Swali: "Je! Umomoni ni dhehebu? Wamomoni wanaamini nini?"
KATIKA KUJILINDA KIIMANI NI MUHIMU KUFAHAMU WANAOJIITA WATAKATIFU WA SIKU ZA MWISHO WANAAMINI NINI ILI TUSIJE KUJIKUTA TUMENASA
NA ELIBARIKI ANDREW.
Jibu:
Dini ya Kimomoni, ambayo wafuasi wake wanajulikana kama Wamomoni na
Latter Day Saints (LSD), ilianzishwa chini ya miaka miambili iliyopita
na mtu anayeitwa Joseph Smith. Alisema kwamba alitembelewa na Mungu Baba
na Yesu Kristo ambaye alimwambia kwamba Makanisa yote na kanunu zao za
imani zilikuwa chukizo kwake. Joseph Smith akatoka na kuanzisha dini
nyigine ambayo ilidai kuwa “ndio kanisa ya kweli duniani.” Kasoro na
Wamomoni ni kwamba inachanganyisha, inarembesha, na kupanua juu ya
Bibilia. Wakristo hawana sababu yo yote ya kuamini kuwa Bibilia si kweli
na kamili. Kumwamini Mungu kwa kweli yamaanisha kuwa unaamini katika
neno lake, na maandiko yote ni pumzi ya Mungu, ambayo yamaanisha
yalitoka kwake (Timotheo 3:16).
Wamomoni wanaamini kuwa kunayo
sehemu nne za pumzi kiungu za neno sio moja tu peke: 1) Bibilia “vile
imefasirwa vizuri sana.” Ni aya gani ambazo zinachukuliwa kuwa si kweli
kila wakati haziwekwi wazi. 2) Kitabu cha Wamomoni, ambacho
“kilifasiriwa” na Smith na kuchapishwa mwaka wa 1980. Smith alidai
ndicho “kitabu peke cha kweli.” 3) Kanuni na maagano, ambayo kilikuwa na
mkusanyiko wa ufunuo wa siku hizi kuhusu “Kanisa la Yesu Kristo vile
limerejeshwa.” 4) Lulu ya dhami sana, ambayo inachukuliwa na Wamomoni
“kufafanua” kanuni na mafunzo ambayo yalipotezwa kutoka kwa Bibilia na
kuongezea .ujumbe ulio wake kuhusu uumbaji wa dunia.
Momoni
wanaamini yafuatayo kuhusu Mungu: Hakuwa kiumbe cha mamlaka ya juu sana
juu ya ulimwengu, lakini alipokea mamlaka hayo kupitia kwa kuishi maisha
takatifu na bidii yake isiyo na mwisho. Wanaamini kuwa Mungu Baba ako
na “mwili wa nyama na mifupa inaguzika kama ya mwanadamu.” Ingawa
alitengwa na viongozi wa siku hizi wa Momoni, Brigham Young alifunza
kuwa Adamu awali alikuwa Mungu na baba wa Yesu Kristo. Kwa ulinganisho,
Wakristo wanajua haya kuhusu Mungu: kunaye Mungu mmoja wa kweli
(Kumbukumbu La Torati 6:4; Isaya 43:10; 44:6-8), amekuwa akiishi na
atakuwa akiishi (Kumbukumbu La Torati 33:27; Zaburi 90:2; 1 Timotheo
1:17), na hakuumbwa bali yeye ndiye alikuwa muumbaji (Mwanzo 1; Zaburi
24:1; Isaya 37:16). Yeye ni mkamilifu na hakuna mwingine amfananaye
(Zaburi 15:29; Hosea 11:9). Yeye ni Roho (Yohana 4:24), na Roho
haitengenezwi kwa nyama na mifupa.
Momoni wanaamini kuwa kuna
viwango tofauti au falme tofauti katika maisha baada ya kifo: ufalme wa
peponi, ufalme wa duniani, na giza la nche. Mahali ambao mwanadamu
atamalizia kutegemea chenye wanaamini na kufanya katika maisha haya. Kwa
ulinganisho, Bibilia inatuambia baada ya kifo, tunaenda mbinguni au
jahannamu kulingana na kama tulikuwa au hatukuwa na imani katika Yesu
Kristo kama Bwana na mwokozi wetu. Kutoweka kutoka kwa mwili wetu
yamaanisha, sisi kama waumini, tuko na Mungu (2 Wokorintho 5:6-8). Wasio
amini watatumwa jahannamu au mahali pa wafu (Luka 15:50-54). Kutakuwa
na mbingu mpya na nchi mpya kwa waumini (Ufunuo 21:1) na wasio amini
watatupwa katika zila la moto (Ufunuo 20:11-15). Hakuna nafasi ya pili
ukombozi baada ya kifo (Waebrania 9:27).
Viongozi wa Momoni
wamefunza kuwa ubadilisho wa Yesu ulitokea kwa minajili ya ule uhisiano
wa kimwili wa Mungu Baba na Mariamu. Wamomoni wanaamini kuwa Yesu ni
mungu , lakini binadamu yeyote anaweza kuwa mungu. Momoni wanafunza
kwamba wokovu unaweza patikana kwa kuweka pamoja imani na matendo
mazuri. Kinyume na hii, Wakristo katika historia wamekuwa wakifunza
hakuna mtu atakaye fikia cheo cha Mungu- ni yeye peke ambaye ni
mtakatifu (1 Samueli 2:2). Tunaweza fanywa watakatifu mbele za Mungu
kupitia kwa imani kwake (1 Wakorintho 1:2). Yesu ndiye Mwana wa peke wa
Mungu (Yohana 3:16), yeye ndiye peke ambaye amewai ishi bila dhambi,
maisha yasiyo na mawaa, na sasa ako na heshima ya juu sana mbinguni
(Waebrania 7:26). Yesu na Mungu wote ni kitu kimoja, Yesu kuwa ndiye
peke aliishi baada ya kuzaliwa kimwili (Yohana 1:1-8; 8:56). Yesu
alijotoa yeye mwenye kama dhabihu kwetu, Mugu akamfufua kutoka kwa
kaburi, na siku moja kila mmoja atalikiri kuwa Kristo ni Bwana (Wafilipi
2:6-11). Yesu anatuambia ni vigumu kuingia mbinguni kwa matendo yetu na
kwamba ni kwa imani peke ndani yake itawezekana (Mathayo 19:26). Wote
tunastahali hukumu ya milele kwa sababu ya dhambi zetu, lakini Mungu kwa
upendo wake usio na mwisho na neema vimetuwezeshea njia. “Kwa maana
wote mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa
milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).
Hakika
kunayo njia moja peke ya kupata wokovu na ni kumjua Mungu na Mwanawe,
Yesu (Yohana 17:3). Wokovu haupatikani kwa matendo, bali kwa imani
(Warumi 1:17; 3:28). Tutaipokea zawadi hii, haijalishi sisi ni nani au
ni nini tumefanya (Warumi 3:22). “Wala hakuna wokovu katika mwingine
awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa
wanadamu litupasalo sisi kuokolwea kwalo” (Matendo Ya Mitume 4:12).
Ingwa Wamomoni ni watu wa urafiki, wa upendo, na ni watu wakarimu,
wamedanganywa na dini za uongo ambazo zageuza hali ya Mungu, utu wa Yesu
Kriso, na njia za wokovu
No comments:
Post a Comment