Monday, November 5, 2012

DALILI 11 ZA DHAHIRI,ZA MTU ALIYEKWISHA KUINGIA MAJARIBUNI,NA KUMEZWA NA SHETANI KWAKUKOSA KUWA NA KIASI NA KUKESHA

DALILI KUMI NA MOJA (11) ZA DHAHIRI, ZA MTU ALIYEKWISHA KUINGIA MAJARIBUNI, NA KUMEZWA NA SHETANI KWA KUKOSA KUWA NA
KIASI NA KUKESHA

1. Kuanza kukosa kuhudhuria kusanyiko la Kanisa la Nyumbani na ibada za Kanisa Kuu kwa visingizio mbalimbali, huku dhamiri yako haiumii; na ukaanza kuwaza moyoni kwamba hata ukijisomea Biblia mwenyewe nyumbani inatosha [WAEBRANIA 10:25].
2. Kuanza kufuata njia zako mwenyewe tofauti na jinsi ulivyojifunza katika mafundisho ya Neno la Mungu [MITHALI 14:14a].
...
3. Kuanza kufanya mazoea ya kwenda Kanisani na kusikia Neno la Mungu lakini hakuna hatua yoyote ya kulitii na kulitenda. Kuanza kuona Neno la Mungu kama wimbo tu.
[EZEKIELI 33:30-32].
4. Kuanza kukataa maonyo ya Mchungaji kwa kujiona kuwa umekua sana kiroho, na eti mshauri wako ni Roho Mtakatifu na Yesu peke yao! [MHUBIRI 4:13].
5. Kuanza kuzifuata njia za mataifa katika mavazi, usemi na matendo mengine; na kusema moyoni kwamba Mungu anaangalia roho tu, haangalii mwili [WARUMI 12:2;
2 WAFALME 17:5].
6. Kuanza kuipenda dunia na kusongwa na kutafuta nguo, mali, elimu, vitu, anasa, n.k. na kuvipa umuhimu wa kwanza kuliko kumtafuta Mungu [I YOHANA 2:15;I TIMOTHEO 6:9-10].
7. Kuanza kutokuona umuhimu wa kuzipitia "Notes" za mafundisho ya Kanisa unapokuwa Nyumbani, na kuyachunguza maandiko zaidi katika Biblia na kuona kwamba inatosha tu Kanisani [MATENDO 17:11].
8. Kutokana na kuongezeka katika kulijua Neno la Mungu [WAEBRANIA 5:12].
9. Kuanza kuona ya kwamba huna haja ya kuongozwa, na kuwaka tamaa ya kutaka kuwa kiongozi na kusema kila mmoja anaweza kujiongoza mwenyewe maana wote tuko sawa [HESABU 16:1-3, 8-10].
10. Kuanza kuona kwamba maombi, kusoma Neno, kufanya kazi ya Mungu ni mambo yasiyofurahisha [UFUNUO 2:4-5; WAEBRANIA 3:14].

11. KUANZA KUONA dhambi ni kitu cha kawaida, na kuona ni kawaida kusema uongo na kusengenya na kuanza kutenda dhambi nyingi kisirisiri ukijionyesha kuwa u mtakatifu mbele ya watu waliookoka na dhamiri haikushuhudii kutubu na kuacha [UFUNUO 3:1].
Kanisa kama limejaa watu wasiokuwa na kiasi na kukesha, Kanisa hilo halikujengwa kwenye Mwamba na ni dhahiri kwamba milango ya kuzimu italishinda. Mwamba Yesu Kristo, alikuwa mwenye kuwa na kiasi na kukesha. Kama kanisa limejengwa kwenye msingi wake, litakuwa na watu wa maombi

No comments:

Post a Comment