Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)
JF Focus: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)
By Mwali
Swali la kwanza:
Rais Kikwete amekuwa madarakani tokea mwaka 2005. Ukilinganisha na
utawala wa Marais wastaafu, Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa, nini
maoni yako kuhusiana na utawala Rais Kikwete? Rais Kikwete ana yapi ya
kujivunia aliyofanya katika kipindi cha miaka aliyokaa madarakani? Jibu
la swali liguse sekta zote kuanzia ya uchumi, afya, usafiri,sheria na
utawala, michezo, n.k.
Una dakika kumi kujibu swali hili, kisha hapo nitamwelekeza Matola.
Kwanza kabisa napenda kuelezea kuwa nimefurahi sana kuwa swali
limelenga moja kwa moja kwenye kulinganisha madaraka ya Rais wa sasa
mpendwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho
Kikwete na awamu zilizopita za “Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa”.
Kama swali linavyojionesha “ana yapi ya kujivunia aliyofanya katika
kipindi cha miaka aliyokaa madarakani?” katika nyanja tofauti, hususan
“uchumi, afya, usafiri, sheria na utawala, michezo, n.k.”
Napenda kuainisha majibu yagu ya awali na kuwajulisha wasimamizi na
wafatiliaji mnakasha huu huu, kuwa kila nyanja imesheheni nakshi na
fasaha na tawimu teletele, kweny "post" hii ntaanza na moja la "uchumi"
na post zifuatazo ntawasilisha yanayohusu mengineyo kama yalivyo kwenye
swali:
Uchumi wakati wa Nyerere;
Ikumbukwe kuwa,
wakati Mwalim Nyerere anapewa madaraka ya nchi hii uchumi wa Tanganyia
ulikuwa mzuri sana hususan katika kilimo, Tanganyika ilikuwa ni muuzaji
mkubwa wa mazao nje ya Tanganyika katika Afrika, Nyerere kwa muda mfupi
tu akatutoa huko na kutufikisha kuwa waagiizaji wakibwa wa chakula.
Under his Presidency, Tanzania slipped from being the largest exporter of food in Africa to the biggest importer of food.
Source: Mwalimu Nyerere | Julius Nyerere; Life Times Legacy
Tanzania slipped from being the largest exporter of food in Africa to the biggest importer of food.
Source: Julius Nyerere - New World Encyclopedia
Kwa kifupi kwa kuwa hatumzungumzii Nyerere, na “sources” zipo nyingi
sana zinazoonesha jinsi uchumi wetu ulivyoporomoka sana wakati wake,
naomba atakae a google “economy collapsed during Nyerere” atajionea
mwenyewe maana nikianza kuyabandika hapa tutatoka nje ya mnakasha.Kwa
kifupi, hatuna cha kujivunia katika uchumi wakati wa Nyerere
tuliushuhudia ukiporomoka kwa kujaribu kwake kufata mfumo wa ujamaa
ambao ulishindwa kabisa.
Uchumi wakati wa Mwinyi;
Ikumbukwe kwamba Mwinyi ndiye alikuwa “savior” wa waTanzania mpaka
akapewa jina la “Ruksa” kwa sababu ni yeye aliyetufungulia milango ya
uchumi huria ni yeye aliyeleta maamuzi ya kufunga mashirika ya umma
yaliyokuwa yananyonya uchumi wote wa Tanzania kwa kupewa ruzuku hata
yanapofanya vibaya. Kwa kifupi Mzee Mwinyi alikuwa na kazi ngumu sana ya
kutuondoa kwenye lindi la umaskini na kutuanzishia mfumo mpya wa uchumi
ambao tunaendelea nao. Kwa hilo tumsifu Mzee Mwinyi:
During
Mwinyi's terms Tanzania took the first steps to reverse the socialist
policies of Julius Nyerere. [2] He relaxed import restrictions and
encouraged private enterprise.
Soma zaidi: Ali Hassan Mwinyi - Wikipedia, the free encyclopedia
In 1986 the newly-appointed Mwinyi Government embarked on a broad-based
Economic Recovery Program supported by the International Monetary Fund
(IMF) and the World Bank. This was reinforced by an Economic and Social
Action Program in 1989. Under these two programs, Government worked to
dismantle the system of state controls and promote private sector
expansion--including liberalizing the trade and exchange system,
eliminating price controls and most state monopolies, and opening the
financial sector to private sector participation. Rehabilitation of key
infrastructure was also made a priority, particularly roads, railways,
and ports.
Source: Foodnet-Uganda > Market Information
Uchumi wakati wa Mkapa;
Mkapa kwenye uchumi aliendeleza aliyoyanzisha Mwinyi nae akatia mkazo
kwenye kukaribisha wageni kuwekeza tukaona “influx” ya makampuni makubwa
ya kigeni yakipewa vitalu vya uwindaji, ardhi kubwa za kuchimba madini,
Ulikuwa ni muelekeo mzuri kiuchumi kinadharia.
Kosa kubwa
nilionalo ni pale “corruption” ya hali ya juu ilipokithiri wakati wa
Mkapa, hususan baada ya kifo cha Nyerere. Madudu wmengi au karibu yote
yanayoibuka sasa utakuta yameanzia au yemetendeka wakati wa Mkapa; EPA,
KIWIRA, BOT, RADAR, kuainisha machache. Sina mengi ya kumsifu kwani
kipindi chake cha mwisho aliharibu sana kwa kutuacha Kiza na kwa tuhuma
nyingi za ufisadi zilizodhihirika “immediately” baada ya kuondoka kwake
madarakani na mpaka leo bado zinatutesa.
Uchumi wakati wa Kiwete;
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ana kila sababu za kujivunia katika uchumi
wakati wa madaraka yake, kwa uchache kuhusu uchumi ni haya hapa
yakiambatana na takwimu zilizo wazi kabisa:
Asalaam Aleykum,
kwanza nawapongeza kwa mara nyingine tena wale wote ambao wako kwenye
mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, nawapongeza na wale wengine wote
wasiopo kwenye mfungo lakini wanauheshimu mwezi huu, wanaheshimu uamuzi
wetu wakufunga na tunawashukuru zaidi kwa kutupa hamasa sisi tulio
kwenye swaum.
Natamani kuingia moja kwa moja kwenye kujibu
swali la kwanza, lakini uungwana hauniachi kufanya hivyo bali
unanilazimisha kutoa pongezi zangu za dhati kwa walioubuni mnakasha huu.
Natoa shukrani zangu pia kwa mshiriki mwenzangu wa mnakasha huu al
maaruf Matola kwa kukubali kushiriki, halikadhalika natoa shukrani zangu
kwa wote waliojitolea kuufatilia mnakasha huu.
Naanza:
Kwanza kabisa napenda kuelezea kuwa nimefurahi sana kuwa swali
limelenga moja kwa moja kwenye kulinganisha madaraka ya Rais wa sasa
mpendwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho
Kikwete na awamu zilizopita za “Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa”.
Kama swali linavyojionesha “ana yapi ya kujivunia aliyofanya katika
kipindi cha miaka aliyokaa madarakani?” katika nyanja tofauti, hususan
“uchumi, afya, usafiri, sheria na utawala, michezo, n.k.”
Napenda kuainisha majibu yagu ya awali kuyapanga kama yalivyo:
Uchumi wakati wa Nyerere;
Ikumbukwe kuwa, wakati Mwalim Nyerere anapewa madaraka ya nchi hii
uchumi wa Tanganyia ulikuwa mzuri sana hususan katika kilimo, Tanganyika
ilikuwa ni muuzaji mkubwa wa mazao nje ya Tanganyika katika Afrika,
Nyerere kwa muda mfupi tu akatutoa huko na kutufikisha kuwa waagiizaji
wakibwa wa chakula.
Under his Presidency, Tanzania slipped from being the largest exporter of food in Africa to the biggest importer of food.
Source: Mwalimu Nyerere | Julius Nyerere; Life Times Legacy
Tanzania slipped from being the largest exporter of food in Africa to the biggest importer of food.
Source: Julius Nyerere - New World Encyclopedia
Kwa kifupi kwa kuwa hatumzungumzii Nyerere, na “sources” zipo nyingi
sana zinazoonesha jinsi uchumi wetu ulivyoporomoka sana wakati wake,
naomba atakae a google “economy collapsed during Nyerere” atajionea
mwenyewe maana nikianza kuyabandika hapa tutatoka nje ya mnakasha.
Kwa kifupi, hatuna cha kujivunia katika uchumi wakati wa Nyerere
tuliushuhudia ukiporomoka kwa kujaribu kwake kufata mfumo wa ujamaa
ambao ulishindwa kabisa.
Uchumi wakati wa Mwinyi;
Ikumbukwe kwamba Mwinyi ndiye alikuwa “savior” wa waTanzania mpaka
akapewa jina la “Ruksa” kwa sababu ni yeye aliyetufungulia milango ya
uchumi huria ni yeye aliyeleta maamuzi ya kufunga mashirika ya umma
yaliyokuwa yananyonya uchumi wote wa Tanzania kwa kupewa ruzuku hata
yanapofanya vibaya.
Kwa kifupi Mzee Mwinyi alikuwa na kazi
ngumu sana ya kutuondoa kwenye lindi la umaskini na kutuanzishia mfumo
mpya wa uchumi ambao tunaendelea nao. Kwa hilo tumsifu Mzee Mwinyi:
During Mwinyi's terms Tanzania took the first steps to reverse the
socialist policies of Julius Nyerere. [2] He relaxed import restrictions
and encouraged private enterprise.
Soma zaidi: Ali Hassan Mwinyi - Wikipedia, the free encyclopedia
In 1986 the newly-appointed Mwinyi Government embarked on a broad-based
Economic Recovery Program supported by the International Monetary Fund
(IMF) and the World Bank. This was reinforced by an Economic and Social
Action Program in 1989. Under these two programs, Government worked to
dismantle the system of state controls and promote private sector
expansion--including liberalizing the trade and exchange system,
eliminating price controls and most state monopolies, and opening the
financial sector to private sector participation. Rehabilitation of key
infrastructure was also made a priority, particularly roads, railways,
and ports.
Source: Foodnet-Uganda > Market Information
Uchumi wakati wa Mkapa;
Mkapa kwenye uchumi aliendeleza aliyoyanzisha Mwinyi nae akatia mkazo
kwenye kukaribisha wageni kuwekeza tukaona “influx” ya makampuni makubwa
ya kigeni yakipewa vitalu vya uwindaji, ardhi kubwa za kuchimba madini,
Ulikuwa ni muelekeo mzuri kiuchumi kinadharia.
Kosa kubwa
nilionalo ni pale “corruption” ya hali ya juu ilipokithiri wakati wa
Mkapa, hususan baada ya kifo cha Nyerere. Madudu wmengi au karibu yote
yanayoibuka sasa utakuta yameanzia au yemetendeka wakati wa Mkapa; EPA,
KIWIRA, BOT, RADAR, kuainisha machache. Sina mengi ya kumsifu kwani
kipindi chake cha mwisho aliharibu sana kwa kutuacha Kiza na kwa tuhuma
nyingi za ufisadi zilizodhihirika “immediately” baada ya kuondoka kwake
madarakani na mpaka leo bado zinatutesa.
Uchumi wakati wa Kiwete;
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ana kila sababu za kujivunia katika uchumi
wakati wa madaraka yake, nnadiriki kusema kuwa hakuna nyanja ambayo
Kikwete hajavunja rikodi zilopo kabla yake katika kuyatimiza. Kwa
uchache kuhusu uchumi ni haya hapa yakiambatana na takwimu zilizo wazi
kabisa:
1. USIMAMIZI WA UCHUMI JUMLA:
Ukuaji wa
Uchumi Katika kipindi cha miaka minne (2005 – 2009). Uchumi umeendelea
kuimarika na Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7.2 kwa mwaka
katika kipindi hicho. Ukuaji huu wa uchumi ulichangiwa zaidi na
kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika sekta za: Bidhaa za viwanda;
ujenzi; fedha; na mawasiliano na uchukuzi.
2. PATO LA MTANZANIA;
Pato la Mtanzania limekuwa likiongezeka katika kipindi chote cha awamu
ya nne kutoka Dola za Kimarekani 392.8 mwaka 2005 hadi dola 525.2 mwaka
2008.
3.MWENENDO WA RIBA;
Viwango vya riba vimeonesha
mwelekeo mzuri hasa kuanzia mwaka wa fedha 2006/07, ambapo riba kwenye
amana za akiba zimekuwa zikiongezeka, wakati riba zinazotozwa kwenye
mikopo zimekuwa zikipungua. Katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka
2009/10 wastani wa viwango vya riba kwa amana za akiba za muda mfupi
(hadi mwaka mmoja)ulikuwa asilimia 8.92 ikilinganishwa na wastani wa
asilimia 5.21 katika mwaka wa fedha 2003/04.
Katika kipindi
hicho, wastani wa viwango vya riba vilivyotozwa na benki za biashara kwa
mikopo ya mwaka mmoja ulipungua hadi asilimia 13.93 kutoka asilimia
15.75. Kutokana na mwelekeo huo wa riba, tofauti kati ya viwango vya
riba kwenye amana za mwaka mmoja na viwango vya riba kwenye mikopo ya
mwaka mmoja ilishuka kutoka 10.54 mwaka 2003/04 hadi 5.01mwaka 2009/10,
sawa na kushuka kwa asilimia 47.5.
4. BIASHARA YA BIDHAA NJE;
Mauzo ya bidhaa nje yaliongezeka kwa asilimia 3.2 hadi kufikia dola za
Kimarekani 2,697.6 milioni mwezi Novemba 2009. Ongezeko hilo
lilichangiwa na mauzo ya dhahabu kwa asilimia 9.0 hadi kufikia dola
1,023.8 milioni, tumbaku kwa asilimia 35.3 hadi kufikia dola 151.4.
Aidha, mauzo ya kahawa nje yaliongezeka hadi kufikia dola 117.2 milioni,
sawa na asilimia 29.0.
5.MAPATO YA NDANI;
Katika
kipindi cha miaka minne, Wizara ya Fedha na Uchumi, kupitia Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), imefanya marekebisho ya mifumo na viwango vya
baadhi ya kodi. Hatua hii imesaidia kuweka mazingira mazuri zaidi ya
uzalishaji kurahisisha ukusanyaji wa kodi. Aidha, wigo wa kodi
umeongezeka katika kipindi hicho.
6.KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MIKOPO;
Mikopo iliyotolewa na mabenki kwa sekta binafsi kwa ajili ya shughuli
mbalimbali za kiuchumi iliongezeka kutoka shilingi bilioni 1,571.0 mwezi
Desemba 2005 hadi shilingi bilioni 4,710.2 mwezi Juni 2009, sawa na
ongezeko la wastani wa asilimia 34.5 kwa mwaka. Mwezi Oktoba 2009 mikopo
hiyo ilikuwa imefikia shilingi bilioni 4,836.0. Aidha, wastani wa riba
kwa dhamana zote ilishuka kutoka asilimia 16.4,
7.KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI;
Mifuko ya Dhamana ya Mikopo (Credit Guarantee Scheme): Kuanzishwa kwa
Mfuko wa Dhamana wa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME
Credit Guarantee Scheme) ambao unaratibiwa na Benki Kuu kumeboresha
mazingira ya wenye mitaji midogo na ya kati waweze kupatamikopo kutoka
kwenye mabenki na taasisi za fedha. Tangu mfuko huu uanzishwe, jumla ya
SMEs 48 zimepata udhamini wa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni
3.054. Kati ya wajasiliamali hao, sekta ya uzalishiji inaongoza
ikifuatiwa na sekta za ujenzi na kilimo. Ili kuleta ufanisi zaidi, mwaka
huu Serikali imetenga jumla ya Shilingi bilioni 10 kuongeza mtaji wa
mfuko wa wajasiliamali wadogo na wa kati.
Kuongeza fedha katika
Mfuko wa Uwezeshaji Kiuchumi wa wajasiriamali wadogo (Mfuko wa JK)
kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB. ilitoa kiasi cha
Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB (Shilingi bilioni 5.25) na
CRDB (Shilingi bilioni 5.25). Kiasi hiki kiliwezesha kutolewa kwa mikopo
ya Shilingi bilioni 37.17 ikiwa in asilimia 118 ya Shilingi 31.5
zilizotengwa kutolewa na benk hizo mbili.
Hayo ni baadhi tu ya
mafanikio ya kujivunia ya kiuchumi Tanzania na yapo mengi sana, kuanzia
mabarabara ya nayoendelea kujegwa hivi sasa, mitambo ya uzalishaji umeme
inayoendelea kujengwa hivi sasa, kiwanda kikubwa cha chuma
kinachoendelea kujengwa hivi sasa.
Licha ya hayo kuna msukumo
ulifanyawa na Kikwete wa makusudi kabisa katika kuendeleza sekata ya
mali asili na katika kipindi chake tumeona makampuni makubwa duniani
yakivumbuwa gas ya asili kwa kiwango kikubwa sana na hili ni jema sana
katika uchumi wetu wa siku za usoni. Hapa nnadiriki kusema kuwa wa kabla
yake "uchumi walikuwa nao lakini waliukalia", Kikwete kabadili hilo
badili ya kuukalia kausimamia kidete na matokeo hakuna asiyeyajuwa,
Tanzania economy inabadilika kutoka kilimo kuwa namba moja kwenda kwenye
Gas ya asili.
Hapo nimegusa uchumi tu, dakika kumi hazitoshi kuelezea mengi mema ya Kikwete.
No comments:
Post a Comment