Tuesday, November 6, 2012

MADHARA YA MATUMIZI YA VIZUIA MIMBA


...Leo Naomba Tuwe wawazi kwa hili.Wale waliowahi kutumia njia mbali mbali za uzazi wa Mpango..kama vile 1.Vidonge vya Majira
2.Njia vijiti.
3.Sindano,
Na wameshapata madhara mpaka ikawapelekea kulazwa,kuumwa sana na matatizo lukuki.Waweke ushahidi wao humu,kutufahamisha madhara hayo.

Nilikuwa nasikiliza Radio frequency 102.00,wadada wameshuhudia matatizo waliyoyapata,ambayo imewapelekea kutaka kuanzisha shirika litwalo HATUTA NYAMAZA,Litakuwa na Wahanga wa njia hizo na watapaza sauti zao kupinga matumizi ya njia hizo.Wao binafsi wamepata madhara makubwa.
Inasemekana hata kansa ya titi,kansa ya mlango wa kizazi,husababishwa na Matumizi ya vidonge kwa Muda mrefu...
Taifa linaitaji kujikomboa
1.kifikra
2.kiuchumi
3.kiafya.

Taasisi za serikali na zisizo za serikali wanatumia hela nyingi kuhamasisha matumizi ya njia hizo kwa kutaja faida bila Madhara.

hii thread walengwa wakubwa ni Wanawake walio kwenye ndoa,Wanaume wanaoshuhudia wake zao haya yakiwapata.Kila aliepata athari atatushuhudia ili tujue na tuelewe.

Kinadharia, athari ya vidonge vya majira zinaweza kuangukia katika makundi mawili:

1) Kabla ya kujipandikiza, itakuwa na athari za kupunguza uwezo wa kusafirisha mimba katika mirija ya uzazi (fallopian tube) na hivyo huzuia mimba kujipandikiza katika mji wa mimba na hali hii inaweza kusababisha kutotambulika kwa mimba hiyo ikiharibika au mimba hiyo kujipandikiza nje ya mirija hiyo.

2) Kuharibika kwa ngozi nyororo ya tumbo la uzazi kwa namna kwamba mimba hiyo baada ya kufikia mji wa mimba, inashindwa kujipandikiza katika ngozi nyororo.

3) Kutoa mimba kunakosababishwa na mimba hiyo kushindwa kukaa katika mji wa mimba;
mimba inajipandikiza lakini baadaye ina kufa kutokana na mji huo kushindwa kuhifadhi mimba hiyo.

1. Mabadiliko ya ngozi nyororo Vidonge (Oral Contraceptives), huathiri moja
kwa moja ngozi nyororo kwa kuifanya ngozi hiyo isiweze kupokea na kutunza mimba iliyotungwa. Hali hiyo hutokea kwa sababu vidonge hivyo huharibu ngozi nyororo ambayo hufanya kazi kama kitanda cha mtoto.

Ngozi hiyo inakuwa nyembamba iliyotanuliwa, iliyochoshwa na nyamanyama zake kubaduliwa kwa kuharibu chembechembe za ngozi nyororo na kwa kuharibu chakula cha mtoto kitengenezwacho katika ngozi hiyo.

2. Mabadiliko ya Chachu ziitwazo ‘Integrin’ Chachu za ‘intergrin’ ni muunganiko wa molekule ambazo hutengeneza mazingira ya upokeaji wa mimba katika ngozi nyororo ya tumbo la uzazi. Chachu hizi zikiharibiwa, mazingira ya upokeaji wa mimba huharibiwa pia yaani, kuifanya mimba isiweze kusafiri kutoka kwenye mirija ya uzazi kwenda kwenye mji wa mimba.

3 Kuongezeka kwa mimba nje ya mji wa mimba Utafiti umeonesha kuwa wanawake wanaotumia vidonge (OC’s) wamo katika hatari kubwa ya kupata mimba nje ya tumbo la uzazi ukilinganisha na wanawake wasiotumia.

Utafiti uliofanywa katika nchi 17 zenye jumla ya vituo 33 na uliowahusu watu 2800 umethibitisha kuwa matumizi
ya vidonge, yanaongeza uwezekano wa kupata mimba nje ya tumbo la uzazi. Mimba hizi za nje ya tumbo la uzazi (ectopic pregnancy) huhatarisha sana uhai wa mama. Watumiao vidonge vya progestin (POP’s) Vilevile wamo katika hatari kubwa ya kupata mimba nje ya tumbo la uzazi. SOURCE JAMIIFORUM MEMBER

No comments:

Post a Comment