MWANAMKE KUVAA MAVAZI YA
MWANAMME
HUAMBATANA
NA ROHO YA KIBURI
Katika kupata picha nzuri ya mada hii ni
vyema tukagawa mada katika vipengele
(1)AKILI YA KAWAIDA TU
Mwanamke yeyote mwenye akili timamu husema kamwe hawezi
kwenda kwa mkwewe na suluali ila ni ajabu mbele za Mungu anaenda
nayo…….inashangaza????
Hii inatokana na roho ya kupendeza wanadamu
{mat 12;3 na alipoona imewapendeza
wayahudi……….}
(2)MUNGU HAPENDI MACHUKIZO
Machukizo ni hali ya kufanya
ukengeufu(kwenda kinyume) kumbukumbu
22;5 {Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamme kila afanyaye
mambo hayo ni machukizo}
(3)WENGI HUSEMA TUKO HURU
Lakini uhuru wetu usiwe kwa kufuata
mwili {Galatia 5;13 maana mmeitwa mpate
uhuru lakini uhuru wenu usiwe kwa kufuata mwili}
(4)ROHO YA KIBURI KTK MAVAZI
Kimsingi roho ya kiburi humfanya mtu
ajiweke sehemu ambayo si yake kama alivyofanya
shetani {Isaya14;14 Nitapaa kupita vimo
vya mawingu nitafanana nay eye aliye juu}
Pia hutufanya tuwe na shahuku ya kufanya
kinyume {Isaya29;16 ninyi mnapindua
mambo je mfinyanzi ahesabiwe kama udongo}
(5)JINSI YA KUFANYA
Hatuwezi kujiondoa katika hali ya mazoea kwa
nguvu zetu{ yer13;23 je mkushi aweza
kuibadili ngozi yake ndivyo ilivyo ngumu kwa mwenye dhambi}
{ Efes 4;5 Bwana mmoja,imani
moja na ubatizo mmoja}
Ubatizo ni wa maji mengi yoh3;23 kwa kuwa
huashiria kuzikwa na Kristo kolosai 2;12
No comments:
Post a Comment