Wednesday, October 31, 2012

Was dance ever a part of worship in the apostolic church or throughout the first few centuries? If so, why was it abandoned?


—Doug

As far as I can tell from my research, dance was not part of worship in the early church. Jewish culture featured dancing at weddings and the Feast of Tabernacles, and of course there are numerous references to David dancing in the Old Testament, but such dancing was spontaneous and celebratory, not liturgical. As a result, early Christians from Jewish backgrounds probably lacked a tradition of dance during formal worship. Dancing only appears in the New Testament in two contexts: Herod's banquet (Mark 6:21-22, with disastrous results for John the Baptist) and the celebration of the Prodigal Son's return (Luke 15:22-27).

By contrast, dance played a prominent role in many pagan cults, such as the orgiastic cult of Dionysius. Because early Christians in no way wished to be associated with such rites, they most likely avoided dancing in church, though their intense, sometimes ecstatic worship (see Acts 2:43, 1 Cor. 14:26 for examples) may well have included motions of some sort. Christians avoided social dancing, too, as it was usually associated with drinking and sexual immorality in Roman culture.

The church fathers paint a generally bleak view of dancing but do not wholly preclude sacred dance. Clement of Alexandria, writing circa 195, interpreted Old Testament Scriptures in such a way as to excise reference to literal dancing: " 'Praise with the timbrel and the dance.' This refers to the church meditating on the resurrection of the dead in the resounding skin." Commodius, writing around 240, associated dancing with worldliness: "You are rejecting the law when you wish to please the world. You dance in your houses. Instead of psalms, you sing love songs." Cyprian, though, writing about a decade later, makes some distinction between godly and ungodly dance: "The fact that David led the dances in the presence of God is no sanction for faithful Christians to occupy seats in the public theater. For David did not twist his limbs about in obscene movements. He did not depict in his dancing the story of Grecian lust."

For more on this topic, see the Catholic Encyclopedia entry on "dancing"

Quotes from church fathers taken from A Dictionary of Early Christian Beliefs, edited by David W. Bercot (Hendrickson, 1998). I also found information in Everett Ferguson's Backgrounds of Early Christianity (2nd ed., Eerdmans, 1993).

Swali: "Biblia inasemaje juu ya kiumbe dinosauri? Je, viumbe hawa dinosauri wamo ndani ya biblia?"

Elibariki Andrew
Biblia inasemaje juu ya kiumbe dinosauri/MIJUSI WAKUBWA? Je, viumbe hawa dinosauri wamo ndani ya biblia?

NA ELIBARIKI ANDREW


Jibu:
Hili ni swali linalotokana na umri wa dunia tunayoikalia. kulengana na muda unaodhaniwa viumbe hawa waliishi, hakuna mwanadamu angekuwako kuwaona wakiishi. Biblia hutaja viumbe waliokuwa wakiitwa kwa kiebrania “tannyn’ kiumbe kikubwa chenye asili ya kufanana na mamba mkubwa. Tafsiri tofauti tofauti za neno hili la kiebrania ndizo zinachangia kiumbe hiki kuitwa dinosauri. Viumbe hawa wametajwa karibu mara thelathini katika agano la kale na wanapatikana nhi kavu na ndani ya maji.

Biblia inataja viumbe wengine ambao wanaitwa behemoth. hawa hutajwa kuwa wenye nguvu kuliko viumbe wote Mungu alivyoviumba wakubwa ambao mikia yao inafananishwa na msonobari (Ayubu 40:15 na kuendelea). Dinosauri alikuwa na mkia mkubwa hivyo kustahili kufananishwa na msonobari.

Karibu kila aina ya michoro ya kizamani ya kila mahali ulimwenguni ina alama za kufanana na viumbe wakubwa wa asili ya mamba. Mabaki ya kazi za mikono ya kizamani kutoka amerika kaskazini yanaashiria kuwako kwa dinosauri.

Katika mabaki yaliyopatikana bara asia na amerika kaskazini yana alama za miguu ya wanadamu na viumbe hawa dinosauri kithibitisho cha kuwako kwa viumbe hawa dinosauri duniani.

Kwa hivyo je, mna dinosauri katika biblia? Sisi kama wachambuzi wa biblia katika kuthibitisha na historia tunaamini yakuwa wanadamu na dinosauri waliishi wakati sawa. Tunaamini dinosauri walikufa wakati wa gharika katika siku za Nuhu na pia kwa vile walikuwa wakiwindwa sana na wanadamu.Na Elibariki Andrew

Swali: "Je! Umomoni ni dhehebu? Wamomoni wanaamini nini?"

KATIKA KUJILINDA KIIMANI NI MUHIMU KUFAHAMU WANAOJIITA WATAKATIFU WA SIKU ZA MWISHO WANAAMINI NINI ILI TUSIJE KUJIKUTA TUMENASA

NA ELIBARIKI ANDREW.
Jibu:
Dini ya Kimomoni, ambayo wafuasi wake wanajulikana kama Wamomoni na Latter Day Saints (LSD), ilianzishwa chini ya miaka miambili iliyopita na mtu anayeitwa Joseph Smith. Alisema kwamba alitembelewa na Mungu Baba na Yesu Kristo ambaye alimwambia kwamba Makanisa yote na kanunu zao za imani zilikuwa chukizo kwake. Joseph Smith akatoka na kuanzisha dini nyigine ambayo ilidai kuwa “ndio kanisa ya kweli duniani.” Kasoro na Wamomoni ni kwamba inachanganyisha, inarembesha, na kupanua juu ya Bibilia. Wakristo hawana sababu yo yote ya kuamini kuwa Bibilia si kweli na kamili. Kumwamini Mungu kwa kweli yamaanisha kuwa unaamini katika neno lake, na maandiko yote ni pumzi ya Mungu, ambayo yamaanisha yalitoka kwake (Timotheo 3:16).

Wamomoni wanaamini kuwa kunayo sehemu nne za pumzi kiungu za neno sio moja tu peke: 1) Bibilia “vile imefasirwa vizuri sana.” Ni aya gani ambazo zinachukuliwa kuwa si kweli kila wakati haziwekwi wazi. 2) Kitabu cha Wamomoni, ambacho “kilifasiriwa” na Smith na kuchapishwa mwaka wa 1980. Smith alidai ndicho “kitabu peke cha kweli.” 3) Kanuni na maagano, ambayo kilikuwa na mkusanyiko wa ufunuo wa siku hizi kuhusu “Kanisa la Yesu Kristo vile limerejeshwa.” 4) Lulu ya dhami sana, ambayo inachukuliwa na Wamomoni “kufafanua” kanuni na mafunzo ambayo yalipotezwa kutoka kwa Bibilia na kuongezea .ujumbe ulio wake kuhusu uumbaji wa dunia.

Momoni wanaamini yafuatayo kuhusu Mungu: Hakuwa kiumbe cha mamlaka ya juu sana juu ya ulimwengu, lakini alipokea mamlaka hayo kupitia kwa kuishi maisha takatifu na bidii yake isiyo na mwisho. Wanaamini kuwa Mungu Baba ako na “mwili wa nyama na mifupa inaguzika kama ya mwanadamu.” Ingawa alitengwa na viongozi wa siku hizi wa Momoni, Brigham Young alifunza kuwa Adamu awali alikuwa Mungu na baba wa Yesu Kristo. Kwa ulinganisho, Wakristo wanajua haya kuhusu Mungu: kunaye Mungu mmoja wa kweli (Kumbukumbu La Torati 6:4; Isaya 43:10; 44:6-8), amekuwa akiishi na atakuwa akiishi (Kumbukumbu La Torati 33:27; Zaburi 90:2; 1 Timotheo 1:17), na hakuumbwa bali yeye ndiye alikuwa muumbaji (Mwanzo 1; Zaburi 24:1; Isaya 37:16). Yeye ni mkamilifu na hakuna mwingine amfananaye (Zaburi 15:29; Hosea 11:9). Yeye ni Roho (Yohana 4:24), na Roho haitengenezwi kwa nyama na mifupa.

Momoni wanaamini kuwa kuna viwango tofauti au falme tofauti katika maisha baada ya kifo: ufalme wa peponi, ufalme wa duniani, na giza la nche. Mahali ambao mwanadamu atamalizia kutegemea chenye wanaamini na kufanya katika maisha haya. Kwa ulinganisho, Bibilia inatuambia baada ya kifo, tunaenda mbinguni au jahannamu kulingana na kama tulikuwa au hatukuwa na imani katika Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wetu. Kutoweka kutoka kwa mwili wetu yamaanisha, sisi kama waumini, tuko na Mungu (2 Wokorintho 5:6-8). Wasio amini watatumwa jahannamu au mahali pa wafu (Luka 15:50-54). Kutakuwa na mbingu mpya na nchi mpya kwa waumini (Ufunuo 21:1) na wasio amini watatupwa katika zila la moto (Ufunuo 20:11-15). Hakuna nafasi ya pili ukombozi baada ya kifo (Waebrania 9:27).

Viongozi wa Momoni wamefunza kuwa ubadilisho wa Yesu ulitokea kwa minajili ya ule uhisiano wa kimwili wa Mungu Baba na Mariamu. Wamomoni wanaamini kuwa Yesu ni mungu , lakini binadamu yeyote anaweza kuwa mungu. Momoni wanafunza kwamba wokovu unaweza patikana kwa kuweka pamoja imani na matendo mazuri. Kinyume na hii, Wakristo katika historia wamekuwa wakifunza hakuna mtu atakaye fikia cheo cha Mungu- ni yeye peke ambaye ni mtakatifu (1 Samueli 2:2). Tunaweza fanywa watakatifu mbele za Mungu kupitia kwa imani kwake (1 Wakorintho 1:2). Yesu ndiye Mwana wa peke wa Mungu (Yohana 3:16), yeye ndiye peke ambaye amewai ishi bila dhambi, maisha yasiyo na mawaa, na sasa ako na heshima ya juu sana mbinguni (Waebrania 7:26). Yesu na Mungu wote ni kitu kimoja, Yesu kuwa ndiye peke aliishi baada ya kuzaliwa kimwili (Yohana 1:1-8; 8:56). Yesu alijotoa yeye mwenye kama dhabihu kwetu, Mugu akamfufua kutoka kwa kaburi, na siku moja kila mmoja atalikiri kuwa Kristo ni Bwana (Wafilipi 2:6-11). Yesu anatuambia ni vigumu kuingia mbinguni kwa matendo yetu na kwamba ni kwa imani peke ndani yake itawezekana (Mathayo 19:26). Wote tunastahali hukumu ya milele kwa sababu ya dhambi zetu, lakini Mungu kwa upendo wake usio na mwisho na neema vimetuwezeshea njia. “Kwa maana wote mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).

Hakika kunayo njia moja peke ya kupata wokovu na ni kumjua Mungu na Mwanawe, Yesu (Yohana 17:3). Wokovu haupatikani kwa matendo, bali kwa imani (Warumi 1:17; 3:28). Tutaipokea zawadi hii, haijalishi sisi ni nani au ni nini tumefanya (Warumi 3:22). “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolwea kwalo” (Matendo Ya Mitume 4:12).

Ingwa Wamomoni ni watu wa urafiki, wa upendo, na ni watu wakarimu, wamedanganywa na dini za uongo ambazo zageuza hali ya Mungu, utu wa Yesu Kriso, na njia za wokovu

Swali: "Mashahidi wa Yehova ni akina nani na wanaamini nini?"

KATIKA KUILINDA IMANI YETU NI MUHIMU KUFAHAMU JUU YA IMANI YA MASHAHIDI WA JEHOVA TUSIJE KUJIKUTA TUMENASA PASIPO KUZIJUA MBINU NA HADAA ZA ADUI SHETANI
NA ELIBARIKI ANDREW MUNA

Jibu:
Dhehebu liitwalo hii leo kama Mashahidi wa Yehova lilianzia Pennsylvania katika mwaka wa 1870 kama darasa la Bibilia likiongozwa na Charles Taze Russell. Russell akaliliita kundi lake “Uchao wa somo la Bibilia wa millennia.” Charles T. Russell alianza kuandika msururu wa vitabu ambavyo aliviita “Uchao wa millennia,” ambao ulikuwa ukubwa wa vitabu sita kabla ya kifo chake na vilikuwa na theolojia ambay mashahidi wa Yehova wanaishikilia sasa. Baada ya Russell kufa mwaka wa 1916, Mfalme J.F. Rutherford, rafiki wa Russell na mrithi, alikiandika kitabu cha saba na cha mwisho cha msururu wa “Uchao wa millennia,” “Fumbo lililo kamilika” katika mwaka wa 1917. Mnara wa mlinzi wa Bibilia na kijitabu cha jamii vilianzishwa katika mwaka wa 1886 na haraka vikawa gari ambalo kupitia kwao kikundi cha “uchao wa millennia” likaanza kusambaza mawazo yao kwa wengine. Kikundi kilijulikana kama “Warussell” hadi mwaka wa 1931 lilipo gawanyika kwa utaratibu, likaitiwa “Mashahidi wa Yehova.” Kikundi ambacho kilijitenga wakajiita “wanafunzi wa Bibilia.”

Mashahidi wa Yehova wanaamini nini? Kwa kuutafakari kwa karibu sana msimamo wa kanuni yao kwa masomo kama, mwili wa Kristo, wokovu, utatu wa Mungu, Roho Mtakatifu na upatanisho wa Mungu na mwanadamu yaonyesha bila shauku yoyote kuwa hawashikilii kanunu ya msimamo wa Kikristo katika masomo haya. Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa Yesu ndiye Mikaeli malaika mkuu, kiumbe kikuu. Hii inahitilafiana maandiko mengi ambayo wazi yamtaja Yesu kuwa Mungu (Yohana 1:1,14, 8:58, 10:30). Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa wokovu unapatikana kwa ushirika wa imani, matendo mazuri na itiivu. Hii inahitilafiana maandiko mengi yasiyo hesabika ambayo yasema wokovu unapatikana kwa neema kupitia kwa imani (Yohana 3:16; Waefeso 2:8-9; Tito 3:5). Mashahidi wa Yehova wanakataa utatu wa Mungu, wakiamini kuwa Yesu ni kiumbe na Roho Mtakatifu kuwa ni nguvu za Mungu zizokuwa na uhai. Mashahidi wa Yehova wanakataa dhana ya Kristo kuwa dhabihu kwa niabaa yetu na badala yake wanashikilia kuwa nadharia ya ukombozi, kuwa kifo cha Yesu fidia ya dhambi ya Adamu.

Ni namna gani Mashahidi wa Yehova wanathibitisha kanuni hii isiyo ya kibibilia? Kwanza, wanasema kuwa Kanisa imeiharibu Bibilia katika karne zilizopita; kwa hivyo wameifasiri tena na tena Bibilia kwa kile wanakiita Fasiri mpya ya ulimwengu. Mnara wa ulinzi wa Biblia na kijitabu cha jamii zilipadilishwa ujumbe wa bibilia kuifanya iingiliane na kanuni yao ya uongo, badala ya misingi ya kanuni yao kuwa katika mafunzo halisi ya Bibilia. Fasiri mpya ya ulimwengu imepitia katika toleo mbali mbali, Pia Mashahidi wa Yehova ndivyo walivyo pata maandiko ambayo yanahitilafiana na kanuni za Mungu.Zaidi ya hayo hawa tumii neno kanisa katika majengo yao ya ibada pia hawaongezewi damu pindi wakipatwa na ajali au upungufu wa damu,

Mnara wa Bibilia unaweka imani na kanuni katika asili ya upanusi wa mafunzo ya Charles Taze Russell, Akimu Joseph Frankli Rutherford, na waridhi wao. Kikao simamizi cha mnara wa Bibilia na kijitabu cha jamii ndio kikao pekee katika dhehebu ambao wadai kuwa na mamlaka ya kuyafasiri maandiko. Kwa maneno mengine, chenye kikao simamizi chasema kuhusu ujumbe wo wote wa bibilia unachukuliwa kuwa maneno ya mwisho na mafikirio binafsi yamekataliwa sana. Hii inahitilafiana moja kwa moja na mafunzo ya Paulo kwa Timotheo (na kwetu pia) kuisoma ili ukubaliwe na Mungu, ili tusihitaji kuahibika tunapofunza neno la Mungu. Mafunzo haya ambayo yanapatikana katika 2 Timotheo 2:15, maelezo wazi kutoka kwa Mungu kwa kila mmojawapo wa mtoto wake kuwa kama Wakristo wa Beroya ambao waliyatafakari maandiko kila siku kuakikisha kuwa mambo ambayo yalikuwa yakifunzwa yaliambatana na neno la Mungu.

Vilevile hakuna kikundi cha kidini ambacho ni kiaminifu kushinda Mashahidi wa Yehova kwa kushiriki injili yao; Kwa bahati mbaya ujumbe umejawa na upotovu, uongo na kanuni ya uongo. Ni maombi yangu Mungu ayafungue macho ya Mashahidi wa Yehova kwa ukweli wa injili na mafundisho ya kweli ya neno la Mungu

Swali: "Je! Wakristo wanastahili kwenda kwa madaktari?"



Na Elibariki Andrew Elly Andrew Muna
Jibu:
Kunao Wakristo wengine wanaoamini kuwa kutafuta msaada wa madaktari kunaonyehsa kutokuwa na imani kwa Mungu. Katika kikundi Neno-Imani, kumwona daktari kila mara inachukuliwa kuwa kutokuwa na imani ambayo itamzuia Mungu kukuponya. Kwa makundi kama, Wakristo Wasayansi, wanaotafuta usaidizi wa matibabu wakati mwingine unatazamwa kuwa kizuizi cha kutumia nguvu zetu za kiroho ambazo Mungu ametupa kujitibu. Utata wa mtazamo huu hasa unajitokeza kwasababu ya kuwepo kwa madhehebu yanayo kataza watu kwenda hospitalini mfano Mashahidi wa jehova. Ikiwa gari lako imearibiwa, unaipeleka kwa makanika au utangoja Mungu kutenda muujiza na kutengeza gari lako? Kama mfereji wa kupitishia maji kwenye nyumba yako umetoboka, unamngoja Munguaende akazibe mfereji wa maji?, au unamwita fundi? Mungu wetu anaweza kutengeneza gari na kuziba mfereji vile vile anafanya uponyaji katika miili yetu. Hoja kwamba Mungu anaweza na anatenda miujiza ya uponyaji haimanishi kuwa kila mara tutarajie muujiza badala ya kutafuta msaada kutoka kwa mtu aliye na ujuzi na maarifa ya kutuzaidia.

Madaktari kwetu tumeelezwa takribani dazeni katika Bibilia. Aya peke ambayo inachukuliwa katika muktadha kwa kufundishawatu kutokwenda kwa daktari ni 2 Mambo Ya Nyakati 16:12. “Akashikwa Asa na ugonjwa wa miguu katika mwaka wa thelathini na kenda wa kumiliki kwake; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta BWANA katika ugonjwa wake, bali waganga.” Shida haikuwa kuwa Asa aliwatafuta waganga, lakini shida ni kwamba “hakumtafuta BWANA.”Chamsingi hapa Hata wakati unamtembelea daktari, upeo wa imani yetu uwe kwa Mungu si kwa daktari.

Kunayo aya nyingi ambazo zazungumzia kutumia “madawa ya matibabu” kama vile kuweka viziba donda (Isaya 1:6), mafuta (Yakobo 5:14), mafuta na divai (Luka 10: 34), majani (Ezekieli 47: 12), divai (1 Timotheo 5: 23), na marhamu, hasa “zeri ya Gileadi” (Yeremia 8:22). Pia Luka mwandishi wa Matendo Ya Mitume na injili ya Luka tunaambiwa kuwa na Paulo yeye ni “tabibu mpendwa” (Wakolosai 4:14).

Mariko 5: 25-30 yahusiana na hadhiti ya mwanamke aliye kuwa na shida ya uvujaji damu, shida ambayo matabibu hawangeweza kuitibu ingawa alikuwa amewatembelea madaktari wengi na akatumia pesa zake zote alizokuwa nazo. Kukuja kwa Yesu, alifikiria kuwa akiguza pindo la nguo yake atapona; akaguza pindo la nguo yake na akaponywa. Yesu kwa kuwajibu Mafarisayo ya kuwa ni kwa nini alichukua muda wake mwingi na wenye dhambi aliwaambia, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi” (Mathayo 9:12). Kutoka kwa aya hii mtu anaweza kusonga kutoka kwa kanuni hizi:

1) Matabibu si Mungu na wazitazamiwe kuwa Mungu. Wakati mwingine wanaweza kuzaidia, lakini kutakuwa na wakati mwingine ambao watakayo yafikia ni kuchukua pesa zako tu.

2) Kumuona tabibu na kutumia njia za kishirikina“kunduia” zimelaaniwa katika maandiko.

3) Katika upungu wo wote wa nje wa mwili lazima tutafute Mungu kuingilia kati (Yakobo 4:2; 5:13). Mungu ahaidi kuwa atajibu sawa na vile tatakavyo hitaji kila wakati (Isaya 55: 8-9), lakini tuko na uakikisho kuwa yote ayafanyayo yatafanywa kwa upendo na kwa hivyo kwa manufaa yetu (Zaburi 145: 8-9).

Kwa hivyo, Wakristo wanastahili kwenda kwa madaktari? Mungu alituumba viumbe werevu na kutupa uwezo kuunda madawa na kujifunza jinsi ya kutibu miili yetu. Hakuna ubaya wo wote kwa kutumia ujuzi huu na uwzo kwa kutibu. Matabibu wanaweza kuonwa kama kipaji cha Mungu kwetu, njia ambayo kwayo Mungu analeta uponyaji. Kwa wakati huo huo, imani yetu inastahili kuwa kwa Mungu, si kwa madaktari au madawa. Kwa maamuzi yote magumu, tumtafute Mungu aliyeahidi kutupa hekima wakati tunajiuliza (Yakobo 1: 5)

Swali: "Wakristo wanastahili kutii sheria ya nchi?"


Pamekuwa na upotoshaji mkubwa kutoka kwa wanasiasa kutumia biblia vibaya katika kutekeleza propaganda za vyama vyao.ukweli fuatana nami .
NA ELIBARIKI ANDREW MUNA
Jibu:
Warumi 13:1-7 yasema, “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye k
isasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; asahiliye heshima, heshima.”

Ufahamu huu unaifanya kamili wazi kuwa tunastahili kutii serikali ambayo Mungu ameiweka juu yetu. Mungu aliiumba serikali ili iweke mpangalio, adhabu ya maovu, na kuendeleza haki (Mwanzo 9:6; 1 Wakorintho 14:33; Warumi 12:8). Tunastahili kutii serikali kwa kila jambo- kulipa ushuru, kutii amri na sheria, na kuonyesha heshima. Ikiwa hatutafanya hivyo, twaonyesha kutokuwa na heshima/madharau kwa Mungu, kwa sababu ni yeye Mwenyewe ameiweka serikali juu yetu. Wakati mtume Paulo aliandika Warumi, alikuwa chini ya serikali ya Rumi wakati wa mfalme Niro, ingawa alikuwa mfalme mwovu kati ya wafalme wote wa Rumi. Paulo bado aliitambua serikali ya Kirumi kuwa na mamlak juu yake. Tunawezaje kufanya chini ya hiyo?

Swali lingine ni “Kunao wakati tunastahili kukaidi sheria ya nchi kimakusudi?” Jibu kwa swali hilo linaweza patikana katika Matendo Ya Mitume 5:27-29, “Walipowaleta, wakawaweka katika baraza, kuhani Mkuu akawauliza, akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu Yule juu yetu. Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.” Hii iko wazi kuwa bora tu sheria ya nchi haitilafiani na sheria ya Mungu, wote tumefungwa kuitii sheria ya nchi. Pindi tu sheria ya nchi inahitilafiana na amri ya Mungu, tunastahili kuikataa sheria ya nchi na kutii sheria ya Mungu. Ingawa hata kwa hali hiyo tunastahili kuikubali mamlaka ya serikali juu yetu. Hii imedhihirishwa kwa hoja kuwa Petro na Yohana hawakuwapinga kwa kuwateswa, bali walifurahi kuwa waliteseka kwa kumtii Mungu (Matendo Ya Mitume 5:40-42)

JOHN MALECELA NA MWL. NYERERE

Suluhu ya uongo wa Malawi na ukimya wa Tanzania



Rai Mwema Toleo la 265
24 Oct 2012
HIVI karibuni yameibuka tena malumbano kuhusu mpaka baina ya Tanzania na Malawi. Malumbano haya ni mwendelezo wa fikra za aliyekuwa Rais wa Malawi, Kamuzu Banda kwamba, Malawi inayo miliki ya eneo lote la Ziwa Nyasa kulingana na makubaliano ya Wajerumani na Waingereza ya mwaka 1890.

Hata hivyo baada ya kulitafakari suala hili na kupata misimamo tofauti, sasa ni bayana kuwa Malawi haikuwahi kupewa wala kujitangazia umiliki wa eneo lote la Ziwa Nyasa.

Ajabu kubwa zaidi ni kwamba pia Malawi haikujadiliwa wala kuandikwa katika makubaliano ya Heligoland. Hivyo inashangaza ni jinsi gani Malawi imeweza kujiingiza kinyemela katika wahusika wa makubaliano yale na kuisukuma Tanzania katika kupambana na uhalali wa makubaliano badala ya upotofu wa tafsiri ya Kamuzu Banda.

Mshangao huu unazidi kukua inapoonekana kuwa Malawi inaanza kufanikiwa katika kuishinikiza Ujerumani iyakane majukumu, matakwa na maumivu yake kuhusiana na makubaliano yale.

Zipo sababu tatu zinazonifanya niamini kuwa Malawi au Rhodesia ya wakati ule si mhusika katika makubaliano ya Heligoland na pia makubaliano yale si ufumbuzi wa mgogoro baina ya Malawi na Tanzania.

Sababu ya kwanza ni kwamba majadiliano ya Heligoland hayakuhusu himaya ya Malawi, Rhodesia au eneo la kusini magharibi la “German East Africa”. Pili, makubaliano yale hayakuhusu umiliki wa eneo lolote la mto, ziwa au bahari. Kadhalika, makubaliano yale hayakuhusu mipaka baina ya himaya au nchi tofauti.

Kuhusu dhana ya kuchangia mipaka, ramani za miaka ya 1890, na hadi miaka ya 1930, zilionyesha mipaka miwili iliyoenda sambamba, ambayo iliachana kabisa kuelekea kingo tofauti za mito au maziwa makubwa. Kwa maana hii himaya iliyoitwa Rhodesia ilikuwa na mpaka wake katika ukingo wa magharibi wa Ziwa Nyasa, sambamba na ule wa “German East Africa” uliokuwa ukingo wa mashariki mwa ziwa hilo. Kwa utaratibu huo Ziwa Nyasa lilibaki katikati ya himaya hizo za kikoloni kama eneo lisilokuwa na ardhi au jamii ya kutawaliwa kama koloni.

Kwa vile Ziwa Nyasa halikumilikishwa mwaka 1890, Wajerumani na Waingereza waliligombea mwaka 1914, ambapo Ujerumani ilishindwa na kuondolewa katika eneo lote la Tanganyika. Baada ya hapo, Uingereza ilikuwa na uhuru na uwezo wa kuamua lolote kuhusu umiliki wa Ziwa Nyasa.

Hata hivyo, nyaraka zilizopo zinaonyesha kuwa hakuna uamuzi wowote uliofanyika kuhusu jambo hilo. Historia inaonyesha kuwa baada ya uhuru, Rais Nyerere alifanya mawasiliano akitaka kujadiliana na Serikari ya Malawi kuhusu umiliki wa ziwa hilo, ambapo Rais Kamuzu Banda alijibu kwamba makubaliano ya Heligoland yanaweka bayana mpaka wa Malawi na Tanzania ni kingo za Ziwa Malawi.

Banda alisema: "But our terms are clear on this. According to the 1890 Heligoland agreement between Britain and Germany, the border between Malawi and Tanzania is the edge of the waters of Lake Malawi.

Kifungu cha makubaliano ya Heligoland ambacho Rais Banda alikipotosha na kukitumia kinyemela ni kile kinachoainisha mwisho wa ardhi ya “German East Africa”, upande wa kusini magharibi, ambacho kilisomeka kwamba: “To the south by the line that starts on the coast of the northern border of Mozambique Province and follows the course of the Ruvuma River to the point where the Messinge flows into the Ruvuma. From here the line runs westward on the parallel of latitude to the shore of Lake Nyasa. Turning north, it continues along the eastern, northern, and western shores of the lake until it reaches the northern bank of the mouth of the Songwe.”

Tafsiri ya kifungu hicho ninayoipata mimi ni kwamba hakikuwa sehemu ya makubaliano au makabidhiano. Badala yake kifungu hicho ni sehemu ya utambuzi wa ardhi ya Tanganyika au “German East Africa”, ambayo haikuwa na uhusiano au mgusano na ardhi ya Rhodesia au Malawi. Japokuwa kifungu hicho kimeandikwa katika makubaliano hayo, hakikutokana na makubaliano ya kukabidhiana vipande vya ardhi vilivyohusika.

Badala yake kifungu kile ni sehemu ya maelezo kuhusu upana wa ardhi ya “German East Africa”. Hakuna sehemu yoyote ya makubaliano yale inayotaja ukaribu au ujirani na himaya nyingine ng’ambo ya maji kama vile Malawi, (Rhodesia) Zambia, Kenya, Burundi, DRC, Uganda, India, Msumbiji au Australia.

Kwa vile Ziwa Nyasa halikuwahi kugawanywa au kumilikishwa, watawala wa Kiingereza waliokuwa upande wa Malawi waliendelea kukiri, kukariri na kukazia kila mwaka ukweli kuwa hawakuwa na miliki ya eneo lote la ziwa hilo.

Nimejitahidi kutafuta mwaka ambapo walikiri hivyo kwa uwazi ulio mkubwa zaidi, na nimegundua kuwa pengine ni mwaka wa 1936, ambapo ripoti ya serikali yao ilikuwa na kifungu cha maneno kilichosema kuwa: “The Nyasaland Protectorate consists of a strip of land some 520 miles in length and varying from 50 to 100 miles in width, bounded on the east by Lake Nyasa, on the south by Portuguese East Africa, on the west by North-Eastern Rhodesia and on the north by the Tanganyika Territory”.

Ingekuwa bora zaidi kama viongozi wa Tanzania wangethibitisha haraka ubatili na upotofu wa mawazo ya Rais Banda. Badala yake Serikali ya Tanzania iliamua kuachana naye kwa matumaini kuwa ingetokea nafasi ya kujadiliana na viongozi wenye busara au bashasha zaidi baada ya utawala wake.

Ni kweli kuwa viongozi hao tayari wametokea na kushika madaraka huko Malawi, ambapo Rais wa sasa ni Joyce Banda. Pamoja na mabadiliko hayo ya kiutawala, bado ni vigumu sana kuziona busara za Banda huyu iwapo Tanzania haitafanikiwa kuibatilisha na kuibomoa kabisa tafsiri potofu iliyojengwa na Banda wa kwanza.

Badala ya kuonyesha upotofu wa tafsiri iliyopandikizwa na Kamuzu Banda, Tanzania imejikita zaidi katika kupingana na makubaliano ya Heligoland, na kusisitiza kwamba raia wake wanaoishi jirani na Ziwa Nyasa wanazo haki za msingi za kuteka maji ya kunywa na kuvua samaki. Japokuwa hatua kama hizo ni muhimu sana, ukweli ni kwamba haki hizo za Mwenyezi Mungu hazitokani na huruma ya Malawi, wala utetezi wa Tanzania, au hata hukumu ya mamlaka yoyote duniani.

Yapo mambo mawili yanayoweza kubatilisha au kuharibu haki za kuteka maji na kuvua samaki kwa upande wa Tanzania. Jambo la kwanza ni uwezekano wa kuimilikisha Malawi jamii za wakazi wa Mbeya, Njombe na Songea, kama Rais Banda alivyowahi kudai na kuona haraka kuwa haingewezekana kabisa.

Jambo la pili, ambalo linawezekana na linaelekea kabisa, ni kujengeka kwa huruma, utetezi au hukumu kuelekea kuiachia Malawi itekeleze mipango ya uharibifu endelevu wa rasilimali za maji, samaki, na viumbe asilia ndani ya Ziwa Nyasa.

Kwa vile ni dhahiri kuwa Malawi haiwezi kuzuia Watanzania kupata haki za kuchota maji, kuvua samaki na kufanya shughuli za kiasili katika Ziwa Nyasa, ni bora Serikali ya Tanzania iwe makini ili kuepuka uwezekano wa kupuuzwa au kuliwazwa kwa kupewa haki hizo.

Jambo la msingi ni kwamba serikali za Malawi na Tanzania zinawajibika kujenga matumizi endelevu ya rasilimali katika Ziwa Nyasa. Katika kufanya hivyo serikali hizi zinawajibika kukubaliana na kuutangazia ulimwengu ni kwa kiwango gani zimefanikiwa kushirikiana katika kutekeleza matakwa ya kimataifa, ambayo ni kuwajibika katika shughuli za maendeleo kwa ushirikiano, badala ya kugawana au kugombea maji.

Bila kuainisha maeneo ya ushirikiano wa pamoja, na bila kupigana vita, mamlaka za kimataifa haziwezi kuona umuhimu wa kutoa hukumu inayohusu mgawanyo wa maji ya Ziwa Nyasa.

Jambo pekee linaloweza kupatikana ni kupuuzwa na kuambiwa kuwa “Nendeni kwanza mkazungumze na kushirikiana katika kutekeleza mipango endelevu ambayo nyote mnalazimika kuikubali”.

Baadhi ya mambo hayo ni kuzuia uvuvi haramu, kulinda mazingira, kusaka majambazi, na kufanya utafiti. Iwapo Serikali ya Tanzania inajihusisha na mikakati kama hiyo ni rahisi kuonyesha kuwa inahitaji matumizi ya boti za doria, askari wa majini na silaha za moto. Kwa maana hii ni muhimu Tanzania iweke bayana majukumu ya msingi inayohitaji kutekeleza ndani ya Ziwa Nyasa yanayohusu maendeleo ya watu wa kawaida, na ni kwa kiasi gani baadhi yake yanakwazwa au kuchafuliwa na shughuli zinazoendelea upande wa Malawi.

Shughuli mojawapo ambayo inatajwa sana ni matarajio ya Malawi kutaka kuchimba mafuta ndani ya ziwa. Bila kujali mafuta yanayotafutwa na Malawi yapo upande wa kusini, magharibi au mashariki, Serikali ya Tanzania inao wajibu wa kuweka pingamizi na kuzuia harakati hizo zisiendelee bila kuwapo mikataba miwili mahsusi ya Ziwa Nyasa.

Mkataba wa kwanza ni ule utakaohusu matumizi endelevu ya maji safi na uhai wa viumbe na mkataba wa pili ni ule wa kuzuia au kudhibiti uchimbaji wa mafuta ndani ya ziwa. Mikataba ambayo Tanzania inataka kutumia katika mzozo huu inaeleza wazi kuhusu usafi wa maji na uhai wa viumbe asilia, bila kujali mipaka ya kisiasa au ile ya kikoloni.

Ziwa Nyasa ni hazina ya maji safi na viumbe adimu duniani, ambavyo kwa ujumla wake vina thamani kubwa zaidi kuliko mafuta au hata dhahabu. Ni makosa kabisa kufikiri kwamba mafuta ni bora kuliko maji safi na viumbe hai ndani ya ziwa.

Kilichotokea Mbagala ni hasira za Waislamu? II


Evarist ChahaliUskochiToleo la 265
24 Oct 2012
KABLA ya kuingia kwa undani katika makala hii ambayo ni mwendelezo wa makala iliyochapishwa katika toleo la wiki iliyopita, naomba niwasimulie wasomaji mkasa ambao unaweza kuwa “funga kazi” katika utitiri wa vimbwanga vya watawala wetu.

Wiki iliyopita, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, aliwatia aibu Watanzania akiwa Afrika Kusini alipodai kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaundwa kwa Muungano kati ya kisiwa cha Bahari ya Hindi cha Pemba na Zimbabwe. Ukidhani ninamsingizia, basi angalia video hii kupitia kiunganishi hiki; http://goo.gl/uW6H2

Na licha ya kufanya madudu hayo, Mulugo ‘alilikoroga’ zaidi alipodai kuwa Muungano huo wa ‘Zimbabwe na Pemba’

ulitokea mwaka, (namnukuu) “one nineteen sixty-four.” Mwaka huo hauleti maana yoyote, iwe kwa Kiingereza au kwa Kiswahili, kwani 1-19-64 inaweza tu kuleta maana kwa mfumo wa tarehe wa Marekani (yaani tarehe 19 mwezi wa kwanza mwaka 64).

Ninaomba nitamke bayana kuwa Naibu Waziri Mulugo ni mzembe wa hali ya juu. Yawezekana aliandaliwa hotuba hiyo, lakini haihitaji busara japo kidogo kuwa huwezi kukurupuka kutoa hotuba kabla hujaipitia. Sijui Rais Jakaya Kikwete alijisikiaje baada ya kuona video hiyo yenye hotuba ya Mulugo, lakini kwa kosa hilo la ajabu kabisa, Naibu Waziri Mulugo sio tu anapaswa kutuomba radhi Watanzania kwa kupotosha historia ya taifa letu bali pia ingefaa aondolewe katika wadhifa wake unaoshughulikia elimu (elimu gani hiyo ambayo wakati Tanzania ‘haijamalizana’ na Malawi kuhusu mpaka kwenye Ziwa Nyasa, yeye ‘anaihamasisha Zimbabwe ‘idai Pemba ni sehemu ya nchi hiyo?’)

Nisiongelee sana suala hilo bali ninawaachiwa Watanzania wenzangu kuhitimisha wenyewe kuhusu madudu haya ‘ya karne.’

Kama nilivyoahidi katika toleo lililopita, wiki hii ninaendelea na mjadala kuhusu vurugu za kidini ambazo kwa siku za karibuni zinaonekana kushika kasi.

Katika makala iliyopita, nilijaribu kuonyesha sababu zilizojenga msingi wa manung’uniko ya Waislamu katika masuala ya elimu na ajira. Mwishoni mwa makala hiyo niliuliza maswali yafuatayo (ninajinukuu)

“Je; kilichotokea Mbagala ni hasira tu za baadhi ya Waislamu waliochukizwa na kitendo cha ‘mtoto wa Kikristo’ kukojolea Kuran Tukufu?

Je; udini ni tatizo kubwa katika Tanzania yetu ingawa halizingumzwi vya kutosha? Binafsi, ninaamini jibu la swali hilo, ni ndiyo. Kama ni ndiyo, kwa nini tunalikwepa tatizo hili?

Je; yawezekana udini ni turufu muhimu kwa baadhi ya wanasiasa mufilisi?”

Kwa swali la kwanza, nilishabainisha kwenye makala hiyo kuwa kwa mtizamo wangu, vurugu hizo za Mbagala zilisababishwa na zaidi ya hasira za baadhi ya Waislamu waliokasirishwa na kitendo cha mtoto kuikojolea Kuran Tukufu.

Yayumkinika kusema kuwa hasira za baadhi (na pengine ni wengi) ya Waislamu huko nyumbani (Tanzania) ni dhidi ya kile kinachotajwa kama ‘Mfumo Kristo.’ Kwa kifupi, wanaoamini hivyo wanauona mfumo huo unawapendelea Wakristo sambamba na kuwabagua Waislamu, hususan katika sekta za elimu na ajira, ambazo kimsingi zinahusiana kwa karibu.

Japo, kama nilivyobainisha katika makala yangu iliyopita kuwa Ukristo kwa kushirikiana na ukoloni ulichangia kutengeneza hali ya kutokuwa na usawa katika elimu na ajira, haimaanishi moja kwa moja kuwa Wakristo wanawabagua Waislamu. Naomba nieleweke hapa: kuna tofauti kati ya mfumo na watu wanaonufaika au kuathiriwa na mfumo huo.

Ninasema hivyo kwa sababu, wakati hoja ya kuwa Wakristo wanawabagua Waislamu ingeweza kuwa na mashiko wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa, ambao wote ni Wakristo, ni vigumu kwa hoja hiyo kuwa na uzito kwenye Awamu ya Pili na hii ya sasa (ya Nne) za marais Waislamu Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete.

Hata hivyo, kwa mtizamo wangu, viongozi hao wote wanne, hawawezi kukwepa lawama kuwa kwa kiasi kikubwa hawajafanikiwa sio tu kuyatupia macho kwa makini malalamiko ya Waislamu bali pia wamekuwa wakikwepa kuyashughulikia kwa uzito unaostahili.

Angalau kwa upande wa Baba wa Taifa tunaweza kukubaliana kuwa sio tu kwamba alishakiri kuwa kukosekana kwa usawa katika elimu na ajira kwa Waislamu ni tatizo, lakini pia alikwenda mbali zaidi na kujaribu kuukarabati mfumo wa elimu ili uweze kutoa fursa kwa Watanzania wote bila kujali imani zao.

Ni muhimu kukumbuka kuwa licha ya ukweli kuwa Mwalimu alikuwa Mkristo na mshika dini, mafanikio yake katika harakati za kupigania uhuru yalichangiwa zaidi na Waislamu.

Lawama ‘kubwa’ inayoweza kuelekezwa kwa Mwalimu ni jinsi serikali yake ilivyoshughulikia suala ‘nyeti’ la uundwaji Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kupigwa marufuku Jumuiya ya Ustawi wa Waislamu wa Afrika Mashariki (East African Muslim Welfare Society- EAMWS).

Kwa kifupi, tangu kuundwa kwake, kwa kiasi kikubwa BAKWATA imeshindwa kujitenganisha na serikali, na pia imeshindwa kufuta hisia kuwa ‘ni chombo kinachotumiwa na serikali kuwagawanya na kuwakandamiza Waislamu.’

Japo EAMWS ilikuwa taasisi ya kidini lakini ilionekana kama ‘mkombozi wa Waislamu’ hususan kwenye sekta ya elimu, na yayumkinika kusema kuwa laiti kuundwa kwa BAKWATA kungeibua taasisi yenye ufanisi kama EAMWS, basi pengine pengo lililopo kwenye maeneo ya elimu na ajira kati ya Waislamu na Wakristo lingekuwa limepungua kwa kiasi kikubwa.

Ufinyu wa nafasi unaninyima fursa ya kuingia kwa undani kujadili hoja za kuifungia EAMWS na hatimaye kuanzisha BAKWATA, lakini ukweli kwamba serikali hiyo hiyo iliyoipiga marufuku EAMWS ilishiriki kikamilifu katika uundwaji wa BAKWATA umechangia kudumu kwa hisia kuwa ‘BAKWATA iliundwa kama chombo cha serikali dhidi ya Waislamu.’

Na katika utafiti wangu, matokeo ya awali yanaonyesha Waislamu wengi hawaridhishwi na mwenendo wa BAKWATA katika kutetea maslahi yao. Kimsingi, moja ya jambo lilionekana ‘kuwaunganisha’ wahojiwa wangu wa Kiislamu (ambao nilieleza katika makala iliyopita kuwa niliwagawanya katika makundi mawili ya ‘walio na msimamo mkali’ na ‘wa kawaida’- kwa minajili ya kiutafiti- ni suala hilo la BAKWATA.

Sasa katika mazingira haya ambacho chombo pekee kikuu kinachotarajiwa kuwaunganisha Waislamu kinaonekana kuwa kinawakandamiza, na-kuwanukuu baadhi ya wahojiwa- ni sehemu ya ‘Mfumo Kristo’ ni wazi kuwa baadhi (na pengine wengi) ya Waislamu wanajiona kama ‘mateka wa mfumo,’ kwa maana ya hisia za kubaguliwa na Wakristo na kubaguliwa na chombo kinachopaswa kutetea maslahi yao (BAKWATA).

Kwa mtizamo wangu, kuwa ‘mateka wa mfumo usiokubalika’ kunasababisha kuuchukia, na kama tujuavyo, chuki huzaa hasira. Hasira hizo zinasubiri mazingira ‘mwafaka’ ili zichomoze hadharani. Na tukio kama la Mbagala lilitoa ‘fursa mwafaka’ kwa hasira hizo.

Na ‘hasira’ hizo zinatoa jibu la swali la pili kuhusu udini. Kwamba Waislamu wanawachukia Wakristo, sitaki kuamini hivyo. Kwamba Waislamu (baadhi au wengi) wanachukizwa na mfumo wanauona kuwa unawabagua na kuwapendelea Wakristo, binafsi jibu langu ni ndio.

Na kwa vile ni vigumu kutofautisha ‘Mfumo Kristo’ na Wakristo kama waumini wa dini, ni muhimu kutambua kuwa kwa namna fulani-kubwa au ndogo- kuna uhasama wa kisaikolojia au kihisia kati ya madhehebu haya mawili. Kinachosaidia ‘kuficha’ uhasama huo ni misingi iliyojengwa huko nyuma ambayo ilisisitiza zaidi Utanzania wetu kuliko Uislamu au Ukristo wetu.

Kwa bahati mbaya-au makusudi-misingi hiyo inavunjwa kwa nguvu na wanasiasa waliokuja baada ya Mwalimu Nyerere. Kwa kifupi, wakati siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ilijenga misingi ya kutuunganisha Watanzania tuwe kitu kimoja, ‘ubabaishaji’ uliofuatwa-kwa mfano kinachoitwa Azimio la Zanzibar- umechangia sana kukuza ombwe lililotokana na ‘kifo cha Ujamaa,’ na wakati huo huo kutoa fursa kwa wenye ‘hasira’ zao kuziweka hadharani.

Kama nilivyowahi kuandika katika makala moja huko nyuma kuhusu unafiki wetu kuhusu suala la ushoga (hoja kubwa ikiwa ni imani zetu za kidini na mila na desturi zetu), kuna unafiki unaoendelea katika sio tu kuzungumzia suala la udini kwa uwazi zaidi bali pia hakuna utashi wa kisiasa (na hata kijamii) kukabili tatizo hili.

Ni nani asiyejua kuwa wakati wa utawala wa Mwinyi kulikuwa na baadhi ya Wakristo waliokuwa wakinung’unika chini chini kuwa teuzi za Mwinyi zilikuwa zinapendelea Waislamu? Ni nani pia asiyejua kuwa alipokuja Mkapa lawama kama hizo ziliendelea kuwapo chini chini kuwa Mkapa alikuwa akiwapendelea Wakristo? Na ni nani atakayejifanya hajui kuwa utawala wa Rais Kikwete umekuwa ukilaumiwa chini chini kuwa unawapendelea Waislamu?

Ninafahamu kuna watakaosema hizi ni hisia zangu tu. Hawa ndio ninaowaita wanafiki. Na unafiki huu ndio miongoni mwa vikwazo vikubwa vya kujadili tatizo la udini, na vurugu zinazohusishwa na tatizo hilo, kwa hofu ya kuitwa mdini. Niseme hivi, bora niitwe mdini kwa kujitoa mhanga kuanzisha mjadala wa suala hili kuliko ‘nionekane mwema’ ilhali tunalipeleka taifa letu mahali kusikofaa.

Nitajitahidi kuhitimisha mfululizo wa makala hizi kuhusu vurugu za kidini kwenye toleo lijalo, au pengine makala mbili zijazo. Hata hivyo, nihitimishe makala hii kwa jibu fupi kwa swali la tatu kuhusu udini unavyotumiwa na wanasiasa mufilisi kwa minajili yao binafsi.

Ninaamini sote tunakumbuka jinsi kampeni za uchaguzi mkuu uliopita zilivyogubikwa na tuhuma za udini. Na hapa nisiume maneno: chama tawala CCM kilifanya kila jitihada kuufanya ‘upadri’ wa mgombea wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, kuwa turufu muhimu ya kumnyima kura za Waislamu. Hili nitalijadili kwa kirefu katika makala ijayo, lakini kwa namna fulani, CCM haiwezi kukwepa lawama kuwa ni miongoni mwa vyanzo vya vurugu za kidini tunazoshuhudia hivi sasa.

Chama cha siasa kinapoamua kwa makusudi kuwagawa wapiga kura kwa misingi ya imani zao za kidini, kinaandaa ‘viungo’ kwa ajili ya vurugu za kidini. Na ikumbukwe kuwa ni CCM hii hii iliyowahadaa Waislamu kuhusu kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi (huku ikitambua kuwa haina dhamira ya dhati ya utekelezaji wa ahadi hiyo) na hadi sasa inaendelea kucheza danadana katika suala hilo.

Nimalizie makala hii kwa kuwakumbusha Watanzania wenzangu kuwa tuna kila kitu cha kupoteza (everything to lose) kwa kutengana kwa misingi ya kidini na hatuna cha kupoteza (nothing to lose) tukiendelea kuwa wamoja, kama majeruhi wa ufisadi, umasikini, magonjwa na dhahma nyingine zinazotukabili ambazo hazijali imani zetu za kidini. Ili Tanzania yetu ifike mahala tunapotamani ifike, au inapostahili kuwa, ni lazima tuwe kitu kimoja. Tukumbuke, UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU

Kilichotokea Mbagala ni hasira za Waislamu?



Raia MWEMA
Evarist ChahaliUskochiToleo la 263
17 Oct 2012
KWA mara nyingine, wiki iliyopita Tanzania imeshuhudia ‘sura mbaya’ (ugly face) ya imani ya kidini. Kwa mujibu wa taarifa zenyewe, kilichoanza kama mchezo wa watoto kilisababisha vurugu kubwa zilizopelekea makanisa zaidi ya matano kuchomwa moto, sambamba na uharibifu wa mali kadhaa.

Inaelezwa kwamba chanzo cha vurugu hizo ni kitendo cha mtoto mmoja kuikojolea Kuran Tukufu baada ya ‘mabishano ya kitoto’ na mtoto mwenzie. Habari zinasema mtoto aliyefanya kitendo hicho alitaka kuthibitisha ukweli wa ‘tishio’ alilopewa na mtoto mwenzie kuwa iwapo atakikojolea Kitabu hicho Kitukufu, basi atageuka nyoka!

Sote tuliwahi kuwa watoto katika hatua za mwanzo za maisha yetu, na kwa kutumia uzoefu huo kama ‘watoto wa zamani’ tunaweza kukumbuka vitu vya ajabu, vya kukera, vya kuchekesha, na vya kila aina ambavyo twaweza kuvihitimisha kwa msemo huu wa Waingereza: ‘kids will always be kids’ (watoto wataendelea kuwa watoto).

Kwamba binadamu, pasipo kujali umri wake, anaweza kukojolea Kitabu Kitukufu cha dini fulani, ni jambo lisilopendeza hata kidogo. Na kwa hakika, kitendo cha aina hiyo, kitamchukiza kila muumini wa dini husika. Lakini kama ilivyo katika maeneo mengine ya maisha ambapo umri unaangaliwa kama kigezo muhimu cha kuhukumu tendo, ukweli kwamba aliyekojolea Kuran Tukufu ni mtoto wa miaka 14, ulipaswa kupewa uzito na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam ambao waliamua kuchukua sheria mkononi kwa kufanya vurugu kubwa ikiwa ni pamoja na kuchoma moto makanisa.

Licha ya kuguswa na tukio hilo la kusikitisha kama Mtanzania na Mkristo, lakini pia nimeguswa kwa vile linahusiana na eneo ambalo nimekuwa nikihangaika nalo kitaaluma kitambo sasa. Miaka michache iliyopita, nilikuja huko nyumbani kukusanya data kwa ajili ya utafiti wa kitaaluma kuhusu harakati za vikundi vya Kiislam nchini Tanzania. Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu, utafiti huo bado haujakamilika japo katika hatua niliyofikia unaweza kutoa majibu fulani kuhusu kinachoendelea huko nyumbani hivi sasa.

Nilipata fursa ya kuzungumza na makundi makuu mawili ya waumini wa dini ya Kiislam. Wale tunaoweza kuwaita ‘wenye msimamo mkali’ na wale wa ‘wenye msimamo wa kawaida.’ Naomba nisisitize kuwa matumizi ya maneno ‘msimamo mkali’ na ‘kawaida’ ni kwa minajili ya mjadala tu. Ninatoa tahadhari hii mapema kwa kuchelea uwezekano wa shutuma kuwa ninawagawa Waislam katika makundi, ambayo kama ilivyothibitika katika utafiti wangu, wengi wao hawapendi mgawanyo wa aina hiyo kwani wanaamini wote ni Waislam.

Moja ya mambo yaliyojitokeza katika mahojiano yangu na ‘makundi’ yote mawili ni manung’uniko (grievances) ambayo yamedumu kwa muda mrefu. Manung’uniko hayo yameshamiri zaidi kwenye suala la usawa katika elimu na ajira. Wahojiwa wengi walionyesha kuwa na hisia ya kubaguliwa kati yao na Wakristo katika upatikanaji wa fursa za elimu na ajira. Kimsingi, ukimnyima mtu fursa ya elimu, unatengeneza mazingira ‘mazuri’ ya kumkwaza kupata ajira.

Takwimu mbalimbali nilizokusanya katika utafiti huo, zinaweza kusapoti madai hayo. Lakini la muhimu zaidi hapa si sapoti ya takwimu hizo, bali mazingira yaliyopelekea uwepo wa hali hiyo. Kutokana na ufinyu wa nafasi ninalazimika kutoa maelezo ya jumla kwani kupitia kipengele kimoja hadi kingine kunahitaji zaidi ya makala moja.

Kwa kifupi, moja ya sababu zilizopelekea ‘ubaguzi’ katika upatikanaji wa fursa za elimu na ajira kati ya Waislamu na wasio Waislam (hususan Wakristo) ni mfumo wa utawala wa kikoloni. Kama tunavyofahamu, wakoloni walikuwa Wakristo, na tunafundishwa kwenye somo la historia kuwa miongoni mwa ‘watangulizi wa ukoloni’ walikuwa wamisionari wa Kikristo.

Moja ya mbinu zilizotumiwa na wamisionari kutengeneza mazingira mazuri ya kutawala jamii za Kiafrika ni ‘kusilimisha,’ japo neno hilo lina maana zaidi kwenye Uislam. Ninalitumia hapa kwa maana ya kuwatoa watu kutoka katika imani yao ya awali na kuwaingiza katika imani mpya.

Lakini historia inatufundisha kuwa Uislam ulifika huko nyumbani karne kadhaa kabla ya Ukristo. Kwa bahati mbaya au makusudi, walioleta Uislam walikuwa wafanyabiashara kutoka Arabuni na Mashariki ya Mbali, na hawakuwekea mkazo sana kusambaza dini yao.

Yayumkinika kuhitimisha kwamba kushindwa kwa watangulizi hao wa Uislam kueneza dini hiyo miaka kadhaa kabla ya ujio wa Wamisionari na hatimaye wakoloni, kulichangia kurahisisha kusambaa kwa Ukristo kwa ama ‘kusilimisha’ Wapagani (ninatumia neno hili kumaanisha dini za asili za Kiafrika) na Waislam.

Tukifupisha historia, mkoloni alitumia Ukristo kama moja ya njia za kuzitawala jamii zetu. Ni katika mazingira hayo, stadi mbalimbali zinaonyesha kuwa kwa namna fulani baadhi ya Wakristo walichelea kuunga mkono mapambano dhidi ya mkoloni kudai uhuru wetu hasa kwa vile wakoloni walifanikiwa kwa kiasi fulani kuulinganisha ukoloni na Ukristo (yaani kumpinga mkoloni ni sawa na kumpinga Yesu/Mungu).

Kwa kutumia Ukristo kama njia ya kurahisisha utawala wao, wakoloni pia walitumia dini hiyo kama chombo cha kuwatenganisha watawaliwa. Kimsingi, kuna aina ya mwafaka wa kitaaluma kuwa si kwamba wakoloni waliwathamini sana Wakristo wa Kiafrika, bali waliwaona kama nguzo muhimu katika kuigawa jamii, na hivyo kuwarahisishia kiutawala jamii husika.

Ingawa kuna wamisionari waliokuja Afrika kwa minajili ya kidini halisi, wengi wao waliendelea kushirikiana na utawala wa kikoloni katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na utoaji elimu. ‘Ushirika’ huu wa wamisionari na wakoloni katika utoaji elimu, unaweza kuelezewa kama mwanzo wa ujenzi wa tabaka la Wakristo wenye elimu na ‘wasio Wakristo’ (hususan Waislam) wasio na elimu.

Kadhalika, baadhi ya Waislam walichelea kujiunga na taasisi za elimu za wamisionari/wakoloni kwa kuhofia kuingizwa katika dini hiyo (Ukristo). Tukiweka hali ilivyokuwa kabla ya uhuru, mazingira yaliyojitokeza baada ya kuondoka mkoloni, yameendelea kwa kiasi fulani kurutubisha ‘ubaguzi’ huo wa elimu na ajira.

Baada ya kupata uhuru, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alikiri hadharani kuwa kuna umuhimu wa kurekebisha hali ya kutokuwapo usawa wa kielimu kati ya Wakristo na Waislam. Licha ya jitihada zake kubwa, hadi anaondoka madarakani ‘usawa’ huo haukuweza kufikiwa kwa kiwango cha kuridhisha.

Kuna maelezo mengine hapa. Shule za seminari za Wakristo ambazo kimsingi ni maalum kwa ajili ya ‘kuzalisha’ viongozi wa makanisa, zilikuwa ‘zikizalisha’ kundi la wasomi wa Kikristo ambao kwa sababu moja au nyingine, hawakuishia kuwa viongozi wa kanisa, bali wakachukua ajira serikalini au kwenye taasisi nyingine. Kwa upande mwingine, shule za kidini za Waislam ziliegemea zaidi kwenye utoaji elimu ya kidini, na katika mazingira hayo, tofauti na ilivyo kwa seminari, ‘hazikuzalisha’ wasomi wa kutosha kuingia kwenye ajira serikalini (naomba nieleweke kwa makini hapa).

Kwamba utawala wa Mwalimu Nyerere uliwapendelea Wakristo na kuwabagua Waislam, ni jambo ambalo halijathibitika kitaaluma. Hoja hiyo ni miongoni mwa masuala yanayojenga manung’uniko kwa baadhi ya Waislam. Kwamba baadhi ya Wakristo, hususan waliotoka seminari na kujiunga na ajira serikalini, waliwabagua Waislam na kuwapendelea Wakristo, ni jambo ambalo halijathibitika kitaaluma ingawa linawezekana kinadharia na kimantiki.

Kimsingi, tatizo si ubaguzi wa msomi/mwajiri Mkristo dhidi ya mwanafunzi/msaka ajira Muislam, bali mfumo ambao ulijengeka wakati wa ukoloni na umeendelea kuwepo. Unatoa nafasi (on merit) kwa Wakristo zaidi ya Waislam. Kama mwajiri anataka kujaza nafasi kwenye ofisi yake, anapaswa kuangalia, pamoja na mambo mengine, sifa za kitaaluma za waomba kazi. Sasa kwa vile mfumo wa elimu tuliorithi kwa mkoloni, na kama nilivyobainisha hapo juu, unatengeneza wasomi wengi wa Kikristo kuliko wa Kiislam, ni dhahiri kutarajia ‘ubaguzi’ wa nafasi za ajira.

Majuzi tumefanya sensa. Watawala wetu wamegoma kujumuisha kipengele cha dini kwa madai mbalimbali. Lakini kwa kufanya hivyo, watawala wanajinyima fursa ya kuelewa, kwa mfano uwiano wa ajira kati ya Wakristo na Waislam. Na cha muhimu hapo si kuelewa tu, bali pia kutafuta namna ya kurekebisha hali hiyo. Na hili ni tatizo la msingi linalofanya ‘tatizo la dini’ kuendelea kuwapo. Kuna hisia kwamba kwa kujaribu kulizungumzia suala hili kwa uwazi, kutazua tafrani kubwa kuliko mwafaka. Lakini sote tunajua kuwa ugonjwa hautibiki kwa kujidanganya kuwa haupo mwilini!

Je; kilichotokea Mbagala ni hasira tu za baadhi ya Waislam waliochukizwa na kitendo cha ‘mtoto wa Kikristo’ kukojolea Kuran Tukufu? Binafsi, naamini kuna sababu za ndani zaidi ya ‘hasira’ hizo na zinazosababisha ‘hasira’ hizo. Je; udini ni tatizo kubwa katika Tanzania yetu ingawa halizingumzwi vya kutosha? Binafsi, ninaamini jibu la swali ilo, ni ndiyo. Kama ni ndiyo, kwanini tunalikwepa tatizo hili?

Jibu linaweza kupatikana kwenye tatizo jingine ‘lisilozungumzika’ la kero za Muungano wa ‘Tanganyika’ na Zanzibar. Kwa kifupi, hadi sasa hakuna utashi wa kisiasa na kijamii kulikabili tatizo hili. Kwenye Muungano, kila Rais anachelea kuvunjikiwa na Muungano, ambao Baba wa Taifa ‘alishatoa radhi’ kwa atakayeuvunja. Kwenye hili la udini, viongozi wetu wanakwepa kulikabili kwa kuchelea kuonekana wadini. Kibaya, baadhi yao walitumia udini kwenye kampeni za uchaguzi mkuu uliopita. Je; yawezekana udini ni turufu muhimu kwa baadhi ya wanasiasa mufilisi?

UDINI BAADA YA UHURU

.
Wakoloni walipoondoka waliacha shule nyingi ambazo hazikuwabagua wananchi wa imani nyingine.Baada ya uhuru shule zote zilizokuwa za kikristu zilifanywa kuwa za serikali, wakristu hawakulalamika. Leo miaka 50 ni generation ya pili tangu uhuru waislaam bado hawatilii mkazo suala la elimu tumebaki kulalamika tunaonewa wakati tuna nafasi sawa na wengine! Mr. Chahali nadhani tatizo kubwa lililopo ni zaidi la kitamaduni kuliko la kidini, nasema ukweli mtupu...siyo suala la kudhania ila ni suala la utafiti tuliofanya tukiwa chuo kikuu huko Tanzania. Mfano, ukiangalia sehemu kubwa ambazo hazikupiga hatua ni za pwani, kwa nini? je ni dini ya kiislaam? inaweza kuwa kweli au hapana, utamaduni wa makabila kama wazaramo kwa kiasi kikubwa hazioni kama kusoma ni moja ya priority yao, na makabila mengine pia ya Dar, Zanzibar,pwani, Tanga, Mtwara, Lindi, Kigoma etc, imekuwa bahati mbaya kuwa wengi wanaoishi katika mikoa hii ni waislaam. Na upande mwingine ukienda ndani zaidi (Hinterland) kama Lushoto, utakuta kuna watu wengi ambao ni waislaam wamesoma kwa kiwango cha kutosha. Kuna waislaam wengi ambao wana msimamo wa kati (moderate) wanaliona hilo na hao wana uwezo wa kujua ukweli ambao ndio wasioamini kila kitu anachosema sheikh akiwa mimbarini. Tatizo kubwa lipo kwa waislaam wasiopenda kubadilika na kuwekeza katika elimu ambayo itawasaidia. wamejikita katika elimu ya dini.....sehemu ya familia yangu ni waislaam nakumbuka tukiwa kijitonyama mwalimu wa madrassa alikuwa akilalamika kwa watoto wa shangazi yangu kutokwenda kusoma madrassa badala yake wanakwenda shuleni siku za wiki, nilijaribu kumwelewesha kuwa watoto lazima wasome ili wafaulu kwenda secondary ili baadaye wapate kazi. Ndiyo najua elimu ya madrassa ni muhimu lakini hata ukimaliza utapata kazi gani? labda utakuwa sheikh....sikatai lakini uwezekano wa kupata kazi nyingine unakuwa finyu. Je utaweza kuwa daktari, rubani,accountant, bwana misitu, n.k bila kusoma elimu ya magharibi? Makamu wa rais Dk. Omar juma aliwaambia waislaam waache kulalamika kwani kazi inatokana na jinsi ambavyo umesoma...huwezi kuwa pilot bila ya kujifunza na hapo bila ya juhudi zako mwenyewe! Wote tuliozaliwa baada ya uhuru tulikuta shule zote za wakristo zimetaifishwa ( maaskofu na macardinals hawakuzidai ingawa ni haki yao kuzidai ) walielewa kila mtanzania anapaswa asome kitu ambacho hata kwenye shule za kanisa zinaendelea hadi leo isipokuwa kwenye seminari tu za madhehebu yote. Tutakuwa si wakweli tukisema kuwa dini fulani haikuwa na nafasi sawa na nyingine na kutaka wapewe upendeleo fulani....tulianza wote baada ya uhuru au hata kabla wakati wa uhuru (mbona kuna waislaam waliokuwa na elimu waliyopata nchini hata kabla ya uhuru). Kwa waislaam inabidi tubadilishe mindset zetu, tuongeze juhudi katika kusoma, ndiyo madrassa ni muhimu hata wakristo nao wanasoma dini yao lakini pia wanazingatia masomo mengine. Huwezi kusoma dini pekee yake ukategemea kupata kazi.......tusitafute wachawi, wachawi ni sisi wenyewe! Kila kiongozi katika nchi yetu amefanya kama inavyotakiwa, hakuna aliyefanya kwa upendeleo. source: RAIA MWEMA

Ndimi mbili za Zitto na kisa cha mkata kuti alilokalia



Evarist Chahal
10 Oct 2012
MIONGONI mwa faida ninazopata kutokana na uandishi wa makala katika jarida hili maridhawa, ni mawasiliano ya kila wiki na baadhi ya Watanzania wenzangu. Wengi wa ninaowasiliana nao, ni wasomaji ambao kwa namna moja au nyingine huwa wameguswa na mada ninazoongelea. Kuguswa huko hufuatiwa na ama pongezi au kukosolewa. Wakati mara nyingi pongezi huandamana na maneno ambayo si tu yananipa moyo na ujasiri zaidi wa kuendelea na uandishi wa makala hizi, mara nyingi kukosolewa huambatana na maneno yasiyopendeza kuyasoma au kuyasikia popote pale.

Baadhi ya wanaopongeza safu hii hudiriki kwenda mbali zaidi na kushauri labda nifikirie kuingia kwenye siasa. Mara zote jibu langu huwa lile lile. Najisikia fahari kuwatumikia Watanzania wenzangu kupitia uandishi wa makala, huku nikiamini kuwa si lazima kuwa mwanasiasa ili uweze kutekeleza jukumu hilo ipasavyo.

Lakini kwa upande mwingine, baadhi ya wanaonikosoa huenda mbali zaidi na kunituhumu kuwa uandishi wangu umeelemea kwenye chuki binafsi, husda na vitu kama hivyo. Jamaa mmoja alifikia hatua ya kudai kuwa makala zangu ni sehemu tu ya mikakati wa dini yangu dhidi ya utawala unaoongozwa na mtu anayetoka dini tofauti na yangu.

Kama ambavyo ninaridhishwa na pongezi kuhusu safu hii, huwa ninajifunza jambo moja au jingine kutoka kwa wakosoaji wangu (wengi wao hupenda kuhifadhi majina yao halisi). Kukosolewa huko, kunanisaidia kwa kiasi fulani, na hasa tukizingatia ukweli kwamba ukiona unamwagiwa sifa tu pasipo kuelezwa japo kasoro kidogo, basi yayumkinika kuhisi kuwa kuna mushkeli mahala fulani.

Nimelazimika kuandika hayo kutokana na ukweli kwamba makala yangu katika toleo lililopita ambayo pamoja na mambo mengine ilimzungumzia mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CHADEMA, Zitto Zuberi Kabwe, imetafsiriwa na baadhi ya wasomaji wangu kama sehemu ya kampeni zangu za kumkwamisha kuingia ‘Ikulu.’

Nimeshaeleza mara kadhaa katika baadhi ya makala zangu zilizopita kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote kile cha siasa, na nimekuwa hivyo kwa miaka kadhaa, tangu nikiwa huko nyumbani. Wakati, kwa kiasi kikubwa nilipokuwa huko nyumbani sheria ilikuwa inanikataza kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, kwa sasa uamuzi wangu wa kuwa neutral unachangiwa zaidi na imani yangu kuwa itikadi bora zaidi kwa mwananchi ni uzalendo na kuitumikia jamii kwa hali na mali.

Moja ya sifa kuu za sheria, ni kwamba iwe mbaya au nzuri, inabaki kuwa sheria hadi itakaporekebishwa au kuondolewa. Kuna nyakati tunalazimika kufuata sheria zinazokinzana na haki zetu (kimsingi sheria inapaswa kuendana na uwiano kati ya haki na wajibu), lakini tunalazimika kuzifuata kwa vile ndizo sheria zinazotawala.

Ni kwa mantiki hiyo, ninarejea tena kutofautiana na Zitto katika dhamira yake ya kutaka kuwa Rais wa Tanzania, kwa sababu kwa mujibu wa sheria tulizonazo, hatokuwa na sifa ya urais hapo mwaka 2015 kutokana na kuwa na umri pungufu ya ule unaotajwa kwenye sheria mama ya nchi, yaani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninaafikiana na Zitto kwamba sheria hii ni ya kionevu kwa sababu kama inawezekana kwa mtu wa miaka 40 kuwa Rais kwanini ishindikane kwa mtu mwenye miaka 39?

Hata hivyo, napenda kumfahamisha kuwa hadi hapo sheria hiyo itakaporekebishwa au kubadilishwa, pamoja na ‘ubaguzi’ inaoubeba, itaendelea kuwa sheria inayopaswa kufuatwa. Na kwa vile kwa mazingira ya kawaida tu inatarajiwa Rais kuwa miongoni mwa vinara wa si tu kufuata sheria, bali pia kuzilinda, itakuwa ni ‘utani mbaya’ kwa mtu anayetaka kuwa Rais kudhamiria kuvunja sheria kama hiyo inayokataza walio chini ya miaka 40 kugombea urais.

Nimesema ninamuunga mkono Zitto kwamba sheria hiyo ni ya kibaguzi. Lakini kama tunachukia ubaguzi kwenye sheria, basi pia tunapaswa kuchukia ubaguzi kwenye kila eneo, iwe kwenye jinsia, imani, asili, rangi na hata kundi la mtu katika jamii. Siku chache zilizopita, kulikuwa na taarifa za kwamba Zitto aliongea na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam na kutamka maneno yafuatayo:

“Wazee wetu walitusaidia sana kutupatia maendeleo ya kisiasa, sasa ni jukumu letu kuleta maendeleo ya kiuchumi. Ila naomba nisisitize kuwa jukumu hilo haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru, na ninatangaza nitagombea urais mwaka 2015.”

Binafsi, ninahitimisha kuwa kauli hiyo ni ya ubaguzi wa mchana kweupe. Lakini pia, licha ya ubaguzi, inaonekana kichekesho kwani imetoka kwa mwanasiasa (Zitto) ambaye hajawahi kuficha hisia zake dhidi ya ubaguzi wa watu kwa vigezo vya umri. Tukiweka kando taratibu za ndani ya CHADEMA kupata mgombea wake, moja ya sababu kuu zinazoonekana kama kikwazo kwa dhamira ya Zitto kuwa Rais, ni hiyo tuliyoiongelea hapo juu ya kutotimiza umri wa miaka 40 mwaka 2015 kama inavyotajwa kwenye Katiba.

Tunaomsapoti Zitto katika hoja yake hiyo, tunazingatia ukweli kwamba japo nchi haiwezi kuongozwa na mtoto wa miaka mitano, kwa mfano, mtu yeyote mzima (kiumri) anaweza kuiongoza nchi yetu pasipo umri wake kuathiri utendaji kazi wake. Utu-uzima si umri maalumu bali masafa (range) ya umri. Utu-uzima unaendana zaidi na uwezo wa mtu kutambua wajibu wake na kumudu kuutekeleza.

Wajibu huo unaweza kuwa katika ngazi ya familia (kama vile kuoa/kuolewa) au katika jamii pana, kama vile kushika dhamana ya uongozi.

Kwa hiyo, kimsingi, kama Zitto amemudu kuwatumikia wapigakura wa jimbo la Kigoma Kaskazini kwa mihula miwili sasa, sambamba na kulitumikia taifa kupitia uenyekiti wake kwenye Kamati ya Bunge, basi hakuna sababu ya msingi kwa umri wake kuwa kigezo cha kumzuwia kugombea urais mwaka 2015 hata kama atakuwa hajatimiza miaka 40. Ndiyo. Katiba inazuwia, lakini ukweli ni kuwa inazuwia kiuonevu!

Sasa wakati tunaafikiana na Zitto kupingana na uonevu huo wa Katiba, inakuwaje tena anatumia kigezo cha umri kuwabagua ‘wazee’ anaodai hawawezi kutuletea maendeleo ya kiuchumi? Busara ndogo tu ingeweza kumfahamisha Zitto-kama msomi-kuwa siasa na uchumi ni maeneo yanayotegemeana. Kama wazee waliozaliwa kabla ya Uhuru walimudu kutuletea maendeleo ya kisiasa, kwanini washindwe kwenye maendeleo ya kiuchumi?

Kama yeye aliyezaliwa baada ya Uhuru ameweza kufanya kazi nzuri kabisa katika uongozi wake wab kisiasa, ni kigezo kipi anachotumia kuwaona wazee waliozaliwa kabla ya Uhuru kuwa hawatoweza harakati za kuleta maendeleo yetu? Kwa hakika kabisa, huu ni ubaguzi, na kamwe mtu mwenye hisia za ubaguzi hapaswi japo kufikiriwa kuongoza nchi yetu.

Ninasema hivyo kwa sababu kama alivyotuusia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ubaguzi huzaa ubaguzi. Leo itakuwa “wazee waaliozaliwa kabla ya Uhuru hawawezi kutuletea maendeleo ya kiuchumi,” kesho itakuwa “Wakristo/Waislamu hawawezi kufanya hili,” “Wapogoro hawawezi kufanya lile,” au “wanawake hawawezi jukumu Fulani na kadhalika.

Naomba nimpe darasa dogo tu Mheshimiwa Zitto kuhusu kikwazo halisi cha maendeleo yetu. Uhaba unaozidi kukua katika uzalendo wa Mtanzania. Uzalendo hauna umri. Historia inatufundisha mengi tu kuhusu mchango wa wazee katika maendeleo ya sehemu zao husika. Mwalimu Nyerere, Nelson Mandela, Mahatma Ghandhi na kadhalika.

Binafsi, niliwahi kupishana kimtizamo na Zitto kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, ambapo katika hali ya kuchokoza mjadala, nilitamka kuwa muundo wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba haukuzingatia uwiano kati ya Wakristo na Waislam. Zitto alikerwa sana na hoja yangu hiyo aliyoiita ya kibaguzi. Alisisitiza kuwa tunapaswa kuangalia wasifu wa wajumbe kwa kigezo cha uwezo na uzoefu wao na si imani zao za kidini.

Cha kushangaza, ndani ya miezi michache tu, mtu huyo huyo aliyekemea vikali virusi vya ubaguzi (wa dini), amegeuka mfuasi wa ubaguzi wa umri. Kama tunapojadili teuzi mbalimbali tunapaswa kuangalia uwezo na uzoefu wa mteuliwa, kwanini basi wazee waliozaliwa kabla ya Uhuru wasitizamwe kwa uwezo na uzoefu wao kutuletea maendeleo ya kiuchumi, badala ya kuwahukumu kwa umri wao?

Ninaibua changamoto kama hiyo ya ‘ubaguzi’ kwa minajili, si ya kukwaza dhamira ya Zitto kuingia Ikulu mwaka 2015, bali kumsaidia kuamsha tafakuri yake iwapo utekelezaji wa dhamira hiyo utakuwa na manufaa kwake na kwa chama chake, au utaishia kuwa njia ya mkato kwa CCM kurejea madarakani huku CHADEMA ikiishia kuonekana chama cha mapambano kati ya vijana na wazee kukimbilia Ikulu.

Nimalizie makala haya kwa kukumbushia tena kauli ya Baba wa Taifa, ya kwamba yatupasa kuwaogopa kama ukoma wale wote wanaokimbilia Ikulu. Kama sisi wengine tunaweza kuitumikia nchi yetu kupitia makala zetu, huku wanasiasa kama Zitto wakimudu kututumikia kama wabunge, kisa cha kukimbilia Ikulu ambako Mwalimu alituasa kuwa anayefanya hivyo aogopwe kama ukoma, ni cha nini?

Simshawishi Zitto aachane na ndoto zake za urais kwani ninatambua hiyo ni haki yake ya kidemokrasia. Hata hivyo, ni muhimu kwa mwanasiasa huyo kijana kutambua kuwa wapenda mabadiliko ya kweli watamwona kama msaliti pindi ndoto zake hizo zitakapoishia kuwa kikwazo kwa CHADEMA kuing’oa CCM madarakani. Japo busara zinatueleza kuwa na ndoto pekee haitoshi, bali ni muhimu kutekeleza ndoto hizo kwa vitendo, ukiota unakata kuti unalokalia, na ukiamka ukaamua kulikata, sote tunajua matokeo yake.

Zitto anataka kusaliti CHADEMA


MWANAHALISI NOV 24,2010

MKUTANO wa kwanza wa Bunge la kumi uliomalizika Alhamisi iliyopita, mjini Dodoma, umeandika historia.

Ni kwa wabunge wa chama kikuu cha upinzani nchini – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kususia hotuba ya rais Jakaya Kikwete na kutoka nje ya ukumbi wa bunge.

Hilo ni tukio la kwanza kumkuta rais wa Jamhuri tangu taifa hili lipate uhuru, miaka 50 iliyopita.

Wengi wamezungumzia tukio hilo, lakini wengi wao, wamejikita katika kulaumu CHADEMA.

Bali, tukio lile lina sura nyingi za kujadiliwa. Kwa mfano, kuna rais anayesusiwa; aliyejibu ususaji kwa njia ya vijembe na kejeli; na kuna wabunge waliozomea badala ya kusikitika.

Kuna waziri mkuu anayelaumu na kulaani badala ya kuchukua hatua kabla ya tukio lenyewe kutokea; kuna serikali iliyoshindwa kuongea na viongozi wa CHADEMA ili kumuepusha mkuu wa nchi na aibu iliyompata.

Yupo spika “mwanafunzi” ambaye ameshindwa kufanya jitihada zozote za wazi kuepusha aibu iliyotokea na ambayo imemfunika yeye na historia yake aliyoiweka siku chache zilizopita.

Kuna CHADEMA na uamuzi wa kutumia njia ya kususia badala ya kutumia nyingine kama kweli zilikuwepo. Vipo vyama vingine vya upinzani ambavyo badala ya kusikitika, viliinuka kuchukua viti vilivyoachwa wazi na CHADEMA.

Kwa ujumla, tukio lile lilikuwa na sura nyingi, lakini ushabiki wa baadhi ya waliojitosa kujadili, umewanyima wananchi wengi fursa ya kuchambua na kujadili sura hizo kwa faida ya vizazi vijavyo.

Makala hii, nayo haitajadili hayo. Badala yake, itajikita katika mjadala ulioibuliwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), naibu katibu mkuu wa chama hicho na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, Zitto Kabwe.

Yeye na baadhi ya wabunge wenzake wachache waliamua kutoingia bungeni kinyume na maelekezo ya chama chao.

Katika utetezi na ufafanuzi alioutoa kupitia televisheni ya taifa (TBC1), Zitto anadai pamoja na mengi, kuwa yeye na wenzake waliamua kutoingia ukumbini kuepuka kumwaibisha mkuu wa nchi ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu.

Kwamba, aliamua kufuata dhamiri na shinikizo la wapiga kura wake ili kuonyesha heshima kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye amefanya maendeleo makubwa mkoani Kigoma kuliko rais yeyote tangu uhuru.

Kwa Zitto, maendeleo mkoani Kigoma ni fadhila kutoka kwa rais na anajisikia deni mbele yake. Alihitimisha kwa kusema, “Rais ni alama ya umoja wa nchi na ni lazima aheshimiwe.”

Kabla ya utetezi wake, kulikuwa na taarifa kwamba Zitto alikuwa “anatumika” kushawishi wabunge wagawanyike katika suala la msimamo mmoja wa chama chao. Ilimlazimu kutumia hata udini ili kukamilisha adhima yake.

Kwa kuwa suala la udini alilizungumzia pia katika mahojiano yake na TBCI, nashawishika kuamini kuwa Zitto anayo ajenda ya udini katika kutimiza malengo yake ya kuigawa CHADEMA.

Iwe anayo yeye kama yeye, au anatumwa na wanaomtuma, kuna kila sababu ya kuamini kuwa Zitto ametekwa na fikra hizi mbaya za udini anaodai anaupinga.

Fikra hizi ni matusi kwa wananchi waliomchagua kutokana na kuamini kuwa ana uwezo wa kuongoza. Kumbe moyoni mwake anaamini kuwa alichaguliwa kwa misingi ya udini!

Kwa mwanasiasa kijana, msomi na aliyewahi kujijengea heshima siku za nyuma, hatua hii inawasaliti maelfu ya vijana waliokuwa na matumaini makubwa kwake, kwani wanaona kauli na vitendo vyake vinachonga jeneza lake na fikra zake.

Naendelea kumwamini hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyesema kuwa wanasiasa waliofilisika au wanaoelekea kufilisika, hujificha ndani ya kwapa la udini na ukabila.

Kwa hili, Zitto amefilisika mapema wakati biashara ya siasa ndiyo inaanza.
Siku mbili kabla ya tukio la bungeni, Zitto alikuwa na mazungumzo ya muda mrefu na alikuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na baadaye akafanya mazungumzo na Rais Kikwete kwa njia ya simu.

Habari hizi alizisema Zitto mwenyewe ili kuwashawishi wabunge wakubaliane naye katika “mpango” wake wa kukigawa chama chake.

Baadaye alikutana na “maofisa maalum” wa serikali aliodai kuwa walikuwa wanampa habari maalum za kusaidia kumaliza aibu ambayo ingetokea kwa kususia hotuba ya rais. Wanafahamika hata kwa majina.

Kwa ujumla, Zitto alionekana kumhurumia Kikwete kuliko hata Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenyewe kinavyomhurumia mwenyekiti wake.

Kwa mtu yeyote anayejali na kupenda kuimarisha siasa mbadala katika nchi, atasikitika kusikia na kuona haya yakifanywa na Zitto.

Hata kama upinzani si uadui, lakini upinzani unaojipendekeza kwa CCM kuliko hata wana-CCM wenyewe ni wa hatari; na wanachama wenyewe wa CCM hawautaki.

Wana-CCM makini hawapendi tabia ya Zitto kujipendekeza kwa viongozi wa juu na wakati mwingine kuwachonganisha kwa kuvujisha habari azipatazo kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine.

Tayari hatua ya Zitto ya kuchukua maneno ya huyu na kumpa yule, imechochea mgogoro wa chinichini ndani ya chama cha Kikwete.

Mgogoro huu unapata nguvu kutokana na utamaduni mpya wa mtendaji mkuu wa CCM, Yusuph Makamba kuthamini wapinzani mamluki wanaorejea CCM baada ya kuwa wameshakibomoa chama hicho kwa kukishushia lundo la shutuma.

Orodha ya wanaopewa kipaumbele na Makamba kuliko wanachama wengi wanaojitolea kujenga chama chao, inahusisha Steven Wasira, Tambwe Hizza, Mbarouk Msabaha, Dk. Amani Kaborou, Sahibu Akwilombe, Daniel Nsanzugwanko, Justine Sarakana na Thomas Ngawaiya.

Ndani ya chama cha Makamba na Kikwete, hawa ni wanachama wanaotoka daraja tofauti.

Naye Zitto anaelekea kupenda kujiunga na orodha hiyo kwa gharama mbili kubwa. Kwanza, kwa kuigawa CHADEMA (yenyewe kwa yenyewe) na pia CHADEMA na wapinzani wengine.

Pili, anaelekea kuanzisha migogoro ya ndani ya CCM kwa sababu anadai anayoyafanya ndani ya CCM anakuwa na ridhaa ya kiongozi mkuu wa chama – Makamba.

Wenye akili wanajua kuwa baadhi ya madai yake si ya kweli. Lakini hata yale machache yaliyo ya kweli, hayana dhamana ya chama hicho, bali utashi binafsi wa mmoja wa viongozi ndani ya chama hicho.

Katika suala la uadilifu kwa chama, CCM ikiwa taasisi, haina mwanachama aliye juu ya sheria hata kama wapo watu wengi nje ya chama hiki ambao wanaweza kupinga dai hili.

Kwa mfano, sidhani kama Zitto ana thamani kubwa ndani ya CCM kuliko Lowassa ambaye pamoja na mengi makubwa aliyokifanyia chama chake, bado wamegoma kumsafisha kutoka katika tuhuma zilizosababisha ateme kiti chake cha uwaziri mkuu.

Wala sidhani kama Zitto ni bora kuliko Samweli Sitta ambaye licha ya kuweka rekodi nzuri ya kusimamia bunge, ni CCM iliyosema Sitta hafai tena kuwa spika.

Ni Sitta na Lowassa waliofanikisha “kampeni za kisayansi” zilizomwingiza Kikwete madarakani mwaka 2005, lakini ni Kikwete huyohuyo aliyesema Sitta hafai na anaelezwa kila siku hadi asadiki kuwa Lowassa hasafishiki.

Mifano hii inatosha kumfundisha Zitto kuwa yuko hatarini pale anapojifanya na kudai kumheshimu mwenyekiti wa CCM kuliko anavyomheshimu mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Usaliti ambao Zitto anaufanyia CHADEMA ni huohuo atakaoifanyia CCM endapo atajiunga na chama hicho.

Inavyoelekea si siku nyingi kutoka sasa Zitto atajisajili katika CCM ambayo anaitumikia sasa kwa mlango wa nyuma.

Nitakuwa wa mwisho kumkaribisha Zitto ndani ya CCM. Chama cha CCM kiko tayari kumtosa yeyote hata kama kwa kufanya hivyo kinapata hasara.

Zitto hajachelewa kuachana na utoto huu kwa kuheshimu chama chake ambacho, siyo tu kinaheshimiwa bali hata kuogopwa na wengi wakiwamo baadhi ya viongizi wakuu wa CCM.

Vinginevyo, Zitto awe tayari kuangamia.

Dk. Slaa hekima imepita kiti cha enzi


Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 15 December 2010

Kisima cha Mjadala

MOJA ya makala niliyoandika mara baada ya uchaguzi mkuu, ilihusu kiongozi mmoja wa kale ambaye dini zote kubwa za Uyahudi, Uislamu na Ukristu zinamtambua kutokana na uongozi wake wa hekima.

Mfalme Solomoni (Sulemani) ambaye maandiko yanatudokeza kuwa alikuwa na hekima kubwa katika uongozi, licha ya matatizo katika maisha yake binafsi.

Aliitwa mtu mwenye hekima kupita wote waliowahi kuishi.

Ninafahamu watu wengi wanataka “viongozi wasomi” wengine wanataka “viongozi vijana” na wengine wanataka “viongozi bora.”

Wapo wanaotaka vyote vitatu. Sijasikia wanaptaka viongozi wenye hekima.

Tatizo la hekima ni kwamba haiji kwa kuvishwa shahada - iwe ya kusomea au heshima.

Hekima huja kwa mtu kujaliwa kipaji ambacho anakiendeleza kwa kutumia uzoefu na ujuzi.

Lakini kama jamii haina viongozi wenye hekima, basi jamii jamii hiyo ina matatizo.

Ninapoangalia mambo yaliyotokea katika chaguzi mbalimbali ambazo zilizofanana na zile za kwetu kwenye utangazaji wa matokeo, ninajikuta niwe wa kwanza kutoa shukrani kwa mtu ambaye nilimuunga mkono na kumpigia debe kuwa rais, Dk. Willibrod Slaa.

Leo nimedhirika kwamba nilikuwa sahihi. Dk. Slaa amethibitisha kuwa siyo Raila Odinga, siyo Quattara na wala siyo Morgan Tsvangarai.

Hawa watatu na mwenzao wa kule Haiti walifikia mahali pa kuweka rehani maisha ya mataifa yao ili waweze kupata nafasi ya kuingia madarakani.

Kabla ya hekima kutawala, Dk. Slaa alikuwa na haki ya kutaka matokeo ya uchaguzi yasimamishwe na kwa hakika baada ya kukataa matokeo yalivyotangazwa alikuwa na haki ya kiasili ya kuyapinga na kuwashawishi wananchi kumuunga mkono.

Hata uamuzi wa kutotambua matokeo yaliyompa rais Kikwete ushindi, aliuchukua kwa tahadhari kubwa ili kuokoa taifa lake lisiingie katika machafuko.

Kwa maneno mengine, Dk. Slaa angeweza kuonesha kiu ya madaraka na kulazimisha siasa za kupata uongozi siyo kwa sanduku la kura tena bali kwa kuwasubiri wasuluhishi, Thabo Mbeki na Koffi Annan.

Lakini baada ya matokeo na hali tete iliyokuwepo nchini, Dk. Slaa aliamua kuchukua mkondo mwingine. Hekima ilipiga hodi mlangoni kwake na kukihoji: “Ili kiwe nini?”

Wapo walioandika na kusubiri kwa hamu wasikie Dk. Slaa aseme neno ambalo lingechochea mwamko wa mapambano.

Baadhi ya vijana walikuwa wanasubiri kwa hamu tu kusikia neno la kwenda mitaani kudai haki yao. Hilo lingefanyika, sote kama taifa tungejikuta katika matatizo makubwa ya kisiasa.

Yangekuwa ni matatizo ambayo yangeweza kweli kusababisha “mazungumzo ya muafaka” kufanyika na hatimaye kwa namna moja au nyingine, Dk. Slaa “kuingizwa madarakani.”

Ni njia iliyotumika Zanzibar na sasa tunamuona Maalim Seif Sharrif Hamad akikatiwa saluti na vyombo vya dola kama makamu wa kwanza wa rais wa visiwa hivyo.

Lakini mwitikio wa Dk. Slaa baada ya hali hii tete umenithibitisha kwa asilimia mia moja kuwa linapokuja suala la uongozi, yeye huwa anasimama peke yake.

Kama Watanzania hawajafikiria kumshukuru na kumpa mkono wa asante, naona mimi nimshukuru. Ninamshukuru kwa mambo kadhaa makubwa.

Kwanza, ametuthibitishia kuwa hana kiu ya madaraka. Taifa hili linashuhudia viongozi kutoka upinzani na kwenye chama tawala wakisema lolote na kufanya chochote ili aidha, waingie madarakani au wabakie madarakani.

Wengine wanapovuliwa madaraka wanaona ni ugomvi na kuwaona wananchi kama ni maadui.

Wapo wengine ambao tunaambiwa baada ya kupoteza nafasi zao, wameamua hata kutoendeleza miradi waliyokuwa wanaifadhili wakati walipokuwa madarakani. Sababu, wamepoteza madaraka.

Dk. Slaa ameonesha tofauti. Ni mwanasiasa mahiri na mwenye umakini. Ukiangalia maneno yaliyokuwa yanatolewa wakati wa kampeni, mtu angeweza kuamini kuwa angeweza kudai madaraka kwa nguvu.

Kwani ukweli ni kwamba amekubalika na zaidi ya watu milioni 2.2 (bila kujali uchakachuaji).

Pili, sina budi kusema asante kwake kwa sababu ametuonesha kitu ambacho ni nadra kufanywa na wanasiasa wengi. Hufikiri kabla ya kusema.

Kati ya mambo ambayo ninaamini wanasiasa wetu vijana wa pande zote mbili wanahitaji kujifunza, ni ile tunu ya ukimya na kutokuharakisha kuzungumza au kutenda.

Kuna wakati kiongozi unatakiwa utulie na kusikiliza pande zote, upime uzito wa unachosikia ili hatimaye uweze kutumia hekima kufanya uamuzi sahihi.

Ninafahamu mara baada ya uchaguzi na matokeo kuanza kuonekana kuvurugwa, Slaa alipokea ujumbe wa tofauti na kutoka makundi mbalimbali.

Wapo waliotaka aongoze maandamano ya kupinga Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), na wapo waliotaka ajitangaze mshindi (kama ilivyotokea huko Ivory Coast ambako sasa kuna watu wawili wanajiita marais).

Nina uhakika wapo wengine waliotaka wapate nafasi ya kutolea usongo mafisadi. Wapo viongozi mbalimbali wa kidiplomasia na kidini waliojaribu kwa ushawishi wote kumtuliza Dk. Slaa ili “kudumisha amani na utulivu.”

Kitendo cha kuwa kimya na kuwasikiliza kimetupa mwanga kuwa yeye si mtu wa kukurupuka katika maamuzi.

Tatu, baada ya matukio ya “kulinda kura” kwenye majimbo mbalimbali nilikuwa na hofu sana na kuandika kitu cha kuwataka vijana watulie kwa sababu siyo mwisho wa dunia.

Kulikuwa na watu wengi waliojawa hasira na wengine walioona kuwa wamedhulumiwa haki yao.

Tatizo ni kuwa kuna watu ambao wanafikiri vijana wanaelewa sana hili la “umoja na utulivu.”

Ushahidi umekuwa wazi kabisa (kama ulikuwa unaangalia TV wakati ule) kuwa vijana wanaanza kuchoka. Dk. Slaa aliweza kutulia na kutofanya kitu ambacho kingechochea hisia za vijana. Sote tunajua nini kingetokea.

Nani ambaye hakuona kilichotokea London wiki iliyopita ambapo mwana wa Mfalme, Charles na mke wake Camilla walishambuliwa na waandamanaji?

Ninachosema ni kuwa wapo watu watakaopongezana na wapo ambao watapeana tuzo na sifa mbalimbali za ushindi.

Wenyewe wataona wanastahili heshima wanayopewa. Lakini ukiniuliza mimi nimekolewa na nini, nitakuambia kuwa nimekolewa si kwa matendo haya, bali kwa maamuzi ya Dk. Slaa.

Nina uhakika hakuna taasisi nchini yenye ujasiri wa kusema wazi “asante Dk. Slaa.” Hakuna chuo ambacho kinaweza kutoa tuzo ya wazi kwa Dk. Slaa kwa kumpa heshima ambayo amejistahilisha.

Naamini wapo watu wengi tu ambao japo wanafahamu ukweli wa kilichotokea, hawana ujasiri wa kumpigia simu au kukaa naye na kumsikiliza. Hivyo ndivyo ilivyo.

Lakini ninaamini, wale ambao wanataka kuwa wa kweli katika dhamira zao, wanajua kabisa kuwa taifa hili limenusurika kuwa Haiti, Kenya, Ivory Coast au Zimbabwe, si kwa matendo ya walio madarakani, bali kwa hekima ya Slaa.

Hivyo basi, hata kama CHADEMA imeamua kumtambua rasmi Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa rais, sote tujue kabisa yamewezekana hayo kwa sababu ya Slaa.

Hata kama hatuwezi kumtunukia nishani yoyote lakini tunaweza kusema asante.

Rais Kikwete anapofikiri kama Kabwe Zitto


Evarist ChahaliUskochiToleo la 261 RAIA MWEMA
3 Oct 2012
NIMEKUWA nikiulizwa swali hili takriban kila wiki baada ya makala zangu kuchapishwa katika jarida hili maridhawa: Hivi kuna wakati unaishiwa na cha kuandika? Na siku zote jibu langu linakuwa lile lile; Tanzania yetu haiishiwi mambo yanayopaswa kujadiliwa-iwe gazetini, mtandaoni, kijiweni au popote pale. Kuweka rekodi sawia, kila ninapoingia mtandaoni huwa ninakumbana na wastani wa angalau habari tano zinazoweza kutengeneza mada za makala zangu.

Wiki hii nitazungumzia matukio mawili makubwa yanayoihusu CCM na CHADEMA. Kwa namna moja au nyingine, matukio yote mawili yanahusiana, na nitajitahidi kuonyesha uhusiano wao mwishoni mwa makala haya.

Tukio la kwanza ni kauli ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwamba CCM haitokufa, na pengine wanaodhani hivyo wanaweza kufa wao kabla ya chama hicho tawala kufa.

Kwa baadhi yetu tunaosoma siasa kama eneo la taaluma, tunatambua ukweli mmoja, kwamba chama cha siasa kinazaliwa, kinakua, na kama ilivyo kwa binadamu, kinaweza kufa. Na tofauti na binadamu ambao hatuna udhibiti mkubwa wa kurefusha au kufupisha maisha yetu (kuna watenda dhambi na wanaotumia kila aina ya ‘sumu’-pombe, dawa za kulevya na kadhalika ama kumkera Muumba au kuharibu afya zao-lakini si tu wapo hai bali pia wana afya za kuridhisha, huku wengine mambo yao yakizidi kuwanyookea, huku upande mwingine kukiwa na wacha Mungu, wanaojali afya zao lakini wanataabika muda huu); Vyama vya siasa vinaweza kurefusha maisha yao kwa kuitumikia jamii kulingana na matarajio ya jamii husika au ikaipuuza jamii hiyo na kujichimbia kaburi.

Pamoja na heshima yangu kubwa kwa Rais Kikwete, ninaomba kutofautiana naye katika kauli hiyo kuwa CCM haitokufa. Si tu kuwa vyama vya siasa hufa, bali pia ninaamini kuwa kila Mtanzania anayefuatilia kwa karibu historia na mwenendo wa chama hicho anaweza kabisa kubashiri kuwa ama mwanzo wa mwisho wake unakaribia au kinaharakisha kifo chake.

Simlaumu Rais Kikwete kwa kauli hiyo kwa sababu kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chama anachoongoza ana jukumu kubwa la kuwahakikishia viongozi na wanachama wenzake kuwa ‘mambo si mabaya’ kama inavyoelezwa na wapinzani wao.

Binafsi, nasema kinachoweza kuiua CCM kabla ya wakati wake, ni pamoja na mtizamo huo wa Rais Kikwete wa kwamba ‘chama hicho kipo imara na kinaendelea kupendwa na Watanzania wengi-uthibitisho (kwa mujibu wao) ni idadi ya wana-CCM waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali kwenye chaguzi zinazoendelea ndani ya chama hicho.

Ni kweli kwamba idadi ya waliojitokeza kugombea inaweza kujenga picha kuwa CCM bado kinapendwa na wengi. Lakini haihitaji ufahamu mkubwa wa siasa zetu kumaizi kuwa baadhi ya wanaokimbilia uongozi ndani ya chama hicho wana ajenda zao binafsi. Ikumbukwe kuwa huko nyuma chama hiki kilishaonyesha dhamira ya kutenganisha biashara na siasa, hatua iliyotafsiriwa na wengi kuwa ni kutambua kuwa kuna kundi la wafanyabiashara wanaokimbilia kwenye siasa si kwa minajili ya kuutumikia umma, bali kusaka ‘kinga’ ya kuwalinda katika biashara zao.

Binafsi, nilikuwa miongoni mwa wapinzani wakubwa wa wazo hilo, si tu kwa sababu siafikiani na aina yoyote ya ubaguzi, bali pia sikuona kuwa tatizo ni wafanyabiashara kujihusisha na siasa bali wafanyabiashara ‘wachafu’ kuruhusiwa kujihusisha na siasa. Kwa kuharamisha biashara kwenye siasa kungeweza kuwa na hatari ya kuwakwaza wazalendo wazuri tu ambao walichagua kujihusisha na biashara kabla ya kuingia kwenye siasa.

Na ingekuwa ubaguzi wa wazi kuwazuia wafanyabiashara kujihusisha na siasa, lakini kuwaruhusu askari wastaafu, wasomi na wanajamii wengineo kufanya hivyo. Sawa, wanasema samaki mmoja akioza basi wote wameoza, lakini usemi huu hauzingatii ukweli kwamba binadamu hutofautiana.

Kwa mfano, kwa vile Mndamba wa kwanza kumfahamu ni mie ambaye pengine ninakukera na kwa mtizamo wangu haimaanishi kuwa kila Mndamba utakayekutana nae maishani atakukera. Waingereza wana msemo kuwa “people vary because we differ” yaani watu huwa na tofauti kwa sababu wanatofautiana, na kwa mantiki hiyo hiyo, mfanyabiashara anayeingia kwenye siasa kwa minajili ya kujitengenezea kinga katika ufisadi wake kwa taifa, haimaanishi kuwa kila mfanyabiashara anayeingia kwenye siasa ana malengo hayo.

Ninaamini kilichopelekea CCM kudhamiria kumtenganisha biashara na siasa ni historia na uzoefu iliopata kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara walioingia kwenye siasa. Na wazo lilikuwa zuri, kwamba mfanyabiashara atakayeamua kuingia kwenye siasa achague moja: biashara au siasa.

Tukirejea kwenye tamko la Kikwete kuwa CCM haitokufa, yayumkinika kuamini kuwa kauli hiyo ni ya kujipa matumaini tu na kukwepa ukweli kwamba kwa kiasi kikubwa chama hicho kinaonekana machoni mwa baadhi ya Watanzania kuwa ni chanzo cha matatizo mengi yanayoikabili nchi yetu. Kwa kifupi, kitakachoiua CCM si kauli za hao wanaoikitabiria kifo bali matendo ya chama hicho ambayo kimsingi ndio ‘pumzi’ inayokifanya kiwe hai.

Tukio jingine ambalo kwa namna moja au nyingine linahusiana na uhai wa chama cha siasa (kwa maana ya kuwa hakitokufa au la) ni tamko la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA), ya kwamba hatogombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015, bali atagombea urais.

Kwanini ninalinganisha tamko la Zitto na kauli ya Mwenyekiti wa CCM, Kikwete? Jibu fupi ni kwamba matamko yote mawili yanaelekea kupuuza hali halisi ya mwenendo wa siasa za huko nyumbani.

Wakati Mwenyekiti Kikwete anajigamba kuwa CCM haitokufa japo kuna mamia kwa maelfu ya wana-CCM wanaokihama chama hicho kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake, huku pia baadhi ya viongozi wa chama hicho kama kina Samuel Sitta wakionyesha hadharani ‘maovu’ ya chama hicho, Zitto hataki kujihangaisha kutambua wengi wa Watanzania wanamtaka mwanasiasa gani kutoka chama chake ili kubeba dhamana ya kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kabla sijaendelea kuijadili kauli ya Zitto, ningependa kuweka bayana masuala matatu ya msingi. Kwanza, Zitto ana kila haki si tu ya kutaka kuwa Rais wa Tanzania, bali pia kutangaza kuwa ana nia hiyo. Ni haki yake ya kidemokrasia, hasa ikizingatiwa kuwa anatoka katika chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Pili, ni suala la kukubalika kwa wapiga kura watarajiwa (potential voters). Kila mara ninapomsikia Zitto akielezea dhamira yake ya kutaka kuwa Rais, huwa ninajiuliza swali moja la msingi; ni lini amefanya ‘utafiti’ wa kutambua Watanzania wanamhitaji awe rais wao?

Wenzetu huku Magharibi, kabla mwanasiasa hajakurupuka kutangaza kuwa anataka kuwa rais huwa inamlazimu kujihangaisha ‘kusoma upepo,’ yaani kufahamu iwapo wapigakura wanamhitaji.

Sawa, Tanzania si nchi ya Magharibi, na pengine hakuna umuhimu wa kusaka mtizamo wa wapigakura. Lakini kwa mwanasiasa anayejali maslahi ya chama chake na wananchi kwa ujumla, yayumkinika kuamini kuwa atajihangaisha kufahamu iwapo dhamira yake ya kugombea ni kwa maslahi ya chama chake na umma kwa ujumla au ni kwa ajili ya kutimiza ndoto zake binafsi tu.

Suala la tatu, na ambalo kwangu si tu ni la msingi zaidi bali pia linanishawishi kuamini kuwa dhamira ya Zitto kugombea urais ni sawa na kubariki ushindi wa CCM hapo 2015, ni uadilifu wa mwanasiasa huyo.

Ninamfahamu Zitto vizuri, na si kupitia social media. Ni mmoja wa wanasiasa wachache wenye kipaji cha hali ya juu katika ujenzi wa hoja. Lakini, kama mwanadamu mwingine, mwanasiasa huyo ana mapungufu fulani. Kwa wanaomfahamu kupitia social media (hususan Twitter) wanaweza kuafikiana nami kuwa si mwepesi sana wa kuafikiana na watu wenye mtizamo tofauti na wake.

Ni rahisi kumhukumu kuwa ana jazba (japo sitaki kuamini hivyo) pindi mtu anapotofautiana naye katika anachoamini yeye kuwa ni sahihi. Nafasi haitoshi kutoa mifano halisi, lakini waliotofautiana nae kimtizamo ndani ya Twitter wanaweza kuwa mashahidi wazuri.

Tatizo la msingi kuhusu Zitto ni ‘tuhuma’ zilizowahi kuandikwa na jarida moja la kila wiki kwamba katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu uliopita, jarida hilo lilinasa mawasiliano kati ya mwanasiasa huyo na mmoja wa viongozi wa juu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Katika mazingira ya kawaida, mwanasiasa wa chama cha upinzani kuwa na mawasiliano na mtumishi wa taasisi hiyo nyeti (ambayo ilishutumiwa na CHADEMA-ambayo Zitto ni mbunge wake-kuwa ilikihujumu chama hicho kwenye uchaguzi huo) inazua maswali kadhaa.

Ndio, watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa ni Watanzania wenzetu kama ilivyo kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani. Lakini mawasiliano kati ya mwanasiasa wa chama cha upinzani kama Zitto na kiongozi wa idara hiyo, yanaweza kuibua maswali mengi. Kibaya zaidi, Zitto hajawahi kutoa ‘maelezo ya kueleweka’ kuhusu mawasiliano hayo.

Kimsingi, Zitto anatambua bayana hisia zilizojengeka baada ya habari hiyo kuchapishwa. Kuna waliotafsiri kuwa mawasiliano hayo yalilenga kukihujumu chama hicho, na kwa kuzingatia mantiki ya kawaida tu hatuwezi kuwalaumu kwa hisia hizo.

Lakini pengine kubwa zaidi ni kwanini bado kuna idadi kubwa tu ya wafuasi wa CHADEMA wanaotafsiri uamuzi wa Zitto kutaka urais kama ‘tamaa ya madaraka.’ Hivi akiweka kando imani yake kuwa ana uwezo na uadilifu wa kuongoza taifa la Tanzania, Zitto ameshawahi kufikiria kuwashawishi sceptics hawa hata kama hoja zao hazina mashiko?

Kubwa zaidi ni ukweli kwamba matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita yanaonyesha bayana jinsi mgombea urais kupitia CHADEMA, Dk Willibrod Slaa, alivyokubalika kwa idadi ya kuridhisha tu wapiga kura. Kama dhamira ya Zitto ni kuona CHADEMA inaingia Ikulu, kwanini asiwekeze jitihada kumsapoti Dk Slaa katika uchaguzi ujao na kusubiri ‘zamu yake’ hasa kwa vile umri bado unamruhusu hata kwa miaka mingine 15 ijayo?

Kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano, mgombea urais sharti awe na miaka 40. Mwaka 2015 Zitto atakuwa na umri pungufu na huo. Hivi kung’ang’ania kuwa anataka kugombea ilhali akijua Katiba haimruhusu si ni dalili ya tamaa ya madaraka?

Nimalizie makala haya kwa kulinganisha matukio mawili haya niliyozungumzia. Kama ambavyo Rais Kikwete hataki kujiuliza kwanini baadhi ya watu wanaitabiria kifo CCM, Zitto hataki kujiuliza kwanini baadhi ya watu wanatafsiri dhamira yake ya kutaka urais mwaka 2015 kama mikakati wa kuirejesha CCM madarakani na kuinyima CHADEMA nafasi hiyo.

Suluhisho katika masuala hayo mawili, linaweza kupatikana katika busara hii ya Waingereza isemayo “never ever put emotions in front of common sense” (kwa tafsiri isiyo rasmi, kamwe usitangulize hisia mbele ya tabasuri/ busara).

Nani anasema kweli kuhusu Kigamboni?



26 Sep 2012 RAIA MWEMA
RAIS Jakaya Kikwete amekanusha kutouza ardhi ya Kigamboni kwa George Bush. Sawa, lakini hajakanusha kuuzwa kwa eneo la Kigamboni. Kama halijauzwa kwa Bush basi tuambiwe limeuzwa kwa nani.

Habari hii ya Kigamboni inarejesha suala la Richmond: nani alijua na nani alitaka kuchukua hatua kuzuia mkataba ule usiingiwe.

Leo tunapoambiwa habari ya Kigamboni mradi wa mji mpya uliojaa ubabe na usiri mkubwa tunapata tabu sana kuamini kauli hizi.

Mambo haya yanauma sana kwa wahanga wa zoezi hilo la mradi wa mji mpya Kigamboni. Sisi Kigamboni tunajua tumeuzwa lakini pengine hatuna uhakika tumeuzwa na nani na kwa nani. Mawakala wengi wanapitapita kurubuni wananchi waukubali mradi, tena wengine ni viongozi.

Madiwani wa Kata za Tungi, Vijibweni, Kigamboni-Ferry na Mjimwema wana mahusiano mabaya sana na wananchi wao tangu siku ile walipoonekana kwenye runinga bungeni Dodoma. Wanatuhumiwa kuendesha uwakala wa uuzaji wa Kigamboni. Wapo wengine pia wakijinadi kama wawekezaji wa upanuzi wa bandari, wajenzi wa kiwanda cha samaki, wawekezaji wa mafuta, kuna watoto wa vigogo pia wanarandaranda huku wakitumia majina ya wazazi wao, nk.

Hatua ya kutimuliwa kwa Mbunge wa Kigamboni kwenye Bunge iliwafanya wakazi wa Kigamboni kuamini kuna jambo linaendelea kuhusiana na suala zima la utwaaji wa ardhi ya Kigamboni.

Wananchi hao wa Kigamboni walimtuma Mbunge wao akaukatae mradi wa mji mpya wa Kigamboni bungeni kutokana na kugubikwa na utata, usiri na ubabe. Kitendo cha kumtimua Mheshimiwa Faustine Ndungulile bungeni kilionyesha juhudi za kumshona mdomo na hivyo kuhalalisha dhuluma dhidi ya wakazi wa Kigamboni.

Kama hiyo haitoshi, wakazi wa Kigamboni tuliandaa mkutano mkubwa wa mapokezi ya Mbunge wetu pale uwanja maarufu wa Machava. Walihudhuria wananchi kutoka Pembamnazi, Yaleyale Puna, Kimbiji, Kibugumo, Mwongozo, Gezaulole, Chekeni Mwasonga, Tundwi Songani, Mikwambe, Kibada, Kisarawe II, Mbagala yote hadi Mbande, Chamazi na Mvuti.

Wanachi walikuwa wamechangishana mamilioni ya shilingi kumkabidhi Mbunge huyo kama posho kufidia ile aliyonyimwa kufuatia kutimuliwa bungeni na hivyo kumfanya kukosa posho za vikao. Cha kushangaza sana na kwa masikitiko ya wana-Kigamboni, makaribisho hayo yalisambaratishwa na jeshi la Kamanda Suleiman Kova saa chache kabla ya makaribisho hayo kufanyika.

Lakini kwa mshangao mwingine, kuna viongozi Kigamboni wanapitapita na kujitapa kwamba wao walihusika “kulishawishi” Jeshi la Polisi kusambaratisha makaribisho hayo ya mbunge kwa madai kwamba alikuwa anataka kuwachafulia hali ya hewa kwa kuwahamasisha wananchi kuukataa mradi wa Mji Mpya Kigamboni.

Viongozi hao ni wale mawakala wa mradi ambao wametajwa hapo juu. Hivi katika hali ya kawaida kiongozi wa kata au serikali ya mtaa anapata wapi ujasiri na mamlaka ya kuamrisha Kanda Maalumu bila kuwa na msimamizi huko juu? Hii haiwezi kuingia na kutulia tuli kwenye akili inayofanya kazi maridhawa, vinginevyo itakuwa ni bongolala.

Wakazi wa Kigamboni tumepewa katazo (stop order) la kutoendeleza maeneo yetu tangu Oktoba 2008 kwa hoja kwamba ni eneo la mradi. Ilisemekana kuwa ramani za satellite zilishachukuliwa kubaini kuna nini, wapi, na kwa nani.

Ukweli ni kwamba hakuna mkazi wa Kigamboni aliyeshirikishwa katika zoezi hilo. Na nikiri tu hapa, kwamba hata hicho kilichomo kwenye hiyo ramani hakuna anayejua. Mungu ni mkubwa akatuongoza vema, ramani hiyo maarufu kwa jina la “Kigamboni: The Blue Diamond” ikaonekana kwenye mitandao ya huko kwa George Bush. Ni fafanuzi (documentary) moja inayofanyiwa maelezo (commentary) na mtu mwenye lafudhi ya Kimarekani akisifia kuwa Kigamboni ni lango/kitovu (hub) ya “maendeleo” ya Tanzania. Siwezi kuamini kwamba mwelezaji (commentator) yule ni Mmatengo au Mhaya, na wala si Mndengereko au Mzaramu. Wasamaria wakatuvuta masikio tukaiona hiyo documentary mtandaoni.

Nikueleze tu ndugu msomaji kulikuwa na mwitiko (rush) mkubwa wa kuipata hiyo documentary miongoni mwa sisi wadau wa Kigamboni. Tulikuwa tunanunua hiyo fafanuzi ili kupata taarifa ambayo ni haki yetu kupata lakini wahusika serikalini wakawa wanatuficha. Hata mimi binafsi niliuziwa na msamaria mwema Dar es Salaam na ikawa bidhaa adimu hapa Dodoma.

Hayo ndiyo mazingira yaliyosababisha kujitokeza maneno (uvumi?) kwamba Kigamboni imeuzwa kwa George Bush.

Kwa mshangao wa tulio wengi, mara baada ya nusanusa yao serikalini kugundua kwamba suala hilo liko hadharani kwa haraka sana Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikatoa kilichoitwa TAMKO LA SERIKALI kwenye gazeti la Mwananchi Jumapili moja ya mwaka 2008 lililokataza uendelezaji wa ardhi katika maeneo ya mradi kwa mujibu wa sheria ya Mipango Miji namba 8 ya mwaka 2007. Katazo hilo lilitakiwa liishie Septemba 2010 ambapo mradi ungekuwa umeanza awamu ya kwanza.

Hadi leo niandikapo makala haya hakuna kinachoendelea ukiachia mbali kuwarudisha nyuma wakazi wa Kigamboni. Tumerudishwa nyuma kwani tunatishwa (intimidated) kwamba chochote tutakachoendeleza kinakula upande wetu. Choo kikianguka usikarabati maana itakula kwako. Na huo wimbo wa fidia kwa mali za watu wa Kigamboni ni nyimbo za kila mwanasiasa asiye makini. Nakumbuka mwanasiasa mmoja aliliambia Bunge la Bajeti kwamba waathirika wa daraja la Kigamboni wameshathaminiwa mali zao hivyo bado malipo tu. Mimi ni mmoja ambaye napitiwa na barabara ya hilo daraja, lakini hadi leo niandikapo makala haya sijathaminiwa kilicho changu.

Halafu anakuja mtu anasema watu wa Kigamboni wamechochewa na wapinzani kupinga ujenzi wa daraja. Nachukia kauli za aina hiyo maana ni za kudhalilishana.

Hivi Kigamboni kuna ma-tabula rasa (wajinga) wanaosubiri wajuaji kutoka upinzani au chama tawala kuja kuwaelekeza cha kufanya? Wote wenye fikra za aina hiyo wanajidanganya na kama walizoea kunadi sera za aina hiyo sehemu nyingine, Kigamboni wameula wa chuya. Wamuulize yule “mwekezaji” wa kiwanda cha samaki pale Vijibweni mwaka 2004 akisaidiwa na kupigiwa debe na aliyekuwa mkuu wa mkoa wakati huo aliishia wapi.

Tulikomaa pale hatukutoka hadi leo tunapitiwa na barabara, nao wakituletea gozi gozi, wembe ni uleule uliomnyoa “mwekezaji” wa kiwanda cha samaki.

Huwezi kusimama bungeni unadanganya umma umethaminisha mali za wananchi pale Vijibweni wakati si kweli, halafu mtu anatarajiwa achekewe chekewe tu. Mtu wa aina hii lazima aitwe kwa jina lake (call a spade a spade) yaani kama ni mwongo basi aitwe hivyo bila kuumauma maneno.

Kama hakuna malipo hakuna barabara kupita pale Vijibweni na wala hatuhitaji mwanasiasa wa upinzani au chama dola kuja kutusemea. Sisi wahanga wa mradi huo tunajua kujisemea wenyewe. Tangu lini funza anikae mimi halafu wewe ndiye uonyeshe wapi funza aliko mwilini mwangu? Hizo ni falsafa zenye mtindio wa mwelekeo.

Badala ya kulaumu wapinzani, Serikali ifanye wajibu wake kuhusu utata wa mji mpya Kigamboni kwa kuwashirkisha wananchi katika hatua zote kama alivyopendekeza Mbunge Ndungulile na kuungwa mkono na wana-Kigamboni.

Kule Kigamboni wakazi wameunda kamati yao ya kufuatitlia maendeleo ya mchakato mzima wa mradi mji mpya. Wameshaongea sana kwenye mikutano ya hadhara, wameongea na waziri, naibu waziri, katibu mkuu na watendaji wengine serikalini na hata NGOs.

Mara nyingi viongozi wa kamati wametokea kwenye runinga mbalimbali. Wafuatiliaji wa vipindi hivi watakumbuka kwamba kamati ilihitimisha kwamba mradi wa Kigamboni ni EPA, Richmond, Dowans, Deep Green, Tangold na miradi mingine ya kifisadi.

Mpaka leo hakuna aliyekanusha na kujenga hoja ya uhalali wa mradi huo.

Halafu si mara moja maofisa kutoka wizarani wameshatimuliwa na wananchi kule Kigamboni lakini hakuna aliyesimama kuwatetea. Mambo (beacons) zilizowekwa na mkandarasi bila wananchi kushirikishwa zimeshang’olewa na wananchi, mbona hawachukuliwa hatua za kisheria kama beacons zile ziliwekwa kihalali?

Kamati imeshatafiti na kugundua kuwapo uvunjaji mkubwa wa sheria za nchi kwa upande wa Serikali katika kutekeleza mradi huo. Hakuna aliyesimama kule serikalini na kutetea utawala wa sheria unavyotumika katika kutekeleza mradi wa mji mpya kule Kigamboni. Ni katika mazingira hayo mbunge wa Kigamboni Faustin Ndungulile alisimama pale bungeni kutoa tamko la wakazi wa Kigamboni kwamba mradi uanze upya kwa kufuata sheria ambazo Bunge limetunga. Akaishia kutimuliwa bungeni kwa sababu ya kutetea haki za watu wa Kigamboni lakini pia kutetea hadhi ya Bunge lenyewe.

Lakini mheshimiwa huyo ni Mbunge wa chama dola si wa upinzani. Kwa mantiki hii hoja ya kusema wapinzani wanapinga mradi wa mji mpya Kigamboni naiona ni dhaifu sana na haina mashiko. Ukweli ni kwamba wananchi wa Kigamboni kwa utashi wetu bila kusukumwa na chama chochote ndio tunaopinga mradi huo unaoendeshwa kinyemela.

Hoja ya kuendeleza Kigamboni kwa faida ya wananchi ni dhaifu na haina mashiko. Kama ukifanikiwa kuziona zile picha (model impessions) za jinsi mji utakavyokuwa nadiriki kusema hapa ni mji ambao wananchi wa Kigamboni hawamo katika makadirio yake. Kule kuna eneo la viwanda, kuna eneo la utalii na burudani, kuna eneo la biashara za kimataifa, kuna eneo la shule na vyuo vya kimataifa na eneo la makazi ni asilimia kama 7% tu hivi. Wengine wamelibatiza eneo hilo la makazi kuwa ni concentration camps.

Majengo yake ni maghorofa yanayofikia 20 hadi 100. Mitaa yake hakuna njia za guta wala mikokoteni. Bustani zake ni za maua si bamia, matembele, viazi wala embe. Nyumba zake si za kupikia kwa kuni wala mkaa, hamna mabanda ya kuku, mbuzi, nguruwe, njiwa wala ng’ombe.

Kwa mazingira hayo wananchi wa Kigamboni itabidi wawapishe wageni na wao wasonge mbele huko Chekeni Mwasonga na Tundwi Songani wanakoweza kulima, kufuga na kuendesha mikokoteni.

Tuache kudanganyana hapa eti kuna mtu ana uchungu na watu wa Kigamboni. La msingi tu watu walipwe vizuri, si kama walivyodhulumiwa wenzetu wa upande wa Kurasini. Serikali iliwalipa shilingi milioni 20 kwa eka yenye wakazi 10 hadi 20. Serikali imeuza maeneo yale baada ya miezi isiyozidi sita kwa wawekezaji kwa shilingi milioni nyingi.

Na wala watu wasitukumbushe yaliyojiri mwaka 2005 kuhusu daraja hilohilo. Juhudi za kuanza ujenzi Oktoba 2005 zilikwamishwa na kwa sababu ambazo hazijawahi kuwekwa wazi. NSSF nadhani wanakumbuka kilichotokea wakati ule licha ya maandalizi yote kuwa yalikuwa yamekamilika.

Tulitangaziwa ya kuwa imepatikana kampuni ya Kichina iliyojenga huko kwao daraja la urefu wa kilomita 30. Watu wakajinadi kwamba Wachina hao wangeweza kutumia muda mfupi sana kujenga daraja la Kigamboni. Lakini mradi uliyeyuka kama theluji kwenye kiangazi.

Walawale waliokwamisha ujenzi wa daraja huko nyuma leo wanatamba hadharani na kudai Dk. Ramadhani Dau apewe nishani ya utendaji bora. Historia ni hakimu makini sana, watu wasifikiri wanaweza kujifanyia watakavyo halafu historia ikawasamehe.

La msingi ni kwamba, kama vile tunavyojinadi kuwa tunafuata utawala wa sheria basi zoezi lile la mji mpya Kigamboni liende kwa kufuata sheria zilizopo. Hiyo ni pamoja na wananchi kushirikishwa kama sheria zinavyotaka. Lakini kwa usiri na ubabe huu unaotawala zoezi zima la mradi wa mji mpya Kigamboni, lazima hoja za kwamba eneo ameuziwa Bush zitaendelea kujitokeza.

Kama si kweli Bush kauziwa eneo la Kigamboni, usiri na ubabe, na hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja vinatoka wapi? Ukweli (reality) unaiishi independent of the subject, si hoja nani anasema; rangi yake, cheo chake, umri wake nk. Hivyo basi, ukweli kuhusu mazingira yanayozunguka mradi wa Kigamboni kama ilivyokuwa kwa EPA, Richmond, Dowans, Simbion, Tangold, Deep Green na mingine mingi utakuja kujipambanua na hatimaye kujulikana tu.

Ole wao wanaojifanya manabii wa injili hii ya Blue Diamond. Watu wasije kulia na kusaga meno ufunuo utakapofunika sayari hii na hila zao kuwekwa hadharani.