UDINI BAADA YA UHURU
.
Wakoloni walipoondoka waliacha shule nyingi ambazo hazikuwabagua
wananchi wa imani nyingine.Baada ya uhuru shule zote zilizokuwa za
kikristu zilifanywa kuwa za serikali, wakristu hawakulalamika. Leo miaka
50 ni generation ya pili tangu uhuru waislaam bado hawatilii mkazo
suala la elimu tumebaki kulalamika tunaonewa wakati tuna nafasi sawa na
wengine! Mr. Chahali nadhani tatizo kubwa lililopo ni zaidi la
kitamaduni kuliko la kidini, nasema ukweli mtupu...siyo suala la
kudhania ila ni suala la utafiti tuliofanya tukiwa chuo kikuu huko
Tanzania. Mfano, ukiangalia sehemu kubwa ambazo hazikupiga hatua ni za
pwani, kwa nini? je ni dini ya kiislaam? inaweza kuwa kweli au hapana,
utamaduni wa makabila kama wazaramo kwa kiasi kikubwa hazioni kama
kusoma ni moja ya priority yao, na makabila mengine pia ya Dar,
Zanzibar,pwani, Tanga, Mtwara, Lindi, Kigoma etc, imekuwa bahati mbaya
kuwa wengi wanaoishi katika mikoa hii ni waislaam. Na upande mwingine
ukienda ndani zaidi (Hinterland) kama Lushoto, utakuta kuna watu wengi
ambao ni waislaam wamesoma kwa kiwango cha kutosha. Kuna waislaam wengi
ambao wana msimamo wa kati (moderate) wanaliona hilo na hao wana uwezo
wa kujua ukweli ambao ndio wasioamini kila kitu anachosema sheikh akiwa
mimbarini. Tatizo kubwa lipo kwa waislaam wasiopenda kubadilika na
kuwekeza katika elimu ambayo itawasaidia. wamejikita katika elimu ya
dini.....sehemu ya familia yangu ni waislaam nakumbuka tukiwa
kijitonyama mwalimu wa madrassa alikuwa akilalamika kwa watoto wa
shangazi yangu kutokwenda kusoma madrassa badala yake wanakwenda shuleni
siku za wiki, nilijaribu kumwelewesha kuwa watoto lazima wasome ili
wafaulu kwenda secondary ili baadaye wapate kazi. Ndiyo najua elimu ya
madrassa ni muhimu lakini hata ukimaliza utapata kazi gani? labda
utakuwa sheikh....sikatai lakini uwezekano wa kupata kazi nyingine
unakuwa finyu. Je utaweza kuwa daktari, rubani,accountant, bwana misitu,
n.k bila kusoma elimu ya magharibi? Makamu wa rais Dk. Omar juma
aliwaambia waislaam waache kulalamika kwani kazi inatokana na jinsi
ambavyo umesoma...huwezi kuwa pilot bila ya kujifunza na hapo bila ya
juhudi zako mwenyewe! Wote tuliozaliwa baada ya uhuru tulikuta shule
zote za wakristo zimetaifishwa ( maaskofu na macardinals hawakuzidai
ingawa ni haki yao kuzidai ) walielewa kila mtanzania anapaswa asome
kitu ambacho hata kwenye shule za kanisa zinaendelea hadi leo isipokuwa
kwenye seminari tu za madhehebu yote. Tutakuwa si wakweli tukisema kuwa
dini fulani haikuwa na nafasi sawa na nyingine na kutaka wapewe
upendeleo fulani....tulianza wote baada ya uhuru au hata kabla wakati wa
uhuru (mbona kuna waislaam waliokuwa na elimu waliyopata nchini hata
kabla ya uhuru). Kwa waislaam inabidi tubadilishe mindset zetu, tuongeze
juhudi katika kusoma, ndiyo madrassa ni muhimu hata wakristo nao
wanasoma dini yao lakini pia wanazingatia masomo mengine. Huwezi kusoma
dini pekee yake ukategemea kupata kazi.......tusitafute wachawi, wachawi
ni sisi wenyewe! Kila kiongozi katika nchi yetu amefanya kama
inavyotakiwa, hakuna aliyefanya kwa upendeleo. source: RAIA MWEMA
No comments:
Post a Comment