondoa kati ya wana wa Israeli, kasha uwatakase. Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa, nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kasha wazifue nguo zao na kujitakasa”. UPOTOFU NI RAHISI KUINGIA KAMA TUTAYATAFSIRI MAANDIKO KAMA TUPENDAVYO. (2 PETRO 1:20; 2TIMOTHEO 2;15).
Maana ya maandiko hayo yanayotumiwa kimakosa kuharalisha ubatizo wa kunyunyiza maji kichwani au usoni. HESABU 19:13 “Mtuawaye yote agusaye maiti ya mtualiyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi, unajisi wake ungali juu yake bado”. Kwahiyo tunaona kuwa wakati wa agano la kale mtu aliyekuwa akiigusa maiti ya mtu aliyekufa, alihesabika kuwa amenajisika kwa kuigusa tu. Alihesabika kuwa ni mwenye dhambi (unajisi) na angeweza kulinajisi hekalu la Bwana (maskani ya Mungu). Mtu aliyenajisika alihesabika kuwa safi baada ya kunyunyiziwa kichani maji ya utakaso yaitwayo FARAKANO. WAEBRANIA 9:10 “kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya”.Hayo maandiko wakati wake ulishapita maana sisi tunaongozwa na agano jipya, again la rohoni, aganin la kale lilikuwa na mapungufu (WAEBRANIA 8:7-9). Dhambi au uchafu unaondolewa na damu ya Yesu kwa njia ya imani (1PETRO 1:2). Hatunyuziwi maji kichwani bali damu ya Yesu ndiyo inayonyunyizwa juu yetu na kuondoa dhambi. Tendo la kunyunyiziwa damu ya Yesu ndilo linaitwa kuzaliwa kwa roho au kuzaliwa mara ya pili (YOHANA 3:3-10). Mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu (YOHANA 3:5; 1:12). Maji yanayotajwa katika YOHANA 3:3-10 ni neno la Mungu siyo ubatizo wa maji kama walimu wengi wanavyopotosha. Neno la Mungu linamsafisha mtu kama vile maji yasafishavyo (1PETRO 1:23)
KABLA YA KUBATIZWA SHARTI MTU HUYO ATUBU DHAMBI ZAKE ZOTE KWA KUMWAMINI YESU KRISTO BAADA YA KUHUBIRIWA AU KUFUNDISHWA . Ili mtu awe na sifa ya kubatizwa kibiblia lazima atubu dhambi zake kwanza kwa kumwamini mwanawa Mungu Yesu Kristo . (MATENDO 2:37-38) “ Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha roho mtakatifu”. MARKO 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.Mtu anabatizwa baada ya kuamini na kutubu dhambi zake zote. Kuamini maana yake ni kuacha njia zako zote za awali na kugeuka au kufanya matendo ya wokovu. MATENDO 2:41 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu”. MATENDO 8:12-13 “ Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njeme za ufalme wa Mungu na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. Na yeye Simon mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; Akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka”. Pia katika MATENDO 8:35-38 Towashi aliamini kwanza kabla ya kubatizwa na Filipo. Mtu baada ya kujifunza Neno la Mungu na kuliamini kwa moyo wake wote na kusafishwa kwa damu ya Yesu kwa njia ya imani aweza kubatizwa (MATENDO 16:31-33; MATENDO 18;8)
UBATIZO HAUFANYWI KWA WATOTO WADOGO.
Kwa kawaida watoto wadogo wanapobatizwa huwa anakuwepo mtu mzima amempakata na kujibu maswali badala ya mtomto huyo, hii siyo sahihi kibiblia EZEKIELI 18:20 “Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa babaye, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe; haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake”. Kwa msingi huo, mtu hawezi kutubu dhambi kwa niaba ya mtu mwingine. Ni muhimu kufahamu kuwa watoto wadogo ufalme wa mbinguni ni wao hata bila kutubu dhambi (MARKO 10:13-14). Sisi sote tunazaliwa tukiwa na dhambi ya asili. Tnazaliwa kwa mfano wa Adamu na si kwa mfano wa Mungu (ZABURI 51:5; ZABURI 58:3). Pasipo sheria hakuna dhambi, dhambi inahesabiwa kwa sheria (WARUMI 4:15; WARUMI 5:12-13). Mtoto anaweza kutenda dhambi kama vila kusema uongo, kutukana, uchoyo, ugomvi, kucheza dansi (mzikiwa kidunia), kuzira n.k .Lakini sasa watoto hawahesabiwi dhambi kwa kuwa hawajui mema na mabaya. Watoto hawana uwezo wa kupambanua au kutofautisha mema na mabaya. Wanafanya bila kujua kuwa ni dhambi, ndiyo maana Yesu alisema ufalme wa mbinguni ni wao.Kabla motto kuzaliwa duniani dhambi ilikuwa imekwisha kuwako. Adanu na Eva walitenda dhambi kabla ya kuwazaa watoto wao (WAEBRANIA 5:13-14). Mwenye uwezo wa kupambanua mema na mabaya ni mtu mzima, motto mdogo akifa anaenda mbinguni moja kwa moja bila kizuizi chochote.
YESU ALIWABARIKI WATOTO HAKUWABATIZA.
Yesu mwenyewe aliwabariki watoto hakuwabatiza. Watoto wadogo wanabarikiwa tu haturuhusiwi kuwabatiza watoto wadogo. Ubatizo unafanya kwa mtu baada ya kulisikia Neno la Mungu na kutubu dhambi zake zote. Lazima mtu asafishwe dhambizake kwanza kwa damu ya Yesu kwa njia ya imani. Yesu mwenyewe alibarikiwa akiwa motto mdogo na kubatizwa akiwa mtu mzima (LUKA 2:27,34; LUKA 3:21-23).
YESU KRISTO ALIBARIKIWA AKIWA MTOTO NA KUBATIZWA AKIWA MTU MZIMA.
Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni kielelezo au mfano wa jinsi tunavyotakiwa kuishi na kutenda , alibarikiwa akiwa motto mdogo (LUKA 2:27,34). Yesu Kristo akaonesha mfano kwa kubatizwa akiwa mtu mzima na akasema ndivyo inavyotupasa kuitimiza haki yote (LUKA 3:21-23; MATHAYO 3:13-17). Tunaona Yesu alibarikiwa na mtumishi wa Mungu Simion akiwa motto mdogo, na kubatizwa akiwa na umri unaokaribia miaka thelathini. Tunapaswa kujifunza kwa Kristo (1 PETRO 2:21; 1WAKORITHO 11;1, MATENDO 2:37-41). Watu waliobatizwa wakati wa kanisa la kwanza walikuwa wengi sana hivyo walikuwa na umri wa miaka tofauti.Kigezo kinachotumika ni utu uzima, yaani uwe na uwezo wa kupambanua mema na mabaya (WAEBRANIA 5;13-14).
.UWEZEKANO WA KUBATIZWA MARA MBILI AU ZAIDI.
Wapo watu wengine watasema mimi nilishabatizwa tangu mwanzo toka utotoni, sasa itakuwaje baada ya kugundua kuwa nilibatizwa kimakosa?. Wapo watu ambao walibatizwa mara mbili katika biblia ingawa mwanzo walibatizwa katika maji tele (MATENDO 19:3-5). Ikiwa mwanzo tulibatizwa kwa ubatizo usio wa kibiblia, tunapaswa kubatizwa ubatizo wa kibiblia kama Yesu alivyosema tujifunze kwake (MATHAYO 11:29). Huhitaji kuomba ushauri kwa mtu yeyote, ni kulitii Neno la Mungu tu bila kulijadili kwanza. Ubatizo wa kibiblia unafanywa kwa mtu mara moja tu. Mtu anayetakiwa kubatiza sharti awe ni mwanafunzi wa Yesu. (YOHANA 4:2). Kama ulibatizwa bila kutubu dhambi kwanza huo sio ubatizo wa kibiblia ni sawa na mtu aliyeoga majini tu. Kama ulibatizwa utotoni unahitaji kutubu dhambi zako mwenyewe na ndipo utaweza kubatizwa kibibli. Kama ulinyunyiziwa maji kichwani au usoni hujabatizwa kibiblia. Lazima uzamishwe katika maji na ndipo unakuwa umeshiriki mauti ya Kristo (WAKOLOSAI 2:12, WARUMI 6:4-5).
TUNABATIZWA KATIKA MAJI MENGI ILI TUWE WA KRISTO.
Hatuna budi kufahamu kuwa safari Yetu ya kuelekea mbinguni inafananishwa na safari ya wana wa Israeli kuelekea Kanani (1WAKORINTHO 10;11). Mungu alimtumia Musa kuwaokoa waisraeli mikononi mwa Farao ili wamtumikie na leo hii kamtuma Mwanae wa pekee Yesu Kristo ili kutuokoa kutoka utumwani mwa Shetanui ili tumtumikie Mungu.
Ni muhimu kufahamu kuwa ubatizo ulikuwepo tangu zamani za agano la kale. Waisraeli walibatizwa ili wawe wa Musa (1WAKORINTHO 1O:1-2). Tunabatizwa sawasawa na agizo la Yesu ili nasi tuwe wa Kristo. Ni muhimu kufahamu kuwa kuzamisha katika maji tele kibiblia ni sawa na kuzikwa ndiyo maana ubatizo ni mara moja tu. Tunazikwa na kufufuka na Kristo kwa njia ya ubatizo. Hapa ndipo tunashiriki mauti ya Kristo (WAKOLOSAI 2:12). Utii wa kwanza kwa mtu baada ya kuokoka ni kukubalikuzikwa na kufufuka pamoja na Kristo (WARUMI 6:4-5). Kwahiyo kubatizwa katika maji mengi kunatufanya kushiriki mauti ya Kristo yaani kuzikwa na kufufuka kwake. Maji yanakuwa kama kaburi tu ambayo mtu anazamishwa ndani yake ili kushiriki mauti ya Yesu kibiblia (WAKILOSAI 2:12, WARUMI 6:4-5).
KUWA TAYARI KUTIMIZA HAKI YOTE.
(MATHAYO 3:13-15)
Yesu Kristo alisema “ndivyo inavyotupasa kutimiza haki yote”.Kutimiza haki yote maana yake nini? Tunaona maana ya haki yote katika (ZABURI 119:172) . Haki yote ni maagizo yote (ZABURI 119:6). Tunapaswa kutimiza haki yote (maagizo yote ) ya Yesu. Yesu Kristo alitimiza haki yote ingawa alikuwa hana dhambi na ndiyo maana Yohana mbatizaji alishangaa na hakutaka kumbatiza akisema kuwa yeye hastahili kabisa kumbatiza. Tunatakiwa kuwa tayari kutimiza haki yote kama Yesu alivyofanya. Wana wa Israeli walibatizwa mara tu walipotoka katika utumwa wa Farao na sisi tunapaswa kubatizwa mara tu tunapotoka katika utumwa wa dhambi au utumwa wa Shetani.
JE, WANAFUNZI WA YESU WALIBATIZWA?
Ni muhimu kufahamu kuwa kuna mambo mengi sana aliyoyafanya Yesu lakini hayakuandikwa, ndiyo maana habari zingine hatuzikuti katika maandiko. Lakini haya yaliyoandikwa yanatosha kutuongoza katika njia ya Bwana. Kwa mfano, neno Television halipo katika biblia lakini kuna andiko linalotukataza kuweka matendo maovu mbele za macho yetu (ZABURI 101:3). Yesu Kristo alifundisha yale aliyoyatendea kazi mwenyewe (MATENDO 1:1). Yesu alibatizwa kwanza ndipo aliposema aaminiye na kubatizwa ataokoka. Pia aliowasimamia wanafunzi wake walipokuwa wakiwabatiza watu wengine (YOHANA 4:2). Kama wangelikuwa hawajabatizwa Yesu kristo asingeliwapa rkibali cha kuwabatiza wengine. Yesu aliwakabidhi kazi ya kubatizwa kwa kuwa hawakuwa wanafiki kama mafarisayo (MATHAYO 23:3-4)
JE, PAULO MTUME ALIBATIZWA KATIKA MAJI TELE?
Katka kitabu cha MATENDO 9:18) biblia zetu za Kiswahili zinasema alibatizwa lakini hazielezi vizuri. Tafsiri nzuri tunaipata latika biblia ya kingreza tafsiri ya king James Vision, ACTS 9:18
18 And straightway there fell from his eyes as it were scales, and he received his sight; and he arose and was baptized;
Paulo mtume katka mafundisho yake alifundisha kwamba watu wamfuate yeye kama anavyomfuata Kristo (1 WAKORINTHO 11:1). Yesu ndiye aliyeagiza kuwabatiza watu mara wanapotubu dhambi zao. Tunamuona Paulo akibatiza (MATENDO 19:3-5). Kama yeye angekuwa hajabatizwa katika maji mengi asingewabatiza wengine katika maji mengi..
JE. ASKARI WA GEREZA NA WATU WA NYUMBANI MWAKE WALIBATIZWA KATIKA MAJI TELE? (MATENDO 16:30-34).
Agizo la Yesu kwa wanafunzi wake kwa kila aaminiye kuwa ni sharti abatizwe, wanafunzi wake hawa walilitendea kazi. Tunaoan kuwa walibatizwa lakini kuna watu ambao siku hizi ambao hutafuta andiko la kupindisha ukweli ili kuharalisha uovu wao
Bila shaka watumishi hawa waliwapeleka mahali penye maji mengi na kuwabatiza kwa kuwazamisha ili washiriki mauti ya Yesu kuzikwa na kufufuka kwake (WAKOLOSAI 2:12; WARUMI 6:4-5).
KAMA MTU YUPO MAHALI AMBAPO HAPANA MAJI MENGI KAMA JANGWANI ATABATIZWA WAPI? (LUKA 14:28-32; MATHAYO 12:42)
Kwa Mungu hakuna udhuru wowote, yeye akiagiza haunabudi kulitendea kazi agizo hilo. Kwa gharama yoyote tunapaswa kuhakikisha tunatimiza haki yote kwa kubatizwa katika maji tele., Hatuna budi kusafiri kuyafuata maji yaliko kwa gharama yoyote. Kama Malkia wa Kushi aliweza kusafiri umbali mkubwa kwenda kuitazama hekina ya Sulemani Yesu anasema huyo atawahukumu watu wenye udhuru wa umbali. Wanadamu wanatafuta visingizio ili wasibatizwe katika maji tele kibiblia.
JE, IKIWA NILIBATIZWA KWA KUFUATA MKUMBO NIFANYE NINI?
Kama ulibatizwa kabla ya kutubu dhambizako na kuzaliwa marapili unatakiwa kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha na ndipo ubatizwe katika maji tele. Hii Ni pamoja na watu wote waliobatizwa utotoni kinyume na Neno la Mungu. Tumeona kuwa watoto wadogo hawabatizwi bali wanabarikiwa tu. Hata Yesu hakubatizwa akiwa motto, alibarikiwa akiwa motto na kubatizwa alipokuwa mtu mzima.. Lazima mtu ahubiriwe injili ya Yesu na aiamini na kutubu dhambi zake zote hapo anakuwa ametimiza sifa ya kubatizwa (MATENDO 2:37-41).
JE, IKIWA NILIBATIZWA NA MTU AMBAYE HAKUBATIZWA KATIKA MAJI TELE NIFANYE NINI?
Ikiwa tulibatizwa na mtu ambaye yeye mwenyewe hajabatizwa kibiblia tunapaswa kubatizwa mara ya pili. Mtu anayetakiwa kubatiza lazima awe ni mwanafunzi wa Yesu kwele kweli anayemfuata Yesu kwa kila jambo. Paulo alisema tumfuate yeye kama anavyomfuata Yesu Kristo (1WAKORINTHO 11:1).
JE, IKIWA NILIBATIZWA NA MTU AMBAYE HAAMINI UBATIZO WA MAJI TELE NIFANYE NINI?
Kama tulivyoona mwanzo, kazi ya kubatiza niya wanafunzi wa Yesu tu. Wanafunzi wa Yesu ni watu wote ambao wameokolewa kwa kutubu dhambi zao na kuwa tayari kuishi sawasawa na Neno la Kristo. Watu wote ambao wanatuimiza haki yote ikiwa ni pamoja na kubatizwa katika maji tele. Yeye mwenyewe anatakiwa awe amekwisha kubatizwa katika maji tele. Ikiwa ulibatizwa na mtu ambaye yeye mwenyewe hajaamini unatakiwa kubatizwa tena.
JE, KAMA MTU ALIBATIZWA KIBIBLIA HATIMAYE AKARUDI NYUMA KIROHO, AKITUBU ATABATIZWA TENA?
Ubatizo wa kibiblia unafanyika mara moja tu kama vile Yesu alivyozikwa mara moja na kufufuka mara moja tu (WAKOLOSAI 2:12; WARUMI 6:4-5). Mtu akirudi nyuma kiroho, akitubu tene hatakiwi kubatizwa tena.
JE, TUNABATIZA KWA JINA LA NANI?
(MATHAYO 3:13-16; MATENDO 8:36-39; MATHAYO 28:19).
Ubatizo wa kibiblia unafanya kwa mtu mara moja tu. Tena tunabatiza kwa jina la Baba,na Mwana, na Roho mtakatifu. Tunachovya au kuzamisha mara moja tu na si mara tatu kama majina yalivyo. Tunazamisha mara moja kama Yesu alivyozikwa mara moja.
JE, MBONA MITUME WA YESU WALIBATIZA KWA JINA LA YESU?
(MATENDO 19:3-5; MATENDO 10:48; MATENDO 8:14-17; MATENDO 2:38).
Kielelezo chetu siyo mitume bali ni Kristo. Paulo anasema tumfuate yeye kama anavyomfuata Kristo (1 WAKORINTHO 11:1). Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake, wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka (YOHANA 13;16). “Kwa jina la” ina maana “kwa ajizo la”. (ESTA 8:7-10). Hii ilikuwa inatumika hivyo wakati wa bablia lakini siku hizi ni tofauti na hapo zamani. (ESTA 13:16). Kwa jina la mfalme yaani kwa agizo la mfalme. (ESTA 13:10). Walitaka kutofautisha ubatizo uliofanyika kwa jina la (agizo la ) Yohana na ubatizo wa jina la (agizo la ) Yesu. ( MATHAYO 3:4-6; 3:1-3). Kutokana na kwamba watu wengi walikuwa wameshabatizwa ubatizo wa Yohana, ndiyo maana mitume wakawabatiza tena kwa jina la (agizo la) Yesu. Yesu ni mkuu kuliko Yohana. Mitume walibatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu., kama lilivyo agizo lake Bwana wetu Yesu Kristo..Mungu akikuagiza jambo la kufanya, usipunguze wala usiongeze lolote au kusahihisha (KUMBUKUMBU 12:32). Kwahiyo, tumeagizwa kubatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu (MATHAYO 28:19).
JE, KAMA MTU AMEBATIZWA KWA ROHO, ANAWEZA KUBATIZWA KWA MAJI TENA? (MATENDO 10:44-46).
Ubatizo wa maji mengi wa kibiblia ni kwa watu wote. Yesu alisema ndivyo inavyotupasa kutimiza haki yote. Yesu Kristo alionesha kielelezo kwa kutimiza haki yote. Kubatizwa kibiblia ni kushiriki mauti ya Yessu kwa kuzamishwa ambako ni sawa na kuzikwa, maji ni kaburi (WAKOLOSAI 2:12;; WARUMI 6:4-5).
The righteous care about justice for the poor, but the wicked have no such concern. PROVERBS 29:7
Wednesday, December 5, 2012
Question: "Is it wrong to say 'Xmas' instead of 'Christmas'?"
Answer: There are many who view the word Xmas as part of an overall “war on Christmas.” They view it as a blatant attempt to take Christ out of Christmas. While it is undeniable that some use Xmas in that manner, the actual origin of the word Xmas has nothing to do with taking Christ out of Christmas.
In Greek, the original language of the New Testament, the word for “Christ” is Χριστός, which begins with the Greek letter that is essentially the same letter as the English letter X. So, originally, Xmas was simply an abbreviation of Christmas. No grand conspiracy to take Christ out of Christmas. Just an abbreviation.
But there is no denying that there is a trend to, in a sense, take Christ out of Christmas. In pursuit of tolerance, inclusiveness, and political correctness, some are attempting to obscure the Christian origins of Christmas—as if our society’s materialism has not already obscured the meaning of Christmas. Whether they refer to it as “Xmas” or “the winter holidays” or something else, some will not be satisfied until the celebration is entirely secularized. In response to this, rather than getting angry or complaining about the use of Xmas, we should be sharing the love of Christ through word and deed.
Thursday, November 15, 2012
RIBA NA REHANI KATIKA UKRISTO.
Kama tunavyojua shetani ni
muwindaji hivyo huweka mitego kutunasa .Na mitego hii haiwi wazi wazi na
hulenga sehemu ambayo ni rahisi kuwanasa watu wengi kwa hila.
2Timotheo 2;26.wapate tena fahamu zao nakutoka katika mtigo
wa ibilisi
Miongoni mwa vitu vilivyoibuka Tanzania na duniani kwa ujumla
makanisani yamekuwa mitego.Nayo ni SACCOS NA RIBA makanisani.Na makanisa
mengine yako mbioni kuanzisha BENKI na SACCOS.Je tunakumbuka Yesu alivyosema
nyumba yangu mmegeuza kuwa nyumba ya biashara? .Yohana 2;13-16…..msiifanye nyumba ya baba yangu kuwa nyumba ya biashara.......
Benki na SACCOS inaendesha biashara
kwa kudai riba .Riba ni mtego mkubwa sana katika ukristo.
Sasa Je mtu aliyeokoka anaweza kumkopesha mtu na kudai kurudishiwa riba?
Riba ni kiasi cha ziada nje na mkopo wenyewe.
Rehani ni kile kitu kilichotolewa kama fidia kwakushindwa
kulipa mkopo.
REHANI.
Kama mtu
ameshindwa kurudisha mkopo ukataka kuchukua rehani kwa mujibu wa maandiko matakatifu
huruhusiwi kumchukua au kumnyang’anya kitu chochote ila unatakiwa mdaiwa
achague mwenyewe anachotoa.Kumbukumbu
24;10-13,..umkopeshapo jirani jirani
yako chochote kikopeshwacho usiingie nyumbani mwake kutwa rehani
kwake...........
Kama mdaiwa
ni maskini hutakiwi kuchukua kitu muhimu kwake mfano nguo,chakula nk ila kwa
idhini yake atatoa chochote kama rehani
.Kutoka 22;26-27........
Kama mtu ni
mjane ni mwiko kabisa kuchukua nguo zake kama rehani au ng’ombe wake..Kumbukumbu 24;17-18.Ayubu 24;2,3b,9b.
Maskini
ndio hao wanao chukua mikopo na wengine ni wajane je kanisa litakwepa vipi
katika utoaji wa mikopo na rehani tena bila upendeleo?
Kitu ambacho ni uhai au la kijisitiri
huruhusiwi kutochukua kama rehani.Au na mna yyoyote ya kumkosesha mtu kula au
riziki ni kosa tena biblia imelifananisha na jiwe la kusagia ukichukua jiwe
lolote kati ya yale mawili la juu au la chini ni kosa kwasababu utakuwa
umemkosesha kula.
Unatakiwa
uwe na moyo wa kusaidia na sio kutafuta faida.Kumbukumbu 24;6-10.
Hatuwezi
kuchukua shamba la mtu au mizabibu kwa rehani.Nehemia alikasirishwa sana na
hilo .Nehemia 1;1-4 ndugu
linamaanisha waliookolewa kwani baba yetu ni mmoja.Warumi 16;14,1;1.Mathayo 18;15-17.Miili yetu kama yao maana yake
nao wanakula kama sisi wanategemea mashamba na chakula.
RIBA
Kama
unamkopesha ndugu yako(aliyeokoka) hautakiwi kumdai riba ila kwa watu wa
mataifa(ambao hawajaokoka)Kumbukumbu
23;19-20. Walawi 25;35=38’Nehemia 5;1-6,5;7-10.Nehemia alikasirishwa sana
kwa habari ya riba.
Sifa za
atakaye ingia mbinguni Zaburi 15;1-5”hakutoa
fedha yake kula riba”Nyakati hizi watu watapernda fedha tuwe makini.2Timotheo 3;2
Tuesday, November 6, 2012
TANZANIA NA OIC:Lijue lengo kuu la Azimio la Abuja
: Lijue lengo kuu la Azimio la Abuja
Katika gazeti hilo nikaona kwa mbali neno "Abuja declaration and the Sharia law." Nikalinunua gazeti hilo. Baada ya kulisoma, nikaridhika na nikaunganisha na yanayotokea katika nchi yetu ya Tanzania, juu ya harakati za wenzetu Waislamu ikiwa ni utekelezaji wa tamko hilo muhimu la Abuja.
Tamko au Azimio la Abuja linahusu nini hasa? Kadiri ya maelezo katika internet na gazeti hilo, inaonekana wazi kuwa Azimio la Abuja ni tamko rasmi juu ya Uislamu barani Afrika (Islam in Africa). Kwa hivi tunaweza kusema au tunasema kwamba hili tamko lilitolewa katika kilele cha kongamano la Uislamu barani Afrika. Kongamano hili liliandaliwa na nchi 46 za Kiislamu zinazojulikana kama OIC (Organization of Islamic Conference).
Lengo la umoja huu ni kuuendeleza Uislamu barani Afrika, kutekeleza mikakati ya kiislamu na kutatua matatizo yanayolikabili Bara la Afrika kama vile ukimwi, kifua kikuu, njaa na majanga mengine. Lakini pia inasemekana hata kuona maadili yanafuatwa katika bara hili. Haya si mambo mabaya lakini swali la msingi ni; je, kwa kutumia sheria gani?
Inadaiwa kwamba katika yote hayo lengo kuu la OIC na hasa kupitia Azimio la Abuja ni kuona kwamba Bara lote la Afrika linakuwa la kiislamu. Huu ndiyo ukweli wa mambo na wala si uchochezi wala propaganda, ukitaka ukweli nenda tu kwenye internet utaupata najisomee maandishi mbalimbali juu ya umoja huo wa nchi za kiislamu, yaani OIC.
Kama mwandishi wa habari (mwanataaluma kamili) kazi yangu ni kuelimisha umma na si kuupotosha kamwe. Inaonekana wazi kwamba umoja huu wa nchi 46 za kiislamu, sijui kama Tanzania imejiunga au bado lakini OIC ndiyo mwakilishi na mzungumzaji wa masuala ya pamoja yanayohusu Waislamu barani Afrika na duniani kote kwa ujumla.
Sehemu ya madhumuni ya OIC, kupitia Azimio au Tamko la Abuja ni; "kufuta katika hali zote imani ya dini isiyo ya kiislamu katika nchi wanachama. Na imani ambazo itabidi zifutwe ni dini ya kikristo, na nyinginezo ambazo hazikubaliani na imani ya kiislamu.
Kwa mantiki hii, ni dhahiri kwamba kama Tanzania itajiunga na Umoja huu wa nchi za kiislamu itabidi dini nyingine zisizokubalika kwa imani ya kiislamu basi zifutwe. Sasa swali; je, hapa kuna uhuru wa kuabudu kweli? Na kama nia ya kutaka Tanzania ijiunge huko ni dhahiri Katiba yetu ya Tanzania ni lazima ibadilishwe kwanza, kwa sababu kwa sasa hairuhusu.
Lakini kwa upande mwingine, madhara ya Azimio hili la Abuja tunayasikia mara nyingi nchini Nigeria ambako Wakristo wengi wamekwishauawa kikatili; je, hii ni halali?
Ukichunguza kwa kina unaweza kubaini kwamba utekelezaji wa Azimio la Abuja unakuja pole pole, hauna haraka. Na ninasema wazi kwamba katika uchunguzi wangu nchini Tanzania, mipango hii pia imeanza kutekelezwa kimya kimya na kwa uangalifu mkubwa sana.
Hata hivyo, kwa namna ya kipekee mambo yameshajulikana juu ya ajenda hii ya siri, Mungu hawezi kuruhusu jambo la namna hiyo kutokea katika ardhi ya Watanzania.
Alama za Azimio hilo la Abuja zimeshaanza kujitokeza kwa mbali katika nyanja mbalimbali nchini Tanzania na kwa hiyo, wale wanaoshabikia suala la Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC) kwanza wajue malengo yake ni yapi. Na ni vema kujiuliza je, Katiba ya nchi yetu, historia ya nchi yetu, utamaduni wa nchi utaweza kuukaribisha umoja kama huo?
Misingi iliyowekwa na muasisi na Baba wa Taifa Mtumishi wa Mungu, Mwalimu Julius K Nyerere ilikuwa ya busara, upendo, usawa, inayokuza haki na amani kwa watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote. Sasa fikiria kama ni kweli lengo kuu ndilo hilo je, Azimio la Abuja lina maslahi gani kwa Watanzania wa leo hii? Kama nilivyosema sifanyi propaganda bali ni kutaka kuelimisha umma wa Watanzania kama mwandishi hii ndiyo kazi yangu, kuwapa watu mwanga wajue wanakwenda wapi.
Pia kama padre ni nabii wa kutahadharisha waumini na wananchi kwa ujumla juu ya mambo mbalimbali na kinyume cha hapo, wito wangu hautakuwa na maana kabisa.
Yesu aliwaambia mitume wake; "Ninyi ni chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu" (Mathayo 5: 13-16). Nisipotimiza wajibu huu kutoka kwa Bwana basi mimi nitakuwa sijitendei haki mbele ya mwenyezi Mungu na mbele ya Watanzania wenzangu ambao wengi hawajui nini kinaendelea kuhusiana na masuala ya jamii na siasa.
Namaliza kwa kusema kwamba, sisi Watanzania na Tanzania yetu ni vema tukaendelea kushikilia misingi iliyojengwa na Baba wa Taifa kama tunataka kuendelea kuishi kwa umoja, upendo, haki na amani.
Nitaendelea kuwaletea habari zaidi kuhusiana na Azimio la Ubuja katika makala zijazo. Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki mawazo ya Mwalimu Nyerere, Mungu wabariki viongozi wa Tanzania. Nawatakieni uchaguzi Mwema huko Arumeru Mashariki, chagua kiongozi bora na siyo bora kiongozi.
Slaa: Bila utafiti ni uvivu wa kufikiri
Mimi ni msomaji wa Gazeti letu la Raia Mwema na magazeti na mitandao mbalimbali hivyo kufuatilia mijadala mbalimbali. Kila nilipoona dalili ya upotoshaji nimekuwa nikijaribu kuweka kumbukumbu sawa. Siku za karibuni nimekuwa nikifuatilia makala zilizokuwa zikitolewa na Mayage S. Mayage kwenye Raia Mwema.
Makala ya mwisho ilitoka katika Raia Mwema la Desemba 7 hadi 13, 2011, ukurasa wa 22. Baada ya kusoma makala yake ya kwanza nilimwandikia ujumbe mfupi wa sms. Kimsingi nikimshauri asipende kufanya mahitimisho kwenye mambo mazito na hasa yanayohusu jamii na taifa kwa ujumla bila kufanya utafiti.
Kabla hata toleo la gazeti lililofuata halijatoka nikaanza kupokea simu na sms kutoka kwa watu waliojiita wapenzi wa CHADEMA, wakilalamikia ujumbe wangu wa sms kwa Mayage.
Nilistuka sana na kujiuliza maswali yafuatayo; mosi, kama ni kweli waliokuwa wakiniandikia sms na kunipigia simu ni wapenzi wa CHADEMA walijuaje majibu yangu ya sms kwa Mayage, kabla gazeti linalofuata halijatoka? Je, walipewa na Mayage na kama ni hivyo, kwa lengo gani?
Pili, lugha iliyotumika kwa wote japo walijitambulisha kuwa sehemu mbalimbali za Tanzania ilifanana na hakuna hata mmoja aliyejielekeza kwenye hoja ya msingi kuwa, Mayage ametoa hitimisho bila kufanya utafiti.
Iweje wote wana lugha inayofanana walikaa wapi kujadiliana na kupanga ujumbe wa kunitumia? Iweje wote hakuna anayezungumzia hoja yangu ya msingi, bali msisitizo ni katika walichokiita “kumtukana Mayage? Hili nalo liliashiria upungufu mkubwa kwa kuwa hitimisho lisilotokana na utafiti wa kina daima lina upungufu mkubwa, hasa katika jambo zito kama mikakati ya chama.
Je, watu hao walitarajia mikakati ya chama ingeliwekwa hadharani? Ni jeshi la ajabu linaloweka mikakati yake hadharani? Ni kwa msingi huo, nilitarajia Mayage kama ni mtu makini na mwenye nia njema kama anavyoonekana kutaka kutushauri, angelifanya utafiti aghalab angegundua mikakati au hatua kadhaa zinazochukuliwa na CHADEMA kujiimarisha na kujikita katika ngazi mbalimbali kwa lengo la kuchukua dola 2015.
Je, Mayage anajua kuwa hakuna kanuni moja na inayofanana katika siasa kwa kuwa siasa “is a game of dynamics” yaani ni mchezo wa mbinu na mikakati.
Hata hivyo, hata hao waliosema kuwa nimemtukana au kumdhalilisha Mayage, hawakueleza ni tusi gani ametukanwa.
Kutokana na mazingira hayo, nimeona nitoe ufafanuzi ufuatao.
Si mara ya kwanza
Si mara ya kwanza tunajibishana na Mayage, baada ya makala au nyaraka zake. Kwa wale wanaokumbuka alikuwa akiandikia gazeti la Rai. Mayage aliwahi kuandika “Waraka wa wazi kwa Dakta Slaa” katika makala tatu mfululizo na zote zilikuwa za upotoshaji. Makala hizo zilikoma pale nilipomjibu kupitia gazeti hilo hilo.
Katika barua zake hizo niliamini tatizo lilikuwa kutokufanya utafiti, lakini baadaye niligundua kuwa licha ya kutofanya utafiti Mayage alikuwa “kuwadi” wa waliomtuma kwa malengo waliyokuwa wakijua wenyewe.
Jambo hilo alilikiri kwangu kwa sms Mayage mwenyewe, baada ya kuondoka Gazeti la Rai. Nami nikampongeza kwa unyofu na uwazi wake. Kama ni mkweli na mnyofu atatoka hadharani na kukiri mawasiliano kati yetu.
Kwa nini niliandika sms
Niliposoma makala ya Mayage katika Gazeti la Raia Mwema, kwa kutumia saikolojia tu ya kawaida nilijua alikokuwa akielekea ndiyo maana nikamtumia sms bila kutaka kumjibu kwenye gazeti ili ajirekebishe kabla hajafika mbali.
Kwa bahati mbaya, nia yangu njema kwa Mayage ikaanguka kwenye jiwe gumu, badala ya kuanguka kwenye udongo wenye rutuba. Hii haikuwa kwa bahati mbaya, kwani wakati anaanzisha safari ndefu ya makala zake alikuwa anajua alitaka kuhitimisha vipi.
Hii imeonekana dhahiri katika makala yake ya sasa “Ombwe….mbadala wa CCM ni chama kipya”. Mengine yote ni kisingizio tu.
Hoja anazotoa kwetu
Hoja zake ni kwanza, CHADEMA ijikite zaidi katika “kufanya siasa badala ya uanaharakati wa maandamano”. Pili, wabunge wa CHADEMA wanatakiwa kuja na programu za maendeleo kwa wananchi wa majimbo yao “ili yasije yakakikuta yaliyokikuta chama cha NCCR-Mageuzi..”
Tatu, katika makala yake ya wiki iliyopita yenye kichwa cha habari “Sababu tunayo, tuwang’oe 2015”, alitoa sababu mbalimbali na hatimaye alitoa “ushauri kwa wazalendo wenye uchungu wa kweli ….kuanzisha chama cha siasa makini sasa, si kusubiri kesho na Watanzania wakiunge mkono kwa nguvu zote…”
Majibu kwa hoja zake
Mimi sina tatizo na ushauri wa kuanzishwa kwa chama kipya kwa kuwa ni haki ya kikatiba ya Watanzania. Msingi wa kumtaka Mayage kufanya utafiti ni katika upotoshwaji dhahiri wa Mayage, ambaye kwa ufundi mkubwa amejenga hoja kinzani (fallacy) inayoonyesha kuwa CHADEMA si chama makini, hakifanyi siasa makini bali kinafanya tu uanaharakati. Huu ndio msingi na kiini cha kumtaka bwana Mayage afanye utafiti kuhusiana na hoja zake.
Kama hoja za Mayage kutaka kianzishwe chama kipya inatokana na hoja za Richmond, ufisadi na sasa Jairo, na kama angelikuwa makini kidogo na kufanya utafiti kidogo tu angeligundua ni kiasi gani CHADEMA ni ‘chama makini’ hadi kujitosa MwembeYanga, Septemba 15, mwaka 2007 na kuibua hadharani (baada ya jitihada za kutumia Bunge kushindikana), hoja za ufisadi wa Benki Kuu, EPA kwa ujumla wake, Twin Tower ya Benki Kuu, Kagoda, Ufisadi kupitia Commodity Import Support (CIS) na nyingine nyingi.
Inatosha kufungua kumbukumbu rasmi za Bunge (hansard) za mwaka 2007/2008/2009/2010. Msomaji na mfuatiliaji makini anaona wazi kupitia hansard jinsi Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, alivyokuwa akipigwa “point of order” kutakiwa kufuta sehemu ya hotuba yake na Spika, bila shaka kwa lengo la kuuficha ukweli usijadiliwe bungeni.
Mayage atakumbuka jinsi Spika wa Bunge, Samuel Sitta alivyokimbilia TBC1 na kutangaza kuwa “Nyaraka alizokuwa nazo Dokta Slaa (kuhusu ufisadi) ni feki na kuwa anaziwakilisha polisi ashitakiwe”.
CHADEMA hatukutetereka
CHADEMA ilishikia bango bila kutetereka, pamoja na vitisho na matusi yote hoja hizi sasa zinajulikana, taifa zima leo linajua ufisadi mkubwa unaokumba nchi yetu katika nyanja mbalimbali.
Leo taifa nzima linaimba na kupinga ufisadi. Hii iliwezekana tu, kwa kuwa baada ya jitihada za bungeni kushindikana CHADEMA, kwa kukodi helkopta ilipita kwenye makao ya mikoa 12 ya Tanzania Bara na kupeleka hoja hizo kwa wananchi, kama Mahakama Kuu kuliko zote kwa wanasiasa. Mzunguko huo ulihitimishwa MwembeYanga kwa kutaja hadharani majina ya mafisadi 11.
Mafisadi wengine wako kortini
Hakuna anayebisha, na hata Mayage atakubali kuwa wengine kati ya watuhumiwa hao wa ufisadi leo wako mahakamani kwa kesi zinazohusiana na ufisadi huo.
Mayage anasema CHADEMA kinafanya kazi “ki uanaharakati” angelifanya utafiti kidogo tu angelijua matokeo ya uanaharakati huo kwa siasa za CHADEMA na kwa siasa za Tanzania baada ya MwembeYanga.
Kwenye sms niliyomtumia nilitumia neno kwa mtu yeyote anayefikia hitimisho (conclusion) bila utafiti ni ‘uvivu wa kufikiri’ na bado nitasimamia hapo kwa kuwa kuacha hoja ya Mayage bila kupata majibu ya kina tutaruhusu upotoshaji unaozidi viwango vyote.
Aidha, Mayage ameshindwa kutoa tafsiri ya neno ‘siasa’ badala yake anaona kinachofanywa na CHADEMA ni ‘uanaharakati’ tu, na hivyo anawashawishi “Watanzania kuanzisha chama cha siasa makini”.
Waanzishe chama makini siyo kwa kuwa chama hicho kipya kina ajenda mpya bali kwa vile tu CHADEMA si makini na kinafanya kazi “ki-uanaharakati”.
Mayage anashindwa kuchambua kwa kina uhusiano wa karibu sana kati ya uanaharakati na siasa. Anashindwa kuona kuwa uanaharakati inaweza kuwa mbinu mojawapo (wakati mwingine ya lazima) ya kufikia malengo ya kisiasa.
Hoja ya Mayage ingekuwa na mashiko angelikuwa amepitia mikoa yote 12 ambako CHADEMA ilifanya mikutano ya hadhara (uanaharakati) na kulishitaki Bunge kuhusiana na ufisadi wa Buzwagi, hoja ya Kabwe Zitto iliyolifanya Bunge kumfukuza Zitto, bungeni kwa miezi takriban mine, na kuwaeleza kinagaubaga Watanzania ni nini matokeo ya mikutano hiyo kwa Watanzania na matokeo yake (impact) kwa siasa za Tanzania leo. Bwana Mayage alipaswa kukumbuka msemo kuwa bila “utafiti hakuna haki ya kuzungumza”(No Research no right to speak).
KUTOKANA na kutokufanya utafiti, Mayage ameshindwa kutambua ni Watanzania wangapi wamejiunga kutokana na hicho anachokiita ‘uanaharakati’ wa CHADEMA, na au ni matawi mangapi yamefunguliwa kutokana na uanaharakati huo.
Ameshindwa kuona ni maeneo mangapi ambayo kabla ya mikutano au maandamano ya CHADEMA hayakuwa na matawi ya CHADEMA na leo si tu kuna wanachama, bali pia matawi yenye uongozi kamili.
Ni kweli CHADEMA imekuwa ikiongoza ‘maandamano’ nchi nzima kupinga ufisadi na aina mbalimbali za matumizi mabaya ya rasilimali za umma. Mayage angelifanya utafiti kidogo tu angeligundua kuwa CHADEMA imefanya kuanzia Januari, 2011 (bila kutaja ya nyuma) maandamano kwenye wilaya za makao makuu ya mikoa 16 ya Tanzania Bara (kupitia Operation Sangara na ziara za Katibu Mkuu) na kwenye makao makuu ya wilaya zote katika mikoa hiyo na takriban kata zote za majimbo yote katika mikoa hiyo ( isipokuwa michache ambayo hatukufika kutokana na sababu mbalimbali kama kuzuiwa na mvua).
Mayage angelifuata ushauri wangu wa kufanya utafiti kidogo katika mikoa hiyo na wilaya, majimbo na kata) angeliweza kugundua ni kwa kiasi gani CHADEMA ni makini katika mipango yake na kujikita vijijini kuliko anavyodhani kwa kutumia “nadharia ya kuandika makala mezani”. Wakati wa kuandika nyaraka mezani umepitwa na wakati wenzako tuko mbali zaidi japo hatuvumi.
Ushauri wa hisia ni kama kelele za debe tupu
Mayage angelifanya utafiti mdogo tu hata ‘sample’ yaani maeneo machache tu yaliyochaguliwa kwa umakini, ambayo inakubalika kisayansi makala yake na ushauri wake ungelikuwa na umuhimu mkubwa na CHADEMA tusingesita kuuzingatia.
Ushauri usio na takwimu zozote, unaotokana na hisia binafsi, utaalamu wa mtu kukaa tu mezani na kutoa hukumu bila kusikiliza kesi ni sawa na debe tu linalolia kwa sauti kubwa lakini “halina kitu ndani”.
Hivyo kwa wale waliodhani nimekataa ushauri wa Mayage, naomba wawe na utulivu niliukataa kwa kufahamu malengo yake binafsi, malengo ya makala yake. Kabila letu la Wairaqw tuna msemo “kuro tsihay a gawti stahha” (tafsiri ambayo kwa Kiswahili “Mwewe mwenye mimba humtambua angali angani)”.
Mimi ni Katibu Mkuu makini
Nilijua mapema Mayage angelihitimisha kama ambavyo anahitimisha katika Raia Mwema la Desemba 7 hadi 13, 2011; yaani “Watanzania waanzishe chama kingine makini” (tafsiri ya anachomaanisha Mayage ni kuwa CHADEMA si makini na ni cha ki-uanaharakati tu).
Ningeacha kuonya katika hatua hiyo nisingelikuwa Katibu Mkuu makini, ambaye wajibu wake daima ni kulinda maslahi ya chama chake, wanachama, wapenzi wa chama na wananchi kwa ujumla.
Nilitimiza tu wajibu wangu kwa kumtaka afanye utafiti kabla hajazungumzia mambo yanayohusu maslahi ya wengi. Wako wenye uwezo wa kuchambua kwa kina na wako wanaochukua mambo yalivyoandikwa. Tuepuke kuwapotosha angalau wale wasiofanya uchambuzi wa mambo.
Sitaki kuzungumzia madhara ya makala hizi kwa kuwa sijafanya utafiti, lakini ni dhahiri kati ya hao anaosema Mayage wamempelekea sms, kama hawakuwa na malengo mengine kama nilivyoonyesha awali, basi hawakufanya uchambuzi wa kina, hawakujua pa kupata taarifa sahihi za chama.
Bila shaka wameamini hakuna mipango wala mikakati yoyote ya kujenga chama katika ngazi zote isipokuwa ni maandamano tu. Mayage angelifanya utafiti angeliwaelimisha angalau kuhusu waraka wa Katibu Mkuu na moja wa mwaka 2011, waraka na mbili wa mwaka 2011.
Waraka namba moja ambao uko katika hatua mbalimbali za utekelezaji kuanzia wilaya, majimbo, kata na matawi. Waraka huu ulitolewa takriban miezi mitano iliyopita kabla Mayage hajafikiria kuandika makala zake katika Raia Mwema kuhusu mada hii.
Angelifanya utafiti angeligundua kuwa Oparesheni Sangara zote huishia kwa kuzindua matawi na kusimika uongozi.
Utafiti ungelimwezesha Mayage kuwa na uwezo, uhalali na haki ya kushauri Watanzania wanaopenda kuanzisha chama kingine ambacho wao wanadhani kwa mtazamo wao ni makini.
Madhara ya kutofanya utafiti
Kukosekana kwa utafiti kunamnyima uwezo, uhalali na haki hiyo, kwa kuwa ni hatari sana kufanyia uamuzi wa kitaifa kwa misingi ya hisia tu ya mtu fulani bila kujali nafasi yake. Kuanzisha chama kipya ni haki yao.
Lakini haki hiyo isitumike kumdhalilisha mwingine kwa misingi isiyo sahihi. Dhamira hiyo ni tofauti kabisa na kutaka kianzishwe chama kingine makini kwa kuwa CHADEMA ni cha ki-uanaharakati na kwa tafsiri yake, si makini.
Chama hakiwi makini kwa kuwa tu mtu mmoja au kundi fulani wanadhani hivyo na au hawafahamu mipango na mikakati ya chama hicho. Fikra hizi ndizo zinazoitwa “fallacious” katika falsafa.
CHADEMA hatukatai ushauri
CHADEMA hatujakataa hata siku moja ushauri wa mtu yeyote. Tumekuwa na tutaendelea kupokea ushauri wa Watanzania wote bila kujali itikadi zao, dini zao, wanakotoka, umri wao, jinsia zao.
Tumekuwa tukipokea ushauri kutoka kwa mtu mmoja mmoja kwenye matawi na kwa viongozi ngazi zote. Huu ni utamaduni wa CHADEMA na Watanzania wengi wanajua hivyo. Ushauri ukitolewa utafanyiwa kazi kama inavyotakiwa.
Lakini upotoshwaji wa dhahiri pia unafanyiwa kazi, tena bila unafiki kwa kuwa ndani ya CHADEMA hatujazoea unafiki wala kudanganyana; “We shall call a spade a spade”, ndiyo maana Mayage alishauriwa afanye utafiti ili ushauri wake uwe na tija na maana kwetu na kwa Watanzania.
Tungeliweza kunyamaza bila kumjulisha, lakini angeendelea kupotosha bila kufahamu madhara ya upotoshwaji wake. Aidha hatua niliyochukua ya kumjulisha imeanzisha mjadala mpana zaidi na sasa nina fursa ya kutoa ufafanuzi wa kina jambo ambalo lisingelitokea ningelimnyamazia.
Ni kweli kila mtu ana uhuru wa kufikiri na kuandika anavyotaka ndani ya misingi ya sheria za nchi. Lakini kwa mwandishi kusema “….nawaomba Watanzania tutoke nje ya ofisi au nyumba zetu kwenda kwa wananchi wenzetu tuwaulize vyama hivyo vinasimamia itikadi au sera gani…” hiki ndicho nilichomtaka Mayage atoke ofisini kwake kwanza aende kwa wananchi kabla yeye mwenyewe hajawaambia Watanzania wengine.
Yeye anawaandikia Watanzania ambao miezi takriban 11 tu iliyopita walionyesha mwelekeo wao kupitia kura (pamoja na hujuma zote zilizofanyika). Sasa nani atoke kwa wananchi, Mayage au wananchi ambao kimsingi siyo tu wanajua wanachotaka, bali wamekwisha kuonyesha kwa matendo.
Nina hakika Mayage angeenda na swali lake; “ni chama gani kimesimamia kwa ustadi hoja yake ya kuwakomboa Watanzania kutoka mikononi mwa madhila ya CCM..” angepata jibu la Watanzania na si kupotosha kama anavyoelekea kuwashawishi kuanzisha chama ambacho hawajakiona, hawajafanya kazi nacho na hawakijui.
Ni kwa nini Mayage atake Watanzania wawe watu wa kufanya majaribio kila wakati? Ni kwa sababu tu yeye kajibiwa vibaya kama anavyosema na Dk. Slaa au kuna sababu nyingine?
Kama ni kweli katukanwa na Dk. Slaa ni kwa vipi anaihusisha CHADEMA yote, kwani hafahamu kuwa leo CHADEMA si Mbowe, si Slaa wala viongozi bali ni taasisi ya Watanzania wenyewe.
Msingi wa mvutano umeya Arusha
Mayage anasema CHADEMA wanalumbana kuhusu umeya wa Arusha! Angekuwa makini angelitafuta misingi ya mgogoro. Amewauliza watu wa Arusha?
Kama hajafanya utafiti ana uhalali gani kuwasemea watu wa Arusha ambao wanajua wanalofanya kwa kuambatana na mbunge wao ambaye alidhalilishwa ubinadamu wake na ubunge wake katika uchaguzi wa meya Arusha.
Ni ulimbukeni kufikiri mtu anajua kwa kuandika tu kutoka mezani. Hiki ndicho walichofikiri madiwani watano wa CHADEMA waliotaka kutikisa kiberiti. Walishindwa kusoma alama za nyakati kama alivyo Mayage.
Mayage anaamini na ‘kusingizia’ CHADEMA inapigania kupata umeya, hajui kuwa CHADEMA inapigania misingi “principle” na si vinginevyo.
Tofauti ni kubwa sana baina ya mawili hayo. CHADEMA imesimamia hoja yake yaani “taratibu za uchaguzi wa meya zimekiukwa.”
Uongozi wa CHADEMA haukuwa tayari kuona taratibu na sheria zinavunjwa na wanaotarajiwa kuzilinda, yaani Serikali. Hii haina maana ya kuwa CHADEMA inataka meya atoke CHADEMA kama anavyotaka ieleweke Mayage. La hasha.
Hili nalo ni tunda la kutojua misingi ya jambo na kudandia hoja kwa kuwa tu ana fursa ya kuandika makala mezani.
Mayage angelifanya utafiti angeligundua hoja ya Katiba mpya ilikuwa ndani ya Ilani ya CHADEMA. CCM imeibeba baada ya kushinda uchaguzi kama walishinda na siyo ‘kuiba kura’ (Katiba hairuhusu kuhoji matokeo hivyo hatuna pa kutolea ushahidi wetu). Sisi hatuna shida na hilo.
Tunasisitiza kama wamechukua hoja ambayo hawakuwa nayo waitekeleze vizuri kama ilivyobuniwa na walioibuni. CHADEMA ndiyo iliyoibuni, na kusema...“ndani ya siku 100 mchakato wa Katiba mpya utaanza” Hakuna chama kingine chochote kilichosema hivyo kwenye ilani yake.
Ni dhahiri Mayage haelewi, kuwa ‘Mchakato ukiwa mbovu, tunda lake yaani Katiba itakayopatikana itakuwa mbovu’. Wengine tuna uzoefu si wa kusoma tu magazetini bali kushiriki mchakato wa Tume ya Rais ya Jaji Kisanga. Ni hovyo. Ndiyo maana tangu siku ya kwanza nimepinga Tume ya Rais badala ya Tume ya Wananchi itakayoundwa na mkutano wa Katiba.
Mayage haelewi kuwa uchaguzi unaendeshwa kwa Katiba na kuwa haki haitapatikana kama Katiba itaendelea kubeba Chama cha Mapinduzi (CCM).
Ni ndoto kufikiria uchaguzi huru na haki 2015 kama Katiba Mpya haitapatikana. Matukio yote ya wananchi kupigwa mabomu, kuzuiliwa mikutano ya upinzani mara kwa mara, kubadilishwa kwa matokeo ya uchaguzi yote haya ni matokeo ya Katiba mbovu.
Mayage hajui kuwa migogoro mingi kwenye ardhi ni matokeo ya Katiba mbovu! Hajui kuwa robo tatu ya bajeti ya taifa leo inatumika kwenye uendeshaji wa Serikali badala ya mipango ya maendeleo kutokana na Katiba mbovu? Mayage siyo tu hajafanya utafiti, lakini pia si makini katika kujenga hoja zake. Anajipinga mwenyewe mara aseme chama gani kimesimamia hoja zake, mara aseme CHADEMA kinapoteza muda kujadili hoja zenye manufaa kwa Watanzania. Tumuamini kwa lipi katika hali hii?
Mayage sisi tuliisha kumaliza utafiti na udadisi kuhusu Katiba. Huhitaji kwenda mbali, nenda Ghana na Kenya. Tunayo michakato iliyotumika kupata Katiba na tunazo pia nakala za Katiba zao.
Nani kapotea kati yako wewe ambaye huna hata mfano mmoja na CHADEMA inayofahamu tangu awali nini kinahitajika kupata Katiba mpya!
Tuache ulimbukeni tunapozungumzia maslahi ya taifa. Mayage anaenda mbali kiasi cha kufananisha CHADEMA na “bundi katika msafara wa ndege dhaifu”! Kama yeye alijisikia kutukanwa je, na CHADEMA ambaye si mtu mmoja inajisikiaje na upotoshwaji na matusi ya kiasi hiki?
Ukisoma kwa umakini, kwake Mayage CHADEMA ni “chama cha ovyo” ndiyo maana anawashawishi Watanzania kuanzisha chama mbadala wa CCM.
Mayage amelundika vyama vyote 17 vya upinzani katika kapu moja. Ni kweli kuwa hafahamu CHADEMA ni chama pekee cha upinzani kinachoongoza halmashauri zaidi ya saba? Hajui kuwa CHADEMA imeshindwa kwa idadi ndogo sana katika halmashauri nyingine nane?
Mayage ameshindwa kutambua kuwa CHADEMA ni chama kinachokua kimkakati na vigezo ni vingi chukua idadi ya madiwani ambayo katika uchaguzi wa 2010 imeongeza kwa asilimia zaidi ya 400, mafanikio ambayo hakuna hata chama chochote cha upinzani kimefikia?
Mayage hajui kuwa katika vyama 17 viko ambavyo tangu vianzishwe havijawahi kupata kiongozi hata serikali moja ya mitaa angalau mwenyekiti wa kitongoji, wakati CHADEMA ina maelfu ya viongozi hao?, Mayage ameamua kuzipuuza makusudi kwa malengo anayojua na pia kwa ‘uvivu wa kutokufanya utafiti’ angalau kupiga simu tu kwa wahusika. Madhara yake ni kuwaambia watanzania “..tulivyonavyo sasa (vyama vya siasa/NGO’s). Hivi haoni hata aibu kulinganisha chama kinachoongoza halmashauri zikiwemo Jiji la Mwanza na NGO ambayo malengo yao si kuchukua dola?
Haya siyo matusi tu kwa Watanzania bali kwake mwenyewe aliyejifanya mtaalamu akashindwa kufikisha ujumbe ambao pengine hata mtoto wa shule ya msingi angeliweza kuufikisha vizuri zaidi.
Wanachama,wapenzi na Watanzania wapenda mabadiliko ambao walikuwa hawajagundua dhamira ya Mayage kuanzia makala ya kwanza ni vema wakarudi kusoma makala zake za mwanzo na kuzichambua kwa kina ili kuepuka upotosha uliojificha kwa hoja za kuuma na kupuliza.
Dk. Slaa nisingeliweza kwa namna yoyote kufumbia macho upotoshwaji huu ambao nia na lengo lake ni dhahiri.
Mayage anaonyesha udhaifu mkubwa pale anaposema hajaridhishwa na CHADEMA kwa kushindwa kusimamia hoja moja tu “…ya posho ya vikao kwa wabunge”. Kwani CHADEMA ndiyo inayolipa posho hiyo?
Hajui mgogoro wa sasa wa posho kulipwa kinyemela na jinsi CHADEMA kama chama inavyopiga kelele, hajui jinsi CHADEMA ilivyodai fomu ya mahudhurio ukumbini bungeni itenganishwe na fomu ya posho, na uongozi wa Bunge umekataa kufanya hivyo?
Labda hajui msimamo wa CHADEMA kwa kuwa si mpenda kusoma wala hajui ilani ya CHADEMA kifungu cha 5.5.1 (2 na 6) ya Agosti 2010, kinasema nini.
Lakini sishangai kwa vile anaandika kwa hisia badala ya utafiti. Kama ambavyo hajui pia kuwa kamati kuu ya CHADEMA kila kikao kwa mujibu wa kanuni, inatakiwa kupokea utekelezaji wa programu ya kazi kutoka kwa wabunge na halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA na kila kamati tendaji ya kata inapokea taarifa ya utekelezaji kutoka kwa madiwani wake.
Inawezekana utekelezaji wa mipango katika maeneo yanayoongozwa na CHADEMA unasua sua na kwa maeneo mengine hauridhishi.
Lakini pia angetafiti kidogo angegundua halmashauri zenye uzoefu za CHADEMA zimepiga hatua kiasi cha kuanzisha chuo chake cha waalimu kupunguza kero ya upungufu wa waalimu, kuanzisha chuo cha madaktari (clinical officers) na manesi kupunguza kero ya upungufu wa wataalamu hao na sasa wako mbioni kuanzisha chuo cha kilimo.
Haya yanapatikana tu kwa wenye nia na dhamira ya dhati ya kutaka kujua bila kutoa hukumu mezani.
RC Mwanza, ma-DC wametuhujumu
Angelifanya utafiti angeligundua jinsi mkuu wa mkoa wa Mwanza alivyoingilia na kuvuruga utekelezaji wa mipango ya Jiji la Mwanza iliyoko chini ya CHADEMA, na vivyo hivyo kwa wakuu wilaya katika halmashauri zingine.
Utafiti ungelimwonyesha kuwa demokrasia kwa wengi wa viongozi wa Serikali iko kwenye midomo zaidi (lip service) lakini yanayoendelea maeneo mengi nchini ni kinyume cha demokrasia. Haya hutayajua kama huna dhamira ya kutaka kuyajua na wala hufanyi utafiti. Ndiyo msingi mkubwa wa ushauri wangu kwa Mayage.
Ni dhahiri Mayage angelifanya utafiti angeligundua maandamano yalivyowaunganisha Watanzania kudai siyo tu haki zao mbalimbali, bali kupaza sauti yao dhidi ya makali ya maisha kama vile sukari, bei ya sembe, mafuta ya kupikia, mafuta ya taa pamoja na kuwakatalia watawala kodi yao isitumike kulipa madeni ya Dowans..
CCM wameiga hawakufanikiwa
Anachokiita Mayage uanaharakati, angelijikita kwenye utafiti angeligundua matokeo yake ni nini hadi CCM wenyewe waliokuwa wakikandia maandamano wakaamua kuyaiga walipojaribu kuandamana Mbeya japo hayakufanikiwa.
Ni dhahiri Mayage amejikita kwenye mbinu mgando akidhani namna pekee ya kufanya siasa ni kufungua matawi kwa mtindo wa CCM.
Kwa kuwa hajafanya utafiti anashindwa kugundua kuwa mbinu za CCM za kufungua matawi haziwezi kufuatwa na chama kingine chochote makini kwa kuwa CCM inatumia mfumo wa dola kufanya kazi zake-watendaji wa vijiji, kata, makatibu tarafa, wakuu wa mikoa, wilaya, kwa ujumla mfumo mzima wa Serikali.
Polisi wanaingilia mipango yetu
Angetafiti angeligundua hata matawi niliyofungua au kufanya yafunguliwe kutokana na ziara ya Katibu Mkuu Jimbo la Mbinga Magharibi (Mbamba Bay), bendera zote zimeshushwa kwa amri ya OCD.
Angelikuwa mtafiti angeligundua chama makini kama CHADEMA kinakumbana na matatizo na vikwazo gani. Angelitoa ushauri jinsi ya kupambana na changamoto hizo nisingelikuwa na sababu ya kumjibu Mayage na au ningemjibu kwa kumpongeza.
Ushauri wake ungetokana na utafiti nina hakika ungewasaidia sana kuwafungua macho Watanzania badala ya kuwapotosha.
Kauli ya Mayage kuwa ‘..Ndani ya siasa wako wanasiasa wazuri tu, lakini hao hawana sauti wala nafasi ya kukielekeza chama hicho…wenye sauti na ushawishi ndani ya chama ni wanaharakati hali inayokifanya chama kiendeshwe kiharakati kwa asilimia 80..” inathibitisha siyo tu Mayage hajafanya utafiti, lakini pia hajui ‘ABC’ ya siasa na hivyo hastahili kuandikia hata mada za kisiasa.
Chama cha siasa hakiendeshwi kwa ‘influence’, au uanaharakati kama anavyodai Mayage bali na Katiba, kanuni na taratibu za ndani ya chama husika kama zipo.
Kwa faida ya wapenzi wa CHADEMA na Watanzania kwa ujumla CHADEMA inaendeshwa misingi ya Katiba yake, na toleo la mwisho ni la mwaka 2006. CHADEMA ni kati ya vyama vichache vyenye kanuni za uendeshaji, maadili ya viongozi na wanachama, kanuni za uendeshaji wa halmashauri zinazoongozwa na na CHADEMA ikiwa ni pamoja na serikali za mitaa zilizoko chini ya CHADEMA na hatimaye kanuni za nidhamu ikiwa ni pamoja na kanuni za nidhamu za wabunge, madiwani, na wenyeviti wa serikali za mitaa (na wajumbe wao).
Uamuzi wa CHADEMA hufanywa kupitia Sekretariati ya Kamati Kuu ya chama, Kamati Kuu, Baraza Kuu na mkutano mkuu ambacho ndicho chombo kikuu na cha mwisho cha uamuzi.
Je, ni kuwadi wa maadui zetu?
Kwamba CHADEMA inaendeshwa na wenye ‘influence’ ni kielelezo cha kile nilichokisema kuwa kauli kama hizo zinatoka tu kwa watu wenye uvivu wa kufikiri na kufanya utafiti.
Vinginevyo Mayage ana ajenda yake ambayo hajaiweka hadharani na au ni kuwadi tu wa maadui wengi wa CHADEMA.
Kama nia yake ni njema kama anavyotaka kuonyesha na kuwa anatoa ushauri kwa nia njema, huwezi kumshauri mtu usiyemfahamu, na huwezi kumfahamu mtu kama angalau humtembelei, kumjulia hali, kuomba nyaraka zake na kadhalika.
Wakati ninawapokea waandishi wengi na wa vyombo takriban vyote ofisini kwangu Mayage hajakanyaga wala hajaomba taarifa yoyote iwe kwa simu iwe kwa mahojiano. Huu ni uthibitisho kuwa Mayage ana ajenda zake anazozijua.
Kwa taratibu hizi uanaharakati na “influence” inapata wapi nafasi? Au Mayage anataka kufanya kazi kwa mapenzi ya mtu mmoja mmoja mathalan hiyo asilimia 20 anayoisema?
Je, ni kweli kuwa hiyo influence imepenya kwenye ngazi zote kuanzia sekretariati, kamati kuu, baraza kuu hadi mkutano mkuu. Kama hivyo ndivyo si ndivyo pia jina letu linavyodhihirisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo?
Au Mayage anataka tukiuke misingi ya demokrasia na asilimia 80 ya viongozi waongozwe na asilimia 20? Huo ni ulimbukeni katika siasa na itakuwa ni mfumo mpya unaobuniwa na Mayage katika chama chake kipya anachosema kitakuwa makini”.
Wapenzi na Watanzania kwa ujumla hakuna sababu ya kuwa na hofu na watu wa aina hii, na kwa taarifa yenu wako wengi wasiotutakia mema.
Naamini ufafanuzi huu wa kina utakuwa umewatoa wote hofu wale waliokuwa na shaka baada ya kusoma makala za Mayage.
Naomba nirudie tena katika hitimisho, sina tatizo na wale wote wenye nia ya kuanzisha chama kingine kipya akiwemo Mayage kama nilivyosema ni haki yao ya kikatiba.
Kwa wale ambao tumekwisha kuanza safari ya kuing’oa CCM kupitia ‘meli yetu’ ya CHADEMA, tuendelee na mikakati yetu na kila mmoja akitimiza wajibu wake, Novemba 2015 CCM itaingia kwenye kumbukumbu ya historia kama ilivyo UNIP (Zambia) na KANU (Kenya), tena vyote ni vyama vinavyojulikana kama vyama vya ukombozi.
Mwalimu aliwahi kusema “play your part, it can be done” kila kiongozi wa CHADEMA kwenye ngazi na nafasi yake atimize wajibu wake na apuuze propaganda za maadui zetu zikiwemo hizi za Mayage.
Tukatae ‘bantu education’
Rai ya Jenerali
NAAMINI
kwamba nimetumia muda wa kuridhisha na nafasi ya kutosha kujadili
umuhimu wa kuwekeza katika kuwajenga wananchi kiakili na kimwili, mkazo
ukiwa katika uwekezaji unaowalenga watoto wa Taifa hili.
Bila shaka hivi ni vipengele vya mjadala vitakavyorejewa kila mara, washiriki tukiwa ni sote tunaoona haja ya kukusanya mawazo yetu na kuyachakata kwa pamoja ili tujenge mwafaka kuhusu mambo muhimu yanayotuhusu.
Tusipofanya mjadala wa dhati tutaendelea kulalamika bila ye yote kutoa maoni juu ya namna ambavyo tunaweza kujikomboa kutoka katika umasikini unaozidi kuwakandamiza watu wetu ambao wamerithishwa nchi tajiri lakini hali zao hazifanani kabisa na utajiri huo.
Tusipoingia katika mchakato wa kweli juu ya masuala yanayohusu kuondoa umasikini na tukajifunza kwamba haya mambo si ya kupapukia bali hupangwa, tutaendelea kufukuzana na wananchi tukiwadai michango ya shule ya kujenga shule zisizo na waalimu wala vitabu; watatuona kama maadui zao wakati sisi tukijidanganya kwamba tunawapelekea ‘maendeleo’.
Bado zinatufikia taarifa za watu wanaokimbia kaya zao ili wasikamatwe kwa kushindwa (au kutokutaka) kulipa michango ya kujenga ‘madarasa.’ Baadhi yao wanaweza wakawa ni watu ambao kwa kweli kabisa hawana uwezo wa kulipa ‘michango’ hiyo, lakini baadhi yao wanaweza kuwa wale ambao, hata kama wanao uwezo wa kutoa fedha, hawaoni faida yo yote inayopatikana na ‘elimu’ inayotolewa ndani ya majumba yasiyo na walimu wala vitabu.
Kinachowafanya watendaji wa maeneo ya vijijini wawasake wananchi kama wahalifu ni maelekezo wanayopewa kutoka kwa waajiri wao wa Dar es Salaam, ambao katika mantiki ambayo inazidi kupinda kila uchao, bado wanaamini kwamba elimu ni sawa na idadi ya vyumba vya tofali na bati.
Maelezo yote yaliyotolewa na wataalamu kuhusu maana halisi ya elimu yamepuuzwa, na shughuli ya kuwahangaisha wananchi inaendelea mtindo mmoja.
Nimemuuliza rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa kijijini katika kipindi cha Noeli na Mwaka Mpya ni kwa nini basi msisitizo huu wa ujenzi wa majengo yasiyokuwa na maana haujajulikana kwa wakuu wa nchi; jibu lake ni kwamba wanajua lakini hawajui wafanye nini kwa sababu walikwisha kuagiza ujenzi ufanyike, na kwa hiyo ujenzi ni lazima ufanyike, na wazee wa kijijini wanaziona hizo ‘shule’ kama vituo vya kuwachunga watoto wa kike wasipate mimba!
Ipo mizaha inayovumilika, lakini huu si aina mojawapo ya mizaha hiyo. Huku ni kucheza na maisha ya watu na ni hatari kwa mustakabali wa Taifa. Siamini kwamba watu wetu wataendelea kuwa wa kusema “E walla” siku zote wakati wanaona mambo yanayofanyika yanawaumiza na kuwafanya watoto wao wasiwe na tumaini angalau la kuweza kuyafanya maisha yao yawe bora kuliko ya wazazi wao.
Hebu tukumbushane tena ( na kwa wale wasio na hadhi ya kukumbuka, kwa sababu hawajawahi kulisikia hili, tuelimishane) katika mambo yote unayoweza kuyafanya kwa ajili ya watoto wako hakuna hata moja linaloweza kulinganishwa na elimu bora na afya njema. Mengine yote yanakuja baadaye.
Kilicho dhahiri ni kwamba watawala wetu ni wazazi pia, na tunaona jinsi wanavyohangaikia elimu na afya za watoto wao. Kwamba hawahangaikii elimu na afya za watoto wa jamii za kimasikini si kwa sababu hawajui umuhimu wake; ni ubinafsi. Nafasi walizo nazo zingeweza kuwapa fursa ya kutumikia wananchi wa matabaka yote, na kwa kufanya hivyo tukapunguza ukali wa mapambano ya kitabaka katika siku zijazo.
Haitusaidii kupoza ghadhabu za wanyonge wanaoona watoto wao wanapewa ‘elimu’ inayofanana na ile iliyoitwa ‘bantu education’ wakati wa utawala wa Makaburu Afrika Kusini, huku watoto wa wakubwa wanapewa kila aina ya fursa, nchini na ughaibuni. Siku moja watalikataa hili… mwenye masikio na asikie.
Aidha, haiwezekani kwamba katika mazingira ya mijadala inayoendelea nchini kuhusu ‘ufisadi’ kwamba wananchi hawatajaribu kuuunganisha huo ‘ufisadi’ na hali zao mbaya za maisha na mifumo inayoonekana kutaka kumlaani mtoto wa mtu wa chini ili asiweze hata siku moja kusimama kwa miguu yake mwenyewe.
Mzee mmoja kutoka Kanda ya Ziwa ameniambia jambo ambalo siwezi kulisahau: Mtoto anapelekwa shule akiwa na miaka saba; anakaa huko kwa kipindi cha miaka 7; ‘anamaliza shule akiwa na miaka 14; shule hakuweza kujifunza hata huo ujuzi wa kusoma na kuandika, na nyumbani hakuwapo kujifunza namna ya kutunza ng’ombe na kulima pamba; kwa hiyo huku hayuko na kule hayuko.
Sasa mzee kama huyu unampa jibu gani anapokuambia kwamba yeye anatoa ‘kitu kidogo’ ili afisa elimu na wale watendaji wanaokuja kuswaga watoto kuwapeleka ‘shule’ wairuke kaya yake kama isiyokuwa na mtoto wa umri wa kwenda shule. Kwa kufanya hivyo angalau mtoto atabaki nyumbani ajifunze kuchunga ng’ombe!
Yote haya yana maana kwamba hatuna budi kujiwekea utaratibu wa kujadiliana kwa pamoja kuhusu hatua zote za maendeleo tunazokusudia kuzichukua. Tabia ya watawala wa nchi hii, na wa Afrika kwa ujumla, ya kufanya mambo wanavyotaka wenyewe imekuwa ni kikwazo kikubwa mno katika maendeleo ya nchi hii na bara hili kwa ujumla.
Maendeleo huletwa na watu wenyewe; hayawezi kuletwa kutoka juu, hata kama watawala wangekuwa na nia njema na dhamira yao ni kuwatumikia watu wao kwa dhati. Wananchi ndio wanaoumizwa na umasikini uliokithiri, na ye yote anayetaka kuwatumikia hana budi kuwasikiliza na kuyatia matakwa yao maanani.
Aidha, wananchi si vipofu; wana macho na wanaona kwamba hao hao watawala wao wanaowajengea ‘shule’ zisizokuwa na walimu na zahanati zisizokuwa na wauguzi wanao utaratibu mbadala wa kuwasomesha watoto wao na kuwapatia matibabu wanapougua.
Si muda mrefu uliopita mtawala mmoja katika mojawapo ya mikoa alikuwa kitetea ujenzi wa ‘shule’ hizo na kuwahimiza wananchi wapeleke watoto wao. Wananchi walikuwa wanamjua mkubwa huyo na walijua watoto wake wanasoma shule ya kweli, yenye walimu na vitabu na kila aina ya vifaa vya kufundishia, ikiwa ni pamoja na kompyuta.
Walipomuuliza ni kwa nini yeye hakupeleka watoto wake katika shule hizo, akawa mkali kweli kweli na mjadala ukaishia hapo.
Napenda kufunga sehemu hii ya makala hizi kwa kusisitiza kwamba iwapo tunataka kujenga mustakabali unaoeleweka kwa ajili ya Taifa letu hatuna budi kujenga utaratibu unaoeleweka wa kutoa huduma muhimu za msingi kwa watu wote wa nchi hii, na huduma hizo ni elimu na afya.
Tujenge shule za kweli kwa kufundisha walimu na kuwapa nyenzo za kufundishia. Tujenge zahanati za kweli kwa kufundisha wauguzi wa kutosha wa ngazi ya msingi watakaosambaa katika vijiji vyetu ambako ndiko wanakoishi watu wetu walio wengi na ndiko waliko wazalishaji wa chakula kinachotuweka hai.
Bila shaka watakuwapo Watanzania wachache watakaotaka kuwapa watoto wao elimu tofauti (nchini au ughaibuni), au watakaotaka kuwapeleka Afrika Kusini kila wanapopata mafua, wafanye hivyo kwa utashi wao wa anasa, lakini nchi iridhike kwamba watoto walio wengi wanapata elimu ya daraja la kwanza na matibabu maridhawa bila kulazimika kuuza nyumba zao au ng’ombe wao.
Siku tutakapofikia hatua hiyo, bila shaka tutakuwa tumeachana na malumbano yasiyoisha hivi sasa baina ya Serikali na wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusu ‘uchangiaji’ wa gharama za elimu, mivutano ambayo mimi naiona kama isiyokuwa na maana kwa sababu uwezo wa kuwasomesha vijana hawa tunao. Tunachotakiwa kufanya ni kuutambua ulipo na kuupeleka hadi kwenye tatizo.
Niliandika mapema kwamba mara nyingi tumeambiwa kwamba tunapenda kukosoa matendo ya watawala bila kutoa mapendekezo ya njia mbadala. Nimejaribu kutoa mapendekezo yangu, na bila shaka wako wengine wengi wenye mapendekezo kama yangu, na yaliyo tofauti. Basi tuyajadili.
Bila shaka hivi ni vipengele vya mjadala vitakavyorejewa kila mara, washiriki tukiwa ni sote tunaoona haja ya kukusanya mawazo yetu na kuyachakata kwa pamoja ili tujenge mwafaka kuhusu mambo muhimu yanayotuhusu.
Tusipofanya mjadala wa dhati tutaendelea kulalamika bila ye yote kutoa maoni juu ya namna ambavyo tunaweza kujikomboa kutoka katika umasikini unaozidi kuwakandamiza watu wetu ambao wamerithishwa nchi tajiri lakini hali zao hazifanani kabisa na utajiri huo.
Tusipoingia katika mchakato wa kweli juu ya masuala yanayohusu kuondoa umasikini na tukajifunza kwamba haya mambo si ya kupapukia bali hupangwa, tutaendelea kufukuzana na wananchi tukiwadai michango ya shule ya kujenga shule zisizo na waalimu wala vitabu; watatuona kama maadui zao wakati sisi tukijidanganya kwamba tunawapelekea ‘maendeleo’.
Bado zinatufikia taarifa za watu wanaokimbia kaya zao ili wasikamatwe kwa kushindwa (au kutokutaka) kulipa michango ya kujenga ‘madarasa.’ Baadhi yao wanaweza wakawa ni watu ambao kwa kweli kabisa hawana uwezo wa kulipa ‘michango’ hiyo, lakini baadhi yao wanaweza kuwa wale ambao, hata kama wanao uwezo wa kutoa fedha, hawaoni faida yo yote inayopatikana na ‘elimu’ inayotolewa ndani ya majumba yasiyo na walimu wala vitabu.
Kinachowafanya watendaji wa maeneo ya vijijini wawasake wananchi kama wahalifu ni maelekezo wanayopewa kutoka kwa waajiri wao wa Dar es Salaam, ambao katika mantiki ambayo inazidi kupinda kila uchao, bado wanaamini kwamba elimu ni sawa na idadi ya vyumba vya tofali na bati.
Maelezo yote yaliyotolewa na wataalamu kuhusu maana halisi ya elimu yamepuuzwa, na shughuli ya kuwahangaisha wananchi inaendelea mtindo mmoja.
Nimemuuliza rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa kijijini katika kipindi cha Noeli na Mwaka Mpya ni kwa nini basi msisitizo huu wa ujenzi wa majengo yasiyokuwa na maana haujajulikana kwa wakuu wa nchi; jibu lake ni kwamba wanajua lakini hawajui wafanye nini kwa sababu walikwisha kuagiza ujenzi ufanyike, na kwa hiyo ujenzi ni lazima ufanyike, na wazee wa kijijini wanaziona hizo ‘shule’ kama vituo vya kuwachunga watoto wa kike wasipate mimba!
Ipo mizaha inayovumilika, lakini huu si aina mojawapo ya mizaha hiyo. Huku ni kucheza na maisha ya watu na ni hatari kwa mustakabali wa Taifa. Siamini kwamba watu wetu wataendelea kuwa wa kusema “E walla” siku zote wakati wanaona mambo yanayofanyika yanawaumiza na kuwafanya watoto wao wasiwe na tumaini angalau la kuweza kuyafanya maisha yao yawe bora kuliko ya wazazi wao.
Hebu tukumbushane tena ( na kwa wale wasio na hadhi ya kukumbuka, kwa sababu hawajawahi kulisikia hili, tuelimishane) katika mambo yote unayoweza kuyafanya kwa ajili ya watoto wako hakuna hata moja linaloweza kulinganishwa na elimu bora na afya njema. Mengine yote yanakuja baadaye.
Kilicho dhahiri ni kwamba watawala wetu ni wazazi pia, na tunaona jinsi wanavyohangaikia elimu na afya za watoto wao. Kwamba hawahangaikii elimu na afya za watoto wa jamii za kimasikini si kwa sababu hawajui umuhimu wake; ni ubinafsi. Nafasi walizo nazo zingeweza kuwapa fursa ya kutumikia wananchi wa matabaka yote, na kwa kufanya hivyo tukapunguza ukali wa mapambano ya kitabaka katika siku zijazo.
Haitusaidii kupoza ghadhabu za wanyonge wanaoona watoto wao wanapewa ‘elimu’ inayofanana na ile iliyoitwa ‘bantu education’ wakati wa utawala wa Makaburu Afrika Kusini, huku watoto wa wakubwa wanapewa kila aina ya fursa, nchini na ughaibuni. Siku moja watalikataa hili… mwenye masikio na asikie.
Aidha, haiwezekani kwamba katika mazingira ya mijadala inayoendelea nchini kuhusu ‘ufisadi’ kwamba wananchi hawatajaribu kuuunganisha huo ‘ufisadi’ na hali zao mbaya za maisha na mifumo inayoonekana kutaka kumlaani mtoto wa mtu wa chini ili asiweze hata siku moja kusimama kwa miguu yake mwenyewe.
Mzee mmoja kutoka Kanda ya Ziwa ameniambia jambo ambalo siwezi kulisahau: Mtoto anapelekwa shule akiwa na miaka saba; anakaa huko kwa kipindi cha miaka 7; ‘anamaliza shule akiwa na miaka 14; shule hakuweza kujifunza hata huo ujuzi wa kusoma na kuandika, na nyumbani hakuwapo kujifunza namna ya kutunza ng’ombe na kulima pamba; kwa hiyo huku hayuko na kule hayuko.
Sasa mzee kama huyu unampa jibu gani anapokuambia kwamba yeye anatoa ‘kitu kidogo’ ili afisa elimu na wale watendaji wanaokuja kuswaga watoto kuwapeleka ‘shule’ wairuke kaya yake kama isiyokuwa na mtoto wa umri wa kwenda shule. Kwa kufanya hivyo angalau mtoto atabaki nyumbani ajifunze kuchunga ng’ombe!
Yote haya yana maana kwamba hatuna budi kujiwekea utaratibu wa kujadiliana kwa pamoja kuhusu hatua zote za maendeleo tunazokusudia kuzichukua. Tabia ya watawala wa nchi hii, na wa Afrika kwa ujumla, ya kufanya mambo wanavyotaka wenyewe imekuwa ni kikwazo kikubwa mno katika maendeleo ya nchi hii na bara hili kwa ujumla.
Maendeleo huletwa na watu wenyewe; hayawezi kuletwa kutoka juu, hata kama watawala wangekuwa na nia njema na dhamira yao ni kuwatumikia watu wao kwa dhati. Wananchi ndio wanaoumizwa na umasikini uliokithiri, na ye yote anayetaka kuwatumikia hana budi kuwasikiliza na kuyatia matakwa yao maanani.
Aidha, wananchi si vipofu; wana macho na wanaona kwamba hao hao watawala wao wanaowajengea ‘shule’ zisizokuwa na walimu na zahanati zisizokuwa na wauguzi wanao utaratibu mbadala wa kuwasomesha watoto wao na kuwapatia matibabu wanapougua.
Si muda mrefu uliopita mtawala mmoja katika mojawapo ya mikoa alikuwa kitetea ujenzi wa ‘shule’ hizo na kuwahimiza wananchi wapeleke watoto wao. Wananchi walikuwa wanamjua mkubwa huyo na walijua watoto wake wanasoma shule ya kweli, yenye walimu na vitabu na kila aina ya vifaa vya kufundishia, ikiwa ni pamoja na kompyuta.
Walipomuuliza ni kwa nini yeye hakupeleka watoto wake katika shule hizo, akawa mkali kweli kweli na mjadala ukaishia hapo.
Napenda kufunga sehemu hii ya makala hizi kwa kusisitiza kwamba iwapo tunataka kujenga mustakabali unaoeleweka kwa ajili ya Taifa letu hatuna budi kujenga utaratibu unaoeleweka wa kutoa huduma muhimu za msingi kwa watu wote wa nchi hii, na huduma hizo ni elimu na afya.
Tujenge shule za kweli kwa kufundisha walimu na kuwapa nyenzo za kufundishia. Tujenge zahanati za kweli kwa kufundisha wauguzi wa kutosha wa ngazi ya msingi watakaosambaa katika vijiji vyetu ambako ndiko wanakoishi watu wetu walio wengi na ndiko waliko wazalishaji wa chakula kinachotuweka hai.
Bila shaka watakuwapo Watanzania wachache watakaotaka kuwapa watoto wao elimu tofauti (nchini au ughaibuni), au watakaotaka kuwapeleka Afrika Kusini kila wanapopata mafua, wafanye hivyo kwa utashi wao wa anasa, lakini nchi iridhike kwamba watoto walio wengi wanapata elimu ya daraja la kwanza na matibabu maridhawa bila kulazimika kuuza nyumba zao au ng’ombe wao.
Siku tutakapofikia hatua hiyo, bila shaka tutakuwa tumeachana na malumbano yasiyoisha hivi sasa baina ya Serikali na wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusu ‘uchangiaji’ wa gharama za elimu, mivutano ambayo mimi naiona kama isiyokuwa na maana kwa sababu uwezo wa kuwasomesha vijana hawa tunao. Tunachotakiwa kufanya ni kuutambua ulipo na kuupeleka hadi kwenye tatizo.
Niliandika mapema kwamba mara nyingi tumeambiwa kwamba tunapenda kukosoa matendo ya watawala bila kutoa mapendekezo ya njia mbadala. Nimejaribu kutoa mapendekezo yangu, na bila shaka wako wengine wengi wenye mapendekezo kama yangu, na yaliyo tofauti. Basi tuyajadili.
Subscribe to:
Posts (Atom)