Monday, November 5, 2012

JE NI AGANO JIPYA AU AGANO LA KALE

JE, AGANO LA KALE AU AGANO JIPYA?

" KWA SABABU HIYO KILA MWANDISHI MWENYE ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI AMEFANANA NA MTU MWENYE NYUMBA ATOAYE KATIKA HAZINA YAKE VITU VIPYA NA VYA KALE. (MATHAYO 13:52)"
1. MWANDISHI:Waandishi walikuwa ni waalimu wa torati au waalimu wa Neno la Mungu. Hawa ndio walioitafsiri torati au neno la Mungu na kuwahubiri watu kwa urahisi mpaka wayafahamu wapasayo kuyatenda sawasawa na torati (NEHEMIA 1: 13; MARKO 9:11; LUKA 5:17). Hata hivyo waliongeza katika maneno ya Mungu mafundisho yao (MATHAYO 23:2-4).
2. MTU MWENYE NYUMBA: (MATHAYO 10:25) Mtu mwenye Nyumba ni Yesu Kristo mwenyewe.
3. VITU VIPYA NA VYA KALE: Vitu vipya na vya kale katika elimu ya Ufalme wa mbinguni, ni kweli yote kutoka katika Agano la Kale na Agano Jipya.

MAFUNZO ANAYOTUPA YESU KUHUSU AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA.
Wahubiri wa leo au waalimu wa Biblia ambao ndiyo waandishi wa leo, wanapaswa kuichambua kweli yote inayohusiana na wakati huu, kutoka katika AGANO LA KALE na AGANO JIPYA kama alivyofanya mtu mwenye nyumba, kichwa cha Kanisa Yesu Kristo. Katika MATHAYO sura ya 13 peke yake Yesu ameitumia kweli kutoka Agano la Kale katika MATHAYO. 13:14-15, 17, 32, 43. Yesu Kristo mara nyingi katika mafundisho na maneno yake alitumia maandiko ya Agano la Kale (MATHAYO. 4:4, 7, 10 n.k. MARKO. 4:12; 7:6-7; 11:17; 12:10-11 n.k. LUKA. l7:27; 17:32; 19:46; 20:41-44; n.k. YOHANA 3:14; 11:34-35; n.k.). Wako waalimu wa Biblia, au Wahubiri wa leo ambao wanatumia Agano la Kale tu katika mafundisho yao. Hivi sivyo Yesu anavyotufundisha. Wako wahubiri wengine hawataki kutumuia kabisa Agano la Kale na wanajisikia vibaya wakiona mtu anahubiri kutoka katika Agano la Kale. Wao wanahubiri kwa kutumia Agano Jipya tu. Hii pia siyo sahihi kulingana na mafundisho ya Yesu mtu mwenye nyumba. Elimu ya Ufalme wa mbinguni ni hazina iliyo na vitu vipya na vya kale. Pamoja na kwamba leo hatuko chini ya Agano la Kale (WAEBRANIA 8:13; 9:1-16; 10:9, 19:20), hata hivyo ziko kweli za kale au za Agano la Kale ambazo bado ni kweli za Elimu ya Ufalme wa mbinguni katika kipindi tulichonacho. Kwa mfano, watoto wanapaswa kuwatii wazazi ili wapate heri katika Agano la Kale na Jipya (WAEFESO 6:1-3; KUTOKA 20:12 n.k.)
SABABU TANO ZA KUTUMIA AGANO LA KALE NA JIPYA KATIKA MAFUNDISHO
Kwa mhubiri au mwandishi wa leo, kuna sababu tano za kutumia Agano la Kale na Jipya katika Elimu ya Ufalme wa mbinguni:-
1. KUONYESHA UWIANO WA MANENO YA MUNGU (WARUMI 10:6-8,KUMBUKUMBU 30:12-14).
2. KUONYESHA MAMBO YANAYOTENDEKA VILEVILE NYAKATI ZOTE (WARUMI 2:21-24 linganisha na EZEKIELI 36:20; WARUMI 8:35-37 linganisha na 1 WAFALME 19:13-18; WARUMI 15:20-22 linganisha na ISAYA 52:15).
3. KUTOA MAELEZO YA KUTOSHA KUHUSU KWELI FULANI (WARUMI 1:17; 4:6-8, 18-21; WARUMI 9:19-21 linganisha na ISAYA 29:16, 45:9; WARUMI 15:9-13; MATHAYO 2:4-6, 13-18 n.k.).
4. KUIHAKIKISHA KWELI FULANI (WARUMI 3:3-4, 10-18, 23; WARUMI 4:2-16; 5:12-19; 9:7-18; 12:19-20).
5. KUHAKIKISHA KUTIMILIZWA KWA UNABII (WARUMI 9:25-26; 10:16; 11:26-27; 15:9-13; MATHAYO 2:4-6, 13-18 n.k.).
Hata hivyo lazima tujue katika majira tuliyonayo leo tunaangalia Yesu amesema nini au Agano Jipya linasema nini kuhusu jambo hilo. Pale ambapo kuna kubatilika kwa amri iliyotangulia, basi tunashika iliyo mpya kwa mfano katika MATHAYO 5:33-37 na YAKOBO 5:12 tunajifunza kwamba sheria ya zamani iliwaambia watu kutimiza viapo vyao, lakini leo, haturuhusiwi kuapa kabisa. Pale ambapo sheria haikubadilika, inabaki ilivyo (KUTOKA 20:12; WAEFESO 6:2). Ndiyo maana inatubidi kulinganisha maandiko ya Agano la Kale na maandiko ya Agano Jipya ili kufahamu yatupasayo kuyafanya katika majira haya tuliyo nayo

No comments:

Post a Comment