HOJA ZINAZOTUMIWA NA WALIMU KUTETEA UVAAJI WA MAPAMBO
HOJA ZINAZOTUMIWA NA WALIMU KUTETEA UVAAJI WA MAPAMBO, KAMA ALIVYOCHAMBUA KAKA David Carol
Ni muhimu kufahamu kuwa mapambo katika biblia yanaitwa mavazi ya
kikahaba (MITHALI 7:10).”Na tazama ,mwanamke akamkuta,Ana mavazi ya
kikahaba,mwelevu wa moyo”.Mapambo yanahusianishwa na kazi za kikahaba
(vyombo vya makahaba)[EZEKIELI 23:26-30,40,42].Sehemu nyingine mapambo
yanaitwa vyombo vya uzuri (KUTOKA 33:4-6).
Ni muhimu kufahamu
kuwa wapo walimu wa Neno la Mungu wanaotofautiana katika mafundisho yao
kuhusiana na mapambo.Kundi moja lina msimamo mkali kinyume na mafundisho
ya walimu wanaobariki uvaaji wa mapambo.Wanakuwa na maandiko
wanayoyasimamia yanayokataza uvaaji wa mapambo .Baadhi ya maandiko hayo
ni kama:-[1 TIMOTHEO 2:9-10; 1 PETRO 3:3-5; MWANZO 35:1-5; KUTOKA
33:4-6; EZEKIELI 23:26-30,40,42; ISAYA 3:16-24;; YEREMIA 4:3O].Mapambo
yanayotakiwa ni mapambo ya rohoni.Mwanamke ajipambe kwa
mapambyasiyoharibika,yasiyoonekana
Yaani,utu wema,utulivu, roho ya
upole. iliyo na dhamani kuu mbele za Mungu (1 PETRO 3:3-5; 1 TIMOTHEO
2:9-10).Walimu hawa wanatilia mkazo sana juu ya kuishi maisha
yanayoendana maagizo yote.Dauni anasema kuwa akiyaangalia maagizo yote
hataaibika mbele za Mungu (ZABURI 119:6).Katika safari ya wana waIsraeli
iliyokuwa na watu zaidi ya milioni mbili ni Yoshua na Kalebu tu
waalioingia mjini Kanani katika hao wote waliotoka Misri.Mungu anatoa
sababu,anasema ‘kwa kuwa walikuwa na roho nyingine ndani yao na
kumuandama kwa moyo wote (HESABU 14:23-24).Kwa kuwa walimwandama Bwana
kwa kila jambo (KUMBUKUMBU 1:35-39).
Safari ya wana Israeli kuelekea
Kanani ni mfano wa safari yetu ya kwenda minguni (1WAKORITHO
10:10)..Kwahiyo,viwango ni vilevile kwa namna ya safari ya Waisraeli.Mtu
ambaye hatafata maagizo yote ya Mungu katika Neno lake atakatiliwa
mbali na uso wake kama alivyowafanya wana wa Israeli.Kwa kila tendo
tufanyalo tulifanye kwa utukufu wa Mungu.Hawa walimu wanafundisha kuwa
utakatifu ni mwili na roho (WAEBRANIA 12:14; 2WAKORITHO 7:1; 1WAKORITHO
7:34;1 WATHESALONIKE 5:23; MATHAYO 23:25-26)
Walimu wengine
wanafundisha kinyume wakitumia maandiko machache kutetea hoja
zao.Tuangalie hoja wanazo tumia na jinsi wanavyotafsiri maandiko kinyume
na Kweli.
HOJA YA KWANZA
Mungu haangalii mambo ya nje,anaangalia mambo ya ndani tuKwamba mavazi hayawezi kumzuia mtu kuingia mbinguni.
Hoa hii siyo sahihi kwasababu Utakatifu ni mwil na roho (usafi wa roho na mwili)
[1WAKORITHO 7:34; 2WAKORITHO 7:1; 1WATHESALONIKE 5:23; MATHAYO
23:25-26).Tunatakiwa kusafisha ndani kwanza kasha nje, hapo ndipo
tutakuwa tumeutimiza utakatifu wote (mwili na roho).Kwa hiyo si sahihi
kuhalarisha mapambo kwa visingizio vya hoja hiyo.
HOJA YA PILI
Tuko huru ndani ya Yesu.palipo na roho wa Mungu ndipo penye uhuru.
Wanasema kuwa tuko huru,hatuko chini ya sheria (WAGALATIA 5:1;
2WAKORITHO 3:17).,Uhuru unaozungumziwa hapa si wa kufanya kitu chochote
kinyume na mapenzi ya Mungu.Uhuru uaozungumziwa hapa ni uhuru wa kuwa
mbali na dhambi.Kabla hatujaokoka tulikuwa watumwa wa dhambi (YOHANA
8:33-36).Yesu alizungumzia uhuru wa kuwa mbali na dhambi..Mtu akiokoka
anakuwa mtumwa wa haki (WARUMI 6:16-18)
Pia wanafundisha wakisema
hatuko chini ya sheria lakini ni muhimu kujua sheria ipi inazungumziwa
(WAGALATIA 4:5).Sheria inayozungumziwa kuwa hatuko chini yake ni sheria
ya Musa.Sisi tuliookolewa kwa damu ya Yesu,hatuko chini ya sheria ya
Musa,tunaongozwa na kutawaliwa na sheria ya Yesu (WAEBRANIA 10:28;
WAGALATIA 6:2).Tukisema kuwa hatuko chini ya sheria tunasemaje kuwa sisi
ni wenye haki? Haki haipatikani pasipo na sheria (WARMI 6:14).Dhambi ni
uasi wa sheria (1YOHANA 3:4).Kwa hiyo,tusidanganywe kuwa sheria ya Yesu
ni lsi ngumu ukilinganisha na sheria ya Musa.Tunamuona Yesu akifanya
marekebisho ya sheria ya Musa tena akiongeza au akikaza viwango (MATHAYO
5:27-28,33-34,43-44).Yesu anasema ukimtaza mke wa mtu kwa kumtamani
tayari unahesabika mzinzi lakini kwa Musa ilikuwa mpaka umefanya kitendo
cha uzinifu.Sheria ya Yesu inaitwa sheria ya Kifalme (YAKOBO 2:8)Sheria
ya kifalme siyo ya kuchezea.Tunapaswa kufanya mapenzi yote ya Bwana
(WAEBRANIA 13:20-21)
HOJA YA TATU
Tuvae vyovyote ili tuwapate na mataifa
Msingi umekwisha kuwekwa,yeyote anatakiwa kujenga juu ya msingi huo
(1 WAKORITHO 3:11).Msingi wa mafundisho yetu ni Yesu mwenyewe.Katika
kanisa lake hakushusha viwango vya mafundisho hata pale ambapo
mafundisho yalionekana kuwa magumu kwao (YOHANA 6:61,66-68).Ukisoma
andiko hilo utaona jinsi Yesu alivyofundisha na wanafunzi wengi
wakalejea nyuma kabisa wasiandamane naye tena.
Lakini Yesu
hakushusha viwango hata kidogo,hata mitume walipobaki aliwauliza kama
wanataka kuondoka,wakitaka waondoke tu.Walikwazwa na mafundisho
yaliyoonekana kuwa magumu kwao.
Ni muhimu kufahamu kuwa Yesu ndiye
mchungaji mkuu wa kondoo .Mchungaji yeyote ni msaidizi kwa Yesu, hivyo
wanapaswa kufuata mfano wa viwango vya mchungaji mkuu.Yesu hakushusha
viwango ili aendelee kuwa na washirika wanaokwazwa na Neno gumu.Pia ni
muhimu kwa wachungaji wa kufahamu kuwa kuna mafundisho ya watoto
wachanga kiroho na mafundisho ya watu waliokuwa kiroho.Mtoto mchanga
ukimfundisha Neno gumu litamfanya kuona wokovu kuwa ni mgumu.Ataona
sheria sheria zimezidi na anaweza hata akarudi nyuma kiroho.
Mchungaji mkuu Yesu Kristo alisema njia iendayo uzimani ni
nyembamba,tena imesongwa, waionao ni wachache (MATHAYO
7:13-14).Hatutakiwi kushusha viwango vya mafundisho yetu ili tuwapate
wengi.Unaweza kuwa na kanisa kubwa sana linaloonekana kwa macho kuwa ni
kubwa kumbe hakuna hata mmoja kati yao aliyeandikwa mbinguni.Kuna kanisa
linaloonekana na kanisa lisiloonekana.Kuna kanisa ambalo majina yake
yameandikwa duniani na kanisa ambalo majina yake yameandikwa mbinguni
(WAEBRANIA 12:22_23).
KWA NINI WANAPOTOSHA NENO LA MUNGU?
Yesu
Kristo alisema kuwa siku za mwisho maasi yataongezeka na upendo wa watu
wengi utapoa (MATHAYO 24:12).Upendo wa kumpenda Mungu,yaani kuzishika
sheria na amri zake zote.Kyatii maagizo yake yote (YOHANA
14:21,23).Unabii huo wa Yesu wa upendo kupoa umekwisha kutimia (UFUNUO
3:15-16).Kanisa la leo limekuwa vuguvugu,ya dunia linataka na mbingu
linataka.Yesu anatutaka tuchague kuwa moto au kuwa baridi wala si kuwa
vuguvugu.Vuguvugu watatapikwa.Kanisa la leo linafananishwa na kanisa
Laodokia (kanisa vuguvugu) linalotaka kufanya chochote kile bila
kukemewa (freedom of right).Paulo alitabiri kuwa utakuja wakati ambapo
watu hatahitaji kuelezwa habari yoyote ya Kweli,wakizifuata hadithi za
uongo.watu ambao watajitafutia walimu wawapendao ambao hawawezi
kuwakemea (2Ttimotheo 4:3-5).
Pia nyakati za nabii Isaya walikuwepo
watu waliopenda kudanganywa,waliopenda mafundisho laini yadanganyayo
(ISAYA 30:9-10).Hata nyakati hizi watu wanapenda sana
kudanganywa.Wanapenda kukaa katika makanisa (madhehebu) ambayo viwango
vyao sivya kibiblia.
Sababu kubwa ya kuchujwa cha viwango vya Neno
la Mungu ni ili washirika wasipungue kanisani.Pia ili wengi waweze kuja
na kanisa liongezeke.Lengo la wachungaji wa namna hii ni kutaka
kujipatia fedha ya aibu..Siku ya mwisho watapata aibu na
kudharaulika,Hawawazii juu ya roho za waumini,jicho lao ni pesa.Waumini
wanapaswa kuwa makini na mafundisho wanayofundishwa.Wanapaswa
kuyachunguza maandiko kuona kama ndivyo yalivyo (MATENDO
17:10-11).Waberoya walikuwa na hekima sana,wao waliyachunguza maandiko
wakati Paulo na Sila wanahubiri.Hata somo hili na maandiko yote
usiyapuzie na kuona kuwa huyu si wa dhehebu langu.Mbingu ni moja,Mungu
mmoja,na njia ni moja Yesu Kristo Mwokozi wetu.
IWENI WATENDAJI WA NENO WALA SI WASIKIAJI TU
[YAKOBO 1:22]
No comments:
Post a Comment