OIC, MBWA MWITU ALIYEVAA NGOZI YA KONDOO.
OIC: Mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo
Jumuiya ya nchi za kiislam OIC[ organization of islamic conference] iliasisiwa mwaka wa 1969,
jumuiya hii ilianzishwa nchini MOROCCO tarehe 21Agust 1969 AD, au 12 Rajab 1389 H,
*. Jumuiya hii ilianzishwa kutokana na mashabulizi ya ISRAEL
yaliyofanywa dhidi ya nchi za kiarabu, na kutekwa kwa mji wa YERUSALEM,[
AL-QUDA], katika vikao viwili kile cha MOROCCO tarehe 25 september
1969, na kile cha mjini JEDDAH cha mwezi machi 1970 kiliweka maazio ya
kuuteuwa kwa muda mji JEDDAH kuwa makao makuu ya muda ya OIC ambapo
kikao hicho kiliazimia kuwa MAKAO MAKUU YA KUDUMU YA OIC YATAKUWA NI
YERUSALEMU.
Moja ya kipaumbele kikuu na lengo kuu la
kuasisiwa kwa OIC ni kuikomboa YERUSALEMU kutoka mikononi mwa ISRAELI
pamoja na msikiti MTAKATIFU WA AL-AQSA ulio sehemu muhimu kwa imani ya
kiislam kwani AL-AQSA ndiyo QIBLA cha kwanza cha waislam kabla
hakijageukia AL-KAABA. hivyo yaliwekwa maazimio matatu muhimu,
1. kujijengea uwezo kwa kufanya yafuatayo. [a] kujenga mshikamano miongoni mwa waislam,
[b] kujenga mashirikiano ya jamii nzima ya kiislam,
[c] kuupigania uislam kwa kulindamaeneo MATAKATIFU pamoja kulinda vitabu VITAKATIFU,
2. kuunganisha nguvu ili [a] kupigania sehemu TAKATIFU.
[B] kuunga mkono harakati za WAPALESTINA KUJIKOMBOA,
3.Kufanya kazi kwa pamoja
[a] kuondoa ubaguzi miongoni mwa waislam na
[b]kueneza dini na utamaduni wa kiarabu. nk.
ili kufanikisha azma na malengo ya jumuiya vilianzishwa vyombo
mbalimbali vya kusimamia shughuli zote kulingana na vipaumbele husika,
ili kuyafikia malengo hayo KIKAO KILIGUSIA maeneo haya. ELIMU, SIASA,
UCHUMI na DINI , mambo haya yaliwekwa chini ya KATIBU MKUU ili
kuhakikisha kuwa malengo yanafanikiwa
1-KUHAKIKISHA KUWA
ZINAANZISHWA SHULE ZA KIDINI[MADRASSA ] zitakazo toa ELIMU ya DINI-SIASA
kazi kubwa ya shule hizi ni kujenga uadui kati ya UTAWALA WA
KIZAYUNI[ISRAEL ] uliolikalia kwa nguvu eneo takatifu la yerusalem ulipo
mskiti wa AL-AQSA , mbinu hii imesaidia sana kwani baada vijana wengi
kufunzwa katika MADRASA hizi za DINI SIASA[ UDINI] tumewashuhudia
wakitamka hadharani kuwa UTAWALA WA KIZAYUNI UNAPASWA KUFUTWA KWENYE
RAMANI YA DUNIA NA PALESTINA LIWE TAIFA HURU,
chini ya
mwamvuli huu mara kadhaa tumewasikia wahubiri wadini ya kiislam kama
vile ABOOD MOHAMEDY ROGO, ANWAR AL AWALAKI, ABU QATADA, na wengineo
wakiwahamasisha vijana wa kiislam kwenda PALESTINA kuwapigania ndugu
zao.
Kivuli hiki cha DINI SIASA kimeendelea kukua hasa pale
mataifa ya MAGHARIBI kuonekana wakiingua mkono ISRAEL, mafundisho haya
ya dini siasa sasa yanazigusa hata nchi hizi zinazoonekana kuwa ni
washirika wa utawala wa KIZAYUNI,
katika mafundisho haya ya DINI
SIASA yaliyoasisiwa na OIC yamefanikiwa kuzalisha makundi ya KIGAIDI na
MISIMAMO MIKALI YA DINI-SIASA[UDINI] ndiyo maana nchi ambazo zilikuwa
za mwanzo kujiunga na jumuiya hii kwa sasa zinakabiliwa na mfumuko wa
siasa kali za udini,
UDINI ulionwa kuwa ndiyo njia pekee ya
kuyayafikia malengo, yaani kuwafundisha vijana wa kiislam kuwa ADUI YAO
NI YULE ANAYEWANYIMA HAKI YA KUWA NA YERUSALEM.
hapa ndipo yalipoanza madai ya kile kinachoitwa MFUMO KRISTO, yaani washirika wa utawala wa MAZAYUNI
unaowanyima haki waislam, kwa kutumia mbinu za hali ya juu za kutengeneza mazingira wamefanikiwa kuziteka nyoyo za wengi.
Madhumuni ni mamoja tuu, KUKUSANYA NGUVU NA KUIKOMBOA YERUSALEM ILI IWE NI MAKAO MAKUU YA OIC.
hata hapa kwetu mafundisho haya tayari yamekwisha kupenyezwa
kazi kweli kweli
ReplyDelete