Friday, May 17, 2013

HIVI UNAJUA KUWA MAJINI (MASHETANI )NI NDUGU ZA WAISLAMU? (JINNIE (EVIL SPIRITS) HAVE SPIRITUAL RELATION WITH MUSLIMS)

HIVI UNAJUA KUWA MAJINI (MASHETANI )NI NDUGU ZA WAISLAMU? (JINNIE (EVIL SPIRITS) HAVE SPIRITUAL RELATION WITH MUSLIMS)

UTANGULIZI:
Majini ni viumbe visivyoonekana kwa macho ya kawaida ya wanadamu. Hii ni kwa sababu viumbe hivi viko katika asili ya roho ya kutokuonekana. Majini huitwa pia Ibilisi, Shetani, Pepo mchafu au Joka la zamani.

ASILI YAO:
Majini yalikuwa ni malaika kabla ya kuungana na yule Muasi Mkuu wa Mungu, yaani Lucifer aliyemuasi Mungu mbinguni na kutaka ukubwa wa kufanana na Mungu, na ndipo akatupwa huku duniani yeye pamoja na malaika zake, na huku wakiwa wamenyang’anywa utukufu waliokuwa nao hapo awali. Vita hiyo iliongozwa na Malaika Mkuu wa Mungu wa Mbinguni yaani Jehova kumtupa chini huyo malaika muasi pamoja na malaika zake. Viumbe hivyo vilivyotupwa ndivyo leo vinavyoitwa MAJINI au MASHETANI au PEPO WACHAFU au IBILISI au JOKA LA ZAMANI.

Uf. 12:7-12 “ Kulikuwa na vita mbinguni, Mikael na Malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake, nao hawakushinda, wala mahala pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa yule mkubwa nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi na shetani audanganyaye ulimwengu wote, akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema sasa kumekuwa wokovu, na nguvu na ufalme wa Mungu wetu kwa maana ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu yeye awashtakiye mbele za Mungu wetu. Mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo na kwa neon la ushuhuda wao ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Kwa hiyo shangilieni enyi mbingu, nanyi mkaao humo. OLE WA NCHI NA BAHARI! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”

Hivyo kwa mistari au aya hizo unaanza kupata taswira ya kile tunachijifunza kuliusiana na majini.

Ki- Biblia Malaika ni viumbe walio katika hali ya roho ila wanaweza kuonekana kwa umbile la mwanadamu Mw. 18:1-18, Lk 1:26-28, Kut 3:1-6

Katika Ebr 1:13-14 “ Yuko Malaika aliyemwambia wakati wowote uketi mkono wangu wa kuume hata nitakapowaweka adui zako chini ya nyayo zako? Je, hao si ROHO watumikao wakitumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?
Biblia inazidi kubainisha namna ya kuumbwa kwao
Mw. 2:1 “ Basi mbingu na nchi zikamalizika na JESHI LAKE LOTE”

Ni katika jeshi hilo ambapo tunawapata hawa viumbe vya kiroho.

Na katika Kol 1:1:16 “ kwa kuwa katika yeye vitu viliumbwa vilivyoko mbinguni na vilivyo juu ya nchi. Vinavyoonekana na visivyoonekana……”

Jeshi hilo ni huru linaweza kujiamulia lolote na ndiyo maana 1/3 ya hao roho yaani malaika waliasi na kufanya machukizo mbele za Mungu na wakafukuzwa (Uf 12:7-12) na wengine wamefungwa.

Katika Yuda 6 “ Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu amewaweka katika vifungu vya milele chini ya fiza kwa hukumu ya siku ile kuu”

Tunasoma pia katika 2 Petro 2:4
“ Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni akawatia katika vifungu vya giza walindwe hata ije hukumu”

kwa hiyo Majini ndiyo mashetani na mashetani ndiyo majini.Katika kitabu Lawi 17:7

“Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale MAJINI ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao, sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao kizazi baada ya kizazi”.

Kwa sababu majini hayo tangu yalipotupwa toka mbinguni wana wa Israel hawakuwa na ufahamu wa kutosha kuyahusu baadhi yao walijikuta wakiyatolea sadaka huku wakiamini kuwa wamemtolea Mungu sadaka. Na kumbuka kuwa mara nyingi wana wa Israel walipotoa sadaka zao nyingi zilikuwa za wanyama na hivyo kutakiwa kuchinja na kutoa damu ambayo ni sehemu kubwa ya chakula cha majini.

Katika Zaburi 106:34-40.

“ Hawakuwaharibu wtu wa nchi kama BWANA alivyowaambia, bali walijichanganya na mataifa wakajifunza matendo yao, wakazitumikia sanamu zao nazo zikawa mtego kwao naam walitoa wana wao na binti zao kuwa dhabihu kwa MASHETANI wakamwaga damu isiyo na hatia, damu ya wana wao na binti zao walio watoa dhabihu kwa sanamu za Kaanani. Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.

Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao, wakafanya uasharati kwa matendo yao. Hasira ya Bwana ikawa juu ya watu wake akauchukua urithi wake.

Hivyo kutokana na kutokuonekana kwao hayo majini yaliwahujumu wana wa Israel hata yakawasababishia wamwasi Mungu kwa kuyatolea sadaka kinyume cha Mungu wa mbinguni aliyehai.

Katika Kumb. 32:17-20.
“ walitoa sadaka kwa Pepo si Mungu, kwa miungu wasioijua, kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu ambayo baba zetu hawakuiogopa,
Humkumbuki muumba aliyekuzaa Mungu aliyekuzaa humkumbuki. Bwana akaona akawachukia kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake. Akasema nitawaficha uso wangu nitaona mwisho wao utakuwaje maana ni kizazi cha ukaidi mwingi watoto wasio Imani ndani yao.

Pia katika Math 12:43-45

“ Pepo Mchafu amtokapo mtu hupitia mahali pasipo maji akitafuta mahali pa kupumzikia asipate. Halafu husema nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka hata akifa aiona tupu imefagiwa na kupambwa, mara huenda akachukua pamoja naye pepo mengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo, na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.

Katika Biblia tunaona kipindi Yesu alipotwaa mwili na kuja duniani, hao majini, au mashetani au Ibilisi au Mapepo wachafu yalimfahamu na yalianza kulalamika mbele zake.

Math 8:28-31 “ Naye alipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo (Majini) walikutana naye, wanatoka makaburuni wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama wakapiga kelele wakisema tuna nini nawe mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya muhula wetu………………. (MK 5:1-9).

Majini hayo yanafahamu kuwa Yesu ndiye atakayewahukumu ila yalichoshangaa ni kwamba mbona amewahi kabla ya kipindi chenyewe cha yeye Yesu kuyahukumu kwenda Jehanamu ya Moto?

Yesu alikuja duniani ili kumwokoa mwanadamu kutokana na mateso ya hayo majini au mashetani kwa sabahu katika Uf. 12:12 Malaika Mikael alipokuwa anawafukuza hao malaika waasi yaani hao majini au mashetani alisema OLE WA NCHI NA BAHARI ndiyo maana Yesu ilibidi aje duniani kupambana na huyo shetani, Joka, Ibilisi kwa niaba yetu maana sisi tusingeweza na wale, majini walisema kumuambia Yesu ukitutoa tuache tukawaingie nguruwe na ngurume wale wapatao 2000 waliona bora kufa baharini kuliko kuishi na viumbe hivi majini au mashetani miilini mwao na hivyo kutimiza ujumbe wa malaika Mikaeli “ Ole wa nchi na bahari”. Baharini ni sehemu mojawapo ambapo majini huishi.

Unabii wa kuangushwa mji mkubwa uliojisifu sana (Babeli) ulipotolewa, ilitabiriwa kuwa, hayatakuwa tena makazi, bali patabaki yatafanya makazi huko.

Isaya 13:12. lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani na nyumba zao zitajaa bundi, mbuni watakaa huko, na majini atacheza huko.

Ndipo tunaposoma katika Yoh 12:31, Yesu anasema “ sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo, sasa Mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje”.

Na katika 1 Yoh 3:8
“ atendaye dhambi ni wa Ibilisi kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za Ibilisi.

Kama tulivyosoma toka sura na aya mbalimbali ndani ya Biblia kuwa majini hayo yanasubiri adhabu Biblia inatueleza atakaye yahukumu.

Math 25:31, 41 “ Hapo atakapokuja mwana wa Adamu pamoja malaika watakatifu pamoja naye…………… Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto ondokeni kwangu mliyolaaniwa mwende katika moto wa milele aliyowekewa tayari Ibilisi na malaika zake”.

Hivyo kwa mujibu wa Biblia Majini yaani mashetani ni Adui yetu na ndiyo maana alipokuja Mohammad yalianza kukanusha kuwa Mungu hana mwana ili kuwavuruga waislamu wasiijue kweli (Soma Quran 112:1-4, Al- Kahf, 18:3) ya kumwamini mwana wa Mungu Yesu.

Kwa bahati mbaya sana mambo yahusuyo majini katika imani ya Kiislamu ni tofauti sana na vile tulivyosoma katika Biblia. Ingawa Quran na Hadithi za Muhammed, Mtume wa Waislamu, Vinatutaka sisi wakristo tumwamini allah S.W. mungu anayeabudiwa na Waislamu Misitikini.

Katika Suratul Waqia 51:56.

“ Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu” katika Quran Suratul Al- Ankabut (Buibui), 29:46-47) “ Wala msibishane na watu waliopewa kitabu (kabla yenu) ila kwa yale (majadiliano) yaliyo mazuri isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao na semeni tunaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja nasi ni wenye kunyenyekea kwake”.

Waliopewa kitabu kwa mujibu wa Quran ni Wayahudi na Wakristo. Je, hoja kuwa Mungu wetu na Mungu wao wanayemwabudu kuwa ni mmoja je ni sahihi?. Tuchunguze kuhusiana na mafundisho ya Allah S.W. wa misikitini kuhusu majini ndipo tutajua ni mmoja au la!.

Muislam yeyote ili imani yake ikamilike ni lazima aamini yanayoonekana na yasiyoonekana katika Suratul Al- Baqarah (Ng’ombe Jike la Njano), 2:1-3.

“ Alif Lam Mym. Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake ni uongozi kwa wamchao mwenyezi Mungu ambao huyaamini yasiyoonekana (maadaam) yamesemwa na mwenyezi Mungu na Mtume wake) husimamisha sala na hutoa katika yale tuliyowapa.

Quran peke yake ukiichunguza utaona kuwa majini yamechukuliwa kama ni viumbe tofauti na mashetani, wanasema hivyo kwa sababu katika uislamu majini yamepewa hadhi kubwa sana na ya kipekee. Hadhi hiyo ni kwa sababu majini waliamini Quaran.

Tusomapo katika Quran Suratul al- Ahqaf, (Kichuguu cha mchanga) 46:29

“ Na (wakumbushe) tulipokuletea kundi la majini (kuja kwako) kusikiliza Quran. Basi walipoihudhuria walisema (kuambiana):- “ Nyamazeni (msikilizeni maneno ya Mwenyezi Mungu)” Na ilipokwisha (Somwa) walirudi kwa jamaa zao wakiwaonya”.

Na ndani ya Quran kuna sura nzima inayoitwa sura ya majini (Mashetani) hiyo ni sura ya 72. katika sura hiyo inasema 72:1-3, 14. “ Sema: imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini liliisikia (Qurani) likasema hakika tumesikia Qurani ya ajabu inaongoza katika uongofu. Kwa hivyo tumeiamini wala hatutamshirikisha yoyote tena na Mola wetu na kwa hakika utukufu wa Mola wetu umetukuka kabisa. Hakujifanyia mke wala mwana……………………. Nasi wamo miongoni mwetu na wamo miongoni mwetu waliokengeuka waliosilimu hao ndiyo waliotafuta uwongofu.

Kwa hiyo aya hizi zinaonyesha kuwa Quran ilipokuja ndipo majini waliposilimu. Kumbuka kuwa Quran imeanza mwaka 610 B.K kipindi ambacho Biblia tayari ili kuwepo kwa karibu karne 6.

Akifafanua asili ya majini Mwanazuoni mkubwa wa kiislamu aitwaye Abdalllah Saleh Farsy aliye kuwa Kadhi Mkuu Zanzibar, kisha akawa Kadhi Mkuu Kenya katika kitabu alichoandika kiitwacho “ Maisha ya Nabii Mohammad” ule Uk. 31 anasema “ Katika safari yake ya kurejea Taif ndipo walipomjia majini wakasilimu kama inavyoonesha haya katika Suratul Jinn. Majini ni viumbe vyepesi vinavyokaa angani. havina viwiliwili kwa hiyo haviwezi kuonekana na wanadamu ila vinapojibadili kwa umbo lenye kiwiliwili. Na vina uwezo huo wa kujibadili kwa sura ya kuweza kuonekana. WAO NA MASHETANI WANA ASILI MOJA. Kwa hiyo asili ya majini ni shetani.

Suala linalohusu malaika linawasumbua sana waislam hata hawana uhakika wake.

Tumesoma ndani ya Biblia kuwa kuna kundi la malaika waliokosa ambao ndiyo wanaoitwa majini lakini tusomapo Quran inatoa maelezo tofauti.

Quran suratul As- Sajdah, (kusujudu) , 32:13 “ Na tungelitaka tungempa kila mtu uwongofu wake (kwa lazima kama tulivyowapa malaika lakini binadamu amepewa huria ya kufanya alitakalo- lililo jema na baya).

Katika ulimwengu wa Kiislamu Malaika wote ni8 wema na wanamwabudu mungu.

Hapa ndiyo tatizo linapoanzia. Quran iliyokuja baadaye inasema malaika wote ni wema wakati biblia kitalu kilichoitangulia Quran kinasema kuna malaika walioasi na wakafukuzwa katika utukufu wa Mungu.

Katika Quran Suratul, al- Kahf, (Pango) 18:50 “ Na (Kumbukeni) tulipowaambia Malaika, Msujudieni Adamu. Basi wakamsujudia isipokuwa Ibilisi yeye alikuwa miongoni mwa majini na akavunja amri ya mola wake……..”

Katika aya hiyo tunaona ibilisi akilaumiwa kwa kutomsujudia Adamu ingawa amri ya kusujudu walipewa malaika kumbe kwa mujibu wa Quran Ibilisi alikuwa miongoni mwao hao malaika yaani na yeye akiwa malaika.

Kwa sababu Quran haina habari kuhusu malaika walioasi yaani majini ndiyo maana wanapata tabu kuhusu jambo hilo. Na ndiyo maana pamoja na kujua kuwa hayo majini ni mashetani, Muilsamu amehiari kushirikiana nayo kwa kuswali nayo msikitini. Na hata mwislamu huyu anapomaliza kusali husalimia kulia na kushoto akiwasalimia watu malaika na majini (mashetani) waliokuja kushiriki naye katika Ibada yake, soma katika (Irshadul Muslimiin, Sheikh Said Musa, Uk. 38).

Katika Tafsiri ya Quran ya Iman Jalalaini Uk. 6:151 anasema kuhusu majini “ Hao ni watoto wa Ibilisi”

Hii ndiyo sababu hata wanawake wa Kiislamu wakiwa katika kipindi cha hedhi hawaendi msikitini kwa sababu kuna majini na chakula cha majini ni damu. Tafakari kwa hiyo sifa ya hayo majini au mashetani kwa ujumla ni kuwa “ hujaribu kwa bidii sana kuwa karibu na waamini wale wanaosali, kufunga na kusoma Qurani “ (Asili ya majini, Dk. Ahmed H. Sakr Uk. 28) ndiyo maana baadhi ya waislam wao binafsi wasingependa kuwa waislamu lakini majini huwashurutisha kwenda kuswali.

Kwa sababu wao waislamu hawajui kupambanua kati ya majini ambayo ni roho chafu na wale malaika watakatifu wa Mungu Jehova, ndiyo maana hata akiwa katika sala yake hana uhakika kwa sababu huyo jinni (shetani) amemteka na anamfanyia atakavyo na yeye ni mtumwa wa huyo jinni (shetani)

Katika kitabu kiitwacho Mkweli Mwaminifu cha Sheikh Said Moosa Mohamed Al- Kindy wa Muscut Oman, juzuu 1-2 Uk 42 Hadithi Na. 74.

“ Anamwijia mmoja wenu shetani (Jini) katika sala basi anapuliza (anampuliza) katika matako yake, basi (yule mtu) inamuijia fikra ya kuwa umemtoka upepo (kafusa) naye haukumtoka, basi akiona namna hiyo asiondoke (kwenye sala}) mpaka asikie sauti ( ya kutoka upepo) au anuse harufu ( ya huo upepo uliyomtoka, ndio aondoke).

Huyo shetani, au jinni anayekuwa karibu sana na huyu mwamini wa kiislamu hamchezei tu mwislamu katika matako yake kama tulivyosoma hapo juu bali pia anapofanya tendo la ndoa .

Katika kitabu kiitwacho Asili ya Majini, cha Sheikh Dr Ahmad H. Sakr Uk. 116 anasema “ Hadithi ya Mtume inathibitisha jambo hili kuwa majini (mashetani) na watu wanaweza kuoana aliposema kwamba iwapo mtu ataingia katika uhusiano wa kindoa na mkewe anatakiwa ataje jina la Mwenyezi Mungu ajilinde kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya shetani aliyefukuzwa mbali na rehema. Vinginevyo shetani hujiviringisha katika dhakari (sehemu ya siri za mwanaume) ya mtu huyo na atashirikiana naye katika tendo hilo. Tafakari yetu kuwa hiyo jinni anayeshiriki naye tendo la ndoa pamoja naye kwa mkewe ametumwa na huyo huyo Mungu wao. Hiyo ni kesi ya ngedere kumpelekea nyani! Utashindwa tu!

• Huhakikisha haweki wazi utambulisho wake vinginevyo watu wanaweza kumkwepa au hata kukimbia. Jina lake linawatisha watu wengi. Hivyo ni vyema asijitambulishe kama ni shetani , jini.
• Huwapotosha watu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili waende naye Jehanamu, badala ya kwenda peke yake. (Kumbuka hukumu ya Yesu kwa Ibilisi na Malaika zake (Math 25:41)
• Huwakatisha watu tamaa kwa sababu hana cha kuwapa ila matumaini ya uongo (Mf Q. 52:20)
• Huhakikisha kwamba watu wanamheshimu kumfuata shetani maana yake ni kuwa mtu wa namna hiyo amejisalimisha (Kumbuka waislamu wanapowasalimia majini kulia na kushoto katika sala (Irshadul Muslimin Uk 38).
• Huhakikisha kuwa hadhihirishi jina lake kama shetani lakini kama rafiki aliyejificha anayewatakiwa mema.
• Huanzisha vurugu vinginevyo maisha yake huwa ya taabu. Huwa anafurahia kuona watu wakipigan wao kwa wao.

Katika kipengele hiki tunaposoma katika Quran, Suratul – Al- Maidah, (Meza) 5:14.

“ Na kwa wale waliosema sisi ni Wakristo tulichukua ahadi kwao, lakini wakaacha sehemu (kubwa) ya yale waliyokumbushwa kwa hivyo tukaweka baina yao (wenyewe kwa wenyewe) uadui na bughudha mpaka siku ya kiama na mwenyezi Mungu atawaambia waliyokuwa wakiyafanya”

allah S.W. ndiye anayewaletea uadui na bughudha wakristo. Yeye atakuwa nani?
Tafakari.

• Hufundisha uchawi watu wanapaswa watoe kiapo cha utii kwake kabla ya kufundisha uchawi wa aina yoyote. Elimu ya uchawi ni kuwadhuru watu wengine hasa hasa waume na wake.

Katika sehemu hii tumwangalie huyo shetani au jinni anayeruhusu na kufundisha uchawi.

Katika Suratul, al- Bagarah, (ng’ombe jike), 2:102 “ Wakafuata yale waliyoyafuata mashetani wakadai kuwa yalikuwa katika ufalme wa nabii suleimani na Suleiman hakukufuru bali mashetani ndiyo waliokufuru, wakiwa fundisha watu uchawi waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani. Na uchawi uliteremshwa kwa malaika wawili Haruta na Maaruta katika mji wa Babeli wala malaika hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie hakika sisi ni mtihani wa kutazamwa kutii kwenu basi usikufuru wakajifunza kwao ambayo waliweza kumfarakisha mtu na mkewe na mengineyo wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu……………………

Katika aya hiyo inaeleza kuwa uchawi ni kazi ya Allah na ndiye anaye idhinisha. Yeye atakuwa nani? Na pia kuna waganga wa kienyeji wa kiislamu ambao hutumia Quran katika uganga wao. Hiyo Quran na majini na uchawi, ulioletwa na Allah S.W. vina uhusiano gani? Tafakari

“ Juhudi kubwa anayoifanya shetani (Jini) ni kuleta mfarakano baina ya waume na wake. Kwa kufanya hivyo huhakikisha kuwa wanachukiana wao kwa wao. Kwa ajili hiyo huishia, katika talaka. Kwa hiyo matatizo yanajengwa katika familia hiyo. Utengano au talaka inapotokea, watoto hawawezi kulelewa kisawasawa na mzazi mmoja. Watakosa uimara katika utu wao, shetani (jinni) anapata urahisi kuingia ndani ya mioyo na akili za watoto. Atawaongoza kuelekea mahali pasipofaa na hapo anawafanya wawe wahalifu katika jamii (Asili ya majini, sheikh Dr. Ahmad H. Sakr Uk 39)

Kwa mujibu wa Quran na vitabu vya kiislam huyo anayeamuru talka ni allah. S.W. Mungu wanayemuabudu waislamu.

Katika suratul, Ahzab(Makundi), 33:49.
“ enyi mulioamini mtakapowaona wanawake wenye kuamini, kisha mkawapa talaka kabla ya kuwagusa hamna eda juu yao mtakayohesabu. Wapeni cha kuwauliza na muachane muachano mzuri”

Katika Suratul al- Baqarah, (Ng’ombe) 2:230.
“ Na kama amempa talaka ya tatu basi mwanamke huyo si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine, na mwanamume huyo mwingine akimwacha basi hapo hapana dhambi kwao mume yule wa kwanza na mwanamke huyo kurejeana wakiona watasimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu.”

Kama shetani (jinni) huleta faraka ili talaka zitokee, basi Allah S.W. yeye ameamrisha talaka kwa wafuasi wake bila kujali athari za watoto zitakazotokea. Tafakari yeye ni nani?

Kumuabudu shetani (Jini)

Katika Suratul Sabaa, 34:40-41
“ Na kumbuka siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia malaika, “ Je hawa walikuwa wakikuabuduni?” waseme umeepukana na kila upungufu! Wewe ndiwe kipenzi chetu si hao bali walikuwa wakiwaabudu MAJINI; wengi wao waliwaamini hao majini”

“ Shetani anapoamuru watu wamfuate pia anawaamuru wafanye madhambi na wakose maadili. Huwataka waseme uongo kuhusu Mwenyezi Mungu kutokana na kutokujua kwao. Wanaweza kusema kuwa sisi wanaadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mungu alijifanyisha na kuwa umbile la kibinadamu. Mungu amezaa, na mwanaye niwa pekee. Zaidi ya hayo mwanaye si mtoto tu bali ni Mungu pia. Huyo mwana ni Bwana Yesu. Asiyeamini hivyo huchukulika kuwa ni kafiri au muasi hivyo ameangamia na atakwenda jehanamu” (Asili ya Majini, Sheikh Dr. Ahmad H. Sakr Uk 54)

Hapa ndipo sura halisi ya huyu shetani yaani jinni inapojitokeza. Yesu alipokuwa duniani kabla Muhammad hajazaliwa, wala Uislamu haujaanzishwa na Mohamed wala Quran haijaandikwa na wale waarabu wanne Seyidna Abubakar, Omar, Othuman na Ally, Majini yaani mashetani yalipomuona Yesu yalimwita “ Mwana wa Mungu tuna nini nawe? Je, umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? (Math 8:28-31) Mwaka 610 B.K majini hayo hayo yakaanza kuwadanganya waislamu kuwa Mwenyezi Mungu hana mwana (Quran 72:1-3) Na bila kuitafakari. Nao wao wanaamini tu kuwa Quran ni maneno ya Mungu bila kupambanua huyo ni Mungu yupi!!.

Katika Suratul An- Nisaa (Wanawake) 4:120

“ Shetani hawaahidi ila uwongo…………..”

Hii ndiyo sababu Mohammad mtume wa waislamu katika kitabu “ Wakeze Mtume Wakubwa na Wanawe kilichoandikwa na Sheikh Abdallah Saleh Farsy Uk. 12, Mohammad anasema:-

“ Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na mashetani na kuni haribu akili yangu na kunizuga………………”

aliyasema maneno hayo baada yakubanwa na shetani (jinni) kule pangoni alikokuwa na baada ya hapo akaanza kujiita mtume. Hoja yetu ni mtume wa nani?

Katika Kitabu cha Ibn Ishaq 132-133
“ Kama huyu shetani (jinni) ambaye amekupagaa wewe ni yule ambaye huwezi kumtoa, tutamtafuta mganga na tutatumia vyote tulivyonavyo kukutibu kwa kuwa mara kwa mara shetani (jinni) humpagaa mtu. Lakini anaweza kuondolewa. Mtume alikuwa akisikiliza kwa makini”

Kisha baadaye na yeye Mohammad katika Sahihi Muslim Juzuu 4 Hadithi na. 2814 kasema
“ Wala hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa amepewa nguvu zinazotokana na majini. Wakasema (maswahaba) hata wewe mtume wa allah? Akasema hata mimi isipokuwa allah hunirahisishia juu yake hunyenyekea wala hayaniamrishi ila yaliyo mazuri”

Kwa hiyo majini ni ndugu za waislam Q. 46:29- ufafanuzi wake. Katika kitabu Asili ya Majini cha Sheikh Dr. Ahmad H. Sakr Uk 80 anasema “ Imepokewa na Khalid Ibn Walid kuwa kuna wakati alipatwa na ukosefu wa usingizi basi mtume (S.A.W) akamwambia “ Nikufundishe maneno ambayo ukiyasema utapata usingizi? Sema Ewe mola! Wewe ni mola wa mbingu saba na kile kilichofunikwa nazo. Nawewe ni mola wa ardhi na kilichomo humo. Nawe ni mola wa mashetani (majini) na maovu yao. Nakuomba uwe mlinzi wangu dhidi ya viumbe vyako vyote………..”

Hadithi hii inaonesha jinsi allah S.W. alivyo na uhusiano wa karibu na mashetani. Je, yeye ni nani?. Pia katika Q: 21:82, 34:12, 38:37 zinaeleza Allah alivyomtishia majini suleiman na yeye akiwa mlinzi wao hata kuwaadhibu wasiofanya vizuri.

Katika Quran 19:83 “ Je, huoni ya kuwa tumewatuma mashetani juu ya makafiri wanaowachochea kufanya mabaya?”

Katika Sahihi Muslim vol. IV H. 2667, Sahihi Al Bukhari Vol Vii H. 6243, Sunan Abuw Daud Vol II H. 2152.

“ Hakika Allah amemkadiria kila mtu kipimo chake cha zinaa, ambavyo haikosi kutimia kwake”

Tumeona kuwa majini au mashetani au pepo mchafu au Ibilisi walikuwa malaika walioasi walipotupwa chini huku duniani walitaka kurudi huko mbinguni lakini walishindwa.

Katika Q 72:8-10 (majini) majini yanasema

“ Nasi tulizigusa mbingu (tulikwenda mbinguni) tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na nyota (zing’arazo) na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza lakini anayetaka kusikiliza sasa atakuta kimondo (kijinga cha moto) kinamvizia. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa katika ardhi au mola wao anawatakia (heri).

Moja kati ya majina ya Allah ni AL-MUQADIM yaani, wa zamani (majina 99 ya Allah) majini yanajieleza kuwa hayajui Mungu wao ana watakia mazuri au mabaya wale wakaao duniani.

Mungu wa mbinguni anasema katika Biblia kitabu kilichokuweko kabla ya Quran.

Yer. 29:11 “ Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi asema BWANA ni mawazo ya mani wala si ya mabaya kuwapa nyinyi tumaini siku zenu za mwisho.

Majini (mashetani) yanajua tu kuwa Yesu atayahukumu na hayajui lolote kuhusu mpango wa Mungu kumwokoa mwanadamu toka kwa shetani (majini)

Mtume Paul katika 2 Kor 11:14 “ Wala si ajabu shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa Nuru…………..” Pia katika 1 Tim 4:1 “ Basi roho anena wazi wazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine (waislamu) watajitenga na imani wakisikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani (majini)” Tafakari Kuu: Allah katuma mashetani (majini) wako katika dini yake ya uislamu, yeye mwenyewe pamoja na wafuasi wake walikuwa wakifanyia kazi Suleiman wa ndani ya Quran na yeye allah S.W. akiwa msimamizi (Foreman) wao, mwisho wao wote pamoja na allah S.W. mwenyewe ni katika Jehanamu ya moto.

Yeye Allah atakuwa nani??? Tafakari wewe ndugu yangu Mkristo shika sana ulichonacho asije mtu akakunyang’anya!!!.

Na wewe rafiki yangu mwislamu okoa roho yako. Nenda kanisani ukajisalimishe upate nusura ya Mwenyezi Mungu!!

No comments:

Post a Comment