Saturday, February 23, 2013

UTHIBITISHO WA UTATU WA MUNGU

SOMO: UTHIBITISHO WA UTATU WA MUNGU

Hatuna budi kila mmoja wetu kutambua kuwa tunaishi katika nyakati za hatari. Nyakati tulizonazo zinaitwa nyakati za hatari kutokana na watu wengi watakaojitenga na imani wakisikiliza mafundisho ya mashetani na roho zidanganyazo- 1TIMOTHEO 4:1; 2 TIMOTHEO 3:1; 2TIMOTHEO 4:3-5.

Moja kati ya mafundisho yaliyo kinyume na imani ni kukana utatu wa Mungu. Kwa mfano kusikiliza mafundisho ya mashahidi wa Yeheva na mahubiri mbalimbali ya akina William Brauham yanayodai kuwa hakuna UTATU wa Mungu bali Yesu ndiye Baba, Mwana na Roho mtakatifu. Pamoja na kwamba alianza vema huduma hii lakini hatimaye akakengeuka. Kwa hiyo somo hili ni la msingi mno kwa kila mkristo ili kuishindania imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu-YUDA 1:3.

Somo hili limegawanywa katika vipengele sita ( 6 ) vifuatavyo:-

1. MAFUNDISHO NA ROHO ZIDANGANYAZO KUHUSU UTATU WA MUNGU
2. NAFSI TATU ZA MUNGU KATIKA BIBLIA
3. UTHIBITISHO KUWA YESU SIYO BABA
4. USIBITISHO KUWA YESU SIYO ROHO MTAKATIFU
5. UTHIBITISHO KUWA ROHO MTAKATIFU SIYO BABA
6. KURIDHIKA NA YALE TULIYOFUNULIWA

Kipengele cha kwanza. ( 1 )

1. .MAFUNDISHO NA ROHO ZIDANGANYAZO KUHUSU UTATU WA MUNGU

Mafundisho ya watu wanaofundisha kwamba Yesu ndiye Baba na Roho mtakatifu yanayotokana na William Brauham yanayofundisha kwamba hakuna UTATU ni kwa sababu eti hakuna neno katika biblia lililo andikwa utatu, ndiyo maana utaona wakikurupuka na kusema hakuna utatu. Sawa lakini hata neno biblia halipo katika kitatu cha Biblia., kwa hiyo hilo halitufanyi kutokuwepo katika neno Biblia. Neno Biblia ni neno la kiyunani lenye maana ya mkusanyiko wa vitatu vya Mungu. Neno hili linatusaidia maneno mengi ya kuweza kuelewa. Vivyo hivyo UTATU wa MUNGU au kwa lugha ya kiingereza TRINITY , maana yake watatu katika mmoja. Wakizungumzia sahihi UTATU WA MUNGU, yaani NAFSI TATU.
MUNGU MMOJA, BWANA MMOJA.

Maandiko yanaeleza kuhusu Mungu mmoja-MALAKI 2:10, Bwana mmoja-KUMBUKUMBU 6:4-5. Hayo ndiyo yanayotumiwa kupinga utatu. Neno la kiebrania ACHAD ndilo linalotumika badala ya MMOJA katika mistari hii na lina maana ya MMOJA katika UMOJA. Neno hili linatumika pia katika kitabu cha ( MWANZO 2:24; MATHAYO 19:5-6 ) Hapa tuna picha ( kitu) kamili kwamba wawili kuwa mmoja ingawa bado ni nafsi mbili tofauti. Neno hili tena tunalikuta katika MWANZO 11:6, “Watu hawa wengi Taifa moja”. Vilevile katika kitabu cha WAEFESO 2:14, “Yeye aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja”. Hapa anazungumzia kanisa yaani watu watu mamilioni ambao katika Yesu tu Umoja. Wote tumeunganishwa lakini bado nafsi ni nyingi tofautitofauti, ni MMOJA katika UMOJA..

Kipengele cha pili ( 2

2.NAFSI TATU ZA MUNGU KATIKA BIBLIA

Katika MWANZO 1:1, tunaona hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Neno hili kwa kiebrania linaitwa ELOHIM Mwenye nguvu. Neno hili linatajwa katika Agano la kale pekee yake mara elfu mbili mia saba ( 2700 ). Sasa tuaangalia mifano ya matumizi ya dhahiri yanayoonyesha wingi katika UMOJA wa Mungu. MWANZO 1:26; MWANZO 3:22; MWANZO 11:5-7, wingi huo unaojitokeza pia katika kila kitabu cha Agano Jipya

IFUATAYO NI MISTERI AMBAYO MAHALI PAMOJA WAMETAJWA, BABA, MWANA, ROHO MTAKATIFU, IKIONYESHA WAZI KUWA NI NAFSI TATU TOFAUTI.

( MATHAYO 3:16-17; MATHAYO 28:19; YOHANA 14:16-17; MARKO 1:10-11; LUKA 1:32-35; LUKA 24:49; MATENDO 1:7-8; MATENDO 7:55-56; MATENDO 10:38-40; WAEFESO 3:14-17; 1WATHESALONIKE 1:1-5; 1PETRO 1:2-3; 1YOHANA 5:7-8; YUDA 1:20-21; UFUNUO 1:4-6 ).

Ifuatayo tena ni mistari ambayo mahali pamoja wametajwa Baba na Mwana au

Baba na Roho Mtakatifu au Mwana na Roho Mtakatifu ikionyesha wazi kuwa ni nafsi tatu tofauti. ( MARKO 13:32; YOHANA 1:18; YOHANA 5:17, 19-23; 1 WAKORINTHO 1:4; 1 WAKORINTHO 2:10; 1WAKORINTHO 1:2-3; WAGALATIA 1:1-4; WAFILIPI 1:1-3; WAFILIPI 1:2; WAFILIPI 2:9-11; WAKOLOSAI 1:2-3; WAKOLOSAI 3:1; 1WATHESALONIKE 3:13; 2WATHESALONIKE 1:1-2; 2WATHESALONIKE 2:16; 1TIMOTHEO 1:2; 2TIMOTHEO 1:2; 2TIMOTHEO 4:1; TITO 1:4; WAFILIPI 1:3; WAEBRANIA 1:5; WAEBRANIA 13:20; YAKOBO 1:1; 2YOHANA 1:3; UFUNUO 2:7; UFUNUO 21:22-23; UFUNUO 22:1-3 ).

Kipengele cha tatu. ( 3 )

3.UTHIBITISHO KWAMBA YESU SIYO BABA.

Kwanza kabisa Yesu alisema “aliyeniona mimi, amemuona Baba” ( YOHANA 14:9 ).

Kwa hiyo hatuna budi kuwa makini na mafundisho potofu yanayotafsiri mstari huu wa

9. Hapo Yesu anatufundisha tabia aliyonayo Baba ndiyo aliyonayo Mwana ( YESU ).

Kwa msingi huo tu kujifunza alivyo Yesu tunajifunza alivyo Baba. Kwa maana Yesu ni chapa ya nafsi ya Baba katika tabia ( WAEBRANIA 1:3 ). Ni mfano wa Baba ambaye Filipo hakuuona hapa Duniani ( WAKOLOSAI 1:15 ). Kwa hiyo Yesu ni sura yake Baba ( 2 WAKORINTHO 4:4 ).

A. ZIPO SABABU ISHIRINI ( 20 ) ZINAZOTHIBITISHA KWAMBA YESU SIYO BABA

Baba alikuwa mbinguni wakati Yesu alikuwa Duniani (MATHAYO 5:48 )
Yesu alisema atakaye mkiri yeye atamkiri mbele ya Baba yake wa mbinguni
3. Yesu alimshukuru Mungu wa mbinguni kwa yale waliofunuliwa akiwa duniani ( MATHAYO 11:25 )
Mungu Baba ni Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na siyo kwamba Yesu Kristo ni Baba kwake mwenyewe ( 2 WAKORINTHO 2:3; WAEFESO 1:3; 1PETRO 1:3; YOHANA 17:1, 5 ).
Mifano ya Yesu inamtofautisha yeye na Baba ( YOHANA 15:1 ). Yesu ni Mzabibu na Baba ni Mkulima.
Yesu anatufundisha kumwomba Baba kupitia kwake YESU na siyo kumwomba Yesu moja kwa moja ( YOHANA 16:23,26 ).
Yesu alisema kwa unyenyekevu hajui siku wala saa ya kuja tena, bali ajua Baba ( MARKO 15:32 )
8. Baada ya Yesu kupaa Stefano alimuona amekaa mkono wa kuume wa Mungu Baba ( MATENDO 7:56 ).
Yesu aliweka roho yake mikononi mwa Baba na siyo mwa Yesu ( LUKA 23:46 )
Petro, Yakobo na Yohana wakiwa pamoja na Yesu duniani walimsikia Baba akizungumza kutoka mbinguni (MATHAYO 17:5, 2PETRO 1:16-18 ).
Hata baada ya kufufuka kwa Yesu alisema napaa kwenda kwa Baba ( YOHANA 20:17 ).
Baada ya kupaa bado anamtaja Baba hukohuko ( UFUNUO 2:27 ).
Yohana mbatizaji alimfahamu Baba hakumfahamu YESU ( YOHANA 1:31-34 ).
14. Yesu ndiye aliyekufa pale msalabani na wala siyo Baba ( 1WAKORINTHO 15:3 ).
Yesu alikuja kufanya mapenzi ya Babake na wala si Baba ( YOHANA 5:30 )
Mafunzo ya Yesu si yake bali ni ya Baba yake aliyempeleka ( YOHANA 7:16 ).
Yesu alikuwa anampendeza Babake aliyempeleka ( YOHANA 8:29 ).
18. Yesu ni njia ya kwenda kwa Baba ( YOHANA 6:37; YOHANA 14:6 ).
Katika ( YOHANA 14:1-10 ), Yesu anajitofautisha na Baba yeke mara sita ( 6 ).

1. Mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi. 3. Mtu haji kwa Baba ila kwa njia yangu mimi 4. Mngalimjua Baba, mngalinijua mimi. 5. Mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba. 6. Baba yu ndani yangu nami ndani yake.

20. Baba, Mwana, Malaika hata Pepo wachafu wote wanamtukuza Yesu kuwa ni Mwana wa MUNGU.

Kipengele cha nne ( 4 )

3.UTHIBITISHO KUWA YESU SIYO ROHO MTAKATIFU

Mafundisho yanayosema kwamba Yesu ndiye Roho Mtakatifu siyo ya KWELI.

Kuna sababu sita ( 6 ) zinazothibitisha kuwa Yesu siyo Roho Mtakatifu. Nazo ni :

Ilimlazimu Yesu aondoke ili Roho Mtakatifu aje ( YOHANA 16:5-7 ).
Yesu alikwisha tolewa kabla ya Roho Mtakatifu ( YOHANA 3:16; YOHANA 7:39 ).
Yesu Kristo alimtaja kwamba Roho Mtakatifu kuwa ni msaidizi mwingine siyo yeye Yesu ( YOHANA 14:16,26; YOHANA 15:26 ).
Kumkufuru Yesu kuna msamaha lakini kumkufuru Roho Mtakatifu hakusameheki ( MATHAYO 12:31-32 )
Watu wa Samalia walikuwa wamempokea Yesu lakini walikuwa hawajampokea Roho Mtakatifu ( MATENDO 8:5-25 ).
Yesu alisema kuwa Roho Mtakatifu atanitukuza mimi na hata nena kwa shauri lake mwenyewe, atatwaa yaliyo yangu ( YOHANA 16:13-15 ).

Kipengele cha tano ( 5 ).

5.UTHIBITISHO KWAMBA ROHO MTAKATIFU SIYO BABA.

Pia wanaofundisha kuwa Roho Mtakatifu ni Baba siyo kweli ni mafundisho ya Uongo. Kuna sababu tatu ( 3 ) zinazothibitisha kwamba Roho Mtakatifu siyo Baba.

Roho Mtakatifu alikuwa duniani wakati Baba alikuwa mbinguni ( MATAHYO 3:16-17 ).
Roho Mtakatifu akitoka kwa Baba na kuja kumtia mafuta YESU ( LUKA 4:18; MATENDO 10:38 ).
Yesu anatofautisha kwamba atakayemwomba ni tofauti na Roho Mtakatifu ( YOHANA 14:16 ).

Kipengele cha sita ( 6 ).

6.KURIDHIKA NA YALE TULIYOFUNULIWA .

Kwa mfano:-

A. BABA anaitwa MUNGU ( 1 WAKORINTHO 8:6 ).

B. MWANA ( YESU ) anaitwa MUNGU ( ISAYA 9:6; YOHANA 20:26-29 ).

C. ROHO MTAKATIFU anaitwa MUNGU ( MATENDO 5:3-4 )

Linganisha ( 2 1 WAKORINTHO 3:16-17 ) na ( 1 WAKORINTHO 6:19-20 ), hii inathibitisha kwamba hakuna Mungu watatu, kuwa kuna Mungu mmoja tu katika UMOJA. Mfano YOHANA 17:21, akisema Baba amesema Mwana, akisema Mwana amesema Roho Mtakatifu akisema Roho Mtakatifu amesema Baba + Mwana hapa tunaona hawatofautishwi katika lolote tangu mwanzo hata milele. Hivyo hakuna haja kuwa na maswali juu ya UTATU, kwani ni mambo ya siri ya Bwana Mungu wetu ( KUMBUKUMBU 29:29 ). Kwa maana hiyo kwa sasa tunaona kwa kioo cha jinsi ya fumbo ( 1 WAKORINTHO 13:12 ). Kama mtu akija kwetu au kwenu haleti mafundisho ya UTATU tusimkaribishe, tusishirikiane naye ( 2YOHANA 1:10-11; WARUMI 16:17

Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya kutoka kwa nabii aliyetumwa kukuletea ujumbe huu, usifanye moyo wako kuwa mgumu. Hii ni nafasi ya kipekee ya kuokoka. Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo? Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2 WAKORINTHO 6:2). Labda utaniuliza, ili uokoke, ufanyeje? Jibu ni rahisi, kwa imani ukitubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77). Je, uko tayari kuokoka sasa hivi? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni, “Mungu baba asante kwa kuniletea ujumbe huu.Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi zangu na kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”. Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika unakwenda mbinguni sasa, hata ukifa leo. Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook ,Twitter n.k kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.Endelea kutembelea blog hii kwa mafundisho mengine zaidi kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe; WWW.davidcarol719.wordpress.com

UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

No comments:

Post a Comment