Toleo la 238
9 May 2012
BAADA
ya mapendekezo ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja nchini kwa lengo la
kutetea haki za binadamu kukwama kinyume cha baadhi ya mataifa ya
Ulaya, mapendekezo mpya kuhusu sheria itakayoruhusu utoaji mimba
yamepata watetezi nchini, Raia Mwema, limeelezwa.
Watetezi hao ni baadhi ya asasi maarufu za kiraia nchini kwa upande mmoja ambazo kwa sasa zimeingia katika mzozo na asasi nyingine zinazopinga mapendekezo hayo.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, mapendekezo hayo kuelekea sheria hiyo kwa sasa yapo kwenye hatua ya maandalizi ya rasimu ya muswada wa sheria hiyo na miongoni mwa asasi zinazotetea mapendekezo hayo ni Care International.
Inadaiwa kuwa Care International inaungwa mkono na baadhi ya asasi za kiraia zikiwamo za kitaaluma na baadhi ya zilizoko kwenye harakati za masuala ya jinsia nchini.
Mvutano mkali unatajwa kuibuka miongoni mwa wanaharakati katika baadhi ya asasi zinazounga mkono mapendekezo hayo kupinga muswada huo uliopewa jina la Muswada wa Uzazi Salama 2012 (The bill on safe motherhood 2012).
Mapendekezo hayo ya asasi hizo za kiraia yanatarajiwa kuwasilishwa kwa ama Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii au Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, baadaye mwezi huu kwa ajili ya kujadiliwa na hatimaye kuwasilishwa bungeni.
Mbali na kudaiwa kukiuka maadili nchini, mapendekezo katika muswada huo, hususan suala la utoaji mimba yanatajwa kukiuka matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.
Katiba inatajwa kukiukwa katika ibara ya 14 inayozungumzia juu ya haki ya kuishi, pamoja na sheria ya kanuni za adhabu vifungu vya 150, 151 na 152 ambavyo vinamtia hatiani mtu anayefanya jaribio, kusaidia na kutumia vifaa kwa ajili ya kutoa mimba na kifungu cha 219, kinachozuia utoaji mimba isipokuwa katika mazingira magumu.
Kauli za viongozi wa asasi za kiraia
Akizungumza na gazeti hili mmoja wa maofisa wa Shirika la kutetea Uhai (Pro-life International) ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini alisema kwa namna fulani muswada huu unakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ingawa kwa “juu juu” unapambwa na lugha nzuri kama; “kurekebisha kasoro zinazotokana na sheria za sasa ambazo ni pamoja na sheria ya ndoa ya mwaka 1971, sheria ya mtoto ya mwaka 2009, sheria ya afya ya jamii ya 2009 pamoja na sheria ya wafungwa 1967.”
Hata hivyo, akichambua kasoro ndani ya mapendekezo yaliyomo kwenye muswada huo ofisa huyo anasema; “Msukumo wa muswada huu si kuhusu kuwasaidia wanawake wajawazito kupata huduma zinazostahili, bali ni kusukuma masuala ya kudhibiti kizazi, matumizi ya vidhibiti mimba, utoaji mimba sambamba na sheria kali za kimabavu. Lengo ni kuhakikisha idadi ya Watanzania inapungua.”
Anaendelea kusema; “Uzito umewekwa pia katika kuharibu afya ya wasichana kwa njia ya vidhibiti mimba ili wapoteze uwezo wao wa kizazi kwa kadiri wanavyoendelea kutumia, vile vile muswada unalenga kuwaondolea wazazi mamlaka katika malezi na makuzi ya watoto wao.”
Akizungumzia namna masuala ya uandikaji rasimu hii yanavyofanyika kwa usiri mkubwa, ofisa huyo alisema “Jambo kubwa zaidi ni usiri mkubwa uliofichika katika muswada huu na nia ya mashirika ya kimataita kutoka Ulaya na Marekani kuhalalisha utoaji mimba.”
Kwa mujibu wa ofisa huyo ambaye ni Mtanzania, mpango wa Umoja wa Mataifa ni kuhakikisha kila nchi duniani inapitisha sheria ya utoaji mimba ifikapo 2015.
Baadhi ya wanaharakati wanaopinga mapendekezo katika muswada huo wameeleza kuwa endapo muswada huo utaridhiwa kuwa sheria, misingi ya maadili ya kiutamaduni nchini kuhusu malezi ya watoto itakuwa inakiukwa.
Katika hatua nyingine, mratibu wa ukusanyaji maoni wa Care International, David Lyamuya alikiri kuwepo kwa tofauti ya kimtazamo miongoni mwa asasi za kiraia.
“Kumekuwa na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya asasi za kiraia kuhusu rasimu hii ya muswada,” alisema David.
NOTE THAT:
NGO ni wale waliopata elimu kisha wakakosa sifa za kuwafanya wapate kazi sehemu nyingine yoyote hapa duniani, na ndio hao wanaopewa misaada kutoka nchi mbalimbali za kibepari kwa masharti ya kutekeleza na eti kuharakatia mambo kwa faida ya waliowatuma! hata kama ni mambo yanayo au yatakayo pelekea kuharibika kwa maadili ktk nchi zao au jamii zao!! as long as wananufaika na misaada wanayopewa wako radhi hata kukaa uchi hadharani ili mradi waonekane wamedhamiria kutetea wanachokiamini (kwani walishaapa kukitetea baada ya kuahidiwa misaada kuendesha NGO zao).
Swali!! Wanaotetea upuuzi wa kutoa mimba na same sex marriage wana akili timamu? na ni madhehebu gani hawa? je kwenye familia zao baba zao na mama zao wangetoa mimba au baba zao wangeoa wanaume wenzao kabla wao hawajazaliwa wangekuwepo leo?
Hawa ni mashetani tunaoishi nao na kula nao majumbani mwetu! tamaa ya fedha na misaada kwa kivuli cha NGO kinawafanya binadamu wamkosee mungu!!
Tanzania hatuna umaskini kiasi cha kuendelea kuwa ombaomba!! kama ni umaskini basi ni wetu na tutakufa nao. Hatuwezi kuuza utu wetu na heshima yetu eti kwa sababu Marekani au Uingereza wamesema bila ya hivyo watatunyima misaada!! wakae nayo misaada yao, hatuhitaji misaada yao ya kishetani, tuna utajiri kiasi gani mwenyezi mungu ametubarikia tuendelee kumpigia magoti shetani na NGO zake??? Uzembe wa kufikiri wa viongozi wetu unafanya nchi zetu za kiafrika ziendelee kuwa ombaomba, na si raia ambao ni ombaomba bali viongozi wenye tamaa wasiotumia akili kusimamia nchi!!
Walaaniwe wote wanaojadili, kuongelea na hata kujaribu kuleta mjadala juu ya huu ushetani wa kimagharibi unaokiuka amri za mwenyezi mungu!!
Hell is waiting for them.....

No comments:
Post a Comment