NJIA KUMI ZA KIBIBLIA ZA KUMPATA MWENZI WA MAISHA.
Na: Patrick Samson Sanga.
Mpenzi msomaji hizi ni dondoo tu zilizomo ndani ya kitabu hiki ndani ya
kitabu cha kwanza, nimeona ni vema walau kwa sehemu nikueleze yaliyomo
ndani.
Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kutoka kwa
babaye bali mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana’.Nianze kwa kusema
kuoa au kuolewa ni mpango kamili wa Mungu. Zipo sababu nyingi za kwa
nini unahitaji mke au mume Moja unakuwa umejipatia kibali kwa Bwana,
mbili ni kwa sababu zinaa (1 Wakorintho 7:20) na tatu unapopata mke
unakuwa umepata msaidizi na mlinzi.
Kibiblia mke /mme mwenye
busara mtu hupata kutoka kwa Bwana, maana yake Mungu ndiye anayehusika
na kumpa mtu mke/mme. Mungu pekee ndiye anayejua nani ana busara ya
kukaa na fulani halafu ndiyo anayekupa huyo mtu. Suala la kumpata mwenzi
ambaye hakika ni wa mapenzi ya Mungu kwa mtu husika, imekuwa ni
changamoto kubwa hasa kwa vijana na pia wale ambao bado hawajaoa au
kuolewa.
Lengo la kitabu hiki ni ;
*kuwasaidia vijana wengi ambao bado hawajaoa au kuolewa kufanya maamuzi sahihi.
*Kuwapa maarifa wale ambao wanafuatwa na vijana wengi kwa lengo la
kutaka kuwaoa, nini wafanye pindi wanapofuatwa na vijana wengi.
*Kuwapa uhakika / uthibitisho wale ambao tayari wameshafanya maamuzi
haya na tayari wana wachumba kwamba wachumba hao wanatokana na Mungu au
la.
*Kuwafariji na kutoa mwongozo kwa wale ambao huenda hamna
anayejitokeza kutaka kuwaoa, wanaokataliwa na wale ambao wamechelewa
kuolewa halafu wao wanafikiri ni laana.
*Kutoa mwongozo kwa
wazazi, wachungaji, walezi, viongozi wa makundi ya kidini kuwasaidia
vijana wao katika kufanya maamuzi haya makubwa .
*Kukusaidia kuzipinga hila zote za shetani katika safari hii ya maamuzi.
Kabla ya kuzitaja njia, ndani ya kitabu hicho nimetaja kwanza misingi unayotakiwa kuijua kabla ya kuzijua hizo njia nayo ni;
*Kwa kila jambo kuna majira yake hivyo hata wewe kuoa au kuolewa kwako kuna wakati wako maalumu.
*Mungu hatumii njia au mfumo wa aina moja katika kukujulisha wewe mwenzi wako.
*Mungu anavyo vigezo vya kwake ya kukupa mke au mme ambavyo si lazima viendane na vigezo vya kwako.
*Si kila mke au mme hutoka kwa Mungu.
*Mungu anapoamua kukupa wewe mke au mme anakuwa ameangalia mbali kuliko wewe unavyofikiria.
*Usimuombe Mungu akujulishe mke au mme wako wakati ndani yako umeshajichagulia wa kwako.
*Ni vema uwe umekomaa na umekua kiakili, kiufahamu, na kiroho kwanza
kabla ya kufanya maamuzi kama haya na hujaokoka fanya maamuzi ya kuokoka
maana ni kwa faida yako mwenyewe.
*Ni vema ukatambua ya kuwa mwenzi wako si lazima atoke kanisa lako, shule au chuo ulichosoma au kazini kwako nk.
Zifuatazo ni njia za kibiblia, ambazo hakika zimewasaidia wengi kuwajua na kuwapata wenzi wao wa maisha;
*Kwa kumcha Mungu, ( kumtii Mungu ).
*Kwa sauti ya Mungu mwenyewe.
*Amani ya Kristo.
*Upendo wa ki –Mungu ( wa Dhati ).
*Mafunuo ya ki-Mungu.
*Kwa kuyatenda mapenzi ya Mungu.
*Kulijua kusudi la Mungu katika maisha yako.
*Kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu.
*Wazazi /walezi/wachungaji/kiongozi wako katika kundi lenu.
*Dhamiri za watu wengine au ushuhuda wa watu wengine.
Mpenzi msomaji hapa nimetaja tu hiyo misingi na njia husika. Lakini
ndani ya kitabu nimefafanua kila msingi na njia kimapana maana
isingekuwa rahisi kuziweka kurasa zote za kitabu hiki humu ndani.
Kama huna kitabu na ungependa kupata kitabu au hata kumchukulia mtu
mwingine nenda katika Category ya vitabu utapata maelekezo huko.
Bwana Mungu akubariki na akutangulie katika safari hii ya maamuzi makubwa katika maisha yako.
NJIA KUMI ZA KIBIBLIA ZA KUMPATA MWENZI WA MAISHA. « “UTAIINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI”. Isaya 58:12
No comments:
Post a Comment