Somo: Dhiki kubwa
Tunajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele saba.
( i ). Dhiki tofauti na zote
( ii ). Muda wa dhiki kubwa
( iii ). Majina yanayotumika kuzungumzia dhiki kubwa
( iv ) Watakaohusika kuileta dhiki kubwa
( v ). Makusudi ya dhiki kubwa
( vi ) Hali itakavyokuwa wakati wa dhiki kubwa
( vii ). Jinsi ya kuikwepa dhiki kubwa
( I ). DHIKI TOFAUTI NA ZOTE
Wanadamu hapa duniani, wanapitishwa katika dhiki za namna namna.
Wanapitishwa katika mateso ya namna namna. Wengine wanapitishwa katika
hali nzito ya njaa nchi nzima hali inakuwa mbaya. Nchi ambazo zimewahi
kushuhudia njaa kali kama Ethiopia na Somaria, watu watakondeana na
kubaki mbavu kabisa. Njaa itakuwa kali kiasi kwamba hata ukipita mjusi
watatamani kuurukia waweze kuula lakini hata nguvu za kuurukia mjusi
zinaweza kukosekena . Watu wengine watafukiwa na vifusi sehemu zile za
India kutokana na matetemeko. Wengine wataweza kupelekwa mbali kwa
kurushwa na vimbunga. Dhiki ulizozipata kwa kuanguka katika maporomoko,
kwa kupanda milima mirefu kwa shida, hizo siyo dhiki ukilinganisha na
dhiki kubwa itakayouijilia ulimwengiu. Dhiki wanazozipata wanadamu kwa
kutupwa magerezani na kuteswa na kuumizwa sana, wengine wakiwekwa katika
viti ambavyo watateswa sana na polisi ili waweze kueleza yale
waliyoyafanya. Watakazwa sehemu zao za siri, watachomwachomwa kwa vitu
vyenye ncha kali, watapigwa mijeredi kwa kuwekewa pilipili kwanza sehemu
za siri. Hizo siyo dhiki kabisa ukilinganisha na ukilinganisha na dhiki
itakayokuja baada ya kanisa kunyakuliwa. Watu waliookolewa nao
wanaweza kupita katika dhiki za namna namna hapa duniani kama vile
kutengwa na wazazi, kupigwa na wazazi, kupigwa na mume au mke kwasababu
ya wokovu. Wengine watafungwa, watapigwa mawe hata kuuliwa, hizo ni
dhiki kidogo tu. Yesu Kristo alisema “duniani mnayo dhiki lakini jipeni
moyo, mimin nimeushinda ulimwengu”.Sikuja kuleta amani bali upanga
watakuwepo watu watakaofarakana pamoja nanyi, amani itavurugika”. Dhiki
unazozipata kwa sababu umeokolewa hizo ni dhiki kidogo sana. Dhiki
hizo zinaitwa dhiki nyepesi katika biblia.
( 2 WAKORINTHO 4:17 ). Watu
wote waliookoka walipita katika dhiki za namna namna kwasababu ya
wokovu ili waukane wokovu wao. Wamkane Yesu Kristo aliyewaokoa. Wengine
walikatwa vichwa na wengine kusulibiwa kwa namna nyingi. Hayo mateso na
mengine mengi waliyoyapata ni dhiki nyepesi ukilinganisha na dhiki
kubwa itakayouijilia ulimwengu. Dhiki itakayouijilia ulimwengu inaitwa
dhiki kubwa kwasababu ya mateso makubwa yatakayokuwepo
( MATHAYO 24:21 ). Wahubiri wengine wanaiita dhiki kuu lakini kitu kinachotajwa hapo ni dhiki kubwa lakini ni kitu kilekile.
(DANIELI 12:1).
Utaweza kuona watu watakaookolewa katika dhiki hii kubwa kuwa ni
Waisraeli tu kutokana na agano ambalo Mungu Alilifanya na baba zao
(Ibrahimu, Isaka na Yakobo).
( II ). MUDA WA DHIKI KUBWA
Dhiki kubwa inatajwa kwamba itakuwa kwa muda wa juma moja la Danieli.
Itakuwa kwa muda wa juma moja la Danieli, juma la savbini. (
DANIELI 9:24-27 ) “Neno juma moja
( DANIELI 9:27)”. Juma Moja linalozungumziwa hapa ndiyo kipindi cha dhiki kubwa. Katika unabii juma moja linazungumziwa kumaanisha miaka saba
. (MWANZO 29:27)
“Timiza siku zako saba, inamaanisha timiza miaka yako saba”. Juma moja
la Danieli linalozungumziwa ni miaka saba ya dhiki kubwa.
Miaka saba ya dhiki kubwa itakuwa imegawanywa katika sehemu kuu
mbili na kila sehemu itakuwa na kipindi cha miaka mitatu na nusu au muda
wa miezi arobaini na mbili
(miezi 42) au siku zipatazo 1260.
Kutakuwa na mambo yatakayotokea katika miaka mitatu na nusu ya mwanzo na
mambo yatakayotokea katika kipindi cha miaka mitatu na nusu iliyosalia
(UFUNUO 11:2-3), Miezi arobaini na mbili (
miezi 42) na siku elfu moja na mia mbili na sitini nazo zimetajwa zikimaanisha miaka mitatu na nusu. (
UFUNUO 13:5). Katika andiko hili inatajwa tena miezi arobaini na mbili
(miezi 42)
ambayo ni sawa na miaka mitatu na nusu ya kwanza katika kipindi cha
miaka saba ya dhiki kubwa. Baada ya kufahamu vipindi hivi viwili vya
dhiki kuwa ni muhimu kufahamu jinsi itakavyokuwa katika vipindi hizi
viwili tofauti.
Katika kipindi cha kwanza cha miaka mitatu na nusu (miezi arobaini na
mbili) ya mwanzo, mpinga kristo atafanya agano pamoja na wana wa
Israeli. Atafanya agano na Taifa la Israeli na watadanganyika kwa kiasi
kikubwa. Katika kipindi hicho cha miaka titatu na nusu ya mwanzo,
kutakuwa na nafuu kwa wana wa Israeli kutokana na agano hilo la uongo
ambalo hatimaye litavunjwa na mpinga kristo mwishoni mwa kipindi hiki..
Katika kipindi cha pili cha dhiki kubwa cha miakamitatu na nusu, dhiki
itaongezeka hususani kwa wana wa Israeli. Wakati huo agano la mpinga
kristo na wana wa Israeli litakuwa limeshavunjika. Kwa nini dhiki
itaongezwa kwa wana wa Israeli na kwa makusudi gain? Tutaona sababu hapo
mbele kidogo.
( III ). MAJINA YANAYOTUMIKA KUIZUNGUMZIA DHIKI KUBWA.
Yapo majina mbalimbali yanayotumika kuizungumzia dhiki kubwa na
tunapokutana nayo tunaweza kuyachanganya na kufikiri yanazungumzia kitu
mambo mengine kumbe yanazungumzia mambo haya. Majina hayo ni :-
( A ). Ghadhabu itakayokuja.
( 1 WAKORINTHO 1:10 )
Tunaweza tukaokolewa na ghadhabu itakayokuja yaani dhiki kubwa.
Kanisa, watu waliookolewa hatutakuwepo wakati huo wa ghadhabu ya Mungu
kwa wenye dhambi walioukataa wokovu wa Yesu.
( B ). Saa ya hukumu.
( UFUNUO 14:7 ).
Wakati wa dhiki kubwa utakuwa ni wakati wa hukumu kama tutakavyoweza kuona hapo mbele kidogo
( C ). Adhabu na ghadhabu.
( ISAYA 24:21; ISAYA 26: 21)
Hapa inazungumziwa dhiki kubwa na siyo kitu kingine
( D ). Saa ya kujaribiwa.
( UFUNUO 3:10 )
Saa ya kujaribiwa itakayoujilia ulimwengu wote ni kipindi cha dhiki kubwa.
( E ). Tabu yake Yakobo.
( YEREMIA 30:7 ).
Andiko hili linazungumzia tabu watakayo wapata hususani wana wa
Israeli. Israeli mwanzo iliitwa Yakobo. Tabu yake Yakobo au Tabu yake
Israeli. Tutaweza kuona jinsi wana wa Israeli watakavyookolewa kipekee
katika dhiki kubwa.
( F ). Uangamivu.
( YOELI 1:15 ).
Utakuwa ni wakati wa kuangamizwa kwa wanadamu.
( G ). Siku ya giza na weusi , siku ya mawingu na giza kuu.
( YOELI 2;1-12).
Watu watakaokuwepo duniani kwenye dhiki kubwa watageuka nyuso zao,
nyuso zitakuwa nyeupe sana kwa hofu. Jasho jembamba lililojaa
chumvichumvi litakuwa limewafunika na watakuwa kama wamepakazwa chumvi
kutokana na hofu na matetemo watakay0kuwa wameyapata.
( IV ). WATU WATAKAOHUSIKA KUILETA DHIKI HIYO KUBWA
Dhiki hii itakuwa kubwa sana kutokana na watatu watakaohusika kwa
wanadamu Itakuwa ni ole kwa yule atakayekuwa ameachwa na kukabiliwa na
hatari itakayokuwa inaujilia ulimwengu. Watatu hao ni akina nani? Watatu
hao ni Mungu, Shetani na Mpinga Kristol.
( i ). M
ungu.
Mungu atahusika kikamilifu kuileta ghadhabu na mapigo kwa watu.
( ISAYA 26:21 )
“Mungu atakuwa anawaadhibu wanadamu walioukataa wokovu”
(UFUNUO14;7 ) Ni hukumu ya Mungu.
(UFUNUO15:7 ) Ghadhabu ya Mungu.
Jaribu kuwaza hapa ni Mungu anashusha ghadhabu yake.
( ii ) Shetani.
Ghadhabu kubwa ya Shetani itashushwa kwa wanadamu. Sasa hivi tunaona
jinsi Shetani anavyosababisha magonjwa ya kila namna , akisababisha
ajari, akiwafanya watu wawe vilema, washindwe kutembea , akiwafanya
watu wapooze, kuleta majipu juu ya watu kama kwa Ayubu. Hayo anayafanya
sasa lakini ghadhabu yake bado haijaja. Shetani atawashukia watu
watakaobaki duniani kwa ghadhabu nyingi akijua kwamba wakati wake
uliobaki kabla ya kutupwa katika ziwa la moto milele na milele utakuwa
unaendelea kuwa finyu au mchache. Kwa hiyo, Shetani atashuka akiwa na
ghadhabu nyingi kwa wanadamu wenye dhambi ambao waliukataa wokovu na
kuachwa wakati wa unyakuo wa kanisa
( UFUNUO 12:12 ). Si hao tu wawili, yupo wa tatu.
( iii ). Mpinga Kristo
Leo tunawapinga Kristo wengi duniani, watu wanaosema Yesu siyo Mwokozi ni wapinga
Kristo,
wanaosema hakuna kuokoka duniani ni wapinga Kristo, wanaosema Yesu siyo
mwana wa Mungu, wanaosema hakuja katika mwili, ( Mungu ) ni wapinga
Kristo. Watu wote waoyapinga maandiko matakatifu ya Mungu katika biblia
takatifu woye ni wapinga Kristo hata kama wanajiita kuwa ni wakristo.
Wapinga Kristo wa namna hii wapo wengi sana duniani bado wanaendelea
kufanya kazi zao lakini yupo mmoja Mpinga Kristo anayekuja
( 1 YOHANA 2:18 ). Angalia neno
“Mpinga Kristo yuaja” huyo anayetajwa ni mmoja ajaye.
Pia kuna wapinga kristo wengi ambaowamekwisha kuwapo. Yupo mmoja
anayeitwa Mpinga Kristo kwa namna ya tofauti na Wapinga Kristo wengi wa
sasa. Yupo mpinga Kristo ajaye, anajulikana kwa majina tofauti katika
biblia zetu.
( i ). Mpingamizi
( ii ) Asi
( iii ) Chukizo la uharibifu
( iv ) Mnyama
Kwa nini anaitwa mnyama?
Anaitwa mnyama kwasababu atakuwa ni mkatiri sana kama wa wanyama
wakali walivyo. Kama jinsi Simba asivyokuwa na huruma, anavyoweza
kumchana Paa. Kama Mbwa mwitu asivyovyokuwa na huruma, kama Chui, Dubu
wasivyokuwa na huruma ndivyo atakavyokuwa. Ukatiri wa kinyama atakaokuwa
nao unamfanya kuitwa Mpinga Kristo kuitwa Mnyama.
( 2 WATHESALONIKE 2:1-8 ).
Kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo hakuji mpaka afunuliwe kwanza
mpinga Kristo ( ufunuliwe ukengeufu ). Hapa ndipo watu wanapochanganya
mambo. Ndiyo maana tunapaswa kujifunza kweli ili tupate kuifundisha kwa
wengine.
Kuna kuja kwa Yesu mara ya mara mbili tofauti. Kuja kwa Yesu duniani
kwa mara ya kwanza kulitimia alipozaliwa duniani kama mwanadamu lakini
kuja kwa Yesu mara ya pili kutatokea baada ya miaka saba ya dhiki kubwa.
Yesu atakuja duniani kutawala kwa miaka elfu moja na ndiyo maana
atashuka kwa utiosho mwingi nautukufu mwingi tofauti na alipokuja mara
ya kwanza ambapo wanadamu waliweza kumpiga, kumburuta na kumtemea mate.
Alipokuja mara ya kwanza alikuja katika udhaifu kwa kuzaliwa katika
hori ya ng’ombe na kuishi maisha ya kimaskini. Atakuja kama Mfalme wa
wafalme na Bwana wa mabwana na hapo ndipo kila jicho litamwona na kila
ulimi kukiri kuwa Yesu ni Bwana. Yesu atakuja na watakatifu ( kanisa )
aliowatwaa miaka saba iliyopita na watatua katika mlima mzeituni
alipoondokea wakati anakwende mbinguni akiwa katikati ya wanafunzi wake .
Yesu atakuja akiwa amempanda Farasi mweupe. Ikimbukwe kuwa miaka saba
hiyo mbinguni kulikuwa na harusi ya mwana kondoo ( Yesu ) na watu
watapokea taji mbalimbali kutokana na kazi waliyofanya wakiwa hapa
duniani. Wakati wa unyakuo wa kanisa siyo wakati wa kuja kwa Yesu mara
ya pili duniani maana Yesu hatatua juu ya uso wa dunia. Baada ya
parapanda kulia watakatifu watatwaliwa kama kwa sumaku na kumlaki Yesu
mawinguni. Yesu atakuwa mawinguni pamoja na mwaliko wa malaika wake.
Siku hiyo hakuna aijuaye lakini kuja kwake mara ya pili duniani itakuwa
baada ya kipindi cha dhiki kubwa yaani miaka saba. Andiko
linalochanganya watu ni
( 2 WATHESALONIKE 2:1-8 ) ambalo lina
maana kuwa, kuja kwa Yesu kutawala dunia miaka elfu moja ni mpaka
afunuliwe kwanza mpinga Kristo ambaye kutawala kwake ni miaka saba.
Lakini huyo mpinga Kristo bado hajafunuliwa kanisa ndilo limezuia
kufunuliwa kwake. Kanisa likinyakuliwa ndipo natakapofunuliwa.
( MATHAYO 24:25 ; UFUNUO 13:1-6)
Mnyama anayetajwa hapa ni Mpinga Kristo atakayekuwa na ukali wa
kinyama Anatajwa kutoka katika bahari. Je, ni bahari gain? Bahari
inayotajwa hapo katika unabii inamaana ya kusanyiko kubwa la watu.
Mahali lilipo kusanyiko kubwa la watu linaitwa bahari
( ISAYA 57:20 )
Wabaya wengi kwa pamoja wote wanaitwa bahari. Sehemu nyingine
inayosema “bahari ikawatoa wafu wake” ina maana ya dunia kuwatoa wafu
wake. Mnyama au mpinga Kristo anatajwa kutoka katika bahari, maana yake
atatoka katikati ya watu walioopo duniani. Huyo mnyama atakuwa ni mtu
kabisa na kwasababu tuko ukingoni mwa haya mambo kutokea inamaana huyo
mtu yupo sasa anangoja kaniosa linyakuliwe ndipo apate kufunuliwa
( UFUNUO 13:1-6 ).Vichwa, Pembe Vilemba ni alama ya nguvuna utawala.
( UFUNUO 17:3, 9-13 )
Ufalme na mamlaka ya kipekee ndiyo nyanazungumzia vilemba saba. Mnyama (
mpinga Kristo ) anatajwa kufananishwa na Chui, Dubu na Simba ambao ni
wanyama wakali sana. Ukatiri wa Chui, Dubu na Simba umo ndani ya mpinga
Kristo Mpinga Kristo atakuwa na mamlaka ya Kishetani, mamlaka ya kifalme
ambayo itamfanya kushirikiana na wafalme duniani ( maraisi )
watakaokuwepo . Kuna wafalme ambao hata falme zao zinazidi kuimarika na
hao watampa nguvu sana ya kiuchumi , nguvu ya kivita na kumfanya awe
tishio kwa wanadamu na watu wote dunia yote watalazimika
kumsujudia.
Watu wanaofundisha kwamba kanisa litakuwepo wakati wa dhiki kubwa,
hawataki watu wajiandae vizuri ndilo lengo la Shetani kuyaleta
mafundisho hayo. Kwamba tutapita kwenye dhiki hivyo hatuna haja ya
kujiandaa kwa lolote. Hao walimu wanaofundisha hivyo wanachanganya
mafundisho.
Mpinga Kristo atakuwa amepewa uwezo wa kishetani kama tulivyosoma
( UFUNUO 13:1-8 ). Kutokana na ishara zake na mateso yake atawafanya watu wengi walioachwa kumwabudu Shetani au siyo kuuawa
( UFUNUO 13:13-17 )..
Kwasababu atakuwa na mamlaka ya kipekee atawafanya watu wengi
wamsujudie . Mtu ambaye hatakubali chapa ya mnyama ambayo ni namba 666
Hataweza kununua wala kuuza na akikubali atalazimika kumsujudia huyo
Mnyama aliyepewa mamlaka na Shetani. Mwenye akili na afahamu. Yesu
alisema, “mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu hamkunipokea lakini
atakuja mwingine kwa jina lake mtampokea”
( YOHANA 5:43 ).Watu
wengi wanaomkataa Yesu leo watalazimika kumkubali mpinga Kristo kutokana
na mamlaka atakayokuwa nayo na unabii kuhusiana na hilo lazima
utatimia. Wanadamu wengi watampokea na kumsujudia wakifikiri kuwa yeye
ndiyo msaada na mkombozi wao kumbe watakuwa wanazidi kuharibikiwa.
( V ). MAKUSUDI YA DHIKI KUBWA
( I ). Kuliandaa Taifa la Israeli kumpokea Yesu Kristo kama masihi wao.
Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu alijifunga katika agano au ahadi na
ahadi za Mungu haziwezi kutanguka. Mungu alijifunga katika agano kwamba
Israeli wote wataokolewa.. Alipokuja kwa ajili yao ( Israeli )
hawakuweza kumpokea kabisa
( YOHANA 1:11 ). Yesu alikuja kwa
ajili ya wana wa Israeli lakini hawakumpokea ndipo akawageukia mataifa.
Mungu alishajifunga katika agano na baba zao kuwa atawaokoa wote.
Makusudi ya dhiki kuu ni kuwatesa waisraeli na kwa mateso hayoi
watamkiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wao Dhiki hiyo kubwa
itawatesa sana waisraeli lakini wote watakaokuwa wamefuata masherti
kama alivyosema Bwana wetu Yesu. Wote watakaokimbilia milimani kwa
kukimbia kukwepe kumsujudia Mnyama ( Mpinga Kristo ) na kukwepe namba
yake 666, hao wote ndio watakaookolewa Yesu atakapokuja mara ya pili
duniani kwa ajili ya utawala wa miaka elfu moja pamoja na watakatifu.
Hawa ndo watakatifu wanaotoka katika dhiki kubwa. Biblia inaposema siku
zitafupishwa kwa ajili ya watakatifu ni hao wanaotoka katika dhiki na si
vinginevyo
( MATHAYO 24:21-22 ). Hawa wanaotajwq ni watakatifu
wanaotoka katika dhiki kubwa na siyo sisi tuliookolewa leo. Baada ya
wana wa Israeli kuokolewa (watakatifu waliotoka katika dhiki )
wataungana na watakatifu ( kanisa ) ambao watakuja na Yesu ili kutawala
pamoja nae. Watakatifu watakaotoka kwenye dhiki wataungana na wale ambao
Yesu aliwatwaa duniani wakati wa unyakuo wa kanisa miaka saba iliyopita
dhiki kubwa ikiendelea duniani na wote kwa pamoja watatawala na Yesu
duniani kwa miaka elfu moja..
AGANO LA MUNGU NA WANA WA ISRAELI ( KUMBUKUMBU LA TORATI 4:30-31 ).
Wakishakupatwa na mambo hayo yote wakati wa dhiki kubwa, hatimaye Taifa
la Israeli litamrudia Bwana. Mungu alijitambulisha kwao kuwa yeye ni
Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Mungu hatasahau agano aliloagana na
baba zao Ibrahimu, Isaka na Yakobo
( YEREMIA 30:7). Yakobo ni
Israeli. AGANO LA MUNGU NA WANA WA ISRAELI ( EZEKIELI 20:37; YEREMIA
30:7; TORATI 4:30-31) UFAFANUZI WA AGANO LA MUNGU NA WAISRAELI
( WARUMI 11:25-27 ). Paulo mtume aliyepewa wingii wa mafunuo kwake tunajifunza mambo ya siku za mwisho
( WARUMI 11:25-27 )
Utimilifu wa mataifa uwasili inazungumzia kunyakuliwa kwa kanisa.
Majira tuliyonayo sasa yanaitwa majira ya mataifa. Kwasababu ni wakati
wa majira ya mataifa ndiyo maana sasa wana wa Israeli ni wagumu sana
kuukubali wokovu. Kuhubiri injili Israeli ni ngumu sana kuliko sehemu
nyingine yoyote duniani
( WARUMI 11:25-27, 27-32 ). Hivyo Israeli wote wataokoka.
Katika miaka mitatu na nusu ya kwanza, wana wa Israeli watakuwa na
unafuu kutokana na agano la uongop ambalo watakuwa wamelifanya na mpinga
Kristo Lakini miaka mitatu na nusu iliyosalia , chukizo la uharibifu
litasisimama kikamilifujuu ya Israeli
( DANIELI 9:27; MATHAYO 24:15-21
). Baada ya miaka mitatu na nusu ya kwanza, mpinga Kristo atavunja
agano lake paoja na wana wa Israeli. na kuwatesa kipekee ili wao nao
wakubari kumsujudia Mpinga Kristo kama mataifa mengine wanavyofanya.
Maandiko hayo yanawazungumzia wayahudi na siyo sisi watanzania ( mataifa
). Biblia katika
( MATHAYO 24: 16 ) inasema kuwa waliop[o
uyahudi wanapaswa kukimbilia milimani ili kukwepa kumsujudia Mnyama.
Hapa Yesu anazungumzia watu wa Uyahudi ( Israeli ). Hao watakaoikwepa
namba
666 ndio watakatifu wanaotoka katika dhiki kubwa. Yesu
anasema ole ni kwa Wanyonyeshao, wenye mamba maana hao watashindwa
kumkimbia Mpinga Kristo na kukamatwa na majeshi yake. Pia anawaambia
Waisraeli waombe siku hiyo isitokee siku ya sabato maana waisraeli ni
washika sabato. Katika sabato huwa kuna mwendo wa sabato
( MATENDO 1:12 ).
Wakati wa sabato, mtu anatakiwa kutembea mwendo wa sabato chini kidogo
ya maili moja.. YUmbali kutoka mlima zeituni hadi Yerusalemu ni mwendo
wa sabato. Waisraeli wanatakiwa kuomba siku hiyo isitokee siku ya sabato
wasije wakashika sheria ya sabato ya kutembea mwendio chini kidogo ya
maili moja na kushindwa kumkimbia mpinga Kristo
( MATHAYO 24;21-22 ).
Siku za dhiki kubwa zimefupishwa kwa ajili ya wateule ambao Mungu
amekusudia kuwaokoa kutokana na agano ambalo tuekwisha kuliona. Walimu
wengine wanachanganya kwasababu ya neno wateule wanafikiri kuwa neno
hilo linazungumzia sisi tuliookolewa leo. Neno mteule linapotumika
katika biblia, linatumika katika namna nne tofauti:-
( I ). Yesu Kristo
( ISAYA 42:1 )
( ii ). Malaika wateule
( 1 TIMOTHEO 5:21 )
( iii ) Sisi tuliookoka (
TITO 1:1; 1 PETRO 1:1-2; WARUMI 8:33; LUKA 18:7 )
( iv ) Wateule vilevile ni Taifa la Israeli
( ISAYA 65:8-9; ISAYA 45:4 )..
Tunatakiwa kupambanua vizuri ili tusichanganye mambo na kujikuta tunafundisha watu uongo bila kujua
( YAKOBO 3:1 ).
( II ). Kuleta hukumu ya adhabu kwa watu wote ambao
hawakuukubali wokovu ( waliokuwa wakisema hakuna kuokoka duniani na
kumkataa Mwokozi Yesu anayeokoa)
( ISAYA 26:20-21; 2 WATHESALONIKE 2: 7-12 )
Kwasababu hawakutaka kuipenda ile kweli wapate kuokolewa, ghadhabu ya Mungu itashuka kwao.
( 2 WATHESALONIKE 2:10-12 )
Nguvu ya upotevu ni nguvu ya mpinga Kristo na ishara zake. Watu wote
walioukataa wokovu , Mungu mwenyewe atawaletea nguvu ya upotevu ili
wauamini uongo wa mpinga Kristo wasije wakaokolewa. Mataifa mengine
yote isipokuwa Israeli pekee, watampokea mpinga Kristo, watamwabudu,
watamsujudia na wataipokea chapa yake ya 666. Watu ambao siyo waisraeli
hawatakuwa na nafasi ya kutubu na kuokolewa. Majira ya mataifa
yatakuwa yamekwisha kupiita wakati wa unyakuo wa kanisa.. Wakati
tulionao ndio wakati ambao ni majira ya mataifa, tunaweza kuokoka sasa
kwa kuwa parapanda ya Bwana kwa ajili ya unyakuo wa watakatifu ( kanisa )
bado haijalia. Yesu Kristo alikuja kwa waliowake (Waisraeli ) lakini
waliowake wakamkataa ( hawakumpokea )
YOHANA 1:11. Ndipo alipoamua kuwageukia mataifa
( MATHAYO 28:19-20; MATENDO 1:8 )..
Wakati tulionao ni wakati wa neema kwa mataifa ( hatukustahili ) lakini
kanisa likinyakuliwa utakuwa ni utimilifu au mwisho wa neema ya wokovu
kwa mataifa. Huo unaitwa utimilifu wa mataifa
( WARUMI 11:25-32
).. Katika andiko hilo kuna siri kubwa sana na ni siri ambayo shetani
hataki watu waijue ili wazidi kudanganyika eti na mataifa wataokoka
katika dhiki kubwa kumbe siyo kweli. Mataifa yote isipokuwa Israeli
tumepewa nafasi moja tu ( one chance ) na hakutakuwa na wokovu kwa
mataifa.
( VI ). HALI ITAKAVYOKUWA WAKATI WA DHIKI KUBWA
Itakuwa ni kilio na kusaga meno. Kutakuwa na mateso na dhiki ambayo
yatafanya watu wauawe na damu yao kumwagwa kama mavumbi na nyama yao
kama mavi. Hatakuwepo mtu wa kumlilia mwenzake wala wa kuzika mwenzake,
wote watakuwa katika hali nzito ya mateso na dhiki kuu ambayo haina
mfano wake. (
SEFANIA 1:15, 17-18 ). Dhiki italetwa
kwasababu watu wamemtenda Bwana dhambi, huu ni uthibitisho kwamba sisi
tuliookolewa leo hatutakuwepo wakati wa dhiki kubwa.. Watu watateswa
mateso makuuu na wengi watakufa na miili yao haitazikwa maana kila mtu
atakuwa katika dhiki hiyo na hakutakuwepo na mtu wa kumlilia mwenzake
maana kila mmoja atakuwa anajililia mwenyewe. Miili ya watu watakaouawa
itakuwa samadi juu ya uso wan chi (
YEREMIA 25:33). Watu leo
wanatenda dhambi na utadhani Mungu hayoko lakini hasira yake Mungu
imewekwa akiba , iefichwa kwa ajili ya wakati ule wa dhiki
kubwa (
SEFANIA 2:1-3 ) Akiba ya hasira ya
Mungu itafunuliwa wakati wa dhiki kubwa. Leo mtu anaweza kusema hakuna
kuokoka, hakuna Mungu, Yesu siyo Mungu, Yesu hakuja katika mwili n.k,
lakini siku ile utalia sana na kusaga meno kutokana na mateso
yatakayokuwepo ambayo hayana mfano wake tangu kuumbwa kwa ulimwengu na
hayatakuwako tena.
MAPIGO YATAKAYOMWAGWA JUU YA WANADAMU WAKATI WA DHIKI KUBWA
Mapigo saba ( vitasa saba vya ghadhabu ) yatamwagwa juu ya wanadamu
wakati wa dhiki kubwa. Hali itakuwa nzito kwa mateso makuu
yatakayokuwepo wakati huo.
( UFUNUO 15:1; UFUNUO 16;1-6 )
1.
Jipu baya bovu ( UFUNUO 16:1-2 )
Watu duniani watakuwa na majipu mabaya, yanayotoa usaha na harufu
mbaya sana. Wataumizwa sana kwa majipu hayo kuliko wakati wa Ayubu.
2. Maji yote yatageuzwa kuwa damu (.UFUNUO 16;3-6 ).
Chemchemi zote zitatoa damu. Bahari, Maziwa na Mito vyote vitageuzwa
kuwa damu. Wanadamu watanyweshwa damu kwasababu ya damu ya watakatifu
iliyomwagwa .Watu waliwaua manabii na mitume hivyo watanyweshwa damu kwa
sababu hiyo. Damu itakuwa nzito kiasi kwamba mtu akiinywa ataweweseka
mara moja na kuanguka chini na kuzimia. Itakuwa ni hali nzito sana
kunywa damu wakati ule. Viumbe vyote viishivyo baharini, kwenye maziwa
na mito vitakufa kutokana na maji yote kuwa damu. Kutakuwa na harufu ya
kutisha kutokana na viumbe vyote kufa.
3..
Jua litashushwa karibu sana na uso wa dunia ( UFUNUO 16:8 )
Jua lina joto kiasi cha sentigredi 1,000,000 unaweza kuona jinsi
mates ohayo ya kuunguzwa na joto hilo yatakavyokuwa makubwa sana. Ndiyo
maana watu wengi watakufa wakati wa dhiki kubwa. Watu watamtukana Mungu
kwa maunguzo hayo ya jua.
4. Matatameko , umeme na radi vitaachiliwa na Mungu juu ya uso wa dunia. ( UFUNUO 16:18 ).
Matetemeko hayo yanatajwa kuwa hayajawahi kutokea tangu dunia kuwako.
Matetemeko yanayoripotiwa katika vyombo vya habari ambayo yanasababisha
maafa makubwa katika mataifa mbalimbali ni matetemeko madogo sana
ukilinganisha na matetemeko yatakayoletwa na Mungu mwenyewe wakati wa
dhiki kubwa. Umeme na radi vitakuwa ni sehemu ya mateso kwa wanadamu
walioukataa wokovu na kuachwa duniani wakati wa unyakuo wa kanisa.
5. Mvua ya mawe makubwa
( UFUNUO 16:21 )
,Mawe yanatajwa kuwa na uzito wa taranta. Taranta moja ni sawa na kg
53 za uzito. Watu watamtukana sana Mungu kutokana na mates ohayo yam
awe.
6. Nzige wenye sumu kali
( UFUNUO 9:2-6 )
Nzige wenye sumu kali kama ya kuumwa na nnge watakuwepo wengi duniani
kwa muda wote wa dhiki kubwa ili kuwatesa wanadamu walioukataa wokovu
wa Yesu. Wakati wote watu watakuwa wakiumwa na Nzige hao.
7. Kutakuwa na giza kuu juu ya uso wa dunia
( UFUNUO 16:10 )
( VII ). JINSI YA KUIKWEPA DHIKI HII KUBWA .
Kila anayetaka kuikwepa dhiki hii kubwa hana budi kujificha ndani na
kufunga milango yote kama vile wakati wa Safina ya Nuhu.
( ISAYA 26:20 )
Kwa kufanya yafuatayo:-
( i ) . Kuhakikisha tunatubu dhambi zetu zote kwa kumaanisha
kuziacha na kuokolewa kwa kumwamini mwana wa Mungu Yesu Kristo. (
MITHALI 28:13 ) “ Afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema”.
( YOHANA 3:36 ) “ Amwaminiye mwana wa Mungu hahukumiwi”.
( ii ) Kukaa ndani ya Yesu Kristo na kulifuata neno lake na maagizo yake yote ( ZABURI 119:9; ZABURI 119:6 )
( iii ) Kukaa mahali ambapo kuna mafundisho ya kweli ya neno la Mungu. Tuwe
tayari kufata kila tunaloelezwa ambalo ni la kibiblia. Tukiambiwa
kumwacha mke wa pili au mume wa pili tuwe tayari. Dhiki utakayoipata kwa
kumwacha huyo mume au mke wa mtu mwingine ni ndogo sana ukilinganisha
na dhiki kubwa inayokuja. Tukiambiwa tuache kuvaa mavazi ya kidunia
( kikahaba
) tusiwe wabishi. Watu wanapoelezwa kuhusiana na mapambo kwamba
hayatakiwi kuvaliwa na mtu aliyeokoka wao wanawasikiliza walimu wao wa
uongo ambao siku zote wanachanganya mafundisho kwa kutojua kweli
ipasavyo. Mapambo yamekatazwa
( 1 TIMOTHEO 2:9-10; 1 PETRO 3:3-5; MWANZO 35:1-5; KUTOKA 33:4-6; EZEKIELI 23:26-30,40, 42; ISAYA 3:16-24; HOSEA 2:13; YEREMIA 4:30, 2
WAFALME 9:30-37, UFUNUO 2:20).
Wanawake wasivae mavazi yawapasayo wanaume wala wanaume kuvaa mavazi
yanayowapasa wanawake, kufanya hivyo ni machukizo kwa Bwana (
KUMBUKUMBU LA TORATI 22:5 ).
Suruali ni vazi la wanaume kibiblia. Sehemu zote zinazotaja suruali
katika biblia inatajwa ikiwa imevaliwa na wanaume. Walimu wa uongo
wanawafariji wanawake wapenda dunia
( 1 YOHANA 2:15-17, YAKOBO 4;4 ) waendelee kuvaa suruali eti hazina shida. Hao ni watumishi wa Shetani ambao wapo kwa mfano wa watumishi wa haki
( 2 WAKORINTHO 11:14 )
Ukiambiwa kubatizwa katika maji tele usibishe ndivyo inavyotupasa (
YOHANA 3:23; WAKOLOSAI 2:12 ). Lazima uzamishwe katika maji kama kuzikwa kwa Yesu ili tushiriki mauti yake.
( iv ). Kukesha wakati wote na kuyatunza mavazi meupe ya utakatifu.
Doa dogo tu husababisha uchafu ( WIMBO ULIOBORA 2:15 ). Lazima
tujihadhari na Mbweha wadogo. Dhambi tunazoziona ndogo zinaweza
kutuingiza katika dhiki kubwa. Adamu na Hava walifanya dhambi ambayo
tungeweza leo kuiita dhambi ndogo. Walikula matunda katika mti
waliokatazwa na Mungu lakini adhabu waliyopewa ni kubwa mno kwa kosa
hilo tu. Wachungaji na walimu wengi wa uongo , wanaotumiwa na shetani
wanaweza kukwambia siyo shida kufanya hili au lile kwa namna ileile ya
nyoka alivyowadanganya Adm na Hawa (
MWANZO 3:1-19 ).
Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya kutoka kwa nabii
aliyetumwa kukuletea ujumbe huu, usifanye moyo wako kuwa mgumu. Hii ni
nafasi ya kipekee ya kuokoka. Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada
ya kulala usiku wa leo? Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (
2 WAKORINTHO 6:2).
Labda utaniuliza, ili uokoke, ufanyeje? Jibu ni rahisi, kwa imani
ukitubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo
akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na
wokovu (
LUKA 1:77). Je, uko tayari kuokoka sasa hivi? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni,
“Mungu
baba asante kwa kuniletea ujumbe huu.Natubu dhambi zangu zote, kwa
kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi zangu na
kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto
wa milele. Asante, kwa kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”.
Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika unakwenda mbinguni sasa, hata
ukifa leo. Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho
katika Kanisa linalohubiri wokovu.
MUNGU AKUBARIKI !!!