HOJA ZINAZOTUMIWA NA WALIMU KUTETEA UVAAJI WA MAPAMBO
HOJA ZINAZOTUMIWA NA WALIMU KUTETEA UVAAJI WA MAPAMBO, KAMA ALIVYOCHAMBUA KAKA David Carol
Ni muhimu kufahamu kuwa mapambo katika biblia yanaitwa mavazi ya
kikahaba (MITHALI 7:10).”Na tazama ,mwanamke akamkuta,Ana mavazi ya
kikahaba,mwelevu wa moyo”.Mapambo yanahusianishwa na kazi za kikahaba
(vyombo vya makahaba)[EZEKIELI 23:26-30,40,42].Sehemu nyingine mapambo
yanaitwa vyombo vya uzuri (KUTOKA 33:4-6).
Ni muhimu
kufahamu kuwa wapo walimu wa Neno la Mungu wanaotofautiana katika
mafundisho yao kuhusiana na mapambo.Kundi moja lina msimamo mkali
kinyume na mafundisho ya walimu wanaobariki uvaaji wa mapambo.Wanakuwa
na maandiko wanayoyasimamia yanayokataza uvaaji wa mapambo .Baadhi ya
maandiko hayo ni kama:-[1 TIMOTHEO 2:9-10; 1 PETRO 3:3-5; MWANZO 35:1-5;
KUTOKA 33:4-6; EZEKIELI 23:26-30,40,42; ISAYA 3:16-24;; YEREMIA
4:3O].Mapambo yanayotakiwa ni mapambo ya rohoni.Mwanamke ajipambe kwa
mapambyasiyoharibika,yasiyoonekana
Yaani,utu wema,utulivu, roho ya upole. iliyo na dhamani kuu mbele
za Mungu (1 PETRO 3:3-5; 1 TIMOTHEO 2:9-10).Walimu hawa wanatilia mkazo
sana juu ya kuishi maisha yanayoendana maagizo yote.Dauni anasema kuwa
akiyaangalia maagizo yote hataaibika mbele za Mungu (ZABURI
119:6).Katika safari ya wana waIsraeli iliyokuwa na watu zaidi ya
milioni mbili ni Yoshua na Kalebu tu waalioingia mjini Kanani katika hao
wote waliotoka Misri.Mungu anatoa sababu,anasema ‘kwa kuwa walikuwa na
roho nyingine ndani yao na kumuandama kwa moyo wote (HESABU
14:23-24).Kwa kuwa walimwandama Bwana kwa kila jambo (KUMBUKUMBU
1:35-39).
Safari ya wana Israeli kuelekea Kanani ni mfano wa
safari yetu ya kwenda minguni (1WAKORITHO 10:10)..Kwahiyo,viwango ni
vilevile kwa namna ya safari ya Waisraeli.Mtu ambaye hatafata maagizo
yote ya Mungu katika Neno lake atakatiliwa mbali na uso wake kama
alivyowafanya wana wa Israeli.Kwa kila tendo tufanyalo tulifanye kwa
utukufu wa Mungu.Hawa walimu wanafundisha kuwa utakatifu ni mwili na
roho (WAEBRANIA 12:14; 2WAKORITHO 7:1; 1WAKORITHO 7:34;1 WATHESALONIKE
5:23; MATHAYO 23:25-26)
Walimu wengine wanafundisha kinyume
wakitumia maandiko machache kutetea hoja zao.Tuangalie hoja wanazo
tumia na jinsi wanavyotafsiri maandiko kinyume na Kweli.
HOJA YA KWANZA
Mungu haangalii mambo ya nje,anaangalia mambo ya ndani tuKwamba mavazi hayawezi kumzuia mtu kuingia mbinguni.
Hoa hii siyo sahihi kwasababu Utakatifu ni mwil na roho (usafi wa roho na mwili)
[1WAKORITHO 7:34; 2WAKORITHO 7:1; 1WATHESALONIKE 5:23; MATHAYO
23:25-26).Tunatakiwa kusafisha ndani kwanza kasha nje, hapo ndipo
tutakuwa tumeutimiza utakatifu wote (mwili na roho).Kwa hiyo si sahihi
kuhalarisha mapambo kwa visingizio vya hoja hiyo.
HOJA YA PILI
Tuko huru ndani ya Yesu.palipo na roho wa Mungu ndipo penye uhuru.
Wanasema kuwa tuko huru,hatuko chini ya sheria (WAGALATIA 5:1;
2WAKORITHO 3:17).,Uhuru unaozungumziwa hapa si wa kufanya kitu chochote
kinyume na mapenzi ya Mungu.Uhuru uaozungumziwa hapa ni uhuru wa kuwa
mbali na dhambi.Kabla hatujaokoka tulikuwa watumwa wa dhambi (YOHANA
8:33-36).Yesu alizungumzia uhuru wa kuwa mbali na dhambi..Mtu akiokoka
anakuwa mtumwa wa haki (WARUMI 6:16-18)
Pia wanafundisha
wakisema hatuko chini ya sheria lakini ni muhimu kujua sheria ipi
inazungumziwa (WAGALATIA 4:5).Sheria inayozungumziwa kuwa hatuko chini
yake ni sheria ya Musa.Sisi tuliookolewa kwa damu ya Yesu,hatuko chini
ya sheria ya Musa,tunaongozwa na kutawaliwa na sheria ya Yesu (WAEBRANIA
10:28; WAGALATIA 6:2).Tukisema kuwa hatuko chini ya sheria tunasemaje
kuwa sisi ni wenye haki? Haki haipatikani pasipo na sheria (WARMI
6:14).Dhambi ni uasi wa sheria (1YOHANA 3:4).Kwa hiyo,tusidanganywe kuwa
sheria ya Yesu ni lsi ngumu ukilinganisha na sheria ya Musa.Tunamuona
Yesu akifanya marekebisho ya sheria ya Musa tena akiongeza au akikaza
viwango (MATHAYO 5:27-28,33-34,43-44).Yesu anasema ukimtaza mke wa mtu
kwa kumtamani tayari unahesabika mzinzi lakini kwa Musa ilikuwa mpaka
umefanya kitendo cha uzinifu.Sheria ya Yesu inaitwa sheria ya Kifalme
(YAKOBO 2:8)Sheria ya kifalme siyo ya kuchezea.Tunapaswa kufanya mapenzi
yote ya Bwana (WAEBRANIA 13:20-21)
HOJA YA TATU
Tuvae vyovyote ili tuwapate na mataifa
Msingi umekwisha kuwekwa,yeyote anatakiwa kujenga juu ya msingi huo
(1 WAKORITHO 3:11).Msingi wa mafundisho yetu ni Yesu
mwenyewe.Katika kanisa lake hakushusha viwango vya mafundisho hata pale
ambapo mafundisho yalionekana kuwa magumu kwao (YOHANA
6:61,66-68).Ukisoma andiko hilo utaona jinsi Yesu alivyofundisha na
wanafunzi wengi wakalejea nyuma kabisa wasiandamane naye tena.
Lakini Yesu hakushusha viwango hata kidogo,hata mitume walipobaki
aliwauliza kama wanataka kuondoka,wakitaka waondoke tu.Walikwazwa na
mafundisho yaliyoonekana kuwa magumu kwao.
Ni muhimu kufahamu
kuwa Yesu ndiye mchungaji mkuu wa kondoo .Mchungaji yeyote ni msaidizi
kwa Yesu, hivyo wanapaswa kufuata mfano wa viwango vya mchungaji
mkuu.Yesu hakushusha viwango ili aendelee kuwa na washirika wanaokwazwa
na Neno gumu.Pia ni muhimu kwa wachungaji wa kufahamu kuwa kuna
mafundisho ya watoto wachanga kiroho na mafundisho ya watu waliokuwa
kiroho.Mtoto mchanga ukimfundisha Neno gumu litamfanya kuona wokovu kuwa
ni mgumu.Ataona sheria sheria zimezidi na anaweza hata akarudi nyuma
kiroho.
Mchungaji mkuu Yesu Kristo alisema njia iendayo uzimani
ni nyembamba,tena imesongwa, waionao ni wachache (MATHAYO
7:13-14).Hatutakiwi kushusha viwango vya mafundisho yetu ili tuwapate
wengi.Unaweza kuwa na kanisa kubwa sana linaloonekana kwa macho kuwa ni
kubwa kumbe hakuna hata mmoja kati yao aliyeandikwa mbinguni.Kuna kanisa
linaloonekana na kanisa lisiloonekana.Kuna kanisa ambalo majina yake
yameandikwa duniani na kanisa ambalo majina yake yameandikwa mbinguni
(WAEBRANIA 12:22_23).
KWA NINI WANAPOTOSHA NENO LA MUNGU?
Yesu Kristo alisema kuwa siku za mwisho maasi yataongezeka na upendo
wa watu wengi utapoa (MATHAYO 24:12).Upendo wa kumpenda Mungu,yaani
kuzishika sheria na amri zake zote.Kyatii maagizo yake yote (YOHANA
14:21,23).Unabii huo wa Yesu wa upendo kupoa umekwisha kutimia (UFUNUO
3:15-16).Kanisa la leo limekuwa vuguvugu,ya dunia linataka na mbingu
linataka.Yesu anatutaka tuchague kuwa moto au kuwa baridi wala si kuwa
vuguvugu.Vuguvugu watatapikwa.Kanisa la leo linafananishwa na kanisa
Laodokia (kanisa vuguvugu) linalotaka kufanya chochote kile bila
kukemewa (freedom of right).Paulo alitabiri kuwa utakuja wakati ambapo
watu hatahitaji kuelezwa habari yoyote ya Kweli,wakizifuata hadithi za
uongo.watu ambao watajitafutia walimu wawapendao ambao hawawezi
kuwakemea (2Ttimotheo 4:3-5).
Pia nyakati za nabii Isaya
walikuwepo watu waliopenda kudanganywa,waliopenda mafundisho laini
yadanganyayo (ISAYA 30:9-10).Hata nyakati hizi watu wanapenda sana
kudanganywa.Wanapenda kukaa katika makanisa (madhehebu) ambayo viwango
vyao sivya kibiblia.
Sababu kubwa ya kuchujwa cha viwango vya
Neno la Mungu ni ili washirika wasipungue kanisani.Pia ili wengi waweze
kuja na kanisa liongezeke.Lengo la wachungaji wa namna hii ni kutaka
kujipatia fedha ya aibu..Siku ya mwisho watapata aibu na
kudharaulika,Hawawazii juu ya roho za waumini,jicho lao ni pesa.Waumini
wanapaswa kuwa makini na mafundisho wanayofundishwa.Wanapaswa
kuyachunguza maandiko kuona kama ndivyo yalivyo (MATENDO
17:10-11).Waberoya walikuwa na hekima sana,wao waliyachunguza maandiko
wakati Paulo na Sila wanahubiri.Hata somo hili na maandiko yote
usiyapuzie na kuona kuwa huyu si wa dhehebu langu.Mbingu ni moja,Mungu
mmoja,na njia ni moja Yesu Kristo Mwokozi wetu.
IWENI WATENDAJI WA NENO WALA SI WASIKIAJI TU
[YAKOBO 1:22]
No comments:
Post a Comment