The righteous care about justice for the poor, but the wicked have no such concern. PROVERBS 29:7
Friday, May 17, 2013
MOHAMMAD S.A.W MTUME WA WAISLMU, HAJAWAHI, SIYO , NA WALA HATAKUWA MTUME NA NABII WA KWELI
MOHAMMAD S.A.W MTUME WA WAISLMU, HAJAWAHI, SIYO , NA WALA HATAKUWA MTUME NA NABII WA KWELI
Nimesoma kwenye blog ya jamii forums na kuona Waislamu wakiwashawishi
watu wengine wamuamini Mohammad kuwa naye ni miongoni mwa manabii na
mitume wa Mungu aliye hai, jambo ambalo si kweli.Fuatilia…..
WAJUE MANABII WA UONGO
Na Mwalimu Daniel Mwankemwa
UTANGULIZI:
Suala linalohusu kuwajua manabii wa uongo , limekuwa linaleta shida
sana kwa watu wengi, kwa sababu manabii hao wa uongo wanapokuja kwa watu
kuleta ujumbe wao hudai “ tumetumwa na Mwenyezi Mungu kuleta ujumbe
wake na hivyo kuwataka wanadamu kuupokea, kuuamini na kuufuata”.
Inapotokea nabii amekuja kwa mtindo huo na akakutana na watu wasiojua
kuwapambanua manabii na mitume kwa misingi ya Neno la Mungu, ndipo
ukengeufu hutokea, na makundi ya aina mbalimbali ya imani za uongo
hujitokeza.
Kwa hapa kwetu Tanzania,unaposoma katika Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Ibara ya 19 (i-iii) utakutana ma maelezo
kuwa ,mfuasi wa dini yoyote anao uhuru wa kubadili dini yake ya awali
na kujiunga na dini nyingine anayoona yeye kwake inamfaa. Lakini pamoja
na uhuru huo si kila dini (njia) inafaa zingine zinaishia kwenye mauti
ya milele.
Mith 14:12 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti”. (Angalia pia Mith 16:25).
Miongoni mwa wanadamu wanaoitwa nabii na mtume, ni mtu aitwaye Muhammad
s.a.w ibn Abdullah,ibn Abdu Mutallib, ambaye ni mtume na nabii katika
dini ya Kiislamu.
Pengine wewe msomaji wa somo hili unaweza
kushangaa ni kwa vipi sisi ambao si Waislamu bali Wakristo tuanze kuhoji
habari za Muhammad s.a.w mtume wa Waislamu?. Jibu lake ni kwamba kitabu
cha Qur’an kinachotumiwa na Waislamu kimetutaja sisi Wakristo mara 62
kikitutaka kuupokea ,kuuamini na hatimaye kuufuata ujumbe wa Muhammad
s.a.w kwa madai ya kuwa yeye ni nabii na mtume wa mwisho hata kwetu
Wakristo, aliyetumwa na Mungu.
Tunasoma hayo ndani ya Qur’an
katika Suratul, Baqarah, (ng’ombe jike wa manjano), 2: 62 “Katika
walioamini (Mitume ya zamani huko ) na Wayahudi na Wakristo na Wasabai,
yoyote miongoni mwao atakayemwamini Mwenyezi Mungu (Sasa kama anavyosema
Nabii Mohammed ) na akaamini siku ya mwisho na akafanya vitendo vizuri
basi watapata thawabu zao kwa Mola wao, wala haitakuwa khofu juu yao
wala hawatahuzunika”.
Kwetu sisi kama Wakristo japo katika aya
hii tumetajwa , kuna swali ambalo tunajiuliza kuhusu unabii na utume wa
Muhammad nalo ni hili “ HIVI MWENYEZI MUNGU ALISAHAU NINI KATIKA KAZI
YAKE YOTE KAMILIFU YA KUMKOMBOA MWANADAMU KUTOKA KATIKA DHAMBI MPAKA
AMLETE MUHAMMAD S.A.W?”.
Nabii ni mtu gani? Nabii ni mtu
aliyeteuliwa rasmi kwa vigezo vya Kiungu ili kuleta ujumbe wa Mungu kwa
wanadamu, kwa maneno mengine nabii ni msemaji wa siri za Mungu.
Nabii: Ni mtu ambaye ni msemaji wa Mungu (a mouthpiece of God) .Husimama
kati ya Mungu na binadamu, mwenye jukumu la kupeleka ujumbe wa Mungu
kwa watu. Nabii anapokuwa msemaji wa Mungu, huvuviwa na Roho wa Mungu,
bila ujumbe wake kuwa na makosa. Nabii hujizuia kabisa utashi wake,
nafsi yake,,na mawazo yake, anapokuwa anatoa ujumbe wa Kinabii toka kwa
Mungu. Wakati mwingine Mungu mwenyewe hutia maneno yake vinywani mwao
(Kum 18:18, Yer 1:9). Nabii ni mtumishi wa Mungu (Zekaria 1:6) na mjumbe
wa Mungu 2 Nyak 36:15). Unabii wao umegawanyika katika makundi matatu:
Unabii unaoelezea hatima ya Waisrael, Nabii zinazohusiana na ujio wa
Masihi, na nabii zinazoelezea mambo yajayo (Eschatological prophets).
Kwa hiyo Sheria na Manabii inahusiana na Torati (Pentateuch) yaani
Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati. Na
manabii ni vile vingine vyote visivyo kuwa Torati.
Kitabu cha nabii
Amos 3:7 “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia
watumishi wake manabii siri yake”Neno nabii asili yake ni katika lugha
ya Kiebrani na maana yake mwonaji. 1Sam 9:9 “ Hapo zamani katika Israel,
mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! twende kwa
mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa mwonaji”.
Katika mstari huo hapo juu unatuonesha kuwa manabii wa kweli wa Mungu ni
lazima chanzo cha ufunuo au ujumbe wao kiwe Mwenyezi Mungu mwenyewe
(Roho Mtakatifu), au ndoto kutoka kwake, au maono kutoka kwake (Hes
12:6), au kupitia malaika watakatifu (Dan 8:15-21) . kinyume na hapo ni
nabii wa uongo .
Tahadhari ya Bwana Yesu: Bwana Yesu alipokuwa
hapa duniani alituonya kuhusu kuwatambua manabii na mitume wa uongo
kabla Muhammad hajazaliwa (amezaliwa 570 B.K), wala kabla Uislamu
haujaanzishwa na Muhammad mwaka 610 B.K, wala kabla ya kuwepo kitabu
kinachoitwa Qur’an. Tunayasoma maonyo hayo ya Bwana Yesu katika
Mathayo 7:15-16 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia
wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali,
mtawatambua kwa matunda yao”.
Mathayo 24:11-13 “Na manabii
wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi na kwasababu ya
kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia mpaka
mwisho, ndiye atakayeokoka”.
Mitume wa Bwana Yesu walisisitiza sana wakikazia kuhusu onyo la Yesu juu ya kuwajua manabii na mitume wa uongo .
1Yohana 4:1-3,15 “Wapenzi msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo
roho, ya kwamba zimetokana na Mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi
wametokea duniani.Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo
kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho
isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo
ambayo mmesikia kwamba yaja na sasa imekwisha kuwako duniani. 15 “ Kila
akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake naye
ndani ya Mungu”
Vigezo hivi tulivyopewa na Biblia Takatifu
kuwajua manabii na mitume wa uongo ni muhimu sana tukavichunguza katika
maisha ya wale wanaoitwa nabii au mtume .
Nabii wa kweli hupata
ufunuo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu:- 2Petro 1:20-21.” Mkijua neno
hili kwanza,ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa
kama apendavyo mtu fulani tu.Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi
ya mwanadamu;bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu,wakiongozwa na
Roho Mtakatifu”.
1 Petro1:10-11 “Katika habari ya wokovu huo
manabii walitafuta tafuta na kuchunguza chunguza ambao walitabiri habari
za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi na wakati wa
namna gani ulioonywa NA ROHO WA KRISTO ALIYEKUWA NDANI YAO ambaye
alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo na utukufu
utakaokuwako baada ya hayo…..” (maneno ya msisitizo kwa herufi kubwa ni
ya mwandishi)
Ufunuo 19:10 “Nami nikaanguka mbele ya miguu
yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli
wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa
maana ushuhuda wa Yesu ndiyo roho ya unabii”
Hivyo manabii
walisema ndani yao wakiongozwa na Roho wa Kristo mwenyewe, kabla hajaja
ulimwenguni katika mwili. Je Muhammad s.a.w ni miongoni mwao hata
tuuamini ujumbe wake?
Muhammad hakujua kusoma wala kuandika
Qur’an 7:157
Ambao wanamfuata mtume nabii aliye ummy (asiyejua kusoma wala kuandika)
na juu ya hivi atafundisha mafundisho hayo ya ajabu ya uislamu……….
Na ushahidi mwingine unapatikana katika kitabu cha Maisha ya nabii
Muhammad uk 8 kilichoandikwa na Sheikh Abdallah Saleh Al-Farsy, tunasoma
kama ifuatavyo katika kipengele cha kujifunza kwake;-
Habari
ya kusoma haijakuwako katika nchi ya hijazi, hivyo mtume aliondokea kama
Makureshi wengine bila ya kujua kusoma wala kusoma kilichoandikwa.
Elimu yao ilikuwa kujifundisha mambo yanayohusu maisha yao ya kibedui,
kama vita, kutunga mashairi ya kujisifu ushujaa wao na kutunga hotuba
zinazoweza kuharakisha watu wapigane bila ya kufikiri.
Hivyo basi Muhammad katika maisha yake hakujua kusoma wala kuandika na ndivyo alivyoishi katika maisha yake yote.
Je Yesu alijua kusoma na kuandika? Luka 4:16-17. HOJA ya Waislamu
wanasema katika Yoh 7:14 Yesu akiwa Yerusalemu watu wakashangaa kuwa
amepataje elimu ambaye hakusoma? Ukweli ni kwamba Yerusalemu siko
alikokulia Yesu. Yeye Yesu amekulia Nazareti ambako wanamfahamu kuwa
anajua kusoma na ndiyo sababu alipewa chuo cha nabii Isaya ili akisome.
JINSI MUHAMMAD (S.A.W) ALIVYOPATA UTUME NA WAHYI (UFUNUO) WAKE
Ufunuo aliokuja nao Muhammad s.a.w , mtume wa Waislamu, ni tofauti sana
na mitume wote walioishi kabla yake wanaotajwa ndani ya Biblia
Takatifu. Tofauti yake ni kwamba manabii na mitume wote waliotajwa ndani
ya Biblia Takatifu, wameandika watu mbalimbali wapatao 40 kwa miaka
mingi sana inayokaribia 1500, lakini ufunuo wao ni wa aina moja (it has
comformity). Ule unabii wa Agano la Kale umetimizwa katika Agano Jipya.
Hii ni kwa sababu chanzo cha ufunuo huo ni kimoja, Roho Mtakatifu.
Lakini kwa upande wa Muhammad s.a.w , mtume wa Waislamu yeye chanzo cha
ufunuo na hatimaye utume wake ni masuala yenye utata sana ambao hata
wafuasi wa dini hiyo na wao hawajui kwa hakika ukweli ni upi.
Hebu tuangalie kwa ufupi utata huo.
Muhammad s.a.w alipotimiza umri wa miaka 38 alihama toka nyumbani
kwake, akahamia katika mapango yaliyokuwa hapo karibu na mji wa Makka.
Alipofikisha umri wa miaka 40 siku moja alitokewa na kiumbe ambacho
Waislamu leo wanakiita Malaika Jibril.
Wahyi (ufunuo) uliokuja
kwa Muhammad alisikia makengele,uso kuwa mwekundu,jasho kumtoka. Katika
Bukhar, Hadithi na 2, Juzuu na 1,Al-Lu’lu Kitabu cha 3.Uk. Na.874
Hadithi na 1505 “Hadithi ya Aisha r.a mama wa waumini amesema, kuwa Al
Harith ibn Hisham r.a alimuuliza mtume wa Allah s.a.w ‘ Ewe mtume wa
Allah hivi wahyi (ufunuo) hukujia vipi?’ mtume wa Allah s.a.w akajibu, “
Wakati mwingine hunijia kama mlio wa kengele, na aina hiyo ndiyo ngumu
zaidi kwangu, inaondolewa hali hiyo kwangu wakati tayari nimeshapata
wahyi. Na nyakati nyengine malaika anakuja kwangu akiwa katika mfano wa
mtu, kwa hiyo ananieleza na ninayazingatia aliyoyasema.” Aisha r.a
alisema , Na hakika nilimwona unamshukia wahyi siku ya baridi kali na
ilipomuondoka hali hiyo, paji lake la uso lilichuruzika jasho.”
Qurani 53:2 – 6 Suratul Najm (Nyota) “Kwamba mtu wenu huyu Nabii
Muhamad (hakupotea kwa ujinga) na wala hakukosa (Na hali ya kuwa
anajua). Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya
(anayosema) ila ni wahyi (ufunuo) uliofunuliwa (kwake). Amemfundisha
(malaika) mwenye nguvu sana. Mwenye uweza na yeye (huyu Jibril)
akalingana sawa sawa.
Huyu malaika Jibril ndiye Waislamu
wanasema alimtokea Muhammad kule pangoni na kwamba yeye huyo malaika
Jibril ndiye Roho Mtakatifu. Tunaposoma ufafanuzi wa aya ya 2:87 ya
Suratul Baqarah, uliyomo ndani ya Qur’an unasema “Kwa Waislamu Roho
Mtakatifu ni Malaika Jibril si yule wanaodai Wakristo kuwa ni mmoja wa
asili ya utatu (Trinity)”.
Jambo ninalopenda ulijue ni kwamba
Waislamu wote hawakubahatika kupewa elimu ya Roho. Hii ni kuanzia mtume
na nabii wao Muhammad . Tunasoma hayo katika Qur’an 3:7 “Yeye ndiye
aliyekuteremshia kitabu (hiki Qur’an) ndani yake zimo aya Muhkam
(nyepesi kufahamika) ambazo ndizo msingi (asili) wa kitabu (hiki) na
ziko nyingine Mutashabihat (zinababaisha kama habari za akhera,za peponi
na motoni na mengine ambayo yamekhusika na Roho).Wale ambao nyoyoni
mwao mna upotofu wanafuata zile zinazo babaisha kwa kutaka kuwaharibu
watu na kutaka kujua hakika yake vipi; na hakuna ajuaye hakika yake vipi
ila Mwenyezi Mungu. Na wale waliozama katika ilimu
husema:”Tumeziamini,zote zimetoka kwa Mola wetu.”Na hawakumbuki
isipokuwa wenye akili.”
Qur’an 17:85 Suratul Ban Israil (Wana
wa Israeli). “Na wanakuuliza habari ya roho.Sema roho ni jambo
lililohusika na Mola wangu (Mwenyezi Mungu),Nanyi hamkupewa katika ilimu
(ujuzi) ila kidogo kabisa.(Nayo ni ilimu ya vitu visivyokhusika na
roho”).
Hivyo katika Uislamu elimu ya Roho hawana kwa mujibu wa
Qur’an. Hii ndiyo sababu mara nyingi wao hushughulikia sana mambo ya
nje (externalistics) zaidi kuliko ya Rohoni k.m kutawadha na kupandisha
maji puani wakiamini wamemtoa Shetani aliyekuwa ndani ya pua. Katika
kitabu kiitwacho Al-Lu’lu’ wal-Marjan, Juzuu 1. Hadithi na 183 uk. 96
inasomeka hivi “Amesimulia Abu Huraira (r.a), Mtume (s.a.w) alisema,
“Mmoja wenu anapoamka kutoka usingizini, basi atawadhe na apandishe maji
puani na apenge mara tatu, kwa sababu Shetani alilala ndani ya tundu za
pua yake”. (Bukhari, Hadithi, Na.516 Juzuu 4)
Baada ya
kufahamu jinsi Waislamu wasivyokuwa na elimu ya Roho, ndipo tunapoanza
kuhoji huyo malaika anayeitwa Jibril ni nani ? Je ni malaika wa Mungu wa
Kweli YEHOVA?.
Biblia Takatifu inaeleza juu ya malaika
walioasi mbinguni kisha wakafukuzwa na kutupwa huku chini. 1Petro 2:4
“Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachia “malaika waliokosa” bali aliwatupa
shimoni akawatia katika vifungo vya giza walindwe hata ije siku ya
hukumu”.
Kwa mafundisho haya ya Biblia yanatuonesha kuwa kuna
kundi moja la malaika liliasi na likafukuzwa na hadi sasa kundi hilo
linasubiri hukumu. Kundi hilo leo linaitwa Shetani,Majini au Mapepo
wachafu.
Lakini tusomapo kitabu cha Qur’an , kitabu kilichokuja
baadaye sana karne ya 7 (610 B.K) ,baada ya kitabu cha Biblia, ndani
yake tunapata taarifa tofauti kuhusu malaika.
Qurani 32:13
Suratul As – Sajdah (Kusujudu) “Na tungalitaka tungempa kila mtu
uwongofu wake (kwa lazima kama tulivyowapa malaika…”
Ufafanuzi wa aya ya 13 ulio ndani ya Qurani unasomeka hivi:.
“Angetaka Mwenyezi Mungu angemuumba binadamu kama malaika hawezi
kufanya mabaya, maumbile yake ni kufanya mema tu; kwa hiyo halipwi kwa
mema yake hayo kwani hayaonei taabu katika kuyafanya. Lakini binadamu
ameumbwa kwa uweza wa yote mawili sawasawa na raha yake zaidi ni kufanya
mabaya”
Aya hii na ufafanuzi wake, vinaeleza kuwa malaika wote
wa Mungu wa Muhammad ni wema hakuna aliyekosa, na kuwa miongoni mwa
malaika hao mmojawao ndiye aliyemtokea Muhammad na kumpa utume na ufunuo
wa Qur’an. Sasa hebu tuchunguze kule pangoni alikokuweko Muhammad ili
kupata utume alitokewa na kiumbe gani?. Tutaongozwa na vitabu vya dini
ya Kiislamu.
Katika kitabu kiitwacho: Maisha Ya Nabii Muhammad
s.a.w uk 16-17 kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy,
tunasoma kama ifuatavyo;-
Hata siku moja- katika mwezi wa
Ramadhani mwezi 17, Jumatatu katika mwaka wa 40 ½ wa umri wake- mtume
alimwona mtu kamsimamia mbele yake bila ya kumwona wapi katokea,
akamwambia; “soma”. Mtume akamjibu; “Mimi sijui kusoma kwani sijapata
kujifundisha kusoma.” Akaja akamkamata akambana, akamwambia tena;
“soma,” Mtume akamjibu jawabu yake ileile. Hata mara ya tau akamwambia;
“soma- Iqraa Bismi Rabbik.” Akamsomea sura hiyo ya 96 mpaka kati yake.
Kisha mtume akaisoma kama alivyosomewa. Hii ndiyo sura ya kwanza kushuka
katika Qur’an, ingawa haijawekwa mwanzo.
Mara, yule mtu
(Malaika) akaondoka machoni mwake- asimwone kenda wapi. Na mtume naye
akarejea kwake-khofu imemshika. Alipofika nyumbani, Bibi Kadhija
alidhani ana homa, akamfunika maguo gubigubi na akakaa mbele yake
akimsikiliza anavyoweweseka. Hata homa ilipomwachia alimweleza Bibi
Kadhija yote yaliyomtokea; na Bibi Kadhija akamtuliza moyo wake,
akamyakinishia ya kuwa hapana lolote baya litakalomzukia. Mara bibi huyu
akaondoka akenda kwa jamaa yake – Bwana Waraqa bin Naufal- akampa
habari yote iliyompata mumewe. Naye akamwamrisha amwite. Na mtume akenda
akamweleza habari yake yote. Bwana Waraqa akamwambia; “ Huyo ndiye
Jibril aliyemshukia Nabii Musa na Nabii Isa. Basi jibashirie kuwa wewe
ni mtume wa umma huu, nami natamani kuwa hai nikuone unavyosimama
kuwatengeneza jamaa zako; Inshaallah nitakuwa mkono wako wa kulia”
Wakarejea kwao na khofu yote imemtoka”.
Alipokuwa pangoni
alichezewa na Shetani: Katika kitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na
Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma
maneno haya
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe
akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe
maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema
“Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na shetani na kuniharibu akili yangu
na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo;
Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani
hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako,
unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu
sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya
hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona
umekwishakuwa mtume”.
Katika tukio hili lililompata Muhammad
akiwa pangoni , ndipo Waislamu wote ulimwenguni wanapolieleza kuwa hapo
ndipo Muhammad s.a.w alipoletewa wahyi (ufunuo) na kupewa unabii na
utume. Lakini unapotafakari juu ya ujumbe huo utaona kuwa hata yeye
mwenyewe hajui nini kilichokuwa kimemtokea kule pangoni. Ndiyo maana
tunasoma kuwa alipofika nyumbani kwake mkewe Bi. Khadija alimfunika nguo
mumewe akidhani ana homa. Muhammad alimweleza mkewe kilichomtokea kuwa
ni “Shetani” hakumsema malaika yeyote kama Waislamu wanavyotaka
kutuaminisha leo. Kwa sababu kama angekuwa ni malaika kama tunavyosoma
ndani ya Biblia ,asingesita kujitambulisha kwa Muhammad kuwa yeye ni
nani. Hii ni hoja ya kwanza.
Hoja ya pili tunaona kuna mtu
anaitwa Waraqah ibn Naufal, binamu yake na mke wa Muhammad s.a.w Bi
Khadija. Yeye Waraqah anamwambia Muhammad huyo aliyekutokea ni malaika
Jibril. Basi jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu !!!!! Je
alikuweko pangoni wakati Muhammad s.a.w akitokewa na kiumbe
asichokijua?.
Hoja ya tatu tunaona hata huyo mkewe Muhammad
anamwambia mumewe utume huo !!!!!!! Je na yeye alikuweko pangoni? Kama
hakuweko ni nani aliyemwambia kuwa yule ni malaika Jibril ikiwa Muhammad
mwenyewe aliyetokewa alisema nimetokewa na Shetani? Tafakari
Katika kitabu kiitwacho Tafsir Al-Kashif, cha Muhammad Jawad Mughniyyah,
uk74 paragrafu ya 7 inasomeka“ Hakuna njia ya kumjua Iblis, Shetani na
Jini, isipokuwa kwa njia ya wahyi (ufunuo) tu”
Qurani Suratul Sad 38:69 Muhammad amenukuliwa akisema “Sikuwa na ilimu ya viumbe watukufu(Malaika)…
Kwa sababu ya Muhammad s.a.w kutowajua malaika kwake yeye anasema
unapomwona punda akilia basi kamwona Shetani. Katika Kitabu kiitwacho
Mkweli Mwaminifu, Juzuu 3-4 Hadith 789 uk 38 “ Punda akilia kamwona
Shatani”
Jambo hilo ni tofauti na jinsi Biblia Takatifu
inavyoeleza kuhusu punda. Mungu anaweza kumtumia hata punda kuongea na
wanadamu ili kuwajulisha ujumbe wake. Katika kitabu cha Hesabu 22:22-31
tunasoma habari ya Balaamu jinsi Mungu alivyomtumia punda kumwambia
Balaamu asiendelee na safari yake , baada ya punda huyo kumwona malaika
wa Bwana akiwa ameshika upanga na amesimama mbele yao akiwa amezuia njia
aliyotakiwa kupita. Punda alimwambia Balaamu ule msitari wa 30-31 “
Yule punda akamwambia Balaamu, Je mimi si punda wako, nawe umenipanda
maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema La!. Ndipo
Bwana akafunua macho ya Balaamu, akamwona malaika wa BWANA amesimama
njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa; naye akainama
kichwa, akaanguka kifudufudi”
Inaonekana kwa tukio hili
lililomtokea Balaamu, Mungu alimfunua macho yake akamwona malaika.
Lakini kwa Muhammad yeye anachokiona ni Shetani tu. Na ndiyo maana
anasema punda akilia amemwona Shetani
Kwa hiyo kama ufunuo wa
Muhammad unaanza na Shetani kama vitabu sahihi vya dini ya Kiislamu
vinavyoeleza, kwa mujibu wa ufafanuzi wa kitabu hicho cha Tafsir Al
Kashif, inaonesha kwamba ufunuo, unabii na hata utume wa Muhammad una
walakini mkubwa ukilinganisha na ujumbe wa manabii na mitume waliotajwa
ndani ya Biblia Takatifu.
Katika Biblia shetani ametajwa kuwa anaweza kujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
2 Wakorintho 11:13-15 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao
kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si
ajabu, maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakajigeuza wawe mfano wa
watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao”.
Muhammad akiwa Medina aliulizwa na Wayahudi ikiwa ufunuo wake umetoka
kwa Mungu wa Kweli kwa kumtaka atoe sifa za manabii. Akijibu swali hilo
alisema:
Mkweli Mwaminifu Juzuu 3-4 Uk.63.Hadithi Na. 880. “Kasema
Mtume (s.a.w):- (Mambo) mane ya sheria za mitume (Kuwa na) na haya,na
kujipaka mafuta mazuri,na kuowa (wake),na kupiga mswaki.
Hizi si sifa za Ki-Mungu kwa nabii na mtume bali ni za kibinadamu tu.
Manabii na watu mbalimbali katika Biblia hawakuona haya. Soma Isaya
50:7 “ Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa
sababu hiyo nimeukaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa
sitaona haya”. Zaburi 34:5 “ Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, Wala
nyuso zao hazitaona haya” Zab 119:46 “ Nitazinena shuhuda zako mbele ya
wafalme, Wala sitaona aibu” Warumi 1:16 “ Kwa maana siionei haya Injili;
kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye kwa
Myahudi kwanza , na kwa Myunani pia” 1Petro 4:16 “ Lakini ikiwa kwa
sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
Zaidi ya hayo tunaona Muhammad alirogwa. Kurogwa ni hali ya mtu
kuathirika na nguvu za giza yaani uchawi.. Je nabii au mtume wa Mwenyezi
Mungu wa Kweli anaweza kurogwa?
Katika Qur’an Suratul
Ban-Israel, 17:47 “ Tunajua sana, sababu wanayosikiliza, na
wanaponong’ona, wanaposema hao madhalimu. Nyinyi hamfuati isipokuwa mtu
aliyerogwa”
Pia katika Suratul Falaq, 113:1-5 “ Ninajikinga kwa mola
wa ulimwengu wote na shari ya Alivyoviumba, na shari ya giza la usiku
liingiapo, na shari ya wale wanaopulizia (vivia) mafundoni (wakavunja)
mashikamano yaliyo baina ya watu yaani shari ya mafatani, Na shari ya
hasidi anapohusudu”
Tunasoma tukio hilo katika ufafanuzi wake
uliyomo ndani ya Qur’an chapa ya nane uk.977 unaofafanua Sura ya 113-114
“Athari ya uchawi juu ya mtume (s.a.w). Swali la pili lijitokezalo
kuhusu sura mbili hizi ni kwamba kwa mujibu wa hadithi uchawi ulifanywa
dhidi ya mtume (s.a.w) naye akawa mgonjwa, na ili kuiondoa athari hiyo
ya uchawi Jibril (a.s) alikuja na kumpa maelekezo Mtume (s.a.w) ya
kusoma sura mbili hizi. Watafiti wengi zamani na wa sasa wamelifanyia
upinzani jambo hilo, kwamba ikiwa hadithi zitakubaliwa, basi mfumo wote
wa sharia utakuwa ni wa kutiliwa shaka, kwa sababu kama mtume (s.a.w)
aliweza kuathirika kwa uchawi, na kwa mujibu wa hadithi hizi kweli
uchawi huo ulionesha athari yake, basi hatuwezi kukaidi au kukana hadi
kiwango gani maadui waliweza kumfanya Mtume (s.a.w) aseme na atende
mambo kwa nguvu ya uchawi, na katika mafundisho yake mambo mangapi
yatoka kwa Allah na mangapi yatokana na athari ya uchawi juu yake. Si
hiyo tu, bali pia wasema kuwa baada ya kuyatambua hayo kuwa ni kweli
katu haitawezekana hata kule kukaidi kuwa (s.a.w) alishawishiwa kudai
utume kwa mauzauza ya kinjozi kuwa alimjia malaika. Pia wanasema hadithi
hizi zapingana na Qur’an, na kama ilivyo katika Qur’an kuwa tuhuma hiyo
batili kwa makafiri ilivyotajwa kuwa mtume s.a.w amerogwa naye
ameathirika na uchawi: wanaposema hao madhalimu, ‘Ninyi hamumfuati
isipokuwa mtu aliyerogwa’.” (17:47), lakini hadithi hizi zinathibitisha
madai ya makafiri kuwa kwa kweli aliathirika na kuongozwa na
uchawi……Kadri historia inavyohusika,ukweli kuwa kiasi fulani cha athari
ya uchawi juu ya Mtume (s.a.w) ni hakika iliyothibiti; na kama kwa
ustadi wa ubishi inawezekana kuthibitisha kuwa kweli.Limesimuliwa jambo
hilo na Bukhari, Muslim, Nasai, Ibn Majah, Ahmad, ‘Abdur Razzaq, Humaid,
Baihaqi, Tabarani, Ibn Sa’d, Ibn Marduyah, Ibn Abi Shaibah, Hakim, Abd
bin Humaid na Muhadithina wengine toka kwa Bi. ‘Aisha (r.a), Zaid bin
Arqam, Ibn ‘Abbas kupitia silsila nyingi mno kiasi kwamba jambo lenyewe
limefikia hali ya ufululizo kamili, isipokuwa kila Hadithi, yenyewe ni
ripoti kamili.
Hii ni uthibitisho mwingine mzito unaoonesha
kuwa utume wa Muhammad una utata. Ikiwa na wao Waislamu kwa mujibu wa
hadithi hizi hawajui ni mambo mangapi Muhammad aliyoyasema yanatoka kwa
Allah na mangapi aliyasema akiwa ameshinikizwa na wachawi , Je ufunuo na
utume wake utakuwa umetoka kwa Mungu wa Kweli? Tafakari !!1
Ndani
ya Biblia Takatifu hakuma kurogwa kwa mtu wa Mungu. Hesabu 23:23 “
Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israel.
Sasa habari za Yakobo na Israel zitasemwa , Ni mambo gani aliyoyatenda
Mungu!”
Kwa mujibu wa kitabu cha Biblia Takatifu, manabii na mitume wa kweli wa Bwana Mungu wanatoka katika taifa la Israel.
Kitabu cha Ezekiel 13:9 “ Na mkono wangu utakuwa juu ya manabii
wanaoona ubatili, na kutabiri uongo;hawatakuwa katika mashauri ya watu
wangu, wala hawataandikwa katika maandiko ya nyumba ya Israel, wala
hawataingia katika nchi ya Israel; Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana
MUNGU” .
Pia kwa mujibu wa kitabu cha Qur’an manabii na mitume
ni lazima watoke kwa Yakobo ambaye ni mtoto wa Is-haqa ambaye naye ni
mtoto wa Ibrahim. Qur’an Suratul Al-Ankabuut, (Buibui), 29:27 “ Na
tulimpa (kumzaa nabii) Is-haqa na (kumjukuu nabii) Yakubu na tukauweka
katika kizazi chake unabii na (kupata) kitabu, na tukampa ujira wake
katika dunia; naye katika akhera kwa yakini atakuwa miongoni mwa watu
wema”.
Aya hii, inaendelea kusisitiza kuwa ni kupitia kizazi
cha Yakobo ndiko uliko unabii na kupata kitabu. Kwa bahati mbaya
Muhammad ibn Abdullah, hatoki katika kizazi hicho wala kwa Ishmael kama
wanavyodai Waislamu . Kwa sababu Ishmael ni Mwebrania kama baba yake
mzee Ibrahim alivyo Mwebrania (Mwanzo 14:13) na Muhammad ni mwarabu
kutoka kabila la Maqureysh. Kwa kutambua hilo ndipo tunamwoma Muhammad
akiwaonya watu wengine wajiepushe na watu wa kabila lake.
Sahih
Al-Bukhari Vol.1.Hadithi Na. 801 na Al-Lu’lu Kitabu cha 3.
Uk.1089.Hadithi Na.1846 inasomeka“Hadithi ya Abu Huraira (r.a) amesema
,“Mtume wa Allah (s.a.w) amesema,Kabila hili la Makuraish litawateketeza
watu.’ Wakauliza, ‘Unatushauri nini?’ Akasema, Nashauri watu wajitenge
nalo.”
Kumzamisha nzi kwenye kinywaji
Bukhar vol. 4 Hadith
537 “ Narrated Abu Huraira: The Prophet said: If a house fly falls in
the drink of any one of you, he should dip it (in the drink) for one of
its wings has a disease and the other has the cure for the disease”
Tafsiri: Ilisimuliwa na Abu Huraira: Nabii alisema kama nzi akiangukia
ndani ya kinywaji cha mmoja wenu, anapaswa kumzamisha kabisa (ndani ya
kinywaji) kwa kuwa bawa lake moja lina ugonjwa na bawa lake jingine lina
dawa
Mitume wa Yesu ndani ya Biblia Takatifu walikwisha
kutuonya kuhusu uchafu huo. Katika 2 Kor 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa
kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili
na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”
Miongoni mwa mafundisho ya Muhammad ni kwamba kuna mambo kumi
yanayokamilisha Uislamu nayo tunayasoma katika kitabu kiitwacho Mkweli
Mwaminifu , Kilichoandikwa na Sheikh Said Moosa Al-Kindy wa Muscut,
Juzuu 3-4 Uk 63.Hadithi Na.880 “ Kasema Mtume (s.a.w) (Mambo) kumi ya
Uislamu (yanayokamilisha Uislamu):Kukata masharubu,na kuziweka
ndevu,nakuziweka ndevu (kutozinyoa) ndevu,na kupiga mswaki,kusafisha
ndani ya pua kwa maji,na kukata kucha,kuosha mikono baina ya vidole,na
kung’oa (au kunyoa) nywele za kwapani,na kunyoa nywele za mbeleni
(mavuzi),na upungufu wa maji. La kumi,kasema sahaba aliepokea hadithi
hii kuwa nimesahau,lakini kasema bila shaka la kumi ni “kutahiriwa.”
Kwa mujibu wa Biblia manabii na mitume wanathibitishwa kwa njia ya miujiza.
Kutoka 14:21” Musa akanyosha mkono wake juu ya bahari,BWANA akaifanya
bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki,usiku
kucha,akaifanya bahari kuwa nchi kavu”.
Matendo 19:11-12 “Mungu
alifanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida . Hata wagonjwa
wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake magonjwa yao
yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka”. Tazama pia Matendo 16:16-18,
20:7-12 na Matendo 13:6-12.
Qur’an nayo inathibitisha kuwa manabii na mitume ni lazima wafanye miujiza.
Qurani 40:78 Suratul Al-Muumini [Waumini] inasomeka “Na kwa yakini
tumewatuma mitume kabla yako wengime katika wao tumekusimulia (majina
yao na habari zao) na wengine hatukukusimulia na haikuwa kwa mtume
yoyote kuleta muujiza wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”
Muhammad hakupewa kufanya muujiza wowote ili kuthibitisha madai ya unabii na utume wake.
Qur’an 29:50 Suratul Al-Ankabuut (Buibui). “Na walisema “Mbona
hakuteremshiwa miujiza kutoka kwa Mola wake? Sema miujiza iko kwa
Mwenyezi Mungu tu (akitaka atakuteremshieni na kama hataki basi),nami
hakika ni mwonyaji mbainishaji (dhahiri tu).” (Taz. Qur,an 6:35-37
13:7,)
Katika Qur’an iko aya ambayo tunapaswa tuitafakari wote
kwa pamoja.Katika Surat An-Nisaa, (wanawake), 4:79 “Wema uliokufikia
unatoka kwa Mwenyezi Mungu na ubaya uliokufikia unatoka nafsini mwako,
mwenyewe umefanya mambo hata yakakufika hayo. Nasi tumekupeleka kwa watu
kuwa mtume na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha (hapaitajiwi shahidi
mwingine)”
Aya hii inaonesha kuwa Muhammad mtume wa Waislamu,
alipelekwa kwa watu kuwa mtume, huku Mwenyezi Mungu akiwa shahidi tu.
Siku zote shahidi si mtendaji bali ni mwonaji tu wa tendo
lililotendeka.Hoja yetu tungependa kuwajua hao watu waliompeleka
Muhammad kwa watu ni akina nani?. Kwa sababu tumeona kule nyuma baada ya
Muhammad kutoka pangoni, mkewe Bi. Khadija anamwambia Muhammad kuwa
“utume huo!!!!!!! Na Bwana Waraqah ibn Naufal akimwambia Muhammad kuwa “
basi jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu” kabla ya Qur’an .Je hao
si wale “Nasi tumekupeleka” wanaotajwa kwenye aya hiyo hapo juu?
Tafakari!! .
Waislamu hudai kuwa Muhammad ametumwa na Mwenyezi
Mungu wao, ambaye ni Mfalme wa Wafalme . Lakini tusomapo Biblia Takatifu
katika kitabu cha Ufunuo 17:14 “ Hawa watafanya vita na Mwanakondoo, na
Mwanakondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme
wa Wafalme; na hao walio pamoja naye ndiyo walioitwa na wateule, na
waaminifu”
Katika Ufunuo 19:11-16 “ Kisha nikaziona mbingu
zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye
Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Na macho
yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi;
naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Naye
amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa Neno la
Mungu. Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na
kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. Na upanga mkali hutoka kinywani
mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma,
naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu
Mwenyezi. Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake,
MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA “
Yesu Kristo ndiye
Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana.Lakini tunaposoma Hadithi sahihi
za Kiislamu zinaeleza kuwa adui mkubwa wa Allah (s.w) Mungu
wanayemwabudu Waislamu, ni yule anayeitwa Mfalme wa Wafalme.
Sahih
Al- Bukhari, Vol.8.Hadithi Na.225, Al-Lu’lu Wal-marjan,Juzuu ya
3,Hadithi Na.1385 “Hadithi ya Abu Huraira (r.a) amesema,Mtume wa Allah
(s.a.w) amesema,”Majina yaliyo dhalili mno na mabaya mbele za Allah ni
mtu kujiita,Malikil-Amlaak (Mfalme wa Wafalme).”
Hivyo, ufunuo
aliopokea Muhammad, ambao anatutaka na sisi Wakristo tuuamini haujatoka
kwa Mungu tunayemwamini sisi Wakristo, yaani, Yesu Kristo.Bali kama
alivyonukuliwa katika vitabu vya Kiislamu, unatokana na kuchezewa na
Shetani, na kwa sababu hiyo kwetu anakuwa nabii na mtume wa uongo’
Biblia Takatifu imetuonya kuwachunguza mitume na manabii. Katika kitabu
cha Ufunuo 2:1-2 “ Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya
ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa
kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua
matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi
kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao
siyo ukawaona kuwa waongo”
Kwa mujibu wa aya hizi Muhammad s.a.w
hastahili kuitwa nabii na mtume wa Mungu wa Kweli, bali anaangukia
katika kundi la manabii na mitume wa uongo. Hatufai
Subscribe to:
Posts (Atom)